Jina la mwanafunzi ________________________
Namba ya upimaji____________________
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI
MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA NNE
L01 KISWAHILI
Muda: Saa 1 Mwaka: 2025
Maelekezo kwa mtahiniwa
KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU | ||
NAMBA YA SWALI | ALAMA | SAHIHI YA MTAHINI |
1. | ||
2. | ||
3. | ||
4. | ||
5. | ||
JUMLA |
SEHEMU A: (ALAMA 20)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Sikiliza sentensi unazosomewa kisha ziandike katika sehemu zilizoachwa wazi (i)- (v)
(i) ___________________________________________________________________________
(ii) ___________________________________________________________________________
(iii) ___________________________________________________________________________
(iv) ___________________________________________________________________________
(v) ___________________________________________________________________________
2. Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye kisanduku.
(i) Mtoto wangu anapenda sana sukari. Wingi wa neno lililopigiwa mstari ni upi?
(ii) Hamisi aliimba vizuri sana wimbo wa shule. Sentensi hii ipo katika wakati gani?
(iii) Fedha innayotumika kulipa usafiri wa dalala huitwaje?
(iv) Kila mmoja darasani alitoa __________________yake kuhusu suala la chakula.
(v) Ni bora uende shule kwa kuchelewa___________________kutokwenda kabisa.
(vi) Aliongea kwa haraka haraka mithili ya kanda ya sauti. Neno mithili lina maana gani?
(vii) Alitumia gari moshi kwenda mkoani Kigoma. Neno lililopigiwa mstari lina maana sawa na neno lipi kati ya haya yafuatayo?
(viii) Neno lipi kati ya yafuatayo halilandani na mengine?
(ix) Kinyume cha neno “polepole” ni kipi?
(x) Methali ipi inatuonya kuhusu kutegemea vitu vya mtu mwingine?
SEHEMU B (ALAMA 20)
Jibu maswali yote kutoka katika sehemu hii.
3. Weka alama za uandishi katika nafasi zilizoachwa wazi
(a) Maimuna ni mwanafunzi mtiifu____
(b) Mtoto huyu ni wa nani____
(c) Alikwenda sokoni kununua samaki____magimbi____na dagaa.
(d) Looh___ kumbe ni jeuri sana.
(e) Mwalimu mkuu ni mwenyeji wetu_____
4. Panga sentensi zifuatazo kwa mtiririko unaofaa ili kuleta habari kamili. Tumia herufi A, B, C, D, E
(i) Huamka mapema kila siku ili afanye usafi na kujiandaa kwenda shule.
(ii) Kisha baada ya usafi anaoga na kupata kifungua kinywa tayari kwenda shule
(iii) Beatrice ni mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Mbezi Juu.
(iv) Akishaamka, huwasalimia wazazi wake na kuanza kufanya usafi.
(v) Wazazi humuaga na kumtakia masomo mema anapoanza safari ya kwenda shule.
SEHEMU C: (ALAMA 10)
Jibu swali la tano (5)
5. Soma kifungu kifuatacho cha habari kisha jibu maswali yanayofuata.
Wanyama walikusanyika katika mkutano mkuu wa wanyama. Mkutano huo uliitishwa na sungura. Sungura alitaka wajadili na wenzake ni kwa jinsi gani wataweza kuwazuia simba wasile wanyama wengine msituni. Wanyama waliohudhuria mkutano huo walikuwa ni swala, nyati, fisi, mbwa mwitu na mbweha.
Kila mmoja alitoa wazo lake lakini mwisho wa siku wakakubaliana kuwa watege mtego ambao utasaidia kuwakamata simba na kuwaua ili waishe wote msituni. Jukumu la kuandaa mitego hiyo aliachiwa mbwa mwitu kwani ilisemekana kuwa yeye ni mtaalamu wa mitego ya msituni.
Maswali.
(i) Kipi kinafaa kuwa kichwa cha habari uliyoisoma?
__________________________________________________________________________
(ii) Mkutano wa wanyama uliitishwa na nani?
__________________________________________________________________________
(iii) Nini lengo la mkutano wa Wanyama?
