STD VII MAARIFA_JAMII ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2006

 MAARIFA YA JAMII 2006

SEHEMU A

URAIA, JIOCRAFIA NA HISTORIA

Chagua jibu lililo sahihi na kisha andika herufi inayohusika mbeleya nambaya kila swali katika karatasiyako ya kujibia.

1. Familia yetu inaweza kupata maendeleo mazuri ya kiuchumi ikiwa:

  1. mama atajishughulisha na kazi za ndani ya nyumba tu
  2. baba ataachiwa ashughulikie kazi ya ajira tu
  3. watoto hawatajihusisha na kazi yoyote isipokuwa kwenda shule na tuisheni
  4. kila ndugu anayeomba msaada atapewa
  5. kila mwanafamilia atashiriki kikamilifu kutimiza majukumu aliyopangiwa
Chagua Jibu


2. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkuu wa Bunge ni nani?

  1. Waziri Mkuu
  2. Spika wa Bunge 
  3. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 
  4. Jaji Mkuu 
  5. Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Chagua Jibu


3. Madhumuni ya kuundwa kwa serikali za mitaa nchini ni:

  1. kuongeza nafasi za kazi kwa wasomi
  2. kuharakisha maendeleo ya wananchi
  3. kuinua maendeleo ya wanawake
  4. kupanua biashara ndogondogo
  5. kuimarisha ukusanyaji wa kodi
Chagua Jibu


4. Latitudo ndogo kuliko zote ni:

  1. ncha ya Kusini na Kaskazini
  2. muhimili wa dunia 
  3. Tropiki ya Kansa
  4. Ikweta 
  5. Grinwichi
Chagua Jibu


5. Ramani iliyokamilika inakuwa na mambo yafuatayo:-

  1. barabara, miji, dira, uoto na mipaka 
  2. kichwa, ufunguo, kipimio, dira na pambizo
  3. uoto, barabara, reli, miji na ufunguo
  4. mazao, pambizo, kipimio, kichwa na dira
  5. dira, ufunguo, kipimio, mipaka na kichwa
Chagua Jibu


6. Mabwawa makubwa yanayozalisha umeme kwa wingi Tanzania ni:

  1. Pangani na Kidatu 
  2. Kihansi na Mtera
  3. Nyumba ya Mungu na Hale 
  4. Mtera na Kidatu
  5. Kidatu na Nyumba ya Mungu
Chagua Jibu


7. Wapelelezi wa kwanza waliofika Afrika ya Mashariki karne ya 19 walikuwa:

  1. Burton na Speke
  2. Rebman na Grant
  3. Rebman na Krapf 
  4. Krapf na Burton
  5. Speke na Livingstone
Chagua Jibu


8. Makaburu walivamia ncha ya Kusini mwa Afrika chini ya uongozi wa nani?

  1. Jan Van Riebelk 
  2. Bartholomew Diaz
  3. Rebman na Kruger 
  4. Von Letton
  5. Vasco Da Gama
Chagua Jibu


9. Jamii ya watu waliohamia Afrika ya Mashariki kati ya mwaka 100 na 500 baada ya Kristo kutoka Magharibi ya Afrika walikuwa:

  1. Wanaoiloti 
  2. Wahabeshi
  3. Mbilikimo
  4. Wabantu 
  5. Wakush
Chagua Jibu


10. Sababu kubwa ya kutokea kwa familia za mzazi mmoja ni nini?

  1. Kutozingatia uzazi wa mpango
  2. Matatizo ya kiuchumi
  3. Ukosefu wa ajira
  4. Kuiga mila za kigeni
  5. Wazazi kutelekeza watoto
Chagua Jibu


11. Chanzo cha nishati ya nyuklia ni madini ya:

  1. uraniamu 
  2. platiniamu 
  3. beriliamu
  4. vanadiamu
  5. titaniamu
Chagua Jibu


12. Idadi ya watu katika nchi hujulikana kwa njia ya:

  1. kupiga kura 
  2. kujua idadiya wanawake wenye umri wa kuzaa
  3. kuhesabu idadi ya vijana 
  4. sensa ya watu 
  5. kusajili wahamiaji na wahamaji
Chagua Jibu


13. Katika muundo wa mahakama, hakimu mkazi ni hakimu katika mahakama . . . . . .

  1. ya Wilaya 
  2. ya Mwanzo 
  3. ya Mkoa
  4. Kuu 
  5. ya Rufaa
Chagua Jibu


14. Kazi kubwa zilizokuwa zikifanywa na wazee wa ukoo katika jamii nyingi za Kiafrika zilikuwa . . . . . . . . .

  1. kulinda mila na desturi, kufanya matambiko na kukata mashauri;
  2. kupanga mahari, kukata mashauri, na kupigana katika vita;
  3. kulinda mila na desturi, kutembelea koo zingine na kupigana katika vita;
  4. kulisha mifugo, kukata mashauri na kufanya tambiko;
  5. kulima mashamba, kuwinda na kulisha mifugo.
Chagua Jibu


13 Wajibu wa Serikali katika kusimamia biashara ya ndani ni

  1. kupanga bei za bidhaa mbalimbali
  2. kukagua bidhaa madukani
  3. kugawa maeneo ya kufanyia biashara
  4. kutunga sheria za kusimamia biashara 
  5. kutoa mitaji kwa wafanyabiashara
Chagua Jibu


16. Maana halisi ya familia ni ipi?

  1. Mama, baba, watoto na jamaa wote katika ukoo
  2. Mama, baba na watoto
  3. Mama, baba, watoto na rafiki wa karibu wote
  4. Baba, mama, watoto, bibi na babu
  5. Baba, mama, watoto, bibi, babu, shangazi na mjomba
Chagua Jibu


17. Teknolojia ya kale ya umwagiliaji maji mashambani barani Afrika ilihusisha .

  1. shadoof 
  2. mifereji
  3. mnyama aina ya punda 
  4. ngamia 
  5. mabomba
Chagua Jibu


18. Soko kuu la biashara ya watumwa Zanzibar lilifungwa mwaka .

  1. 1840
  2. 1900 
  3. 1890 
  4. 1884 
  5. 1873
Chagua Jibu


19. Sehemu zenye mvua kidogo sana, joto jingi mchana na baridi sana usiku ni za hali ipi ya nchi?

  1. Kimediteranean
  2. Kisavanna
  3. Jangwa 
  4. Kiikweta
  5. Kitropiki
Chagua Jibu


20. Uchumi wa nchi ya Libya unategemea zaidi:

  1. tende 
  2. dhahabu 
  3. almasi 
  4. mafuta 
  5. gesi
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  




Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256