STD VII KISWAHILI ONLINE SELF NECTA TEST FOR YEAR 2010

KISWAHILI 2010

SEHEMU A

SARUFI

Katika swali la 1-5 andika herufiya jibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.

1. "Ukitaka cha mvunguni inama". Hii ni sentensi ya aina gani?

 1. ambatano 
 2. changamano 
 3. shurutia 
 4. nyofu 
 5. sahili
Chagua Jibu


2. Katika neno "hatutakamilisha", kiambishi kinachoonesha nafsi ni kipi?

 1. -ka- 
 2. -ta- 
 3. -ha- 
 4. -sha- 
 5. -tu-
Chagua Jibu


3. "Kampeni ya upandaji miti wilayani Kishapu ilifanikiwa sana na wananchi." Sentensi hii ipo katika kauli gani?

 1. kutendwa
 2. kutendewa
 3. kutenda
 4. kutendana
 5. kutendeka
Chagua Jibu


4. Kisawe cha neno "beseni" ni kipi?

 1. debe 
 2. karai
 3. ndoo 
 4. pipa
 5. chupa
Chagua Jibu


5. Wingi wa sentensi isemayo, "Ubao umetumika" ni ipi?

 1. Mbao itatumika
 2. mbao umetumika
 3. mbao zitatumika 
 4. mbao imetumika
 5. mbao zimetumika
Chagua Jibu


6. Katika sentensi ifuatayo, ni neno lipi limetumika kama kiwakilishi? "Huu ni wa maziwa."

 1. ziwa 
 2. huu 
 3. Ni 
 4. Wa 
 5. Maziwa
Chagua Jibu


7. Ubegete ameshinda kondeni akiamia ndege. Kielezi katika sentensi hii ni kipi?

 1. Kondeni 
 2. Akiamia 
 3. Ameshinda 
 4. Ndege 
 5. Kondeni akiamia
Chagua Jibu


8. Mwalimu alikuwa anatunga mtihani. N eno "anatunga" limetumika kama aina ipi ya kitenzi?

 1. Kishirikishi 
 2. Kitenzi Kikuu 
 3. Kisaidizi 
 4. Kitenzi kipungufu 
 5. Kitenzi jina
Chagua Jibu


9. Alfajiri na mapema tuliondoka ukumbini. Mzizi katika neno lililopigiwa mstari ni upi?

 1. -ondo-
 2. -iondoka
 3. -ondok-
 4. ondoka
 5. -iondok-
Chagua Jibu


10. Kinyume cha neno "Tandika" ni kipi?

 1. Tandaza
 2. Tandua
 3. Tanzua
 4. Tanzia
 5. Tandiko
Chagua Jibu


11. Umoja wa sentensi "Machungwa mabichi yana ladha ya uchachu” ni...

 1. Chungwa bichi lina ladha ya uchachu
 2. Chungwa bichi lina ladha yake
 3. Chungwa bichi lina kaladha ka uchachu
 4. Chungwa bichi lina ladha kali
 5. Vichungwa vibichi vina ladha ya uchachu.
Chagua Jibu


12. Fundi atengenezaye herein, pete an mikufu huitwaje?

 1. Sofara 
 2. Mfuaji 
 3. Sonara 
 4. Mnajimu 
 5. Fundi
Chagua Jibu


13. "Zena amemnunulia mwanae kizibao” limetumika kwa maana ipi?

 1. Suti yenye mikono mirefu
 2. Jaketi kubwa
 3. Shati la mikono mifupi
 4. Koti fupi lisilo na mikono
 5. Koti lenye mikono mirefu
Chagua Jibu


14. Neno "kindumbwendumbwe” lina silabi ngapi?

 1. Saba
 2. Nne 
 3. Tano
 4. Mbili 
 5. Tisa
Chagua Jibu


15. Watalii wengi hufika Tanzania ili .mlima Kilimanjaro. Ni neno lipi linalokosekana kukamilisha sentensi hiyo?

 1. kuzuru 
 2. kuthuru 
 3. kudhuru
 4. kufuru 
 5. kudhulu
Chagua Jibu


SEHEMU B

MSAMIATI

Katika swali la 16 - 25 andika herufiyajibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.

