JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA, OFISI YA RAIS TAWAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA NNE
A07 HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI
Muda: Saa 1:30 Mwaka: 2025
Maelekezo
KWA MATUMIZI YA MPIMAJI TU | ||
NAMBA YA SWALI | ALAMA | SAINI YA MPIMAJI |
1. | ||
2. | ||
3. | ||
4. | ||
5. | ||
6. | ||
JUMLA | ||
SAINI YA MHAKIKI |
SEHEMU A (Alama 20)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
1. Jibu vipengele (i) - (x) kwa kuchagua jibu sahihi na kuandika herufi yake katika kisanduku ulichopewa.
(i) Misingi ya ukuzaji na utunzaji wa maadili katika jamii za Kitanzania kabla ya ukoloni ilisisitiza mambo gani? [ ]
(ii) Njia gani ilitumika kufundisha maadili katika jamii za kale? [ ]
(iii) Siku rasmi ya soko kwa ajili ya kununua na kuuza bidhaa baina ya jamii za Kitanzania kabla ya ukoloni iliitwaje?
(iv) Ugunduzi wa madini gani ulichochea kukua na kuimarika zaidi kwa shughuli za uzalishaji mali kabla ya ukoloni? [ ]
(v) Shughuli gani za kiuchumi husaidia kujenga uhusiano mwema katika jamii?[ ]
(vi) Ili watoto wakue katika maadili mema, wazazi wanapaswa kufanya nini? [ ]
(vii) Elimu ya maadili na afya ya uzazi kwa vijana iliyotolewa kabla ya ukoloni ilijulikana kama [ ]
(viii) Mtoto wa kaka wa mama yako anaitwaje? [ ]
(ix) Uhusiano mzuri baina ya ndugu au jamaa wa karibu unajengwaje? [ ]
(x) Bainisha njia mojawapo ya kujenga uhusiano wa kirafiki uwapo nyumbani au shuleni [ ]
2. Jibu vipengele (i) – (v) kwa kuoanisha maelezo kuhusu majukumu ya viongozi mbalimbali wa shule katika Orodha A na mfumo wa uongozi katika ngazi ya shule katika Orodha B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi kwenye mabano uliyopewa.
Orodha A | Herufi | Orodha B |
(i) Husimamia mambo ya taaluma na nidhamu za wanafunzi shuleni. | [ ] |
|
(ii) Hufuatilia maadili na taaluma shuleni katika ngazi mbalimbali. | [ ] | |
(iii) Huongoza wanafunzi wengine katika kukuza na kutunza maadili mema. | [ ] | |
(iv) Hukuza, hutunza na husimamia maadili ya wanafunzi na walimu shuleni. | [ ] | |
(v) Huratibu mitihani ya ndani na kupanga ratiba ya masomo shuleni. | [ ] |
3. Jibu vipengele (i) - (v) kwa kuchagua jibu sahihi katika mabano na kuliandika katika sehemu iliyoachwa wazi.
(i) Wazazi wanawahimiza watoto wao kuzingatia usafi wa mwili, nguo na vyombo ili kuepuka nini? _____________________________________ (Ukorofi, Magonjwa, Uvivu)
(ii) Kuwahi shuleni na kuwepo darasani kwa wakati humuwezesha mtoto kuepuka nini? ______________________________________________ (Ukaidi, Adhabu, Utukutu)
(iii) Unashauriwa kufanya nini ukiona mtoto mwenzio anafanyiwa vitendo vibaya? __________________________________________________________ (Kuondoka haraka, Kutoa taarifa, Kujificha)
(iv) Tabia ipi humaanisha utayari wa kutekeleza amri za viongozi shuleni? _________________________________________________________ (Upole, Ucheshi, Utii)
(v) Tabia ipi humaanisha kukiuka maagizo na ushauri wa wazazi au walezi? _________________________________________________________ (Ukatili, Utukutu, Ubinafsi)
SEHEMU B (Alama 18)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
4. Chunguza kielelezo kifuatacho cha mti wa familia kisha jibu maswali katika vipengele (i) - (v)
|
(i) Familia inayoonekana katika mchoro huo inaundwa na jumla ya watu wangapi? _______________________________________________________.
(ii) Uhusiano wa Baba na Mama katika familia hiyo unaitwaje? _______________________________________________________.
(iii) Juma anamuita jina gani Asha linalowakilisha uhusiano wao kama wanafamilia? _______________________________________________________.
(iv) Asha na Juma wanawaita jina gani Baba na Mama linalowakilisha uhusiano wao kama wanafamilia? ____________________________.
