STD VII KISWAHILI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2011

KISWAHILI 2011

SEHEMU A

SARUFI

Katika swali la (1 - 20) andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi yako ya kujibia.

1. Neno "jenga" likinyumbulishwa katika kauli ya kutendeka litakuwa neno lipi?

 1. Jengwa
 2. Jengea
 3. Jengeka
 4. Jengesha
 5. Jengewa
Chagua Jibu


2. Neno "wamewalisha" linadokeza hali gani ya kitenzi?

 1. Kuendelea
 2. Mazoea
 3. Masharti
 4. Matarajio
 5. Timilisho
Chagua Jibu


3. "Yeye hupenda sana kusoma Kiswahili". Katika sentensi hii ni neno lipi limetumika kama kiwakilishi?

 1. Hupenda
 2. Kiswahili
 3. Sana
 4. Yeye
 5. Kusoma
Chagua Jibu


4. Katika sentensi zifuatazo ni ipi ipo katika hali ya mazoea

 1. Roda alisoma gazeti la Mtanzania.
 2. Roda atasoma gazeti la Mtanzania.
 3. Roda husoma gazeti la Mtanzania.
 4. Roda amesoma gazeti la Mtanzania.
 5. Roda anasoma gazeti la Mtanzania.
Chagua Jibu


3. Sara alimwambia Heri kwamba hakusafiri bali alikuwepo pale pale. Kauli halisi itakuwa ipi?

 1. Sara alimwambia Heri, "Sikusafiri nipo hapa hapa".
 2. Sara alimwambia Heri, "Sitasafiri nipo hapa hapa".
 3. Sara alimwambia Heri, "Sisafirinipo hapa hapa".
 4. Sara alimwambia Heri, "Hajasafiri yupo hapa hapa".
 5. Sara alimwambia Heri, "hakusafiri yupo hapa hapa".
Chagua Jibu


6. "Alikuwa anajibu kihuni". Neno "kihuni" limetumika kama aina gani ya neno?

 1. Kielezi
 2. Kiwakilishi
 3. Kivumishi
 4. Kitenzi
 5. Kihisishi
Chagua Jibu


7. "Mtu anayetaka msaada wa aina nitampa". Neno linalofaa kukamilisha tungo hiyo ni lipi?

 1. wowote
 2. yoyote
 3. yeyote
 4. vyovyote
 5. lolote
Chagua Jibu


8. "Wanafunzi wanaendelea kusoma Kiswahili ingawa hawana mwalimu". Neno "wanaendelea" limetumika kama aina gani ya kitenzi?

 1. Kikuu
 2. Kishirikishi
 3. Jina
 4. Kisaidizi
 5. Kitegemezi
Chagua Jibu


9. Mahali pale panatisha. Neno "pale" ni aina gani ya neno

 1. Kivumishi
 2. Kiwakilishi
 3. Kiunganishi
 4. kihisishi
 5. Kielezi
Chagua Jibu


10. "Kinyonga anatembea". Ukanushi wa sentensi hii ni upi?

 1. Kinyonga hakitembei
 2. Kinyonga hakutembea
 3. Kinyonga hajatembea
 4. Kinyonga haternbei
 5. Kinyonga hatatembea
Chagua Jibu


11. "Mama anapika lakini baba abapangamawe". Neno lakini limetumika kama aina gani ya neno?

 1. Kivumishi
 2. Kiwakilishi
 3. Kielezi
 4. Kitenzi
 5. Kiunganishi
Chagua Jibu


12. "Kiburi si maungwana". Neno "si" limetumika kama aina gani ya kitenzi

 1. Kikuu
 2. Kishirikishi
 3. Jina
 4. Kisaidizi
 5. Kitegemezi
Chagua Jibu


13. "Baba yangu ni mwenyekiti wa lopp". Neno "mwenyekiti ni nomino ya aina gani?

 1. Dhahania
 2. Kawaida
 3. Pekee
 4. Jumla
 5. Mguso
Chagua Jibu


14. Wingi wa neno chuma ni upi kati ya maneno yafuatayo?

 1. Machuma
 2. Mavyuma
 3. Vichuma
 4. Vyuma
 5. Michuma
Chagua Jibu


15. "Wanafunzi walitumiana salamu". Sentensi hii ipo katika kauli gani?

