STD VII KISWAHILI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2013

11. Sentensi ipi kati ya hizi ipo katika hali timilifu?

 1.  Mheshimiwa Rais anahutubia mkutano
 2.  Mheshimiwa Rais alihutubia mkutano
 3.  Mheshimiwa Rais atahutubia mkutamo 
 4. Mheshimiwa Rais amehutubua mkutano
 5.  Mheshimiwa Rais alikuwa anahutubia mkutano.
Chagua Jibu


12. Neno lipi ni tofauti na maneno mengine kati ya yafuatayo?

 1.  Maji 
 2.  Maziwa 
 3.  Soda 
 4.  Juisi 
 5.  Samli
Chagua Jibu


13. "Kitabu chako ni kizuri, ukienda dukani nami uninunulie ... ......” Ni kifungu kipi cha maneno hukamilisha sentensi hiyo?

 1.  kama hivyo 
 2.  kama hiko 
 3.  kama icho
 4.  mfano wa iko 
 5.  kama hicho
Chagua Jibu


14. Tunda huachwa mpaka likauke." Setensi hiyo ikiwa katika hali ya ukanushi itakuwa ipi kati ya zifuatazo?
 1.  Tunda haliachwi mpaka likauke
 2.  Tunda haliachi mpaka likauke
 3.  Tunda halikuachwa mpaka likauke
 4.  Tunda halitaachwa mpaka likauke
 5.  Tunda halijaachwa mpaka likauke
Chagua Jibu


15. Mkutano haukufanyika kwa sababu mwenyekiti na katibu hawakufika. Kifungu kipi cha maneno kati ya vifuatavyo kinasadifu sentensi hiyo?

 1.  Mkutano uliairisha 
 2.  Mkutano uliahirishwa
 3.  Mkutano ulihairishwa 
 4.  Mkutano uliharishwa 
 5.  Mkutano ulihairisha
Chagua Jibu


16. Mlinzi wa mlangoni huitwaje?

 1.  Boharia 
 2. Baharia 
 3. Bawaba
 4.  Banati 
 5.  Bawabu
Chagua Jibu


17. Joshua yuko jikoni anapaa samaki. Neno "anapaa” kama lilivyotumika katika sentensi hii lina maana ipi?

 1.  Kuwapaka samaki chumvi 
 2.  Kuondoa magamba ya samaki 
 3.  Kuondoa mifupa katika samaki 
 4.  Kukausha samaki kwa moto 
 5. .Kuwakata samaki vipande vipande.
Chagua Jibu


18. "Mtoto wa ngombe anaitwa ndama, watoto wa kuku, bata, kanga wanaitwa vifaranga, kimatu ni mtoto wa nani?

 1. Nzige
 2. Nyuki
 3. Inzi
 4. Kipepeo
 5. Buibi
Chagua Jibu


19. Kisawe cha neno ”eupe” ni kipi?

 1. Chokaa
 2. Angavu
 3. Theluji
 4. Ukungu
 5. Angaza
Chagua Jibu


20. Siku ya nne baada ya leo huitwaje?

 1. Mtondo
 2. Mtondo kutwa
 3. Mtondogoo
 4. Kesho kutwa
 5. Mtondogoo kutwa
Chagua Jibu


SEHEMU C

UFAHAMU

Soma kifungu cha habari na kishajibu maswaliyanayofuata:

Maji ni moja kati ya vitu vitatu muhimu sana vinavyotuwezesha kuishi. Vitu vingine ni hewa na chakula. Hewa ndiyo yenye umuhimu wa kwanza, ikifuatiwa na chakula. Kusingelikuwa na maji maisha ya binadamu na ya viumbe wengine yasingewezekana. Kila mtu anaelewa umuhimu wa maji katika maisha. Maji yanatawala maisha kwa kiasi kikubwa sana. Baadhi ya viumbe kama vile samaki, mamba, kasa, konokono, nyangumi na wengineo maskani yao ni majini, hivyo maji yakikosekana viumbe hao huweza kuaga dunia.

