MAARIFA YA JAMII 2012
SEHEMU A
URAIA
Chaguajibu sahihi kisha andika katika karatasiyakoya kujibia.
1. Mwakilishi wa wananchi katika vikao vya Wilaya vya Serikali za Mitaa ni ....
- Mkuu wa Wilaya.
- Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji.
- Afisa Mtendaji Kata.
- Mwenyekiti wa Wilaya wa Chama Tawala.
- Diwani wa Kata.
Chagua Jibu
2. Mojawapo ya majukumu ya Halmashauri ya Wilaya ni kutoa ruzuku kwa .....
- Serikali za Kata.
- Serikali Kuu.
- Vyama vya siasa.
- Serikali za Vijiji.
- Mashirika yasiyo ya kiserikali.
Chagua Jibu
3. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya au Manispaa huteuliwa na .....
- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Baraza la Madiwani la Halmashuri au Manispaa husika.
- Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
- Katibu Mkuu Kiongozi.
Chagua Jibu
4. Katika Bendera ya Taifa rangi ya kijani kibichi inawakilisha ...
- madini
- maji
- uoto wa asili
- kilimo
- ardhi
Chagua Jibu
5. Ni wakati gani Bendera ya Taifa hupeperushwa nusu mlingoti?
- Wakati wa ziara za viongozi wa mataifa mengine.
- Rais anapotangaza hali ya hatari.
- Linapotokea janga la kitaifa au tukio la huzuni.
- Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa wa Taifa.
- Rais anapokuwa nje ya nchi.
Chagua Jibu
6. Uchaguzi wa Rais na Wabunge hapa Tanzania hufanyika kila baada ya
- miaka 10
- miaka 3
- miaka 4
- miaka 5
- miaka 6.
Chagua Jibu
7. Haki za binadamu zinapaswa kutolewa kwa watu wote bila kujali .
- vyama vya siasa.
- katiba ya nchi.
- haki za makundi maalumu.
- umri wa mtu.
- rangi, dini, jinsi na kabila.
Chagua Jibu
8. Kazi mojawapo ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni .........
- kupokea na kuhakiki taarifa ya rasilimali na madeni ya viongozi wa umma
- kusuluhisha migogoro baina ya viongozi wa umma
- kufanya utafiti na kuelimisha jamii kuhusu haki za binadamu na utawala bora
- kuchunguza tuhuma zozote dhidi ya Afisa wa serikali anayehusishwa na rushwa
- kuthibitisha uteuzi wa mawaziri.
Chagua Jibu
9. Ni chombo gani chenye jukumu la kulinda nchi yetu na mipaka yake?
- Jeshi la Polisi Tanzania.
- Jeshi la Magereza la Tanzania.
- Jeshi la Kujenga Taifa.
- Jeshi la Wananchi la Tanzani.
- Jeshi la Mgambo.
Chagua Jibu
10. Lengo kuu la Polisi jamii ni .........
- kufundisha raia kazi za Polisi.
- kujenga mahusiano ya kirafiki baina ya Polisi na raia.
- kuwezesha Maafisa wa Polisi kuishi na raia.
- kuwafanya raia kuwa wakakamavu kama polisi.
- kuzuia matumizi ya dawa za kulevya katika jamii.
Chagua Jibu
11. Mila zinazoathiri afya ya uzazi wa kinamama ni pamoja na .........
- mahari na uzazi wa mpango.
- ukeketaji wanawake na uzazi wa mpango.
- ndoa za utotoni na mahari.
- ukeketaji wanawake na ndoa za utotoni.
- kunyonyesha watoto kwa muda mrefu.
Chagua Jibu
12. Mojawapo ya changamoto wanazozipata wajasiriamali ni pamoja na .......
- ukosefu wa leseni za biashara.
- kutokuwepo kwa benki na taasisi za fedha.
- upatikanaji wa masoko ya bidhaa na huduma.
- uwepo wa askari polisi na mgambo wengi maeneo ya mijini.
- kutokuwepo sera ya uwekezaji.
Chagua Jibu
13. Ni chombo gani chenye jukumu la kumchagua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa?
- Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa.
- Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
- Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
- Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa.
- Mahakama Kuu ya Kimataifa.
Chagua Jibu
14. Mtumishi wa umma ambaye ni Mbunge kwa mujibu wa nafasi yake katika utumishi wa umma ni ....
- Jaji Mkuu
- Katibu Mkuu Kiongozi
- Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
- Msajili wa vyama vya siasa.
- Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Chagua Jibu
SEHEMU B
HISTORIA
Chagua jibu sahihi uliandike katika karatasi yakoya kujibia.
15. Mabaki ya Zinjanthropus yaligunduliwa .........
- Kondoa Irangi.
- Kalenga.
- Olduvai.
- Isimila.
- Engaruka.
Chagua Jibu
16. Wafanyabiashara wa mwanzo wa kigeni kuja Tanganyika walitoka .........
- Amerika.
- Amerika Kaskazini.
- Asia
- Ulaya.
- Amerika Kusini.