 1. Kutendeana
 2. Kutendana
 3. Kutendewa
 4. Kutendea
 5. Kutendeka
Chagua Jibu


16. Kinyume cha neno "elea" ni kipi?

 1. [buka
 2. Ibukia
 3. Zamia
 4. Zama
 5. Zamisha
Chagua Jibu


17. "Huyu mwanangu mpendwa". Neno lipi ni sahihi iii kukamilisha sentensi hiyo.

 1. ndiye
 2. ndio
 3. ndiyo
 4. ndie
 5. ndiwe
Chagua Jibu


18. "Mbwa ameonekana". Neno lipi ni sahihi kukamilisha tungo hiyo?

 1. aliyepotea
 2. aliopotea
 3. alipotea
 4. amepotea
 5. alivyopotea
Chagua Jibu


19. Hall ya kuwa na fedha au mall nyingi huitwaje?

 1. Ukachero
 2. Ukapa
 3. Ukata
 4. Ubahili
 5. Ukwasi
Chagua Jibu


20. Ni sentensi ipi inawakilisha kauli ya kutendwa?

 1. Nyumba imeharibiwa na mvua.
 2. Nyumba imeharibishwa na mvua.
 3. Nyumba imeharibika na mvua.
 4. Nyumba imeharibika kwa mvua.
 5. Nyumba imeharibiwa kwa mvua.
Chagua Jibu


SEHEMU B

LUGHA VA KIFASIH1

21. "Uzi mwembamba unafunga dume kubwa". Kitendawili hiki kina maana gani?

 1. Mawingu
 2. Usingizi
 3. Ndoto
 4. Mvua
 5. Ugonjwa
Chagua Jibu


22. "Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha". Methali ambayo ina uhusiano na hii ni ipi kati ya hizi zifuatazo?

 1. Ufalme kama mvua, hupiga na kupita.
 2. Ujana ni tembo la nazi, halikawii kupita.
 3. Usiache mbachao, kwa mswala upitao.
 4. Usishindane na kari, kari ni mja wa Mungu.
 5. Ukiwa na lako, usitizame la mwenzio.
Chagua Jibu


23. "Watoto wangu wote wamevaa hirizi nyeupe" Kitendawili hiki kina maana gani

 1. Mwewe
 2. Kunguru
 3. Njiwa
 4. Kasuku
 5. Chiriku
Chagua Jibu


24. Hali ya kumfanya mtu atii kila analoambiwa ina maana sawa na nahau ipi kati ya zifuatazo?

 1. Kutia akili
 2. Mkalia kitako
 3. Kumweka kiganjani
 4. Kumkalia kichwani
 5. Kumkalia kooni
Chagua Jibu


25. Ni muhimu kwa kila mtu kuwa mwangalifu kwa wanaojitangazia kutibu kisukari. Ni usemi upi kati ya ifuatayo ina maana sawa na "kuwa mwangalifu"?

 1. Kuwa macho
 2. Kuwa hima
 3. Kuwa mweledi
 4. Kuwa hadhiri
 5. Kuwa shupavu
Chagua Jibu


26. "Mambo mema na mabaya hayafungamani", kifungu hiki cha maneno kinatoa maana ya methali ipi kati ya zifuatazo?

 1. Gongo la mbuyu si la mvule.
 2. Liwapo lako ni jema, la mwenzako ni baya.
 3. Lila na fila havitengamani.
 4. Lako ni lako, likikufika lina mwenzako.
 5. Padogo pako si pakubwa pa mwenzako.
Chagua Jibu


27. Tegua kitendawili kisemacho "Gari langu halitumii mafuta ya waarabu"

 1. Nywele
 2. Ngozi
 3. Miguu
 4. Mikono
 5. Macho
Chagua Jibu


28. "Umejuaje kuwa mimi ni mgeni hapa?" methali ipi kati ya zifuatazo inawajibu swali hilo?

 1. Jogoo wa shamba hawiki mjini.
 2. Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba.
 3. Mtoto wa nyoka ni nyoka.
 4. Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
 5. Aibu ya maiti aijuaye mwosha.
Chagua Jibu


29. Juma alipumzika chini ya mti, alipoulizwa anafanya nini pale alijibu kuwa, "Navinjari to mwalimu". Jibu sahihi alilotakiwa kutoa ni lipi?

 1. Napiga domo.
 2. Napunga upepo.
 3. Nimepigwa na butwaa.
 4. Napiga kambi.
 5. Nazunguka mbuyu.
Chagua Jibu


30. "Babu kafa kaniachia pete". Kitendawili hiki kina maana gani?