__________________________________________________________________________
(iv) Wanyama walikubaliana nini katika mkutano huo?
__________________________________________________________________________
(v) Kwanini mbwa mwitu aliachiwa jukumu la kutega mitego?
__________________________________________________________________________
STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 54
STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 54
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
01 MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA NNE
KISWAHILI - 2024
Maelekezo
SEHEMU A: IMLA
1. Sikiliza kwa makini na uandike sentensi kama zitakavyosomwa na msimamizi wa mtihani
(i) ________________________________________________________________
(ii) ________________________________________________________________
(iii) ________________________________________________________________
(iv) ________________________________________________________________
(v) ________________________________________________________________
SEHEMU B: MSAMIATI
2. Chagua herufi ya jibu sahihi
(i) “Sisi ni watoto” umoja katika sentensi hii ni ipi?
(ii) Bakari anakula wali ___________________kijiko
(iii) Neno “kombamwiko” lina maana sawa na lipi?
(iv) Mtaalamu wa mambo ya sayansi ya nyota anaitwa__________
(v) Neno “kinguluwila” lina silabi ngapi?
3. SEHEMU C: METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI
(i) Tegua kitendawili hiki “Tatu tatu mpaka ulaya”________________________________
(ii) Koti la babu limejaa chawa ____________________________________________________
(iii) Nini maana ya nahau hii “kupiga mbiu” ________________________________
(iv) Kamilisha methali hii “kidole kimoja ______________________________________________
(v) Kulala fofofo maana yake ni ___________________________________________________
SEHEMU D: UTUNGAJI
4. Kamilisha nafasi iliyowazi kwenye barua kwa kuchagua majibu sahihi uliyopewa kwenye kisanduku
baba shikamoo, S.L.P 250, 25/7/2014, dhumuni, Bakari Saidi |
Shule ya Msingi Bondeni
(i) _________________________
Dar es Salaam
(ii) _________________________
Mpendwa (iii)____________________________
Ni matumaini yangu unaendelea vizuri na shughuli za kilimo. Na mimi pia sijambo ni buheri wa afya ,naendelea vizuri na masomo yangu.
(iv) __________________________la barua hii ni kutaka kukujulisha kuwa ninatarajia kufanya mitihani ya upimaji ya darasa la nne, ninaomba unitumie pesa kwa ajili ya nauli ya kurejea nyumbani.
Ninashukuru kwa kunihimiza kusoma kwa bidii, ninakuahidi kuwa nitafanya mtihani kwa bidii ili nifaulu. Ninaomba uwasalimie wadogo zangu.
Ni mimi mwanao
(v) _________________________
5. SEHEMU E: SHAIRI
Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu maswlai yanayofuata kwa kuandika jibu sahihi katika nafasi iliyoachwa wazi
Tusidharau wazazi, heshima kuwafanyia,
Wanafanya kubwa kazi, kutuzaa kutulea,
Wanatupa na mavazi, sisi tunachekelea,
Wazazi wetu ni nguzo, kwetu sisi wana wao.
Wanatutunza vizuri, kwa chakula na mavazi,
Wananunua sukari, chai pia maandazi,
Wanapika na achari, wanatupa na malazi,
Wazazi wetu ni nguzo, kwetu sisi wana wao.
Vile vile zahanati, tunakwenda kutibiwa,
Twaenda kila wakati, ugonjwa tukizidiwa,
Hutupepea kwa dhati, kwa joto tukizidiwa,
Wazazi wetu ni nguzo, kwetu sisi wana wao.
Maswali
(i) Shairi hili linahusu nini? ______________________________________________________
(ii) Shairi hili lina beti ngapi? _____________________________________________________
(iii) Taja mkarara katika shairi hili _________________________________________________
(iv) Neno “malazi” lina maana gani kama lilivyotumika katika ubeti wa pili?_________________________________________
(v) Taja vina vya kati na vya mwisho katika ubeti wa tatu ______________________ na__________________________________
STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 58
STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 58
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU
MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA IV TAREHE 23 NA 24 AGOST 2023
KISWAHILI
MUDA: SAA 1:30 AGOST 2023
MAELEKEZO
SEHEMU A: IMLA
1. Sikiliza kwa umakini sentensi zinazosomwa kisha andika kwenye nafasi zilizo wazi.
i.
ii.
iii.
iv.
v.
