2014: KISWAHILI
SEHEMU A: SARUFI
Katika swali la 1 - 20, andika herufi ya jibu lililo sahihi katika karatasi yaka ya kujibia.
1. "Yeye amefaulu mitihani yake vizuri." katika sentensi hii neno lipi limetumika kama kielezi?
2. "Dada ameandika barua kwa baba." Sentensi hii iko katika kauli gani?
3. Katika sentensi zifuatazo ipi ni sahihi?
4. Neno lipi ni tofauti na maneno mengine kati ya maneno yafuatayo?
5. "Tunu angalisoma ..... mtihani wake." Neno lipi linakamilisha sentensi hiyo kwa usahihi?
6. "Mnyama mkali amekamatwa leo." Katika sentensi hii neno "mkali" limetumika kama aina gani ya neno?
7. "juma amefika na hatacheza mpira" Kitenzi "hatacheza" kipo katika half gani?
8. "Alisema hanywi dawa tena." Kauli halisi ya sentensi hii ni ipi?
9. "Walikotoka kuna mvua." Sentensi hii ipo katika wakati gani?
10. "Hamisa na Hanifa ni mapacha walioungana." Katika sentensi hii neno "na" limetumikakama aina gani ya neno?
11. Panya huyu anakula unga wangu. Wingi wa sentensi hii ni upi?
12. Siku ile ya maandamano kulikuwa na...........wa pikipiki. Ni neno lipi linakamilisha sentensi hii?
13. "Mpira wetu umechanika vibaya" Sentensi hii ipo katika kauli gani?
14. Neno mchwa lina silabi ngapi?
15. "Hapa ...............alipoishi chifu Mirambo." Ni neno lipi linakamilisha sentensi hii kwa usahihi?
16. Atakapomnyonyoa yule hata ......... kwenye moto. Kitenzi kipi kinakamilisha tungo hii?
17. "Kitabu changu ni cheusi, chako ni cheupe." Neno "chako" ni aina gani ya neno?
18. Yeye ni kijana mdogo. Neno "yeye" lipo katika nafsi gani?
19. Kinyume cha kitenzi "paa" ni kipi?
20. Mwalimu J. K. Nyerere ni mwasisi wa chama cha TANU. Neno "ni" limetumika kama ainaipi ya kitenzi?
SEHEMU B
LUGHA YA KIFASIHI
Katika swali la 21- 30 chagua herufi ya jibu lililo sahihi kisha andika kwenye karatasiya majibu.
21. "Ulichokitupa pwani ................" Kifungu kipi cha maneno hukamilisha methali hiyo?
22. "Mkiweza..............katika kazi hiyo, hatimaye mtafanikiwa." Nahau ipi inakamilisha tungo hii?
23. Methali isemayo, "Ngoma ikilia sana hupasuka" hulingana kimaana na methali ipi kati yahizi zifuatazo?
24. "Ukukuu wa kamba si upya wa ukambaa." Methali hii ina maana sawa na methali ipi?
25. "Hamadi kibindoni." Kati ya tafsiri zifuatazo ni ipi inayotoa maana sahihi ya msemo huo?
26. "Samaki mkunje angali mbichi." Methali ipi kati ya zifuatazo ina maana sawa na hii?
27. Methali isemayo. "Chanda chema huvikwa pete" inatoa funzo gani?
28. "Ukitaka kuruka agana na nyonga" Methali hii inaasa kuhusu jambo gani?
29. Methali isemayo. "Mpofuka ukongweni.................. " hukamilishwa na kifungu kipi cha maneno kati ya hivi vifuatavyo?
30. Nikikutana na adui yangu nanyongea. Jibu la kitendawili hiki ni lipi?
SEHEMU C
UFAHAMU
Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu maswali 31 - 40 kwa kuandika herufi ya jibu lililo sahihi katika karatasi ya majibu.
Mabadiliko ya hali ya hewa yamekuwa makubwa kiasi cha kutisha. Zamani mababu wetu walitabiri mvua wao wenyewe pasi na kuwa na vyombo vya kisasa. Suala linalozungumziwa sana siku hizi ni mabadiliko ya hali ya hewa na athari zake kwa jamii nzima. Kila mtu ana wasiwasi kuhusu mvua ambazo huchukua muda mrefu bila kunyesha.