16. Baada ya mshenga kutoa wageni waliondoka na kurudi makwao. Chagua neno sahihi kati ya maneno yafuatayo ili ukamilishe sentensi hiyo.

 1. fahari
 2. posa
 3. barua
 4. mahali
 5. mali
Chagua Jibu


17. Neno "msimu” lina maana gani?

 1. Majira
 2. Muda
 3. Mvua
 4. Kipupwe
 5. Masika
Chagua Jibu


18. Yule bwana amelima kwa bidii na amevuna . . mwingi sana.

 1. mipunga
 2. mchele
 3. mpunga 
 4. wali 
 5. michele
Chagua Jibu


19. Kisawe cha neno ”hitimisho” ni kipi?

 1. Hitima
 2. Tamati
 3. Mwanzo
 4. Katikati 
 5. Tanguliza
Chagua Jibu


20. Katika vifungu vya maneno vifuatavyo ni kifungu kipi chenye maneno yanayoshabihiana?

 1. Kuku, chiriku, njiwa, mwewe.
 2. Almasi, dhahabu, kitok, chui
 3. Maembe, mapera, shaba, matopetope
 4. Shati, kiwiko, ukucha, kidole
 5. Tembo, nyani, kondoo, mtende
Chagua Jibu


21. Kinyume cha neno "shaibu" ni kipi?

 1. Barubaru 
 2. Ngariba 
 3. Banati
 4. Ajuza 
 5. Kijana
Chagua Jibu


22. Ng'ombe dume aliyeachishwa ambaye hutumika kwa kufanya kazi kama vile kuvuta mkokoteni au plau huitwaje?

 1. Fahali 
 2. Maksai 
 3. Dume
 4. Beberu 
 5. Fahari
Chagua Jibu


23. "Mfanyabiashara alipatwa na nuksi kubwa baada ya bidhaa zake kuungua moto". Ni neno lipi linalandana na neno "nuksi" kati ya yafuatayo?

 1. Ghasia
 2. Balaa 
 3. Dhahama
 4. Mkasa  
 5. Tashititi
Chagua Jibu


24. Kisawe cha neno "runinga" ni kipi?

 1. Mninga 
 2. Ninga
 3. Televisheni
 4.  Tovuti
 5. Kinakilishi
Chagua Jibu


25. Kinyume cha neno "kunyanyapaa" ni kipi?

 1. Kutunza 
 2. Kusifia
 3. Kuhifadhi
 4. Kubembeleza 
 5. Kustahi
Chagua JibuSEHEMU C

METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI

Katika swali la 26 - 30 Andika herufiyajibu lililo sahihi katika karatasi yakoya kujibia.

26. Wanafunzi wa darasa la tano wanafanya kazi zote bega kwa bega. Neno lililopigiwa mstari lina maana gani?

 1. Kuwasilishana 
 2. Kuegemeana 
 3. Kutegeana
 4. Kushirikiana 
 5. Mabega mawili
Chagua Jibu


27. Kifungu cha maneno kisemacho, "Anayefanya juhudi katika masomo au jambo Iolote hufanikiwa" kinashabihiana na methali ipi kati ya zifuatazo?

 1. Nazi haishindani na jiwe
 2. Mwenye nguvu mpishe
 3. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu
 4. Ukitaja nyoka shika fimbo mkononi
 5. Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti
Chagua Jibu


28. Baada ya John kupanda cheo, alimtilia Sara kitumbua chake mchanga. Maana ya msemo "kutilia kitumbua mchanga" ni upi?

 1. Kumsifia mtu asiye na sifa
 2. Kumharibia mtu sifa zake au mambo yake mazuri
 3. Kumharibia jina wakati hana jina
 4. Kumtangaza maovu wakati hana
 5. Kumtangazia mtu sifa asizokuwa nazo
Chagua Jibu


29. Wanafunzi wa darasa Ia saba wamesoma kwa makini hadi wamehitimu masomo yao. Ni methali ipi kati ya zifuatazo inasadifu sentensi hiyo?

