STD VII MAARIFA_JAMII ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2011

MAARIFA YA JAMII 2011

SEHEMU A 
URAIA

Chagua jibe sahihi kisha andika herufi inayohusika mbele ya namba ya kilo swali katika karatasi yako ya kujibia.

1. Kuna aina mbili za uongozi katika Serikali za Mitaa ambao ni uongozi wa:

 1. kulipwa na kujitolea.
 2. kuchaguliwa na kuteuliwa.
 3. kidemokrasia na kidikteta.
 4. kuteuliwa na kujitolea.
 5. kuteuliwa na kulipwa.
Chagua Jibu


2. Katibu wa vikao vya Halmashauri ya Wilaya ni:

 1. Mkuu wa Wilaya. 
 2. Mkurugezi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya.
 3. Afisa Mipango wa Wilaya. 
 4. Katibu Tawala wa Wilaya.
 5. Meya wa Halmashauri.
Chagua Jibu


3. Nguzo kuu tatu za mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni:

 1. Baraza la Mawaziri, Bunge na Mahakama.
 2. Baraza la Mawaziri, Jeshi na•Mahakama.
 3. Baraza la Mawaziri, Polisi na Mahakama.
 4. Baraza la Mawaziri, spika wa Bunge na Mahakama.
 5. Rais, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge.
Chagua Jibu


4. Aina mbili za mazao yanayooneshwa katika Nembo ya Taifa ni:

 1. Kahawa na Katani 
 2. Katani na Karafuu.
 3. Chai na Tumbaku 
 4. Karafuu na Pamba.
 5. Pamba na kahawa.
Chagua Jibu


5. Lengo mojawapo la Mwenge wa Uhuru ni:

 1. kuzindua miradi ya maendeleo.
 2. kutengeneza barabara na kujenga shule za Kata.
 3. kuwaunganisha Watanzania wote.
 4. kuunganisha vyama vya siasa.
 5. kuwafichua wala rushwa.
Chagua Jibu


6. Usalama wa mali ya shule unaweza kuimarishwa kwa:

 1. kuzuia wageni kuingia katika eneo la shule.
 2. kushirikisha Jeshi la Wananchi la Tanzania.
 3. kuepuka mahusiano ya karibu na jamii inayozunguka shule.
 4. kuwekea bima mali ya shule dhidi ya wizi.
 5. kujenga uzio kuzunguka shule.
Chagua Jibu


7. Mkuu wa Jeshi la Magereza huitwa:

 1. Kamishina Mkuu. 
 2. Inspekta Jenerali.
 3. Mkurugenzi Mkuu. 
 4. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.
 5. Mkurugenzi wa Mashitaka.
Chagua Jibu8. Sanaa za maonesho zinajumuisha mambo yafuatayo:

 1. Matambiko, ngonjera na unyago.
 2. Ushonaji, jando na ususi.
 3. Jando, maigizo na unyago.
 4. Ngoma, mashairi na maigizo.
 5. Ngoma, mashairi na ususi.
Chagua Jibu


9. Katika nchi ya kidemokrasia mabadiliko ya uongozi wa nchi hufanyika kwa njia ya:

 1. mapinduzi ya amani. 
 2. kurithi madaraka.
 3. kura ya maoni. 
 4. mfumo wa vyama vingi vya siasa.
 5. uchaguzi mkuu.
Chagua Jibu


10. Mambo ambayo kila mwanadamu anastahili kupata bila kujali kabila, utaifa au jinsia huitwa:

 1. Utawala bora. 
 2. Haki za binadamu.
 3. Utawala wa sheria. 
 4. Demokrasia. 
 5. Usawa wa kijinsia.
Chagua Jibu


11. Umri wa mgombea Urals wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania unapaswa usiwe chini ya miaka

 1. 40
 2. 18 
 3. 35 
 4. 60
 5. 45
Chagua Jibu


12. Mtu anayewekeza mtaji katika mradi au biashara iii kupata faida huitwa:

 1. Dalali.
 2. Mhisani.
 3. Mlanguzi.
 4. Mchumi.
 5. Mjasiriamali.
Chagua Jibu


p>13. J

 1. Tanzania, Malawi, Uganda, Rwanda na Burundi.
 2. Kenya, Tanzania, Uganda, Burundi na Rwanda.
 3. Zambia, Tanzania, Kenya, Uganda na Malawi.
 4. Burundi, Tanzania, Kenya, Sudani na Uganda.
 5. Tanzania, Kenya na Uganda.
Chagua Jibu


14. Kazi mojawapo ya Bunge la Tanzania ni:

 1. kupendekeza jina la Makamu wa Rais.
 2. kupendekeza jina la Spika wa Bunge.
 3. kuteua Katibu wa Bunge.
 4. kuthibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu.
 5. kuthibitisha uteuzi wa Jaji Mkuu.
Chagua Jibu


SEH EMU B HISTORIA

Chagua jibu sahihi kisha andika herufi inayohusika mbele ya kila swali katika karatasi yako ya kujibia.

15. Baba, mama na watoto kwa pamoja huunda:

 1. ukoo.
 2. familia pana 
 3. jamii 
 4. familia 
 5. jumuiya
Chagua Jibu


16. Lipi kati ya yafuatayo lilikubaliwa katika mkutano wa Berlin mwaka 1884 - 1885?

 1. Kukomesha biashara ya utumwa.
 2. Kuundwa kwa serikali za kidemokrasia.
 3. Kukomesha vita vya kikabila.
 4. Kuimarisha ukabila.
 5. Kudhoofisha ukabaila.
Chagua Jibu


17. Ni nani alikuwa Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar?

 1. Ali Hasan Mwinyi.
 2. Mohamed Shamte. 
 3. Kukomesha vita vya kikabila.
 4. Kuimarisha ukabila. 
 5. Aboud Jumbe.
Chagua Jibu


18. Lengo la elimu katika Afrika huru lilikuwa:

 1. kuleta walimu toka Ulaya.
 2. kupunguza kiwango cha wasiojua kusoma.
 3. kutoa elimu kwa ubaguzi wa rangi.
 4. kutoa elimu kwa kufuata dini.
 5. kutoa elimu kwa watoto wa machifu.
Chagua Jibu


19. Zipi katika nchi zifuatazo zilipata uhuru kwa njia ya mtutu wa bunduki?

 1. Angola, Ghana na Kenya.
 2. Zimbabwe, Angola na Kenya.
 3. Mozambique, Liberia na Zimbabwe.
 4. Uganda, Rwanda na Tanganyika.
 5. Kenya, Uganda na Liberia.
Chagua Jibu


20. Mkataba uliokataza kusafirisha watumwa nje ya Afrika Mashariki ulijulikana kam mkataba wa:

 1. Moresby wa 1822. 
 2. Hamerton wa 1845.
 3. Frere wa 1873. 
 4. Berlin wa 1885.
 5. Heligoland wa 1890.
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  
Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256