Chagua Jibu
17. Mojawapo ya athari ya utawala wa Waingereza katika visiwa vya Unguja ilikuwa ....
- kukomesha biashara ya utumwa.
- kuanzishwa kwa dini ya kikristu.
- kuondoa umaskini.
- kuanzisha kilimo cha karafuu.
- kuanzisha vyama vya siasa.
Chagua Jibu
18. Uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi vya siasa katika Tanzania ulifanyika mwaka
- 1992
- 1990
- 1961
- 2005
- 1995.
Chagua Jibu
19. Elimu kwa wote (UPE) nchini Tanzania ilianzishwa mwaka ...
- 1974
- 1970
- 1972
- 1980
- 1977
Chagua Jibu
20. Nchi ya Afrika iliyokuwa inafuata mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1980 ni .....
- Zimbabwe.
- Tanzania.
- Botswana.
- Ghana.
- Ethiopia.
Chagua Jibu
21. Makabila maarufu katika Afrika ya Mashariki yaliyojihusisha na biashara kabla ya ukoloni ni
- Wangoni, Wakikuyu na Wachaga.
- Wayao, Wangoni na Wakikuyu.
- Wanyamwezi, Wayao na Wakikuyu.
- Wanyamwezi, Wayao na Wazaramo.
- Wayao, Wanyamwezi na Wakamba.
Chagua Jibu
22. Familia inaweza kujikwamua kiuchumi iwapo .
- mama atajishughulisha na kazi za ndani.
- baba ataajiriwa.
- watoto watajishughulisha na masomo.
- wanafamilia watatimiza wajibu wao.
- wanafamilia watasali pamoja.
Chagua Jibu
23. Kabla ya ukoloni elimu ya jadi ilitolewa kwa njia ya .........
- sheria za serikali.
- jando na unyago.
- kwenda vitani.
- kusoma vitabu.
- shule za awali.
Chagua Jibu
24. Makoloni ya Ujerumani katika Afrika yalikuwa ..
- Naijeria, Namibia na Togo.
- Gambia, Togo na Namibia.
- Kameruni, Togo na Namibia.
- Namibia, Tanganyika na Naijeria.
- Kameruni, Tanganyika na Senegal.
Chagua Jibu
25.Ni mataifa yapi kati ya yafuatayo yalianzisha umoja wa nchi zisizofungamana na upande wowote?
- Ulaya Mashariki.
- Nchi zinazoendelea
- Ulaya Magharibi.
- Amerika ya Kusini
- Amerika ya Kaskazini
Chagua Jibu
26. Wajerumani walitawala Tanganyika baada ya .....
- Vita Kuu ya Kwanza.
- Vita Kuuya Pili.
- Mkutano wa Berlin.
- Kuundwa kwa UNO.
- Kushindwa kwa Wareno.
Chagua Jibu
27.Katika Zama za Mwanzo za Mawe binadamu .....
- alianza kufuga wanyama na ndege.
- aligundua moto.
- alijihusisha na kilimo na biashara.
- aliongeza uwezo wa kuzalisha chakula.
- aliishi kwa kutegemea mazingira.
Chagua Jibu
28. Jamii zilizokuwa maarufu kwa kufua chuma hapa Tanganyika ni pamoja na ...
- Wapare na Wazinza.
- Wapare na Wagogo.
- Wazinza na Wasukuma
- Wapare na Wajaluo.
- Wazinza na Wagogo.
Chagua Jibu
29. Soko kuu la watumwa Zanzibar lilifungwa mwaka ......
- 1873
- 1822
- 1845
- 1820
- 1900
Chagua Jibu
30. Mojawapo ya athari za kugawanywa kwa bara la Afrika ilikuwa .........
- kukua kwa viwanda vya Afrika.
- kudumaa kwa viwanda vya Afrika.
- kuboreshwa kwa uchumi wa jadi.
- kudumisha utamaduni wa Kiafrika.
- kuanza kwa biashara ya utumwa.
Chagua Jibu
31.Taifa la pili kuitawala Zanzibar lilikuwa ......
- Uingereza.
- Ujerumani.
- Ureno.
- Oman.
- Ufaransa.
Chagua Jibu
32. Bidhaa zilizoletwa Tanganyika kutoka Bara la Asia kuanzia karne ya nane zilikuwa ni pamoja na ....
- pembe za ndovu na dhahabu.
- Ngozi na bunduki
- Chumvi na shaba
- Nguo na ngano
- Nguo na watumwa
Chagua Jibu
SEHEMU C
JIOGRAFIA
Chaguajibu sahihi na kuandika herufi inayohuska mbeleya nambaya kila swali.
33. Katika kuonesha mahali kwa kutumia mistari ya gridi katika ramani huanza kusomwa namba za mstari gani? .
- Ulalo halafu wima.
- Wima halafu ulalo.
- Kushoto halafu kulia.
- Kulia halafu juu.
- Kulia halafu kushoto.
Chagua Jibu
34. Mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa shughuli za uchukuzi ni: .....
- mtaji, sura ya nchi, uzalishaji na biashara.
- teknolojia, serikali, mtaji na biashara.