Binadamu anatumia maji kwa shughuli mbalimbali. Shughuli hizo ni pamoja na kupikia, kufulia, kusafishia vyombo, kuoga na kunywa. Katika sehemu nyingi za nchi yetu watu hutumia maji kwa kumwagilia bustani za mboga, maua na miti. Katika maeneo yenye mito mikubwa na maziwa maji yake hutumika kwa kumwagilia mashamba kama yale ya mpunga na mahindi. Kilimo cha umwagiliaji kinafaa kwa sababu mkulima anakuwa na uhakika wa kuvuna.

Maji ya mvua huwezesha watu kulima na kupanda mazao ya chakula na ya biashara. Hivyo zipo sehemu ambazo wakulima hulima kilimo cha umwagiliaji lakini sehemu kubwa ya wakulima hutegemea kilimo cha mvua.

Kwa ujumla maji yawe ya mvua au yanayotokana na mito au maziwa yana umuhimu mkubwa mno kwa binadamu kama walivyosema wahenga maji ni uhai, hivyo inashauriwa kwamba ni muhimu kwa kila mtu kunyvva maji safi na salama ili kulinda siha zetu.

MASWALI

31.Vitu vitatu muhimu vinavyomwezesha binadamu kuishi ni vipi?

 1. Hewa, chakula na nyumba 
 2. Hewa, maji ma chakula
 3.  Maji ushauri na hewa 
 4. Maji, hewa na mvua
 5. Chakula, mvua na hewa
Chagua Jibu


32.Wakulima wengi kama ilivyoelezwa katika habari hii hulima kilimo kinachotegemea nini?

 1.  Mito 
 2.  Umwagiliaji 
 3. Mvua
 4. Mabwawa 
 5.  Maziwa
Chagua Jibu


33. Kiumbe yupi kati ya wafuatao halandani na wenzie?

 1.  Kima 
 2.  Mamba
 3. Nyangumi
 4. Kasa
 5. Samaki
Chagua Jibu


34.Kilimo cha umwagiliaji kina sifa gani kubwa?

 1.  Uvunaji upo dhahiri 
 2. Kinatumia maji ya maziwa makubwa
 3. Kinatumia maji yaliyohifadhiwa 
 4. Mazao hayapati magonjwa 
 5. Kinalimika majira yoyote
Chagua Jibu


35.Neno "siha" kama lilivyotumika katika kifungu hiki cha habari lina maana gani?

 1. Afya njeme
 2. Sifa njema
 3. Maisha mema
 4. Tabia njema
 5. Kinywa safi
Chagua Jibu


36. "Kuaga dunia" ni msemo wenye maana gani?

 1. Kuzirai 
 2. Kuzimu
 3. Kulala fofofo
 4. Kufariki 
 5. Kufia mbali
Chagua Jibu


37. Ni kwanini mtunzi wa habari hii anashauri watu kunywa maji safi na salama?

 1.  Ili kuondokana na kiu 
 2.  Ili kulinda vinywa vyetu
 3.  Ili kuburudisha mwili 
 4.  Ili kuondokana na kichocho 
 5.  Ili kulinda afya zetu
Chagua Jibu


38.Neno "maskani" kama lilivyotumika katika kifungu cha habari lina maana gani?

 1.  Nyumba 
 2.  Makao 
 3.  Maisha 
 4.  Mahitaji 
 5.  Shughuli
Chagua Jibu


39.Kichwa cha habari kinachofaa kwa kifungu hiki ni kipi?

 1.  Hewa ni muhimu 
 2.  Maji ni uhai
 3.  Maji salama 
 4.  Hewa na chakula
 5.  Siha bora
Chagua Jibu


39.Kichwa cha habari kinachofaa kwa kifungu hiki ni kipi?

 1.  Hewa ni muhimu 
 2.  Maji ni uhai
 3.  Maji salama 
 4.  Hewa na chakula
 5.  Siha bora
Chagua Jibu


  BOFYA HAPA KUPAKUA APP YA LEANING HUB
ILI KUFUNGUA MTIHANI MZIMA  
Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256