SEHEMU B:
2. Chagua herufi ya jibu sahihi
i. Kuku, bata, njiwa, kunguru na mwewe kwa jina moja huitwaje?
A: Wanaotaga B: Ndege C: Vikembe D: Wenye mabawa [ ]
ii. Mtu anayeongoza meli huitwa
A: Nahodha B: Rubani C: Dereva D: Mwalimu [ ]
iii. Ni neno lipi tutalipata tukidondosha herufi moja kwenye neno UJUZI?
A: Juzi B: Uzi C: Uuzi D: Juu [ ]
iv. Watoto watakula pilau kesho. Bainisha umoja wa sentensi hiyo
A: Watoto wanakula pilau B: Mtoto atakula pilau kesho
C: Mtoto wanapenda kula mapilau D: Mapilau yameliwa na watoto [ ]
v. Wanafunzi walifagia uwanja. Sentensi hii iko katika wakati gani?
A: Wakati ujao B: Wakati timilifu C: Wakati uliopo D: Wakati uliopita [ ]
SEHEMU C: METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI
3. Tumia majibu yaliyoko kwenye kisanduku kujibu maswali yafuatayo.
Mchoyo, haina baraka, mlango, hajikwai, mafiga, hutunzwa |
i. Tatu, tatu mpaka Tanga. Jibu la kitendawili hiki ni
ii. Malizia methali hii. Mwenda pole
iii. Kila mtu humwabudu apitapo
iv. Andika maana ya Nahau hii. Ana mkono wa birika
v. Malizia methali hii. Mcheza kwao
SEHEMU D: UTUNGAJI
4. Panga sentensi zifuatazo kwa mfuatano sahihi kwa kuzipa herufi A, B, C, D, na E ili kuunda habari sahihi
i. Rehema alimwambia mwalimu kuwa Hamidu anaumwa [ ]
ii. Mwalimu Lupogo anafundisha somo la Sayansi [ ]
iii. Mwalimu alimgusa Hamidu akagundua ana joto kali [ ]
iv. Hamidu alipelekwa zahanati [ ]
v. Alipoingia darasani wanafunzi walisimama na kumsalimia [ ]
SEHEMU E: UFAHAMU
5. Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali kwa usahihi
Amina na Ali ni pacha. Wanaishi katika kijiji cha Kamachumu. Wote ni wanafunzi katika shule ya msingi Izigo. Kila siku huamka mapema na kujiandaa kwenda shuleni. Kabla ya kwenda shuleni, huwasalimia wazazi wao. Baada ya hapo, huagana nao na kuelekea shuleni. Wafikapo shuleni, huungana na wenzao kufanya usafi.
Kisha huingia darasdani na kuanza masomo. Watoto. Hawa wanapendwa na walimu wao kwa sababu ni watiifu.
MASWALI
i. Amina na Ali wanasoma shule gani?
ii. Amina na Ali wanapendwa na walimu wao kwa sababu
iii. Pacha waliotajwa kwenye habari hii ni
iv. Amina na Ali wafikapo shuleni huungana na wenzao kufanya nini?
v. Amina na Ali wanaishi katika kijiji gani?
STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 27
STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 27
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
UPIMAJI WA UTAMILIFU MKOA DARASA LA NNE
MKOA WA NJOMBE
01 KISWAHILI
Muda: Saa 1:30 Mwaka :2023
MAELEKEZO
KWA MATUMIZI YA UPIMAJI TU | ||
NAMBA YA SWALI | ALAMA | SAINI YA MPIMAJI |
1 | ||
2 | ||
3 | ||
4 | ||
5 | ||
JUMLA | ||
SAINI YA MHAKIKI |
SEHEMU A: IMLA
1. sikiliza kwa makini sentensi zitakazosomwa kisha ziandike kwa usahihi.
i. __________________________________________________________
ii. ___________________________________________________________
iii. ___________________________________________________________
iv. ___________________________________________________________
v. ___________________________________________________________
2. chagua jibu sahihi na uandike herufi ya jibu sahihi.