 1. Ngoja ngoja yaumiza matumbo 
 2. Kuuliza si ujinga
 3. Ahadi ni deni 
 4. Mwenda pole hajikwai
 5. Mvumilivu hula mbivu
Chagua Jibu


30. "Mwana wa ndugu kirungu, mjukuu mwanangwa." Methali ambayo haifanani na mehtali hii kati ya hizi zifuatazo ni ipi?

 1. Ndugu chungu jirani mkungu
 2. Damu nzito kuliko maji
 3. Ndugu bora kuliko rafiki
 4. Adui aangukapo mnyanyue
 5. Mwana kidonda mjukuu kovu
Chagua Jibu


31. Kifungu kipi cha maneno kinakamilisha methali ifuatayo? "Ikiwa kilemba kimelowa..."

 1. kanzu nayo imeloa 
 2. na mkuti uhali gani?
 3. uhali gani mkuti? 
 4. na mkuti umeloa
 5. mwili wote umeloa
Chagua Jibu


32. Aisatu hujulikana sana kwa "majina ya lakabu". "Majina ya lakabu" maana yake ni ipi?

 1. Majina ya kujipa au ya watu wengine
 2. Majina ya kupanga au kuchekesha
 3. Majina ya kujipa au ya ukoo
 4. Jina Ia kupanga au kupewa na watu 
 5. Majina ya wazazi na ya ukoo
Chagua Jibu


33. Binetuu anawachukua wazazi wake. "Kuwachukua" lina maana gani?

 1. Huwatunza wazazi wake
 2. Huwakaribisha wazazi wake
 3. Huwakidhi haja za maisha 
 4. Huwabeba kila wachokapo 
 5. Huwagomboa wazazi wake.
Chagua Jibu


34. Mama Chakupewa alipotokeza tu sebuleni, wapangaji wenzake wote yyaliangua-kichelo Msemo uliopigiwa mstari una maana gani?

 1. Kucheka hadi mtu anatokwa na machozi
 2. Kucheka sana 
 3. Kucheka sana kwa sauti
 4. Kucheka bila sababu 
 5. Kucheka kwa muda mrefu
Chagua Jibu


35. Kasanga alitegewa kitendawili na babu yake na akakitegua kwa kusema "Mwangwi". Kitendawili hicho ni kipi?

 1. Huko ng'o na kule ng'o
 2. Jinamizi laniita lakini silioni
 3. Huku pi na kule pi
 4. Kaa hapa nikae pale tumfinye mchawi
 5. Kila niendako ananifuata
Chagua Jibu


SEHEMU D

UFAHAMU

Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kashajibu swali la 36 - 45 kwa kuandika herufi yajibu lililo sahihi katika karatasiyakoya kujibia.

Hapo kale watu walikuwa wakila vyakula vibichi. Kadri miaka ilivyokwenda mbele watu igundua matumizi ya moto kwa njia ya kupekecha vijiti. Ugunduzi huu uliwasaidia kuanza kuchoma nyama na kupika vyakula.

Kadri miaka ilivyoendelea ndivyo maendeleo yalivyopatikana. Baada ya watu kupata moto kwa kupekecha vijiti, waligundua pia njia nyingine. Njia iliyotumiwa na watu wengi ni ile ya kutumia viberiti. Hivyo waliweza kutumia majiko ya aina mbalimbali kama jiko la mafuta ya taa, jiko la mkaa, jiko la gesi na waliweza kupika kwa kutumia kuni.

