STD VII KISWAHILI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2016

Katika swali la 1 — 20, weka kivuli katika herufiyajibu lililo sahihi.

1.  "Wachache wamehamia Boro". Katika sentensi hiyo "Wachache" limetumika kama aina gani ya neno?

 1. Kivumishi
 2. Kielezi     
 3. Kiwakilishi
 4. Kitenzi 
 5.  Kiunganishi
Chagua Jibu


2.         Alimwita nyumbani kwake kwa dhamira ya kumpa karo ya shule. Neno "dhamira" lina maana ipi?

 1. Dhamana 
 2. Madhumuni
 3. Thumuni  
 4.  Dhumuni 
 5. Dhamini
Chagua Jibu


3.         Kauli ipi inaonesha hali ya kutendewa?

 1. Tumechimba visima vyetu. 
 2.  Tunachimbisha kisima chetu. 
 3. Tulichimbiwa kisima chetu. 
 4. Tumechimba kisima chetu.
 5. Tutachimba kisima chetu.
Chagua Jibu


4.         Katika vifungu vya maneno vifuatavyo, kifungu kipi kipo katika kauli taarifa?

 1. Unataka kuondoka lini? 
 2. Alitaka kukuuliza unaondoka lini. 
 3. Ni lini wewe utaondoka? 
 4.  Aliuliza, utaondoka lini?
 5. Aliuliza kuwa ataondoka lini?
Chagua Jibu


5.         Mwenyekiti hakufika mkutanoni leo. Kitenzi "hakufika" kipo katika hali gani?

 1. Mazoea  
 2. Kuendelea  
 3. Timilifu
 4. Matarajio 
 5.  Kanushi
Chagua Jibu


6.         "Wapiganaji wetu walipowasili visiwa vya Comoro walishangiliwa kwa   Ni neno lipi linakamilisha sentensi hiyo?

 1. hofu   
 2.  mzaha  
 3. shangwe
 4. mayowe
 5. dhihaka
Chagua Jibu


7.         Mawaziri wote wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa. Neno "wote" limetumika kama aina gani ya neno?

 1. Nomino  
 2.  Kiwakilishi 
 3. Kitenzi
 4. Kivumishi   
 5. Kiunganishi
Chagua Jibu


8.         Babu amemhamishia yule mbuguma kwenye zizi kubwa. Neno "mbuguma" lina maana

 1. Mbuzi dume anayelima  
 2. Ngombe dume anayelima
 3. Kondoo jike aliyezaa 
 4. BWombe jike anayelima
 5. Ngombe jike anayeendelea kuzaa
Chagua Jibu


9.         "Chama kimeteka nyara sera ya serikali." Wingi wa sentensi hiyo ni upi?

 1. Vyama vimeteka nyara masera ya serikali. 
 2.  Vyama vimeteka nyara sera ya serikali. 
 3. Vyama vimeteka nyara serikali.
 4.  Vyama vimeteka sera za serikali.
 5. Vyama vimeteka nyara visera vya serikali.
Chagua Jibu


10.     Nyumba ya ndege huitwaje?

 1. Mzinga 
 2. Kiota 
 3. Korongo
 4.  Banda 
 5.  Shimo
Chagua Jibu


11.     "Wanafunzi hodari watapewa zawadi". Sentensi hiyo ipo katika wakati gani?

 1. Ujao 
 2.  Timilifu 
 3. Uliopita   
 4.  Mazoea 
 5. Uliopo
Chagua Jibu


12.     Maji yamejaa "pomoni" Neno "pomoni" ni aina ipi ya neno?

 1. Nomino  
 2.  Kiwakilishi   
 3. Kielezi
 4. Kihisishi  
 5. Kivumishi
Chagua Jibu


13.     Kati ya maneno "Sherehi, Sherehe, Shamrashamra, Hafla, Tafrija" neno lipi halihusiani na mengine?

 1. Sherehi  
 2. Sherehe 
 3.  Shamrashamra 
 4. Hafia 
 5. Tafrija
Chagua Jibu


14.     Neno lipi kati ya maneno yafuatayo lina maana sawa na "thubutu"?

 1. Ufidhuli  
 2. Ujasiri 
 3. Umahiri 
 4. Ukakamavu 
 5. Utashi
Chagua Jibu


15."Kuzua kizaazaa" ni msemo wenye maana gani?