i. Ninaomba_____________________________kwa kosa nililofanya
ii. Kinyume cha neno rejea ni:
iii. Baba aliniambia nimwandikie __________________ ya vitu ninavyohitaji kwa ajili ya shule.
iv. Kanusha sentensi hii “Mwanahamisi hula matunda”
v. Walimu huwa hawapendi kelele madarasani. Sentensi hii ipo katika hali gani? ________________________________
SEHEMU C : METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI
3. i. Wanafunzi wengi hawampendi mzee Kalinga kwa sababu ana mkono mrefu pia ana mkono wa birika. Kuwa na mkono wa birika ina maana gani?
____________________________________________
ii. Mwalimu alipoingia darasani aliandika maneno haya ubaoni. Tia moyo, Tia nanga, Piga marufuku na piga yowe. Kwa neno moja maneno haya yanaitwaje?
_______________________________________________
iii. Babu alituuliza vitendawili akasema ‘Jibu la kitendawili hiki ni lipi? “Nikimpiga mwanangu nalia mwenyewe’
_________________________________________
iv. Mimi ni mbwa ninapenda methali mbalimbali, ndondondo si chururu, fuata nyuki ule asali. Je, asiyesikia la mkuu _______________________________________
v. Malizia methali isemayo ________________________________ hali wali mkavu.
SEHEMU D: UTUNGAJI
4. Panga sentensi hizi katika mtiririko ulio sahihi kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E
i. | Mama yake aliporudi alifurahi sana. | [ ] |
ii. | Aliosha vyombo na kufua nguo zake. | [ ] |
iii. | Nguo zilipokauka alizianua na kuzinyoosha. | [ ] |
iv. | Zawadi aliondoka kuelekea nyumbani kwao. | [ ] |
v. | Kisha akaingia jikoni na kupika chakula. | [ ] |
SEHEMU E: UFAHAMU
5. Soma habari kisha jibu maswali
Nyumbani kwetu tupo watoto watatu tu, mtoto wa kwanza ni mimi Aisha ninasoma darasa la saba. Mtoto wa pili ni Hamisi ambaye anasoma darasa la tano. Anayemfuata Hamisi anaitwa Juma ana umri wa miaka mitano, yeye anasoma darasa la awali.
Baba na mama ni wakulima hodari wanalima mazao mbalimbali pamoja na kilimo wanafanya kazi zingine kwa bidii. Baba na mama wanatusisitiza tufanye kazi kwa bidii hawataki mtu mvivu. Pia wazazi wanatusisitiza kufanya bidii katika masomo ili tuwe na maisha bora hapo baadaye.
MASWALI.
i. Baba na Mama ni _____________________________________ hodari.
ii. Ili uwe na maisha bora hapo baadaye inakupasa?____________
iii. Kifungua mimba ni____________________________________
iv. Mziwanda ana umri wa miaka mingapi?____________________
v. Nyumbani kwa Aisha kuna jumla ya watu wangapi?__________
STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 22
STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 22
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA
NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM
UPIMAJI WA UTAMILIFU WA KATA DARASA LA IV - 2023
KISWAHILI [01]
MAELEKEZO
JINA LA MTAHINIWA: _____________________________________
JINA LA SHULE: _______________________________________
WILAYA: ____________________MKOA:__________________
Muda: Saa 1:30 Julai , 2023
KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU | ||
NAMBA YA SWALI | ALAMA | JINA LA MTAHINI |
1. | ||
2. | ||
3. | ||
4. | ||
5. | ||
JUMLA | ||
SAINI YA MWINGIZA | ||
SAINI YA MHAKIKI |
SEHEMU A: IMLA
1. Sikiliza kwa umakini sentensi utakazosomewa na uziandike kwa usahihi.
i. ___________________________________________________________
ii. ___________________________________________________________
iii. ___________________________________________________________
iv. ___________________________________________________________
v. ___________________________________________________________
SEHEMU B: SARUFI NA MSAMIATI
2. Chagua jibu sahihi kisha uandike herufi kwenye parandesi
ulizopewa.
i. Uwanja wa ndege wa Tanzania ni mzuri sana. Wingi wa neno uwanja ni_____
A. Mauwanja B. Wanja
C. Nyanja D. Viwanja [ ]
ii. Orodha ipi ya maneno inajumuisha wadudu kati ya hizi?