5. Chunguza kwa makini picha ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata.
|
Maswali
(a) Ni shughuli gani inayofanywa na watu wanoonekana katika picha? ________________________________________________________
(b) Ni kifaa gani kinatumika katika shughuli inayoonekana katika picha? ________________________________________________________
(c) Ni mbinu gani itakayowezesha mazao yanayoonekana katika picha kustawi wakati wa ukame utokanao na uhaba wa mvua? ________________________________________________________
(d) Vitu gani viwili vitawezesha mazao yanayoonekana katika picha kukua na kustawi?
(i) _____________________________________________________
(ii) _____________________________________________________
(e) Faida zipi zinatokana na mavuno ya mazao yanayoonekana katika picha? Taja faida mbili
(i) _____________________________________________________
(ii) _____________________________________________________
SEHEMU C (Alama 12)
Jibu swali la sita (6)
6. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho, kisha jibu maswali katika vipengele (a) – (f) kwa kuandika jibu lililo sahihi katika sehemu zilizoachwa wazi.
Jamii za kale zilitumia dawa za asili kutibu magonjwa mbalimbali. Dawa za asili zilitokana na vitu vya asili kama mimea. Dawa hizo zilitayarishwa kwa kutumia maarifa na ujuzi wa asili. Maarifa na ujuzi wa asili ulizingatia maadili katika utayarishaji na matumizi ya dawa. Maadili yaliyozingatiwa katika utayarishaji ni usafi. Dawa zilitayarishwa kwa njia za asili kama kuchemshwa, kupondwa, kutwangwa na kusagwa. Usafi ulizingatiwa katika njia zote hizo.
Maadili yaliyosisitizwa katika matumizi ya dawa ni kuzingatiwa maelekezo ya matumizi ya dawa. Maadili ya kuzingatia maelekezo ya matumizi ya dawa yalisisitizwa ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na matumizi yasiyo sahihi ya dawa. Maelekezo ya matumizi ya dawa yalitolewa na watu wenye maarifa na ujuzi wa kutayarisha dawa hizo.
Maswali
(a) Jamii za kale zilitumia dawa za asili kufanya nini? _________________________________________________________
(b) Dawa za asili zilitokana na nini? _________________________________________________________
(c) Maadili gani yalizingatiwa katika utayarishaji wa dawa? _________________________________________________________
(d) Njia zipi zilitumika katika kutayarisha dawa za asili. Taja njia mbili
(i) ____________________________________________________
(ii) ____________________________________________________
(e) Maelekezo ya matumizi ya dawa yalitolewa na watu wenye sifa ipi? _________________________________________________________
(f) Kwa nini maadili ya kuzingatia maelekezo ya dawa yalisisitizwa? _________________________________________________________
STANDARD FOUR HISTORIA EXAM SERIES 64
STANDARD FOUR HISTORIA EXAM SERIES 64
Jina la mwanafunzi ________________________
Namba ya upimaji____________________
Mkoa____________________________
Halmashauri___________________
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI
MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA NNE
A07 HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI
Muda: Saa 1 Mwaka: 2025
Maelekezo kwa mtahiniwa
KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU | ||
NAMBA YA SWALI | ALAMA | SAHIHI YA MTAHINI |
1. | ||
2. | ||
3. | ||
4. | ||
5. | ||
6. | ||
JUMLA |
SEHEMU A: (ALAMA 20)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye kisanduku kwa kila kipengele (i)-(x)
(i) Hali ya kupiga hatua mbele au kuongeza kitu kutoka kiwango cha chini kwenda cha juu huitwaje?
(ii) Mifano ipi inaeleza stadi za elimu kabla ya ukoloni?
(iii) Kwanini elimu wakati kabla ya ukoloni ilitolewa kwa lugha ya jamii husika?
(iv) Shughuli ya ususi ilichangiaje maendeleo ya jamii kabla ya ukoloni?
(v) Teknolojia ya chuma ilisaidia vipi maendeleo ya kilimo?
(vi) Katika utunzaji wa mazingira, jamii iliweka sheria gani ili kutunza mazingira kabla ya ukoloni?
(vii) Miongoni mwa maadili yaliyokuwa yanazingatiwa kwa wataalamu wa sayansi asilia kabla ya ukoloni ilikuwa ni___
(viii) Jamii ipi kati ya hizi ilitengeneza mavazi kwa kutumia magome ya miti na ngozi za wanyama?
(ix) Eneo maarufu kwa kilimo cha umwagiliaji kabla ya ukoloni ni lipi kati ya haya?
(x) Ni teknolojia ipi ya asili ya kuhifadhi samaki ilikuwa ikitumika hapo kale?