 1. Ushabiki   
 2. Upendeleo
 3. Malumbano
 4. Masikitiko  
 5. Majungu 
Chagua Jibu


16. Mtu anayetafuta kujua jambo fulani kwa kuuliza maswali huitwaje?

 1. Mawazo
 2. Mbeya
 3. Mfitini
 4. Mdadisi
 5. Mjuaji 
Chagua Jibu


17. Neno Mchakato lina maana ya mfululizo wa................

 1. Mawazo
 2. maoni
 3. shughuli
 4. safari
 5. fikra
Chagua Jibu


18. Neno lipi kati ya yafuatayo lina maana sawa na neno shehena

 1. roda
 2. furushi
 3. mizigo
 4. bidhaa
 5. robota
Chagua Jibu


19. Mtu aliyezaliwa na wazazi wa rangi mbalimbali huitwaje?

 1. Albino
 2. Mkimbizi
 3. mhamiaji
 4. chotara
 5. mzawa
Chagua Jibu


20.      Baada ya miaka minne Kalunde ... ...... mafunzo yake ya udaktari. Ni neno lipi linakamilisha sentensi hiyo?

 1. aliitimu 
 2.  alihimidi
 3.  aliitimisha
 4. alihitimu 
 5.  halihitimu
Chagua Jibu


Katika swali la 21 — 30, weka kivuli katika herufiyajibu lililo sahihi.

21.      Methali isemayo, "Katika msafara wa mamba na kenge wamo" iko sawa na methali ipi kati ya zifuatazo?

 1. Akutukanaye hakuchagulii tusi. 
 2.  Kila kiboko na kivuko chake.
 3. Amulikaye nyoka huanzia miguuni mwake. 
 4. Tajiri na mali yake maskini na mwanawe. 
 5.  Hakuna masiki yasiyo na mbu.
Chagua Jibu


22.      Diengi anapenda kuwarairai watu. "l<urairai watu" ni msemo wenye maana ipi?

 1. Kuwasihi watu ili apate cheo anachokipenda
 2. Kusema na watu kwa maneno mazuri
 3. Kusema na watu ili uwape chochote
 4.  Kusema kwa watu kwajili ya kuwatapeli
 5. Kuwabembeleza watu ili wasimpangie kazi
Chagua Jibu


23.      Msemo "kubarizi" maana yake ni kukusanyika kwa ajili ya .

 1. Sherehe 
 2.  mkutano 
 3.  mazungumzo ya kawaida 
 4. burudani 
 5.  chakula cha pamoja
Chagua Jibu


24.      Methali isemayo "Kila mtoto na koja lake" ina maana gani? 

 1. Kila binadamu ana mapungufu yake.
 2.  Kila mtoto ana matatizo yake.  
 3. Kila mtoto ana mapungufu yake. 
 4.  Kila mtoto ana wazazi wake.  
 5. Kila binadamu ana tabia yake.
Chagua Jibu


25.      Nahau isemayo "kuvishwa kilemba cha ukoka" ina maana gani?

 1. Kupewa sifa unazostahili 
 2.  Kupewa sifa mbaya 
 3.  Kupewa sifa nyingi 
 4.  Kupewa sifa chache
 5. Kupewa sifa usizostahili
Chagua Jibu


26.      Tegua kitendawili kifuatacho: "Nyumbani kwangu kuna jini mnywa maji."

 1. Kikombe 
 2.  Kata 
 3. Kinywa 
 4.  Kibatari  
 5. Mtungi
Chagua Jibu


27.      "Wakulima wa kahawa wa wilaya ya Mbinga wamepewa heko kwa kuzalisha kahawa bora".

Msemo "wamepewa heko" hufanana na msemo gani kati ya ifuatayo?

 1.  kupewa tunzo 
 2. kupewa pongezi   
 3.  kupewa heri 
 4.  kupewa zawadi  
 5. kupewa hawala
Chagua Jibu


28.      Methali isemayo, "Mwenda pole hajikwai" inafanana na methali ipi kati ya zifuatazo?

 1. Haba na haba hujaza kibaba. 
 2.  Fuata nyuki ule asali. 
 3.  Mchumia juani hulia kivulini.
 4. Awali ni awali hakuna awali mbovu.
 5. Baada ya dhiki faraja.
Chagua Jibu


29.     Methali ipi kati ya hizi zifuatazo haifanani na zingine?

 1. Mtegemea nundu haachi kunona. 
 2. Nazi haishindani na jiwe. 
 3. Mlinzi wa kisima hafi kiu. 
 4.  Mchumia juani hulia kivulini.
 5. Baada ya dhiki faraja.
Chagua Jibu


30.     Mwamba ngoma    .. Kifungu kipi cha maneno kinakamilisha methali hiyo?

 1. hualika watu wengi   
 2. hufanya maandalizi mengi
 3. huimba nyimbo nyingi
 4. ngozi huvutia kwake
 5.  hucheza na jamaa zake
Chagua Jibu


SEHEMU C

UFAHAMU

Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu maswali 31 — 40 kwa kuweka kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi.