Kazi ya kupika ilikuwa rahisi baada ya ugunduzi huu, walianza kula vyakula vya mchanganyiko. Walitambua kwamba vyakula vinavyopikwa kwa mchanganyiko kama mseto na vinginevyo vina manufaa makubwa. Vyakula hivi hujulikana kama mlo kamili. MIO kamili huimarisha siha ya mlaji.

Matumizi ya viberiti hayakuishia katika kuwasha majiko. Viberiti hadi leo vinatumika kuwashia kandili, karabai, vibatari na mishumaa ili kuweza kupata mwanga katika nyumba zetu. Tunatumia viberiti kupata moto tunaoutumia kuchoma mabiwi na takataka nyingine ili kuondoa uchafu katika mazingira yetu.

Moto pia huweza kupatikana kwa njia ya umeme ambao aghalabu hutumika katika sehemu za miji. Ugunduzi wa umeme umesaidia katika shughuli za upishi. Huwawezesha akina mama kupika vyakula kwa kutumia majiko ya umeme. Hupika vyakula vingi kwa urahisi na kwa haraka zaidi. Hali hii imeleta uwezekano wa kupika vyakula vya mchanganyiko yaani mlo kamili. Vyakula hivi huwa na mchanganyiko wote, yaani vyakula vinavyotia nguvu na joto mwilini, vyakula vya kulinda mwili na kujenga mwili. Watu walao mlo kamili kwa nadra huwa goigoi.

Moto pia huweza kupatikana kwa kutumia lensi, kwani lensi ikielekezwa kwenye mwanga wa jua kwa muda mrefu basi karatasi itakayowekwa chini yake hushika moto.

Faida za moto ni nyingi. Hutupa mwanga wakati wa usiku, hutumika katika kuendesha mashine na mitambo mbalimbali. Kama moto usingegunduliwa, maisha ya watu yangekuwa duni.

Aidha, moto una madhara mbalimbali usipotumika vema. Madhara haya hutukumbusha kwamba "uzuri wa mkakasi, ndani kipande cha mti". Athari zake ni kama kuunguza majengo na mitambo, majengo yanapoungua wakati mwingine husababisha maafa ya watu kuungulia ndani ya majengo na mali zao.

Kuepuka madhara na hasara zitokanazo na moto hatuna budi kuwa waangalifu. Tuweke viberiti, mishumaa na taa mbali na watoto; tuunganishe nyaya za umeme kwa kutumia wataalamu, warina asali kufuata njia za kisasa kwa kutumia mavazi ya kitaalamu, kulima kwa kuepuka kuchoma mapori na mashamba. Tusipochukua tahadhari hiyo tutajuta, kwani "Hamna! Hamna! Ndimo mliwamo".

MASWALI

36. Kichwa cha habari hapo juu ni kipi?

 1. Moto 
 2. Umeme
 3. Viberiti 
 4. Taa 
 5. Mkaa
Chagua Jibu


37. Neno "Mseto" lina maana sawa na kifungu kipi cha maneno kati ya vifuatavyo?

 1. Mchanganyiko wa matunda na mboga
 2. Mlo kamili wenye virutubisho
 3. Mlo uliotengenezwa kwa mboga mbichi
 4. Kachumbari na wali
 5. Mchanganyiko wa mchele na choroko
Chagua Jibu


38. "Watu walao mlo kamili kwa nadra huwa goigoi". Sentensi hii ina maana ipi?

 1. Watu walao mlo kamili maridhawa huonekana goigoi 
 2. Watu walao mlo kamili maridhawa huonekana wanyonge
 3. Watu walao mlo kamili mara chache huonekana dhaifu na wanyonge.
 4. Watu walao mlo kamili mara nyingi huonekana wenyenguvu 
 5. Watu walao mlo kamili mara moja moja huwa si wasikivu
Chagua Jibu


39. "Hamna! Hamna! Ndimo mliwamo". Methali hii ina maana gani?