 1. Mjusi
 2. Tandu
 3. Nyoka
 4. Konokono
 5. Jongoo
Chagua Jibu


SEHEMU C

UFAHAMU

Soma kwa makini habari ifuatayo kisha jibu maswali 31 - 40 kwa kuchagua herufi ya jibu lililo sahihi na kuandika katika karatasiyakoya kujibia.

Umewahi kusikia viumbe wanaoitwa dinozo? Hawa ni wanyama ambao walikuwepo duniani zaidi ya miaka milioni 65 iliyopita. Wanasayansi wamegundua mabaki ya mafuvu na mifupa yao ardhini. Wanasayansi wamechunguza sana sababu za kutokomea kwa dinozo. Mpaka leo hii haijapatikana sababu rasmi ya tukio hilo. Hata hivyo, bado uchunguzi unaendelea kufanywa katika kutafuta sababu za kupotea kwa wanyama hao.

Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani zenye wanyama wa aina nyingi. Watalii wengi kutoka kila pembe ya dunia huja kuwaangalia wanyama hawa. Hali hiyo huongeza pato Ia taifa.

Aidha, vitendo mbalimbali vinahatarisha usalama wa viumbe hao; kwa mfano makazi ya wanyama yanaharibiwa kwa kuchomwa misitu na kukata miti ovyo. Hali hii husababisha misitu kubaki vichaka tu, hivyo wanyama hukosa makazi na mwishowe hupotea. Vile vile binadamu huwinda wanyama kama tembo kwa ajili ya pembe zao.

Sasa umefika wakati kwa kila mmoja wetu kukemea vitendo hivi. Wanyama na mimea ni urithi wa taifa letu. Ni fahari iliyoje kwetu kuwa navyo. Tusipokuwa waangalifu wanyama hao na mimea adimu kama mianzi vitatoweka kabisa. Vizazi vijavyo vitabaki kusimuliwa kama tunavyosikia kuhusu dinozo.

MASWALI

31. Dinozo ni wanyama wenye sifa ipi kati ya hizi zifuatazo?

 1. Waliotoweka duniani
 2. Wanaovutia watalii
 3. Walioishi duniani miaka mingi
 4. Wanaoishi duniani
 5. Wenye mifupa na Mafuvu
Chagua Jibu


32. Kwa kuzingatia habari uliyosoma mambo mawili yanayoathiri ustawi wa wanyama ni yepi?

 1. Uoto wa maji
 2. Mvua na utalii
 3. Uwindaji na ujangili
 4. Vichaka na uwindaji
Chagua Jibu


33. Sababu kubwa ya watu kuwinda na kuwaua ndovu ni ipi?

 1. Kupata kitoweo
 2. Kupata pembe
 3. Kupata ngozi
 4. Kupata mkonga
 5. Kupata malighafi
Chagua Jibu


34. Kutokana na habari hii ni sababu ipi inayowafanya watalii kuja Tanzania?

 1. Kuwinda wanyama
 2. Kuongeza pato Ia taifa
 3. Kupata malighafi
 4. Kupata pembe
 5. Kuwaangalia wanyama
Chagua Jibu


35. Tanzania hupata faida gani kubwa kutokana na sekta ya utalii?

 1. Kupata fedha za kigeni
 2. Kupata wageni mbalimbali
 3. Kuuza bidhaa nyingi
 4. Kuongeza pato la taifa
 5. Kujulikana nchi za nje
Chagua Jibu


36. Mwandishi anatoa wito gani kwa jamii kuhusiana na usalama wa viumbe hai?

 1. Kukemea vitendo vinavyohatarisha usalama wa viumbe hai
 2. Kulinda mianzi iliyopo iii isitoweke kabisa
 3. Kuhudumia na kuvitunza viumbe hai kwa umakini zaidi
 4. Kuthamini na kutambua kuwa viumbe hai ni urithi wa taifa
 5. Kulinda na kutunza tembo wallop iii wasitoweke
Chagua Jibu


37. Athari zipi zinapatikana kutokana na kuchoma misitu?

 1. Kuwepo kwa jua kali na uoto wa asili
 2. Kuwepo kwa vichaka na ukame wa kutisha
 3. Makazi na malisho ya wanyama kuharibika
 4. Mimea na mianzi kutoweka kwa haraka
 5. Tembo na mimea kutoweka kwa kasi
Chagua Jibu


