STD IV KISWAHILI ONLINE NECTA EXAM REVIEW FOR YEAR 2015

MTIHANI WA KISWAHILI DARASA LA NNE 2015

SEHEMU A

Sikiliza sentensi zinazomwa kisha uziandike.

1. . . . . . . . . . . . . . .

2. . . . . . . . . . . . . . .

3. . . . . . . . . . . . . .

4. . . . . . . . . . . . . . .

5. . . . . . . . . . . . . . .

Fungua Jibu


SEHEMU B

Jibu swali la 6 - 10 kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi na kuiandika katika kisanduku pembeni ya kila swali.

6. Mama yangu .............. chakula kizuri jana jioni

 1.  anapika 
 2.  atapika 
 3.  alipika 
 4.  hupika
Chagua Jibu


7. Siku ya pill baada ya leo huitwa ..........

 1. juzi
 2. kesho kutwa
 3. mtondogoo
 4. mtondo
Chagua Jibu


8. Wingi wa neno ufundi ni upi kati ya maneno yafuatayo

 1. Mafundi
 2. fundi
 3. vifundi
 4. ufundi 
Chagua Jibu


9. Ni neno lipi kati ya maneno yafuatayo lenye maana inayojumuisha maneno; upinde, bunduki, mkuki na mshale?

 1. silaha
 2. vipuri
 3. malighafi
 4. samani
Chagua Jibu


10. . Mwakani........... darasa la tano . Ni neno lipi linakamilisha sentensi hiyo kwa usahihi 

 1. niliingia
 2. ninaingia 
 3.  nitaingia
 4. nimeingia
Chagua Jibu


SEHEMU C

Jibu swali la 11 - 15 kwa kukamilisha vitendawili, methali na nahau zifuatazo

11. . . . . . . . . . . . . . . si mkulima

Fungua Jibu


12. Biashara . . . . . . . . . . . . . .

Fungua Jibu


13. . . . . . . . . . . . . . . huumiza matumbo

Fungua Jibu


14. Mpiga ngumi ukuta . . . . . . . . . . . . . .

Fungua Jibu


15. Dua la mnyone . . . . . . . . . . . . . .

Fungua Jibu


16. Nahau "Kumpa heko" maana yake ni ipi? . . . . . . . . . . . . . .

Fungua Jibu


17. Kitendawili kisemacho "Tajiri wa rangi" jibu lake ni lipi? . . . . . . . . . . . . . .

Fungua Jibu


18. Nahau "Kuzunguka mbuyu" maana yake nini? . . . . . . . . . . . . . .

Fungua Jibu


19. Kitendawili kisemacho "rafiki yangu ni muharibifu lakini bado namuhitaji" maana yake nini? . . . . . . . . . . . . . .

Fungua Jibu


20. "Nyumba yangu haina mlango" Jibu la kitendawili hiki ni. . . . . . . . . . . . . .

Fungua Jibu


SEHEMU D

Soma habari ifuatayo kisha jibu swali la 21 -25.

Mzee magali anaishi katika kijiji cha Mailisita. Mke wa mzee magali anaitwa Roza, ni mwanamke mkarimu sang familia hiyo hujushughulisha na kilimo cha mboga na matunda. Kila mwaka mzee magali huvuna mboga nyingi sana pamoja na matunda. Siku ya ijumaa hupeleka sokoni mchicha, nyanya, biringana, bamia na nyanya chungu. Aidha, siku ya jumamosi hupeleka pia parachichi, maembe, matango na machungwa.

Mzee magali anawasomesha watoto wake kwa kutumia pesa anazopata kutokana na kuuza mazao. kutokana na faida aliyoipata kila mwaka alinunua trekta na mashine ya kusaga. Trekta hiyo inainsaidia katika kilimo. Pia humpatia pesa kwa kuwa hutumia kuwalimia wanakijiji wenzake.

Maswali

21. Mzee magali anaishi katika kijiji gani? . . . . . . . . . . . . . .

Fungua Jibu


22. Mke wa mzee magali anaitwa nani? . . . . . . . . . . . . . .

Fungua Jibu


23. Familia ya mzee magali hulima nini?. . . . . . . . . . . . . .

Fungua Jibu


24. Siku ya jumamosi Mzee Magali hupeleka nini sokoni?. . . . . . . . . . . . . .

Fungua Jibu


25. Mwaka jana Mzee magali alinunua vitu gani? . . . . . . . . . . . . . .

Fungua Jibu


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256