Mpendwa kaka Yohana,

Natumani hujambo na unaendelea vizuri na masomo yako. Nimefurahi kusikia kwamba umechaguliwa kujiunga na masomo ya Sekondari. Ndugu wote wanakupongeza na kukutakia kila la kheri katika masomo yako. Soma kwa bidii zaidi kwani elimu ni bahari na haina mwisho.

Baba na mama walifurahi sana baada ya kupata taarifa za kuchaguliwa kwako kwa-njia ya simu kutoka kwa shangazi. Wanamshukuru sana shangazi kwa kukuwezesha na misaada yake mingi kwako ya hali na mali. Baba ameahidi kumtembelea shangazi tarehe ishirini mwezi wa kumi na moja mwaka huu ili kumkabidhi zawadi aliyomwandalia kutokana na ukarimu wake kwako.

Rafiki yako Juma alifika hapa nyumbani akasema kwamba ataniletea picha nikutumie. Hamisi amekuandalia zawadi ambayo atakukabidhi utakapokuja nyumbani wakati wa likizo yako ya mwisho wa muhula. Tunu amesema atakutembelea, lakini uwe mwangalifu unapoongea naye asije akakuchezea shere. Siku hizi ni msanii.

Nisalimie sana shangazi na wanae wote, yaani Amani, Anasitazia na Asia. Sisi sote tunakutakia kila la kheri katika masomo yako.

Akupendaye daima, Mdogo wako, Tumaini.

31.     Neno "ukarimu” lina maana sawa na lipi kati ya maneno yafuatayo?

 1. Fadhila  
 2. Fadhaa  
 3.  Fedheha 
 4.  Faraja 
 5. Fanaka
Chagua Jibu


32.     Mwandishi wa barua hii ametumia msemo "kuchezea shere” Msemo huo una maana ipi?

 1. Fujo   
 2.  Mzaha
 3. Sheria
 4. Shindano
 5. Wivu
Chagua Jibu


33.     Ushindi wa Yohana na mafanikio yake katika masomo umetokana na nini? 

 1. Kuwahi shuleni asubuhi na mapema
 2. Kuhimizwa na wazazi wake
 3. Msukumo kutoka kwa shangazi
 4. Masomo ya ziada kutoka kwa walimu wake  
 5. Kuiga maendeleo aliyonayo Tunu
Chagua Jibu


34.     Wazazi na ndugu zake Yohana walipata taarifa ya kufaulu kwake kwa njia gani?

 1. Kwa njia ya barua
 2. Kwa njia ya simu
 3.  Kutoka kwa walimu
 4. Kupitia matangazo
 5. Vyombo vya habari
Chagua Jibu


35.     Uhusiano wa Yohana na watoto wa shangazi yake ni upi?

 1. Binamu zake 
 2.  Wapwa zake 
 3. Wadogo zake 
 4. Wakubwa zake 
 5.  Ami zake
Chagua Jibu


36.     Katika barua hii mwandishi anafananisha elimu na nini?

 1. Ufunguo wa maisha   
 2. Bahari isiyo na mwisho
 3. Njia ndefu 
 4.  Njia ya maisha 
 5. Marefu yasiyo na ncha
Chagua Jibu


37.     Unafikiri ni sababu ipi ilimfanya baba yake Yohana kumwandalia dada yake zawadi?

 1. Kumpongeza kwa kumsaidia Yohana. 
 2.  Kwa kuwa hajaonana naye muda mrefu. 
 3. Dada yake hupenda sana kupata zawadi.
 4. Alitaka asimchukie Yohana.
 5.  Alipata ushauri kutoka kwa mkewe.
Chagua Jibu