 1. Ni hatari kutegemea mashine na mitambo kwani huleta madhara
 2. Ni vizuri kuchukua tahadhari kabla ya janga kutokea
 3. Tusizoee kusema hamna! Hamna! Mara kwa mara ili tusipate madhara.
 4. Heri kusubiri tatizo ili upambane nalo kuliko kubashiri mambo yajayo 
 5. Ni vizuri kuepuka madhara ya moto
Chagua Jibu


40. Neno "siha" kama lilivyotumika katika kifungu cha habari Ilina maana gani?

 1. Afya njema 
 2. Sifa njema
 3. Maisha mema
 4. Tabia njema 
 5. Bora afya
Chagua Jibu


41. Kwanini watu wa kale walikula vyakula vibichi?

 1. Moto ulikuwa na nguvu hafifu
 2. Moto ulitumika kidogo
 3. Moto ulikuwa haujagunduliwa
 4. moto ulikolea polepole
 5. Hawakuwa na vyakula vya kupika
Chagua Jibu


42. MIO kamili huwa na mchanganyiko wa vyakula vyenye virutubisho mwilini. Vyakula hivyo ni vipi?

 1. Vyakula vya kutia nguvu na joto, vya kujenga na kulinda mwili.
 2. Vyakula vya protini, vinavyojenga mwili na hamirojo
 3. Vyakula vinavyotia nguvu, joto na vitamin na vinavyolinda mwili
 4. Vyakula vinavyojenga miili, hamirojo, vinavyotia nguvu na joto mwilini
 5. Vyakula vinavyolinda mwili, hamirojo na vitamin.
Chagua Jibu


43. Moto una faida nyingi katika maisha ya kila siku. Taja faida tatu za moto.

 1. kupasulia miamba, kuota na mwanga
 2. kupikia, kuota na kuzuia umande
 3. kupikia, mwanga na kuteketeza uchafu
 4. mwanga, kupasulia miamba na kulimia mashambani
 5. kupasulia miamba, kupikia na kujenga
Chagua Jibu


44. kama ilivyotumiwa na mwandishi, methali inayosema "Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti" ina maana gani?

 1. Hakuana marefu yasiyokuwa na ncha
 2. Kitu kizuri lazima kitengenezwe kwa kutumia kipande cha mti
 3. Usipochukua tahadhari mapema utapata mdhara
 4. Kila chenye mwanzo kina mwisho
 5. Hakuna kizuri kisicho na kasoro
Chagua Jibu


45. Madhara yasababishwayo na moto kama yalivyoelezwa kwenye kifungu cha habari ni yapi?

 1. Huleta uharibifu wa rasilimali na mazingira
 2. Huteketeza nyumba na mitambo na husababisha vifo
 3. Huleta maafa kwa viumbe hai, mali na huharibu mazingira
 4. Husababisha vifo, uharibifu wa migodi na mabwawa ya samaki
 5. Huteketeza nyumba, mali na huharibu miundo mbinu.
Chagua Jibu


SEHEMU E

UTUNGAJI

Umepewa insha yenye sentesi tano (5) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo. Zipange sentensi hizi ili ziwe na mtiririko wenye mantiki kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E ili ujibu maswali 46 - 50.

46. Ili mpate kuyajua ni lazima mjifunze kwa bidii na maarifa muweze kufaulu mitihani yenu.

Chagua Jibu


47. Ninyi ni vijana wadogo bado wenye matumaini ya kupata maendeleo katika maisha yenu ya baadaye.

Chagua Jibu


48. Endeleeni kusoma na kujifunza kwa bidii kwani Elimu ni bahari, haina mwisho.

Chagua Jibu


49. Elimu ndiyo itakayoweza kuwafungulia njia za kupata maendeleo hayo, katika safari hii ya kuelimika zaidi.

Chagua Jibu


50. Katika safari hiyo ya kuelimika zaidi, utagundua kuwa yapo mambo mengi muhimu ambayo hamyajui.

Chagua Jibu


Try Another Test | 
Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

Bofya Hapa Kupakua
App Ya Learning Hub Tanzania
GO TO NECTA EXAMS