STD VII MAARIFA_JAMII ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2009

MAARIFA YA JAMII 2009

URAIA, JIOGRAFIA NA HISTORIA

Chagua jibu kisha andika herufi inayohusika mbeleya nambaya kila swali katika karatasi yako ya kujibia.

1.  Kati ya mambo yafuatayo lipi siyo haki ya raia wa Tanzania?

 1. kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu katika umri wowote
 2. kuishi popote pale ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
 3. Uhuru wa kuabudu 
 4. kupata ulinzi
 5. Uhuru wa kujieleza
Chagua Jibu


2.  Kiongozi gani nchini Tanzania mwenye mamlaka ya kulivunja Bunge?

 1. Spika wa Bunge
 2. Naibu Spika wa Bunge
 3. Waziri Mkuu 
 4. Rais 
 5. Mwanasheria Mkuu
Chagua Jibu


3.  Kabla ya karne ya 16 mji wa Kilwa ulikuwa maarufu kutokana na biashara ya:

 1. meno ya ndovu 
 2. shaba 
 3. watumwa
 4. dhahabu
 5. viungo
Chagua Jibu


4.  Chifu wa Wanyamwezi aliyepigana na utawala wa Wajerumani kati ya 1891 na 1894 alikuwa:

 1. Mazengo
 2. Mirambo 
 3. Isike 
 4. Msiri 
 5. Mkwawa
Chagua Jibu


5.  Mwinuko wa kati wa Bonde la Ufa wenye milima ya Rungwe, Livingstone na Kipengele ni chanzo cha mito ipi?

 1. Ruaha Mkuu Wami na Rufiji
 2. Tana, Mara na Pangani
 3. Njombe, Galana na Katonga
 4. Luwengu, Ruvuma na Malagalasi
 5. Ugalla, Wami na Galana
Chagua Jibu


6.  Ipi kati ya mambo yafuatayo siyo njia ya kueneza UKIMWI?

 1. kuchangia vifaa vya kutogea na vya kuchoma sindano
 2. kushikana mikono na mtu aliyeathirika na UKIMWI
 3. kujamiana na mtu aliyeathirika na UKIMWI
 4. kuongezewa damu yenye virusi vya UKIMWI
 5. mtoto kunyonya kutoka kwa mama mwenye virusi vya UKIMWI
Chagua Jibu


7.  Wakati wa ukoloni, utamaduni wa Mwafrika ulidhoofika kwa sababu zifuatazo isipokåwa:

 1. upigaji marufuku baadhi ya mila na desturi
 2. ubezaji wa utamaduni wa Mwafrika kupitia elimu ya kikoloni
 3. uhimizaji wa matumizi ya lugha za Kiafrika uliofanywa na wasomi wa Kiafrika
 4. Waafrika wengi kuiga mila za kizungu
 5. elimu ya kikoloni kushindwa kurithisha mila na desturi za Kiafrika
Chagua Jibu


8.  Tabia ya hali ya Savana hupatika kati ya latitude ......... kaskazini na kusini mwa Ikweta:

 1. 0 0 - 5  
 2. 23 0 - 35  
 3. 5 0 - 15 0
 4. 0 0 - 15 0
 5. 20 0 - 30 
Chagua Jibu


9.  Mila na desturi za Kiafrika ni muhimu kwa sababu:

 1. zinakuza sayansi na teknolojia
 2. zinadumisha utamaduni wa Kiafrika
 3. zinaimarisha imani za Kiafrika
 4. zinazuia ukame na njaa
 5. zinazuia mipango baina ya nchi na nchi
Chagua Jibu


10.  Maeneo yanayopata mvua nyingi kwa mwaka nchini Tanzania ni:

 1. yenye mito mingi 
 2. yaliyo karibu na bahari, maziwa na milima
 3. maeneo ya kati ya Tanzania 
 4. maeneo yaliyopo kando ya Bonde la Ufa 
 5. maeneo yenye makazi
Chagua Jibu


11.  Nini maana ya Serikali za Mitaa:

 1. mfumo wa utawala katika ngazi ya Wilaya na Mkoa
 2. mfumo wa utawala katika ngazi ya Halmashauri za wilaya na vijiji
 3. mfumo wa utawala ulioundwa kisheria
 4. mfumo wa utawala usio na madaraka kamili ya kujiendesha
 5. mfumo wa utawala wenye halmashauri
Chagua Jibu


12.  Lipi kati ya yafuatayo ni miongoni mwa madhara ya ukoloni?

 1. kuzorota kwa viwanda vya serikali
 2. kukua kwa utamaduni wa Kiafrika
 3. kukomeshwa kwa ubaguzi wa rangi
 4. kuwepo kwa demokrasi
 5. elimu ilitolewa bure
Chagua Jibu


13.  Tarehe 21 Machi na 23 September jua linakuwa utosini katika

 1. ncha ya kaskazini
 2. mstari wa Kaprikoni
 3. mstari wa Kansa 
 4. Griniwichi
 5. Ikweta
Chagua Jibu


14.  Majukumu makuu ya kiongozi wa familia ni yapi?

 1. kuwapatia wanafamilia mahitaji ya msingi
 2. kupeleka watoto shule
 3. kuwasaidia ndugu, jamaa na marafiki
 4. kufanya kazi kwa bidii 
 5. kurekebisha tabia za wanafamilia
Chagua Jibu


15.  Wakoloni wa Wajerumani walianzisha kodi ya kichwa kwa lengo la

 1. kuwapatia maskini nchini Ujerumani
 2. kutoa huduma za jamii vijijini
 3. kuongeza pato la gavana
 4. kuongeza pato la wananchi
 5. kuwafanya watu wafanye kazi katika mashamba ya wakoloni
Chagua Jibu


16.  Chama cha Afro Shiraz kilitokana na muungano wa vyama vya:

 1. Afrika Association na Pemba People's Party
 2. Shirazi Association na Muslim Association
 3. Zanzibar and Pemba People's Party na Umma Party
 4.  Afrika Association na Shirazi Association
 5. Zanzibar National Party na Zanzibar Pemba People's Party
Chagua Jibu


17.  Watu wengi wamehamia mjini kutoka vijijini kwa sababu gani?

 1. vijijini hakuna barabara za lami
 2. mijini kuna burudani
 3. vijijini kuna mashamba
 4. mijini hakuna umaskini 
 5. mijini kuna ajira na huduma za jamii
Chagua Jibu


18. Vipimo vya ramani huoneshwa kwa njia za:

 1. sentensi, uwiano wa mstari 
 2. sehemu, sentensi na namba
 3. skeli kubwa, za kati na ndogo
 4. Uwiano, sehemu na kilometa
 5. sentensi, skeli ndogo na maili
Chagua Jibu


19. Aina kuu tatu za uchukuzi ni:

 1. nchi kavu, maji na anga 
 2. anga, barabara na redio
 3. simu, nchi kavu na barabara 
 4. televisheni, redio na mtandao
 5. nchi kavu, maji na simu
Chagua Jibu


20. Kazi za Serikali kuu ni zipi?

 1.  kutoa huduma za afya, elimu na usalama
 2.  Kuhimiza uanzishwaji wa vyama vya siasa
 3.  kushawishi wapinzani kujiunga na Serikali kuu
 4.  kupiga marufuku upinzani
 5. kufanya biashara
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  
Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256