- mtaji, sura ya nchi, watu na viwanda.
- serikali, mashirika, mtaji na watu.
- teknolojia, mtaji, uzalishaji, biashara na sura ya nchi.
Chagua Jibu
35. Biashara ya ndani ni ile inayohusisha bidhaa ...
- zinazotengenezwa nje ya nchi.
- zinazotengenezwa na kuuzwa ndani ya nchi.
- zinazozalishwa ndani ya nchi.
- zinazotengenezwa na kuuzwa nje ya nchi.
- zinazouzwa nje ya nchi.
Chagua Jibu
36.Iwapo umbali wa kilometa 25 kwenye ardhi unawakilishwa na urefu wa sentimeta 5 kwenye ramani. Kipimo cha ramani ni ...
- 1:20000
- 1:100000
- 1:50000
- 1:500000
- 1:10000
Chagua Jibu
37. Jua la utosi katika mwezi Disemba huwa katika .
- Kizio cha Kusini.
- Tropiki ya Kansa.
- Ikweta.
- Kizio cha Kaskazini.
- Tropiki ya Kaprikoni.
Chagua Jibu
38. Bainisha vyanzo vya umeme kati ya vifuatavyo: ....
- Nguvu ya maji, madini na nyaya.
- Upepo, nguvu ya maji na transfoma.
- Nguvu ya maji, upepo na jua.
- Makaa ya mawe, nyaya na transfoma.
- Nguvu ya maji, transfoma na makaa ya mawe.
Chagua Jibu
39. Picha iliyopigwa katika uoto wa savanna huonesha ...
- misitu minene.
- nyasi ndefu.
- miti iliyochongoka juu.
- miti yenye umbile la mwavuli.
- nyasi fupi.
Chagua Jibu
40. Athari kuu za viwanda katika mazingira ni .....
- kuchafua maji, hewa na harufu mbaya.
- kutoa moshi na matumizi makubwa ya nguvu ya nishati.
- uchafuzi wa hewa, udongo na harufu mbaya.
- kumwaga kemikali na kutoa moshi.
- uchafuzi wa hewa, maji na ardhi.
Chagua Jibu
41. Zao la mkonge hulimwa katika mikoa ipi Tanzania? ....... .
- Tanga na Mbeya.
- Morogoro na Pwani.
- Morogoro na Tanga.
- Kilimanjaro na Manyara.
- Mtwara na Singida
Chagua Jibu
42. Mambo muhimu katika ramani ni
- uoto, dira kipimio, mistari na jina la ramani.
- rangi, jina la ramani, kipimio, ufunguo na fremu.
- mistari, jina la ramani, dira, fremu na kipimio.
- jina la ramani, ufunguo, fremu, kipimio na dira.
- jina la ramani, ufunguo, kipimio, dira na mistari.
Chagua Jibu
43.Ipi kati ya zifuatazo ni njia ya kuzuia mafuriko?
- Kujenga nyumba imara.
- Kupanda miti.
- Kukata miti.
- Kuchoma misitu.
- Kujenga nyumba mabondeni.
Chagua Jibu
44. Sehemu ya jangwa ambayo maji hupatikana huitwa ....
- Chemchem.
- Visiwa
- Oasis.
- Mito
- Bonde.
Chagua Jibu
45. Faida ya matumizi mrudio katika utunzaji wa mazingira ni ...
- kupanga kazimradi
- uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.
- kupunguza taka
- kutengeneza taka
- kuuza taka.
Chagua Jibu
46. Jua linaonekana kubwa kuliko nyota zingine kwa sababu ...
- lina joto kali kuliko nyota zingine.
- lina mwanga mkali kuliko wa nyota zingine.
- linatupatia nguvu ya jua.
- liko mbali sana na dunia.
- liko karibu zaidi na dunia.
Chagua Jibu
47. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uthibitisho wa ubora wa mazao huitwa
- UNICEF
- FAO
- WHO
- UNESCO
- UNHCR
Chagua Jibu
48.Maeneo ambayo ufugaji wa jadi hufanyika kwa kiwango kikubwa nchini Tanzania ni ...
- Lindi, Mtwara, Shinyanga, Mwanza na Mbeya.
- Kigoma, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha na Lindi.
- Shinyanga, Mwanza, Dodoma, Arusha na Mara.
- Mwanza, Shinyanga, Mbeya, Tanga na Morogoro.
- Mwanza, Shinyanga, Mbeya, Tanga na Lindi.
Chagua Jibu
49. Mgawanyo wa Bonde la Ufa la Afrika Mashariki na kuunda tawi la Mashariki na Magharibi umeanzia Ziwa .........
- Victoria.
- Tanganyika.
- Natroni.
- Nyasa.
- Manyara.
Chagua Jibu
50. Soma ramani ya mistari ya kontua kisha jibu swali lifuatalo:
Herufi b inawakilisha umbo gani la sum ya nchi? .....
- Genge.
- Ronde.
- Mwinuko.
- Kigongo.
- Kilimo.
Chagua Jibu
Try Another Test |