Ukosefu wa mvua ambao mwishowe huleta ukame na njaa umechangiwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za binadamu ambazo zinaongezeka kwa haraka siku hadi siku. Shughuli hizo mbalimbali ambazo kwa upande mmoja zimeonekana kama za kimaendeleo ni kuongezeka kwa matumizi ya maliasili. Mifano mbalimbali ambayo inaonesha matumizi hayo ni pamoja na ujenzi wa nyumba nyingi zaidi, kupata nishati ya kutosha kwa ajili ya kupikia na upatikanaji wa mbao na magogo kwa wingi kwa matumizi ya ndani na hata ya nje ya nchi.
Hata hivyo, iii maendeleo hayo yawe na mwelekeo chanya jamii inalazimika kupanda miti kwa wingi iii kukidhi mahitaji hayo. Aidha ni vema kuzingatia kuwa ukataji miti ni chanzo kikubwa cha mito na vijito kuwa na maji haba au kukauka kabisa.
MASWALI
31. Kichwa cha habari kinachofaa habari hii ni kipi?
32. Tatizo kubwa zaidi ambalo husababishwa na ukosefu wa mvua kwa muda mrefu ni lipi kati ya haya yafuatayo?
33. Mwandishi anayaelezea mabadiliko ya hali ya hewa kuwa yalikuwa.
34. Neno "haba" kama lilivyotumika katika kifungu cha habari lina maana gani?
35. Dalili mojawapo kubwa ya maendeleo ni ipi kama ilivyoelezwa katika kifungu cha habari?
36. Mabadiliko ya hali ya hewa yana maana sawa na ipi kati ya hizi zifuatazo?
37. Kisawe cha neno "mwishowe" kama kilivyotumika katika habari hii ni kipi?
38. Watu wa zamani waliweza kutabiri mvua kwa kutumia:
39. Mito na vijito huwa na maji haba au kukauka kutokana na nini?
40. Nishati ni neno lenye maana sawa na lipi?
SEHEMU D
USHAIRI
Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswali 41 - 46 kwa kuandika herufi ya jibulililosahihi kwenye karatasi ya majibu.
Msituni nikakuta, nyuki wamo mzingani,Kwa juhudi wanakita, mara nje mara ndani,Husuda wameikata, hata hawasengenyani,
Nyuki ni wadudu duni, wanashinda kwa umoja,
Mchwa nao nikaona, wamejenga maskani,Wafanya bidii sana, uvivu hawatamani, Wao husaidiana, tena hawadanganyani,
Mchwa wadudu wa chini, wanaishi kwa umoja.
Nalojeshi la siafu, hutandawaa njiani, Laenda bila ya hofu, maana lajiamini,Silaha zao dhaifu, menu tena hawaoni,Wa kuwatania nani, kwani wanao umoja
Nao chungu wachukuzi, nyamarima wa njiani,Maskani wapagazi, mizi,go yao kichwani,Ingawa si wachokozi, wakali ukiwahini,
Katu hawafarakani, wanadumu kwa umoja
41. Mwandishi wa shairi hili anasisitiza kuhusu nini?
42. Shairi hili lina mizani mingapi kwa kila mstari?
43. Neno "husuda" kama lilivyotumika katika shairi hili lina maana gani?
44. Kisawe cha neno "Tadi" ni kipi?
45. Kina cha kati katika ubeti wa pili ni kipi?
46. Kichwa cha habari kinachofaa kwa shairi hill ni kipi?
SEHEMU E
UTUNGAJI
Umepewa habari yenye sentensi nne (4) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo katikaswali la 47 - 50. Zipange sentensi hizo iii ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A,B,C na D. Andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi ya kujibia.
47. Kwa njia hii, vizazi vilivyofuata viliweza kujua uvumbuzi uliofanywa kabla yao.
Chagua Jibu48. Jambo muhimu lililofanywa na mababu zetu ni kuhifadhi kumbukumbu za uvumbuzi waokwa kuchora kila kifaa walichovumbua.
Chagua Jibu49. Kwa kutumia vizazi vilivyotangulia nasi pia tunaweza kuvumbua vitu vipya ambavyovitaweza kutuletea maendeleo zaidi.
50. Hivyo maisha ya binadamu yakaendelea kuwa bora na yenye manufaa kila siku.
Chagua Jibu