A. Mawio, machweo, zama, kunguni B. Kupe, chawa, kunguru, papasi
C. Suruali, gauni, nyigu, mchwa D. Kupe, papasi, chawa, kunguni [ ]
iii. Kwangu anapenda sana usafi, mtu mwenye tabia ya kuwa safi daima huitwa?
A. Mweupe B. Mzuri
C. Mtanashati D. Mfagiaji [ ]
iv. Shangazi amemkodolea macho utingo. Ukanushi wa sentensi hii ni upi?
A. Shangazi hajamkodolea macho utingo
B. Shangazi hamkodolei macho utingo
C. Shangazi humkodolea macho utingo
D. Shangazi huwa hamkodoleagi macho utingo [ ]
v. Mbwa wetu mweusi si mkali. Kinyume cha neno mkali ni;
A. Mweupe B. Mwizi
C. Mkaidi D. Mpole [ ]
SEHEMU C: LUGHA ZA KIFASIHI
3. METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI
i. Nahau mkono wa birika ina maana gani?
____________________________________________________________
ii. Kamilisha methali hii hakuna masika ______________________________
iii. Kabudi alipokea chakula alichopewa na mama yake kwa shingo upande.
Nahau shingo upande ina maana gani? ____________________________
iv. Nina chemchemi isiyokauka. Jawabu la kitendawili hiki ni
____________________________________________________________
v. _______________________________ si dawa ya pengo. Maneno yapi ni
mwanzo mzuri wa methali hiyo?
SEHEMU D: UTUNGAJI
4. Tumia maneno yafuatayo kujaza katika nafasi zilizoachwa wazi.
Epua, kuchemka, upishi, vifaa, viungo
Mwalimu wetu wa somo la Sayansi alieleza hatua za kuandaa chai kama ifuatavyo;
Tulijifunza kuchemsha chai ya rangi kwa kutumia jiko la gesi.
Andaa
(i) ________vyote vinavyohitajika katika
(ii) _________________ wa chai. Weka sufuria yenye maji kwenye jiko lililowashwa. Weka tangawizi na
(iii) _______________________ vingine kama utapenda. Maji yanapokaribia
(iv)____________________________ weka majani ya chai na uiache ichemke kwa muda.
(v) _____________________, Chai yetu iko tayari kunywewa.
SEHEMU E: UFAHAMU
5. Soma Habari ifuatayo kisha jibu maswali
Ilikuwa ni wakati wa usiku. Siku hiyo kulikuwa na mvua kubwa iliyoambatana na radi. Nilikuwa chumbani kwangu nikisoma kitabu cha hadithi. Mara nilimsikia baba akiniita Mboni! Mboni! zima taa ulale kuna radi sana. Baada ya muda mfupi nikalala fofofo na kuota ndoto nzuri sana. Niliota tumekwenda Zanzibar kutembelea makumbusho tulipokuwa huko tulikwenda Forodhani kuona jumba la mfalme. Tulipoingia ndani tukaona vitu mbalimbali vya kale. Tuliona vitu kama mapanga, sarafu, mbuzi za kukunia nazi na majiko ya asili. Pia tuliona samani na vitanda vyenye besera na magodoro ya sufi. Siamini macho yangu natamani ndoto yangu irudie!
MASWALI
i. Nani aliota ndoto nzuri baada ya kulala fofofo?
______________________________________________________________
ii. Kwanini baba yake alimwambia azime taa?
_____________________________________________________________
iii. Nahau lala fofofo kama ilivyotumika kwenye habari ina maana gani?
_____________________________________________________________
iv. Nyumba anayoishi mfalme huitwaje? _______________________________
v. Neno besera kama lilivyotumika katika habari hii lina maana gani?
