STD VII MAARIFA_JAMII ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2010

MAARIFA YA JAMII 2010

URAIA, JOGRAFIA NA HISTORIA 

SEHEMU A

Chagu jibe hullo sahihi kisha andika herufi inayohusika mbele ya kilo swali katika karatasi ya kujibia uhyopewa.

1. Ukoo ni muungano wa:

 1. familia zinazokaa karibu 
 2. familia nyingi zenye asili moja
 3. familia nyingi zilizo rafiki 
 4. baba, mama na watoto.
 5. familia zilizoungana kufanya kazi pamoja.
Chagua Jibu


2. Utamaduni maana yake ni

 1.  imani, desturi, mila na miiko ya jamii ya watu
 2.  kuimba na kucheza kwa pamoja
 3.  namna ya kufanya matambiko katika jamii
 4.  desturi na mila za jamii Fulani
 5.  utaratibu wa kuishi
Chagua Jibu


3. Kiongozi wa serikali ngazi ya kata ni

 1. Diwani 
 2. Afisa mtendaji wa kata
 3. Mwenyekiti wa kata
 4. Katibu kata
 5. Afisa mifugo wa kata
Chagua Jibu


4. Ili Afrika ijitegemee kiuchumi inahitaji

 1. misaada toka nje 
 2. Ongezeko kubwa la watu
 3. sayansi na teknolojia 
 4. mikopo ya masharti nafuu
 5. wawekezaji wa kiafrika.
Chagua Jibu


5. Lengo kuu la kuanzishwa kwa Jumuiya ya Madola lilikuwa

 1.  kupata makoloni zaidi barani Afrika
 2.  kuimarisha uhusiano baina ya Uingereza na nchi ilizozitawala
 3.  kuoongeza kiasi cha malighafi zilizokuwa zinahitajiwa na wazungu.
 4.  kuwaachia watumwa ambao bado walikuwa hawajawa huru
 5.  kumfanya malkia wa Uingereza aogopwe na ulimwengu mzima.
Chagua Jibu


6. Mahakama inayotoa hukumu ya kesi za mauaji ni

 1. Mahakama ya mwanzo 
 2. Mahakama ya wilaya
 3. Mahakama kuu 
 4. Mahakama ya hakimu mkazi
 5. Mahakama ya Rufaa
Chagua Jibu


7. Nchi zinazopakana na Tanzania upande wa kusini ni

 1.  Msumbiji na Malawi
 2.  Msumbiji na Zimbabwe
 3.  Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo na Malawi
 4.  Burundi na Malawi
 5.  Rwanda na Malawi
Chagua Jibu


8. Nini tofauti kati ya nyota na sayari?

 1.  Nyota humweka wakati sayari hazimweki
 2.  Nyota zinatoa mwanga mweupe, wakati sayari hutoa mwanga wa rangi ya njano.
 3.  Sayari huonekana mchana lakini nyota huonekana usiku tu.
 4.  Nyota hazina mwanga wakati sayari zina mwanga
 5.  Sayari zote zina viumbe hai wakati nyota hazina viumbe hai
Chagua Jibu


9. Bonde la ufa limegawanyika sehemu ya Mashariki na Magharibi katika nchi gani?

 1. Kenya 
 2. Uganda 
 3. Tanzania 
 4. Burundi 
 5. Ethiopia
Chagua Jibu


10. Vifuatavyo vilikuwa ni vyama vya ukombozi kusini mwa Afrika isipokuwa

 1. ANC 
 2. PAC 
 3. SWAPO 
 4. KANU 
 5. UNITA
Chagua Jibu


11. Mkusanyiko wa shughuli zinazohusisha wafanyabiashara na walaji au watumiaji huitwa 

 1. Soko 
 2. duka
 3. Bidhaa 
 4. mteja 
 5. fedha
Chagua Jibu


12. Bara la pili kwa ukubwa ulimwenguni ni

 1. Asia 
 2. Afrika 
 3. Australia
 4. Amerika ya Kaskazini 
 5. Amerika ya kusini
Chagua Jibu


13. Rais wa kwanza wa Bunge la Umoja wa Afrika lililoanzishwa Machi 2004 ni

 1. Dr. Salim Salim 
 2. Dr. Emek Anyauko
 3.  Mh. Getrude Mongela 
 4. William Erek 
 5. Peter Omu
Chagua Jibu


14. Mtanzania anaruhusiwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu anapofikia umri wa miaka 

 1. 15 
 2. 25 
 3. 40 
 4. 21 
 5. 18
Chagua Jibu


15. Hapo awali mabara yote yalikuwa yameshikana na kuwa bara moja lililojulikana kama 

 1. Andes 
 2. Pangaea
 3. Australia 
 4. Eurasia 
 5. Antaktika
Chagua Jibu


16. Tabaka la ozone huweza kuharibiwa na

 1.  kuongezeka kwa gesi ya oksijeni
 2.  Kuongezeka kwa gesi ya haidrojeni kwenye anga
 3.  moshi wenye kemikali unaotoka viwandani na kwenye magari
 4.  kupungua kwa gesi ya kaboni daioksaidi kwenye anga
 5.  vumbi linalosambaa angani kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini
Chagua Jibu