38.     Lengo la Tumaini kumwandikia kaka yake barua lilikuwa lipi?

 1. Kumshauri 
 2.  Kumshawishi 
 3. kumzawadia
 4.  Kumsalimia 
 5.  Kumpongeza
Chagua Jibu


39. Kifungu hiki cha habari ni aina gani ya barua?

 1. Barua ys kirafiki
 2. barua ya wito
 3. barua rasmi
 4. barua ya shukrani
 5. barua ya pongezi
Chagua Jibu


40. Ni methali ipi inatoa fundisho kutokana na ushindi wa Yohana?

 1. Asiyejua maana haambiwi maana. 
 2. Mtumaini cha ndugu hufa masikini. 
 3. Mtoto wa nyoka ni nyoka. 
 4.  Mchuma janga hula na wa kwao.
 5. Mcheza kwao hutuzwa.
Chagua Jibu


   

Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali 41 - 46 kwa kuweka kivuli katika herufiya jibu.

Nimekwisha peleleza, karibu kila mahali,

Mule wanamotangaza, matangazo lugha mbili, Juu kuwa Kingereza, Chini kuwa Kiswahili, Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza.

Kitangazwe Kingereza, baada ya Kiswahili

Hivi tutapotimiza, lugha itakuwa ghali,

Hivi mnavyofanyiza, sana mnaidhalili,

Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza

Serikali bembeleza, tafakari tafadhali,

Jambo hili kueleza, kwa zingine serikali Kiswahili kutangaza, kuwa Chini twakidhili Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza.

Tuache kukipumbaza, kwa andiko au kauli, Kwa nyuma kukisogeza, kukipa kisulisuli,

Lazima kuyafukuza, yawezayo kikatili,

Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza

Na wenyewe kujikaza, kwa bidii za kimwili kiswahili kutukuza, tukivalie bangili,

Ngomani kutumbuiza, waume na wanawali Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza.

41. Katika shairi hilo mstari wa pili katika ubeti wa pili una mizani mingapi?

 1. Tano
 2. mbili
 3. kumi na sita
 4. nane
 5. thelathini na tatu
Chagua Jibu


42. Katika ubeti wa nne, vina ni vipi?

 1. Za na li
 2. La na li
 3. La na ya
 4. Ju na za
 5. Tu na li
Chagua Jibu


43.      Kituo ni kipi katika shairi hili?

 1. Nimekwisha peleleza, karibu kila mahali
 2.  Kitangazwe Kingereza, badala ya Kiswahili 
 3. Serikali bembeleza, tafakari tafadhali
 4. Tuache kukipumbaza, kwa andiko na kauli
 5. Juu kiwe Kiswahili, Chini kiwe Kingereza
Chagua Jibu


44.      Shairi hili linahimiza kuhusu nini?

 1. Kudumisha na kuendeleza mila
 2. Kudumisha na kuendeleza jadi zetu
 3. Kudumisha lugha ya Kingereza
 4.  Kudumisha na kuendeleza Kiswahili 
 5.  Kudumisha na kuendeleza lugha
Chagua Jibu


45.      Ujumbe unaopatokana katika shairi hili unafanana na methali ipi?

 1. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. 
 2.  Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
 3. Mkono usioweza kuukata ubusu. 
 4.  Ukitaka cha uvunguni sharti uiname.
 5. Ukipata chungu kipya usitupe cha zamani.
Chagua Jibu


46.      Kutokana na shairi ulilosoma neno "kutukuza” lina maana ipi?

 1. Shutumu 
 2.  Laumu
 3. Heshimu 
 4. Fadhaisha
 5. Kasirisha
Chagua Jibu


SEHEMU E

UTUNGAJI

Umepewa habari yenye sentensi nne(4) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo katika swali 47 — 50. Zipange sentensi hizo ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C, na D. Weka kivuli katika herufi yajibu sahihi.

47. Hivyo mazoezi huleta afya, kwa hiyo ni muhimu kwa kila mmoja wetu kufanya mazoezi.

Chagua Jibu


48. Mtu asiyefanya mazoezi anapata maradhi ya moyo; atanenepa kupita kiasi, kwa hiyo atapata ugonjwa wa kuumwa mgongo na magoti.

Chagua Jibu


49. Mazoezi ya viungo yanachangamsha misuli ya mwili, mifupa na ubongo.

Chagua Jibu


50. Lakini mtu anayefanya mazoezi anaepuka magonjwa ya moyo na msukumo wa damu.

Chagua Jibu


Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

Bofya Hapa Kupakua
App Ya Learning Hub Tanzania
GO TO NECTA EXAMS