2. Oanisha maneno kutoka Orodha A na yale ya Orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihi kwenye sehemu uliyopewa.
Orodha A | Majibu | Orodha B |
(i) Dini | [ ] |
|
(ii) Kupewa kazi kinyume na umri wako | [ ] | |
(iii) Shughuli za uvuvi | [ ] | |
(iv) Kusaidia kazi ndogo ndogo za nyumbani | [ ] | |
(v) Kusalimia na kuongea lugha nzuri | [ ] |
3. Chagua jibu kutoka kwenye kisanduku kisha liandike kwenye nafasi zilizoachwa wazi.
China, Litti, Mkwawa, Mirambo, Mangi sana, Machemba, Ushujaa wa vita, Ujerumani |
(i) Chifu wa jamii za wahehe kabla ya ukoloni ___________________________________
(ii) Mtemi wa jamii za wanyaturu kabla ya ukoloni _______________________________
(iii) Mtemi wa wanyamwezi kabla ya ukoloni ___________________________________
(iv) Njia mojawapo ya kupata uongozi hapo kale_______________________________
(v) Jamii nyingi zilipambana na wavamizi kutoka wapi?__________________________
SEHEMU B: (ALAMA 18)
Jibu maswali yote kutoka sehemu hii.
4. Soma mchoro ufuatao kisha jibu maswali yanayofuata.
Maswali
(a) Mchoro huo hapo juu unawakilisha nini?
_________________________________________________________________
(b) Kiongozi gani wa shule anahakikisha wanafunzi wanafuata sheria za shule?
_________________________________________________________________
(c) Ni ngazi ipi inahusika kuhakikisha wanafunzi wenzao wanafuata sheria za shule?
_________________________________________________________________
(d) Ni nani anahakikisha darasa lake linakuwa na maadili?
_________________________________________________________________
5. Soma picha ifuatayo kisha jibu maswali.
Maswali
(i) Vitu unavyoviona pichani kwa jina moja huitwaje?
______________________________________________________
(ii) Ni wageni kutoka maeneo gani walileta vitu hivyo pichani?
______________________________________________________
(iii) Nini matumizi ya vitu hivyo?
______________________________________________________
(iv) Ni aina gani ya urithi unaoonekana pichani?______________________________________________________
(v) Ni urithi gani mwingine ulioletwa na watu walioleta vitu vinavyoonekana hapo pichani?
______________________________________________________
SEHEMU: (ALAMA 12)
Jibu swali la sita (6)
6. Sentensi zifuatazo zimechanganywa haziko katika mtiririko wenye kuleta mantiki. Zipange sentensi hizo kwa kuzipa herufi A-F ili kupata habari yenye kuleta mantiki kuhusu familia.
(i) Uhusiano huo ni wa asili kwani mtu hujikuta tu yupo katika familia fulani na watu fulani.
(ii) Baada ya mtu kuwa na ndugu hao, anapaswa atambue kuwa baba na mama ni viongozi wa familia.
(iii) Vile vile, anapaswa kujua na kutambua mchango wa kila mwanafamilia ili kuwa na familia yenye upendo.
(iv) Familia ni uhusiano wa damu uliopo baina ya watu fulani.
(v) Hivyo anapaswa awaheshimu na kuwajali kwa kila hali kwani ni sababu ya yeye kupatikana.
(vi) Katika kujikuta huko, mtu huwa ana baba, mama, kaka na dada zake katika familia husika.
STANDARD FOUR HISTORIA EXAM SERIES 50
STANDARD FOUR HISTORIA EXAM SERIES 50
Jina la Mwanafunzi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
Shule . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS UTAWALA WA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MKOA WA DODOMA
MTIHANI WA MUHULA DARASA LA NNE
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI [06E]
MUDA : Saa 1:30 2025
MAELEKEZO:
KWA MATUMIZI YA WATAHINI TU | |||
Namba ya Swali | Alama | Sahihi ya Mtahini | Sahihi ya Mhakiki |
1. | |||
2. | |||
3. | |||
4. | |||
5. | |||
6. | |||
JUMLA |
SEHEMU A: (ALAMA 26)
1. Chagua herufi ya jibu sahihi kisha ujaze kwenye kisanduku ulichopewa
i. Kitendo cha kutoa au kupokea kitu chochote kwa lengo la kupewa upendeleo katika jambo fulani au kupata huduma fulani huitwaje? [ ]
A. Zawadi C. Nidhamu B. Rushwa D. Msaada
ii. Tanzania ni nchi iliyoundwa na mataifa mawili; Tanganyika na Zanzibar. Ni lini muungano wan chi hizo ulifanyika?