38. Mwandishi anadai kuwa fahari ya taifa letu bi kuwa na vitu gani?

 1. Mimea na mianzi
 2. Maji na misitu
 3. Wanyama na mimea
 4. Mimea na maji
 5. Wanyama na utalii
Chagua Jibu


39. Kuna tofauti gani kati ya msitu na kichaka?

 1. Msitu ni nyasi na kichaka ni miti.
 2. Msitu ni miti na kichaka ni nyasi.
 3. Misitu ni miti mirefu na kichaka ni miti midogo.
 4. Misitu ni miti mikubwa na kichaka ni miti mifupi.
 5. Misitu ni nyasi ndefu na kichaka ni nyasi fupi.
Chagua Jibu


40. Kwa ujumla habari hii inahusu nini?

 1. Viumbe hai
 2. Manzingira
 3. Dinozo
 4. Usalama wa viumbe
 5. Tembo
Chagua Jibu


SEHEMU D

USHAIRI

Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali 41 - 46 kwa kuandika herufi ya jibu lililo sahihi katika karatasi ya kujibia.

Kasimama kizimbani, popo anatetemeka,

Kuitwa mahakamani, popo kujibu shitaka,

Atakiwa abaini, kwa ulimi kutamka,

Ajitetee bayana, ni mnyama au ndege.


Hakimu nashukuru, shitaka kunisomea,

Sina jadi na kunguru, ila na Pundamilia,

Mimi ni mnyama huru, amini ninakwambia,

Tukidaiwa ushuru, kwa wanyama nalipia.


Ni kweli popo napaa, na mabawa nimepata,

Lakini mimi nazaa, hilo halina utata

Kuwa ndege nakataa, sina undugu na bata

Nakataa katakata, mimi si ndege nasema.


Hakimu nathibitisha, kwa moyo wangu thabiti,

Nazaa na kunyonyesha, vipi niwe msaliti,

Wale wanaopotosha, niwaonyeshe matiti,

Hakimu simama kati, nipatie kaki.

MASWALI

41. Popo anakataa kuwa si ndege kwa sababu gani?

 1. Anataga
 2. Ana mabawa
 3. Anazaa
 4. Anapaa
 5. Ana manyoya
Chagua Jibu


42. Katika ubeti wa pill popo anasema "sina jadi na kunguru", usemi "sina jadi" una maana gani?

 1. Hana uhusiano
 2. Hana ushirikiano
 3. Hana nasaba
 4. Hana urafiki
 5. Hana muafaka
Chagua Jibu


43. Popo alitakiwa kujitetea bayana. Usemi "Kujitetea bayana" una maana gani?

 1. Kujiteta waziwazi
 2. Kujitetea hadharani
 3. Kujitetea kwa hadhari
 4. Kujitetea kwa kificho
 5. Kujitetea kwa hadhira
Chagua Jibu


44. Mstari wa mwisho katika kila ubeti wa shairi hill huitwaje?

 1. Kituo vina
 2. Kituo kimalio
 3. Kituo bahari
 4. Kituo kitoshelevu
 5. Kituo kikamilifu
Chagua Jibu


45. "Kitendo cha kuzaa na kunyonyesha hufanywa na viumbe ambao ni " Neno linalokamilisha sentensi hiyo ni lipi?

 1. Bata
 2. Wadudu
 3. Samaki
 4. Kunguru
 5. Wanyama
Chagua Jibu


46. Kichwa cha shairi hill chafaa kiwe kipi?

 1. Hakimu
 2. Popo
 3. Popo mahakamani
 4. Hakimu mahakamani
 5. Wanyama
Chagua Jibu


SEHEMU E

UTUNGAJI

Umepewa habari yenye sentensi nne (4) zilizoaandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo katika swali la 47 - 50. Zipange sentensi hizo iii ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C, na D.

47. Alipomaliza kusema hayo Mzee komba akauliza, "Tupande miti wakati inaota kwa uwezo wa Mungu?"

Chagua Jibu


48. Mkutano ulipomalizika kila mtu alirejea nyumbani kwake akiwa na dhamira ya kupanda miti.

Chagua Jibu


49. Bwana miti akasema "Yapasa kupanda miti kwa sababu matumizi yake yameongezeka sana siku hizi".

Chagua Jibu


50. "Tusipopanda miti mipya tutaishiwa miti kabisa". Bwana miti alijibu.

Chagua Jibu


Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

Bofya Hapa Kupakua
App Ya Learning Hub Tanzania
GO TO NECTA EXAMS