17. Rhoda anachemsha maji ya kunywa kila siku kwa sababu maji yaliyochemshwa

 1. ni safi na salama 
 2. yana ladha nzuri
 3. hukata kiu haraka 
 4. huua wadudu walioko katika matumbo yetu
 5. huwa na virutubisho vingi
Chagua Jibu


18. Lengo mojawapo la michezo shuleni ni

 1. kutumia viwanja vya shule vizuri
 2. kuleta umoja na ushirikiano
 3. kuwapa zawadi washiriki
 4. kutambua shule zisizo na viwanja vya michezo
 5. kupata wachezaji wa kulipwa
Chagua Jibu


19. Serikali za mitaa zina aina ......za Halmashauri

 1. moja 
 2. nne 
 3. tano 
 4. tatu 
 5. sita
Chagua Jibu


20. Idadi kubwa ya wakimbizi katika bara la Afrika inasababishwa na

 1. umaskini katika nchi nyingi za Afrika
 2. migogoro ya kifamilia 
 3. miundo mbinu duni
 4. upungufu wa ajira 
 5. machafuko ya kisiasa
Chagua Jibu


21. Vituo vikuu vya misafara ya watumwa Tanganyika vilikuwa

 1. Ujiji, Kilwa na Tanga 
 2. Tabora, Mpwapwa na Tanga
 3. Tabora, Ujiji na Bagamoyo 
 4. Pangani, Mpwapwa na Dodoma
 5. Kilwa, Bagamoyo na Dodoma
Chagua Jibu


22. Vyama vingi vya kisiasa nchini Tanzania viliruhusiwa kisheria kwa mara ya pili mnamo mwaka .........

 1. 1995
 2. 2000 
 3. 1992 
 4. 1990 
 5. 1964
Chagua Jibu


23. Tanzania ipo kusini mwa

 1. lkweta 
 2. Tropiki ya kaprikoni
 3. Greenwich 
 4. Ncha ya kaskazini
 5. Muhimili wa dunia
Chagua Jibu


24. Ikiwa kwenye longitude 0° ni saa 4 asubuhi, je itakuwa saa ngapi Afrika Mashariki nyuz: 45° Mashariki?

 1. saa 6 mchana. 
 2. saa 12 jioni 
 3. saa 4 usiku
 4. saa 7 mchana 
 5. saa 2 asubuhi
Chagua Jibu


25. Yafuatayo ni mambo yalisababishwa na uharibifu wa uoto isipokuwa:

 1. Kimbunga na tufani
 2. upungufu wa maji na nusu jangwa
 3. mmomonyoko wa udongo na kupotea kwa viumbe hai
 4. njaa na mifugo mingi ku fa
 5. Uchimbaji madini na utengenezaji barabara
Chagua Jibu


26. Miinuko ya mlima Mlanje nchini Malawi ni maarufu kwa kilimo cha

 1. pamba 
 2. Kahawa 
 3. katani 
 4. chai 
 5. pareto
Chagua Jibu


27. Nini maana ya biashara ya rejareja?

 1. Kuuza bidhaa kidogo kidogo
 2. Kingiza bidhaa za kutoka nje
 3. Kuuza bidha ya aina moja tu.
 4. Kuuza bidhaa bila kuwa mwangalifu.
 5. Kuuza bidha za vitu vinavyotumika majumbani
Chagua Jibu


28. Bahari ya Shamu na bahari ya Mediterranean zimeunganishwa na

 1. mfereji wa Suez 
 2. mfereji wa panama
 3. Mto wa Nile 
 4. Mlango bahari wa Gibraltar
 5. milima ya Atlas
Chagua Jibu


29. Zifuatazo ni sababu za kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UNO) isipokuwa:

 1. kuepusha vita kuu ya Dunia
 2. kudumisha amani na usalama
 3. kukuza na kuendeleza uchumi
 4. kutatua migogoro sehemu mbalimbali
 5. kutoa upendeleo kwa mataifa makubwa
Chagua Jibu


30. Sera ambazo hutuongoza katika kutekeleza mambo ya maendeleo ya uma hutokana na

 1. Chama tawala 
 2. Vyama vya upinzani
 3. baraza la mawaziri 
 4. Vyombo vya dola 
 5. kamati za serikali
Chagua Jibu


31. Ukanda wa kitropiki hupatikana kati ya latitude

 1.  0° - 5° kaskazini na kusini ya Ikweta
 2.  0°- 15° kaskazini na kusini ya Ikweta
 3.  0° - 30° kaskazini na kusini ya lkweta
 4.  35° - 65° kaskazini na kusini ya lkweta
 5.  30° - 60° kaskazini na kusini ya lkweta
Chagua Jibu


32. Kwanini mito mingi ya Afrika haitumiki kwa usafirishaji

 1. Ina maporomoko
 2. Ina magugu mengi 
 3. Ina mamba wengi
 4.  Haina bandari kubwa
 5. Mingi ni mifupi
Chagua Jibu


33. Mtu akiugua UKIMWI ni muhimu

 1. kumtengea chumba
 2. kumtengea chombo cha chakula
 3. kumpa upendo na huduma
 4. kumkabidhi kwa wazee
 5. Kutocheza nae
Chagua Jibu


