STD IV SAYANSI ONLINE NECTA EXAM REVIEW FOR YEAR 2010

SAYANSI 2010

SEHEMU A

Chagua jibu sahihi na andika herufi yake kwenye karatasiya kujibia

1. Mahitaji ya msingi ya binadamu ni . . . . . . . . . .

  1. makazi, mavazi na matibabu
  2. matibatu, mavazi na chakula
  3. chakula, mavazi na makazi
Chagua Jibu


2. Dalili za malaria ni pamoja na . . . . . . . . . .

  1. kutetemeka na kuvimba miguu
  2. kutapika na kupungua uzito
  3. mwili kuchoka na homa kali
Chagua Jibu


3. Kundi lipi la chakula huimarisha meno na mifupa yetu kati ya makundi yafuatayo . . . . . . . . . .

  1. Kabohaidreti
  2. Vitamin
  3. Madini
Chagua Jibu


4. Maelezo au taarifa za uchunguzaji huitwa . . . . . . . .

  1. data
  2. kizio
  3. kipimo
Chagua Jibu


5. Sauti iliyogonga ukuta na kurudishwa huitwa . . . . . . . . . .

  1. mwamba
  2. mwanga
  3. mwangwi
Chagua Jibu


6. Ukavu macho ni ugonjwa unaotokana na upungufu wa . . . . . . . . .

  1. Protini
  2. Vitamini
  3. Mafuta
Chagua Jibu


7. Mtu aliyekosa chakula bora afya mbaya na dhaifu . . . . . . .

  1. Afya mbaya na dhaifu
  2. Hupendeza
  3. Anakuwa na afya bora
Chagua Jibu


8. Ni kundi lipi la chakula huimarisha kinga ya mwili? ... ... ...

  1. Mchicha, maembe na karoti
  2. Wali, nyama na viazi
  3. Machungwa, muhogo na nyama
Chagua Jibu


9. Rula ikizamishwa kwenye glasi yenye maji huonekana kama imepinda kwa sababu mwanga .........ukitua katika maji.

  1. hutengeneza kivuli
  2. hutengeneza taswira
  3. hupinda
Chagua Jibu


10. Joto kutoka kwenye moto hufikia ngozi zetu kwa njia ya ... ... ...

  1. mnunurisho
  2. mpitisho
  3. msafara
Chagua Jibu


SEHEMU B

Jaza nafsi zilizoachwa wazi

11. Kujisaidia haja ndogo mtoni na ziwani . . . . . . . . . .

Fungua Jibu


12. Nyuzi za pamba na katani asili yake ni . . . . . . . . . . 

Fungua Jibu


13. Chomo kinacho tumiwa kuchunguza vitu vidogo sana huitwa . . . . . . . .

Fungua Jibu


14. Onesha mpangilio wa nguvu katika sumaku zifuatazo zinapo karibiana


Fungua Jibu


15. Hewa iliyo kwenye mwendo huitwa . . . . . . . . .

Fungua Jibu


16. Wakati wa usanisinuru mmea huhitaji mwanga wa jua, chumvichumvi, rangi ya kijani na hewa ya . . . . . . . . .

Fungua Jibu


17. Hali tatu za maji ni kimiminika, gesi na . . . . . . . . .

Fungua Jibu


SEHEMU C

Jibu Kweli au Si Kweli

18.  Hewa ya kabonidioksaidi inawasha moto . . . . . . . . . . .

Fungua Jibu


19.  Mkasi, mizani na vifaa vya kufungulia soda ni mifano ya mashine daraja la . . . . . . . . . . .

Fungua Jibu


20.  Ugonjwa wa kansa na kisukari hupunguza kinga ya mwili . . . . . . . .

Fungua Jibu


SEHEMU D

Oanisha fungu A na B ili kupatajibu sahihi

FUNGU A FUNGU B

21. Seli za damu zenye wajibu wa kulinda mwili dhidi ya magonjwa

22. Ni kazi mojawapo ya mgandamizo wa hewa

23. Unyafuzi

24. Nazi na mbegu za alizeti

25. Taswira

  1. Kusukuma chini vitu vinavyoelea
  2. Huupa mwili joto
  3. Chembe nyekundu za damu
  4. Kunyonya juisi kwa mrija
  5. Hujenga mwili
  6. Chembe nyeupe za damu
  7. Matokeo ya kusharabu mwanga
  8. Matokeo ya kuakisi mwanga
  9. Ukosefu wa protini
  10. Ukosefu wa mlo kamili
Fungua Jibu


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256