A. 9/12/1961 C. 14/10/1999 B. 26/12/1964 D. 26/4/1964
iii. Ipi miongoni mwa tabia zifuatazo huonyesha kitendo cha heshima?
iv. Katika historia ya Tanzania, Ni mreno gani wa kwanza kuingia pwani ya Afrika Mashariki?
v. Kitu chochote ambacho mtu anastahili kupewa huitwaje?
A. Haki C. Mali B. Wajibu D. Majukumu
2. Oanisha maelezo yaliyopo kwenye orodha A na majibu yaliyopo kwenye orodha B, na kisha uandike herufi ya jibu sahihi kwenye chumba ulichopewa.
ORODHA A | MAJIBU | ORODHA B |
(i) Majengo ya zamani yaliyobaki kama sehemu ya historia na utamaduni. |
| |
(ii) Sehemu ambapo nyaraka na taarifa mbalimbali za kihistoria huhifadhiwa. | ||
(iii) Maeneo yanapopatikana masalia ya mambo ya kale na utamaduni wa mwanadamu. | ||
(iv) Maeneo yanayotumiwa kuhifadhi vitu vyenye historia na urithi wa kiasili na kiutamaduni. |
3. Chagua jibu sahihi kutoka kwenye kisanduku kasha jibu maswali yanayofuata;
Kaole, Zanzibar, Olduvai Gerge, Zinjanthropus, Link |
(i) Mji palipogundulika mabaki ya Dinosaria wa Tendaguru.
(ii) Sehemu ambapo lipo jengo la maajabu ambalo lina historia ya kuwa jengo la kwanza kuwekwa lifti za umeme.
(iii) Eneo lilipogunduliwa fuvu la Binadamu wa kale na Dr. Louis Leakey.
(iv) Jina lilopewa fuvu la binadamu wa kale lililogunduliwa mwaka 1959.
(v) Mji yanapopatikana magofu ya msikiti na kituo cha kuhifadhia watumwa.
SEHEMU B: (ALAMA 24)
4. Ainisha matendo yafuatayo kwa kusoma maelezo yake na kuweka alama ya vema (√) katika chumba sahihi. Kipengele cha tano (v) kimefanywa kama mfano kwa ajili yako.
Kitendo | Kitendo cha kimaadili | Kitendo kisicho cha kimaadili |
(i) Kupigana na wenzako | ||
(ii) Kusalimia watu wakubwa | ||
(iii) Kushirikiana na watu wengine | ||
(iv) Kuwatukana watu wazima | ||
(v) Kumsaidia mzee kubeba mizigo | √ |
5. Tazama picha hizi kwa makini kasha jibu maswali yanayofuata
![]() |
Maswali
i. Mwanamke aliyeoneshwa katika picha A anafanya nini?
ii. Mwanaume anayeonekana kwenye picha B anafanya nini?
iii. Jamii ya mtu aliyeoneshwa kwenye picha B hupendelea kula chakula gani.
iv. Aina ya nguo aliyoivaa mtu aliyeoneshwa kwenye picha B inaitwaje?
6. Soma habari ifuatayo kasha ujibu maswali yanayofuata;
Jamii za Tanzania hapo Kale zilifanya biashara na wafanyabiashara kutoka Mashariki ya Mbali na ya Kati. Nchi hizo ni India, Irani, Iraki, Kuwait, China na Saud Arabia. Biashara hii ilifanyika katika miji iliyopo katika mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi kama vile Dar es Salaam, Bagamoyo, Tanga, Kilwa na Zanzibar. Biashara hizi zilifanyika kwa kubadilishana bidhaa. Bidhaa kubwa katika biashara hii kutoka nchini ilikuwa dhahabu na pembe za ndovu. Dhahabu ilitoka Zimbabwe kupitia bandari ya Sofala, Msumbiji. Kutoka kwa wageni kuja nchini, bidhaa kubwa zilikuwa shanga na vyombo vya ndani kama vile mabakuli na sahani za udongo. Baadhi ya mabaki ya bidhaa hizi yapo katika Makumbusho hapa nchini, kama vile makumbusho ndogo iliyopo Kaole, Bagamoyo.
Maswali
(i) Mabaki ya bidhaa zilizotumika katika biashara na watu wa Mashariki ya mbali zimehifadhiwa wapi?
(ii) Taja bidhaa mbili zilizokuwa zinaletwa kutoka kwa wageni?
(iii) Tja nchi mbili za Mashariki ya mbali zilizotajwa kwenye habari hii?
(iv) Taja miji miwili iliyopo katika Mwambao wa Pwani
STANDARD FOUR HISTORIA EXAM SERIES 48
STANDARD FOUR HISTORIA EXAM SERIES 48