 34. Aina kuu madawa ya kulevya ni pamoja

 1. Bangi, kokeini na heroini
 2. Gongo, Kokeini na bangi 
 3. Tumbaku, bangi na mihadarati
 4. Sigara, valiamna gongo 
 5. Bangi, Sigara na gongo
Chagua Jibu


35. Mahali penye genge huoneshwa namna gani kwa mistari ya kontua kwenye ramani?

 1. Kwa alama ya U au V
 2. Kukaribiana kwa mistari ya kontua
 3. Kutengana kwa misitari ya kontua
 4. Mistari ya kontua huonekana kama imekutana
 5. Mistari ya kontua iliyonyooka
Chagua Jibu


36. Zao kuu la biashara linalolimwa wilaya ya mbinga mkoani Ruvuma ni 

 1. Korosho 
 2. Karafuu 
 3. Chai 
 4. Kahawa 
 5. Pamba
Chagua Jibu


37. Nani huwateua Mawaziri na Manaibu mawaziri katika serikali ya Tanzania 

 1. Spika wa bunge 
 2. Rais
 3. Katibu wa bunge 
 4. Makamu wa Rais 
 5. Waziri Mkuu.
Chagua Jibu


38. Sababu kubwa zinazochangia idadi ya vifo barani Africa ni pamoja na

 1. maisha ya starehe na michezo ya hatari
 2. njaa, maradhi na milipuko ya vita
 3. ukeketaji na mimba za utotoni
 4. mila potofu na makazi yasiyo na uhakika
 5. Rushwa, udikteta na ukuaji wa miti.
Chagua Jibu


39. Yapi ni madhara ya ukataji wa miti katika maeneo jirani na ziwa Victoria?

 1. kupunguza idadi ya samaki
 2. kuharibu vyanzo vya maji vinavyoleta maji ziwani
 3. Kuongeza mafuriko katika ziwa Victoria
 4. kuongezeka kwa maji ya mto Nile unaoanzia ziwa Victoria
 5. kuongezeka kwa wanyama wakali maeneo ya jirani na ziwa
Chagua Jibu


40. Moja ya matatizo yanayovikabili viwanda na biashara Tanzania ni

 1. uhaba wa wateja wa bidhaa zinazozalishwa
 2. upungufu wa gharama kubwa ya nishati
 3. uhaba wa wafanyabiashara
 4. hall mbaya ya hewa
 5. uhaba wa wafanyakazi.
Chagua Jibu


41. Kwanini usafirishaji wa malighafi na bidhaa za viwanda hutumia zaidi njia ya maji?

 1. Ni njia ya haraka ya usafirishaji wa bidhaa
 2. Gharama nafuu na husafirisha mizigo mingi
 3. Sehemu kubwa ya dunia imezungukwa na maji
 4. Ni njia salama zaidi kuliko nyingine
 5. lnapunguza uchafuzi wa mazingira
Chagua Jibu


42. Ardhi, misitu, mito, bahari na madini kwa ujumla tunaviita 

 1. bidhaa muhimu 
 2. Dunia
 3. uoto wa asili 
 4. maliasili
 5. mahitaji muhimu
Chagua Jibu


43. Ipi kati ya zifuatazo sio miongoni mwa sababu za uchafuzi wa mazingira?

 1. Teknolojia duni
 2. Kuwepo kwa watu wengi
 3. Kutokuwa na Elimu
 4. Kutumia mbolea za asili zaidi katika kilimo
 5. Utaratibu mbaya wa kutupa takataka
Chagua Jibu


44. Nchi zilizopo Mashariki mwa Afrika ni

 1. Zambia, Malawi, Tanzania na Kenya
 2. Sudan, Zambia, Tanzania na Uganda
 3. Rwanda, Burundi, Tanzania na Malawi
 4. Kenya, Tanzania, Uganda na Malawi
 5. Kenya, Uganda, Tanzania na Somalia
Chagua Jibu


45. Zama za mawe zimegawanyika katika sehemu ngapi?

 1. Tatu 
 2. Mbili 
 3. Nne 
 4. Tana 
 5. Moja
Chagua Jibu


SEHEMU B

Soma kwa makini ramani ifuatayo (Kielelezo Namba 1) kisha jibu maswali 46 - 50 kwa kuandika en o moja to katika karatasi ya kujibia.

46. Hifadhi ya Taifa inayooneshwa kwa herufi A inaitwa........

Chagua Jibu


47. Taja aina ya madini yanayopatikana katika eneo lililooneshwa kwa herufi . . . . . . . . .

Chagua Jibu


48. Zao gani la biashara linastawi kwenye mteremko wa mlima uliooneshwa kwa herufi C?

Chagua Jibu


49. Kisiwa kilichooneshwa kwa herufi kinaitwaje?

Chagua Jibu


50. Reli iliyooneshwa kwa herufi EF inaitwa . .....

Chagua Jibu


Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

Bofya Hapa Kupakua
App Ya Learning Hub Tanzania
GO TO NECTA EXAMS