STD VII MAARIFA_JAMII ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2008

MAARIFA YA JAMII 2008

URAIA, JIOGRAFIA NA HISTORIA

Chaguajibu lililo sahihi na andika herufi inayohusika mbeleya nambaya kila swali katika karatasiya kujibia uliyopewa.

1. Jukumu la ulinzi na usalama katika familia ni la:

 1. baba na mama
 2. baba
 3. baba, mama na watoto
 4. mlinzi aliyeajiriwa
 5. wanafamilia wa kiume
Chagua Jibu


2. Mbinu zinazoweza kutumika katika kuwarekebisha watu wenye mienendo mibaya katika jamii ni:

 1. kuwatenga wale wenye mienendo mibaya
 2. kuwahamishia kwenda mbali na sehemu wanakoishi
 3. kutumia njia ya sanaa za maonyesho kama vile hadithi, maigizo na nyimbo
 4. kuwapeleka mahakamani
 5. kuwapeleka kifungoni kwa muda mrefu
Chagua Jibu


3. Katibu Tawala wa Wilaya huteuliwa na:

 1. Spika wa Bunge 
 2. Waziri Mkuu 
 3. Rais 
 4. Mkuu wa Wilaya 
 5. Makamu wa Rais
Chagua Jibu


4. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi huitwa:

 1. UNESCO 
 2. UNICEF 
 3. UNDP
 4. UNHCR
 5. WHO
Chagua Jibu


5. Wangoni walihamia Afrika Mashariki wakiwa wametokea kusini mwa Afrika wakikimbia vita vya kikabila vilivyoitwa:

 1. Mfecane
 2. majimaji
 3. maumau 
 4. vita kuu vya pili vya dunia
 5. vita ya kwanza ya dunia
Chagua Jibu


6. Hifadhi ya wanyamapori ni muhimu kwa nchi yetu kwa sababu

 1. huchangia pato la taifa kutuingizia fedha za kigeni
 2. tunapata fursa ya kuona wazungu wengi wanaokuja kuwaona wanyama
 3. wanapata fursa ya kuzaliana na kuwa wengi
 4. husaidia kuhifadhi mazingira yetu ya asili
 5. husaidia kulinda wanyama adimu ili wasitoweke
Chagua Jibu


7. Chanzo kipi kati ya vifuatavyo vya kuzalisha nishati kimegundulika maeneo ya kusini mwa Tanzania hivi karibuni?

 1. Makaa ya mawe
 2. madini ya uranium
 3. umeme wa jua
 4. gesi
 5. umeme utokanao na maji
Chagua Jibu


8. Nyota iliyo karibu na dunia kuliko nyota zote ni:

 1. Asteroid 
 2. mwezi 
 3. jua 
 4. kimondo 
 5. Jupita
Chagua Jibu


9. Uoto wa Savana wa Afrika Mashariki una sifa zipi?

 1. vichaka na miti mirefu
 2. misitu ya mikoko, nyasi na vichaka
 3. misitu ya miombo na nyasi ndefu
 4. Misitu minene na nyasi fupi
 5. nyasi, vichaka virefu na miti michache
Chagua Jibu


10.Ni mto gani kusini mwa Afrika unamwaga maji yake katika bahari ya Atlantiki?

 1. Zambezi
 2. Limpopo
 3. Orange 
 4. Shire
 5. Mkoamati
Chagua Jibu


11. Zifuatazo ni kazi za benki katika biashara isipokuwa:

 1. kuwezesha ulipaji na upokeaji wa fedha
 2. kutunza na kuhakikisha usalama wa fedha
 3. kutoa mikopo kwa wafanya biashara
 4. kuwagawia wafanyabiashara fedha kiholela
 5. kutoa kumbukumbu sahihi ya mapato na matumizi kwa wateja
Chagua Jibu


12. Bara la Afrika lina jumla ya nchi huru:

 1. 51
 2. 65 
 3. 53 
 4. 104
 5. 96
Chagua Jibu


13. Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa sasa ni nani?

 1. Mwai Kibaki
 2. Mwanawasa
 3. Thabo Mbeki
 4. Idriss Deby Itno
 5. Yoweri Museveni
Fungua Jibu


14.Mwanasheria Mkuu wa Serikali huteuliwa na .........

 1. Wabunge
 2. Rais
 3. Jaji Mkuu
 4. Meya 
 5. Wananchi
Chagua Jibu


15. Ipi kati ya zifuatazo ni sifa ya mimea inayopatikana kwenye uoto wa kijangwa?

 1. matawi yenye miiba na mizizi mirefu
 2. mashina makubwa na mizizi iliyosambaa
 3. majani mapana na matawi marefu
 4. matawi mafupi na majani membamba
 5. shina lenye ganda jembamba
Chagua Jibu


16. Ili kupunguza matatizo ya mazingira yanayosababishwa na ufugaji holela na mifugo mingi, jamii zihamasishwe:

 1. kuacha shughuli za ufugaji
 2. kupunguza mifugo na kufanya ufugaji wa ndani
 3. kuhamisha mifugo yote na kuagiza nyama na maziwa toka nje
 4. kuchoma moto maeneo yote yaliyo wazi kupata nyasi za kutosha
Chagua Jibu


17. Familia bora ni ile yenye kupata:

 1. chakula, lishe, usafiri na mshahara
 2. chakula bora, malazi, mavazi na lishe
 3. maradhi, chakula bora, mavazi na lishe
 4. mavazi, maradhi, lishe na matibabu
 5. elimu, usafiri, chakula na maradhi
Chagua Jibu


18. Michoro ya mapangoni hapa Tanzania inapatikana:

 1. Oldvai Gorge
 2. Russinga
 3. Kondoa Irangi 
 4. Isimila Iringa 
 5. Pangani Tanga
Chagua Jibu


19. Mwenyekiti wa serikali za mitaa hupatikana kwa:

 1. kuteuliwa na mkuu wa wilaya
 2. kuajiriwa na serikali 
 3. kuchaguliwa na wananchi 
 4. kuchaguliwa na madiwani
 5. kuchaguliwa na Wabunge
Chagua Jibu


20. Idadi kubwa ya wakimbizi barani Afrika inasababishwa na:

 1. umasikini katika nchi nyingi
 2. vita baina ya mataifa jirani
 3. migogoro ya mipaka
 4. uhaba wa maeneo ya kukaa
 5. vita vya wenyewe kvva wenyewe
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  
Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256