STD IV KISWAHILI ONLINE NECTA EXAM REVIEW FOR YEAR 2020

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA NNE

KISWAHILI-2019

1. Sikiliza kwa makini sentensi zinazosomwa, kisha ziandike kwa usahihi katika nafasi zilizoachwa wazi.

 1. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 
 2. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 
 3. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
 4. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
 5. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .  . . . . 
Fungua Jibu


SEHEMU B

2. Katika Kipengele (i) –(v), andika herufi ya jibu lililo sahihi katika nafasi iliyoachwa wazi

(i)Neno “tumeimba” lipo katika hali gani?

 1. Timilifu
 2. Iliyopita
 3. Iliyopo
 4. Ijayo
Chagua Jibu


(ii) Nilinunua matunda matamu. Neno “nilinunua” lipo katika wakati gani?

 1. Mtimilifu
 2. Ujao
 3. Uliopita
 4. Uliopo
Chagua Jibu


(iii) Watoto . . . . . . . . . . . . . . pilau juzi. Neno lipi kati ya haya maneno yafuatayo linakamilisha sentensi hii?

 1. Watakula
 2. Wanakula
 3. Walikula
 4. Hula
Chagua Jibu


(iv) Neno lipi linaonesha wakati ujao kati ya maneno yafuatayo?

 1. Niliimba
 2. Nitaimba
 3. Huimba
 4. Ninaimba
Chagua Jibu


(v) Mwalimu . . . . . . . . . . somo la kiswahili sasa hivi

 1. Amefundisha
 2. Alifundisha
 3. Hufundisha
 4. anafundisha
Chagua Jibu


SEHEMU C

3.

(i) Toa maana ya nahau zifuatazo kwa kuandika jibu lililo sahihi katika nafasi iliyoachwa wazi.

 1. kufa kishujaa. . . . . . . . . .
 2. kifungua kinywa. . . . . . . . . .
 3. mkono wa birika. . . . . . . . . .
Fungua Jibu


(ii) Kamilisha methali zifuatazo kwa kuandika jibu lililo sahihi katika nafasi iliyoachwa wazi.

 1. Maji yakimwagika. . . . . . . . . .
 2. Fuata nyuki
Fungua Jibu


SEHEMU D

4. Sentensi zifuatazo zimechanganywa. Zipange katika mtiririko unaoleta maana kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E. Sentensi ya (i) imetumika kama mfano.

 1. Nikifika shuleni ninaanza masomo.
 2. Kila siku ninaamka asubuhi.
 3. Kisha ninaondoka kwenda shuleni.
 4. Ninapiga mswaki na kuoga
 5. Dada ananipa chai na chapatti
 6. Ninakunywa chai kwa chapati.
Fungua Jibu


5. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata kwa kuandika jibu hililo sahihi katika nafasi iliyoachwa wazi.

Yoya na Bura wanaishi katika Kipp cha Ulanga. Watoto hao walikuwa na tabia ya ukaidi. Kila walipoonywa na wazazi wao hawakutii. Walimu pia walitimiza wajibu wao wa malezi, hivyo mara kwa mara waliwashauri kuacha tabia ya ukaidi. japokuwa walionywa na walimu pamoja na wazazi lakini hawakubadilika.

Walipofika Darasa la Nne, watoto hao walianza tabia ya utoro na hatimaye waliacha shule. Walikubaliana kuanza biashara ya kuuza mkaa. Kila siku walikwenda msituni kukata miti kwa ajili ya kuchoma mkaa. Wazazi wao waliwaonya kwa kuwakumbusha katazo la serikali kuhusu ukataji wa miti ovyo.

Siku moja walipokwenda kukata miti msituni, viongozi wa serikali ya waliwavizia na kuwakamata. Waliwapeleka kwenye ofisi ya Kulp. Huko walipata adhabu kali na kuamriwa kupanda miti ishirini kila mmoja. Walijutia ukaidi wao na kuomba radhi kwa wazazi na walimu wao. Walisamehewa na walirudi shuleni kuendelea na masomo. Toka wakati huo watoto hao walikuwa na heshima na watiifu sana.

Maswali

 1. Ni tabia zipi mbaya walizokuwa nazo yoya na bura?
 2. Fungua Jibu


 3. Ni tabia gani ailiwafanya Yoya na Bura kuacha shule?
 4. Fungua Jibu


 5. Baada ya kupewa adhabu Yoya na bura walianya nini?
 6. Fungua Jibu


 7. Habari hii inahusu nini?
 8. Fungua Jibu


 9. Habari hii inakufundisha nini?
 10. Fungua Jibu


  Fungua Jibu


  Fungua Jibu


  Fungua Jibu


  Fungua Jibu


  Fungua Jibu


  Fungua Jibu


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256