SEHEMU A: SARUFI Katika swali la 1 — 20, weka kivuli katika herufl ya jibu lililo sahihi katika karatasi yako ya kujibia
1. Neno lipi ni tofauti na maneno mengine kati ya haya
2. Mto Ruvu umefurika mwaka huu. Katika sentensi hii, maneno "mwaka huu" ni ya aina gani?
3."Mimi sitakuja" Sentensi hii iko katika kauli gani?
4.Mama mdogo amepika ugali mwingi". Maneno gani ni vivumishia sentensi hii?
5. "Wakulima wamehamisha mizinga ya nyuki kutoka mashambani mwao. "Umoja wa sentensi hii ni upi?
6. "Mwajuma amemwibia Mwanahamisi kalamu yake". Katika sentensi hii. "Mwajuma ni nani?
7. Kinyume cha neno "duwaa" ni kipi?
8. "Uvumilivu ulimfanya Pendo apate zawadi. "Uvumilivu ni aina gani ya neno?
9. Yupi kati ya wafuatao ni lazima awe mwanaume?
IO. "Walimu watafundisha masomo yao vizuri". Sentensi hii ipo katika wakati gani?
11. "Wanafunzi wenzake walimnyanyapaa. Neno walimnyanyapaa lina maana gani kati ya hizi zifuatazo?
12.
Neno nimerudi lipo katika nafsi ipi?
13. Kiwanda hutoa ajira kwa wananchi "kiwanda" ni aina gani ya neno?
14. Mashine nyingi hupatikana" kiwandani" ni aina gani ya neno
15.Kisawe cha neno "ndovu" ni kipi kati ya maneno yafuatayo?
16, "Mlima meru unafuka moshi" Ukanusha wa sentensi hii ni upi?
17. Panga maneno yafuatayo kwa kuanzia na neno ambalo katika familia hiyo linaonesha aliyetangulia kuzaliwa hadi wa mwisho kuzaliwa: Baba, kitukuu, babu, kilembwe,
mjukuu, kilembwekeza.
18. Kisawe cha neno ”kinyinginya” ni kipi katika maneno yafuatayo?
19.Kisawe cha neno ”mviringo” ni kipi?
20.Mtu anayechonga vinyago anaitwaje?akaokota,
21. Alipomwona Yule Chui, Juma akapiga moyo konde na kuanza kumshambulia kwa mpini wa jembe. Maana ya msemo kupiga moyo konde ni ipi?
22. Nimeugua kwa kipindi kirefu sana, lakini sasa ni wa afya. Neno lipi linakamilisha sentensi hii?
23. Wakikua mama yao huwatupa mbali kwa kishindo.Jibula kitendawili hiki ni lipi?
24.Kati ya methali zifuatazo ni ipi haitoi msisitizo wa kufanya juhudi katika jambo?
26 sihimili kishindo"kifungu kipi cha maneno kinakamilisha methali hii?
27. "Asiyeuliza" maneno yapi
yanakamilisha methali hii kwa usahihi
28." Gari langu halitumii mafuta jibu la kitendawili hiki ni lipi?
29. "Anatengeneza mchuzi mtamu sana lakini hapiki jikoni" kitendawili hiki jibu lake ni lipi?
30. "Ukiona vyaelea vimeundwa" methali hii ina maana gani?
UFAHAMU.
Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu maswali 31-40 kwa kuweka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi katika karatasi yako ya kujibia.
Jua lilikuwa linaunguza mithili ya moto. Hapakuwa na nyasi wala miti iliyokuwa na majani ya rangi ya kijani.Kila uoto ulikuwa wa rangi ya kahawia kavu! Aidha kupata tone la maji ya kunywa ilikuwa ndoto kwani mito na visima vyote vilikauka kau.Baada kuhangaika kwa njaa na kiu, ndipo wanyama waliamua waitishe mkutano ili wajadili hatua ya kuchukua. Makundi • ya wanyama wa aina mbalimbali walikutana chini ya mbuyu. Swala, nyani, mbawa na tembo wote walikuwepo.
"Kama mjuavyo mimi ndimi mfalme wa wanyama wote.Niungurumapo hapana achezae kwa hiyo bila shaka mtakubali kuwa mimi ndiye mwenyekiti wa mkutano huu."alitangaza simba.Wanyama wote walitazamana na kutikisa vichwa kwa ishara ya kuafiki. Kisha alisimama na kusema "Mheshimiwa mwenyekiú, jana nilisikia mlindimo toka upande wa magharibi. Hivyo ninashauri sote tuhame na kuelekea upande huo ili tuokoe maisha yetu kwani huko kuna dalili ya mvua."Wanyama wote waliunga mkono hoja hiyo,isipokuwa kobe ambaye alisema, "mheshimiwa mwenyekiti, endapo kweli tumeazimia kuhama, sisi akina kobe tunaomba mtubebe kwani kasi yetu ya kutembea ni ndogo mno."
Baada ya kila mnyama kutoa rai yake ,Mwenyekiti alisimama na kusema, "Nimesikia yote mliyosema, kabla ya kuanza kuhama nakutuma wewe ngombe upeleke ujumbe wetu kwa binadamu ili waache kuharibu mazingira, kwani hicho ndicho kiini cha matatizo yanayotusibu.Wewe ni kiungo baina yetu na binadamu." ngombe alikubali.
Baada ya kufika ujumbe ule, binadamu alijibu kuwa alikwishaelewa tatizo Ia mazingira na tayari alikuwa na mpango kabambe wa kuchinja mifugo yote ili kutekeleza ushauri wa wataalamu wa mazingira wa kuiokoa dunia na janga Ia jangwa. Kusikia hivyo ngombe alichanja mbuga kuelekea kwa wanyama wengine.
31. Kwa mujibu wa habari uliyo soma, mkutano wa wanyama ulifanyika wapi?
32. Mwenyekiti wa mkutano wa wanyama alikuwa nani?
33. Hali ya kukauka kwa mito,visima nyasi na miti kunakutokana na ukosefu wa mvua inaitwaje?
34. Jina lingine Ia mnyama aliye washauri wanyama wote kuhamia upande ambako kulikuwa na dalili ya mvua ni lipi kati ya
yafuatayo.
35.Katika habari uliyo soma sababu iliyomfanya kobe kutoafiki moja kwa moja hoja ya kuhama ni ipi?
36. kwa mujibu wa habari hii ,uharibifu mkubwa wa mazingira hufanywa na nani?
37. Neno lipi kati ya yafuatayo lina maana sawa na neno janga?
38. Kifungu cha maneno "alichanjambuga"kinamaana gani?
39. Binadamu alikusudia kuchinja wanyama wa aina gani
40. Kichwa cha somo uliyosoma kingefaa kiwe kipi?
41. Kituo cha shairi hili ni kipi?
42. Katika shairi hili vina vya kati na mwisho ni vipi?
43. Shairi hili lina mizani ngapi?
44. Shairi hili lina beti ngapi?
45. Neno "kuangua" kama lilivyotumika katika shairi hili lina maana ipi?
46. Neno "Mizozo" kama lilivyotumika katika shairi hili lina maana gani?
SEHEMU E:
UTUNGAJI
Panga sentensi nne (4) zifuatazo ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi
A, B, C na D.
47. Zizi hilo limegawanywa katika sehemu mbili
Chagua Jibu48. Baba yangu anafuga ngombe, mbuzi na kondoo.
49. Nje ya nyumba yetu kuna zizi kubwa.
Chagua Jibu50. Sehemu moja ni ya ngombe na nyingine ni ya mbuzi na kondoo.
Chagua Jibu