_____________________________________________________________
STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 13
STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 13
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI
MTIHANI WA KUJIPIMA DARASA LA NNE
KISWAHILI
SEHEMU A:IMLA
1.Sikiliza kwa makini sentensi zinazosomwa kisha ziandike kwa usahihi
(i)……………………………………………………………
(ii)………………………………………………………………
(iii)……………………………………………………………..
(iv)…………………………………………………………….
(v)……………………………………………………………..
SEHEMU B:MATUMIZI YA LUGHA
2.Chagua jibu sahihi kwa kuandika herufi ya jibu sahihi kwenye kisanduku ulichopewa
(i)Mtoto mwenye adabu ………………..
(A)Hulia hovyo(B)Hupendwa na watu wengi(C)Huosha hovyo(D)Hupigwa na walimu ( )
(ii)Mama alinunua hereni za ………………………..
(A)Dhahabu(B)Zahabu(C)Dhaabu(D)Zaabu( )
(iii)Majira yapi huwa na mvua za rasharasha?
(A)Masika(B)Kiangazi(C)Kipupwe (C)VVuli ( )
(iv)………………..ni mtu anayeendesha meli.
(A)Mahiri(B)Dereva(C)Nahodha (D)Rubani ( )
(v).Binamu ni motto wa …………
(A)Babu(B)Mjomba(C)Dada(D)Kaka ( )
SEHEMU C : METHALI, NAHAU NA VITENDAWILI
3.Kamilisha kazi za kifasihi zifuatazo kwa kuandika jibu sahihi kwa kila swali.
Kamilisha methali zifuatazo
(i)Usipoziba ufa …………………….
(ii)Kuishi kwingi……………………..
(iii)Nini maana ya nahau “amevaa miwani”………………………
(iv)Tegua kitendawili kifuatacho.”mjoma hataki tuonane”
(v)Kuvunjika moyo maana ake ni ……................................
SEHEMU D:UTUNGAJI
4.Chagua maneno kutoka kwenye kisanduku kukamilisha habari
Zangu,jokofu,ndoto,thamani,pangaboi |
Siku moja niliota ndoto(i)………….nzuri sana.Niliota nikiwa kwenye jumba kubwa zuri lenye kila kitu cha(ii)………….Kulikuwa na viyoyozi vilivyoleta hewa nzuri mno(iii)……….lilijaa vinywaji na matunda.Ghafla nilistuka na kukuta(iv)………likiendelea kuzunguka juu ya dari na siye kiyoyozi.Sikuwasimulia rafiki(v)……………ile ndoto kwani wangeishia kunicheka.
SEHEMU E:UFAHAMU
5.Soma shairi kwa makini kisha jibu maswali yafuatayo
Pata ung’oapo jino,uwazi unabakiza
Sura ya huzuni mno,tena ya kufurahia
Nataka unga mkono,penye nia pana njia
Ishirini moja tano,maua yangu chanua
MASWALI
(i)Shairi hili lina beti?..............
(ii)Neno huzuni ni kisawe cha neno gani?...............
(iii)Andika kituo cha hili………………………………………….
(iv)Unapong’oa jino kuna baki nini…………………………
(v)Ubeti huu una mishororo mingapi……………………..
IMLA
(i)Mama anakula ugali na dagaa
(ii)Shuleni kwetu kuna maua
(iii)Baba na mama ni wafanyakazi
(iv)Nitaenda shuleni jumatatu
(v)Nitaimba wimbo
STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 8
STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 8
Jina la Mwanafunzi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
Namba ya Upimaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI
MTIHANI WA UJIPIMAJI WA WILAYA DARASA LA NNE
01 KISWAHILI
Muda:SaaI: 45 Septemba, 2022
Maelekezo
KWA MATUMIZI YA MPIMAJI TU | ||
NAMBA YA SWALI | ALAMA | SAINI YA MPIMAJI |
1. | | |
2 | | |
3 | | |
4 | | |
5 | | |
JUMLA | | |
SAINI YA MHAKIKI | |
SEHEMU A(A1ama 10)
IMLA
1. Sikiliza kwa makini sentensi zinazosomwa na msimamizi wa mtihani kisha uziandike kwa usahihi.
SEHEMU B
(Alama 10)
2. Chagua herufi yajibu sahihi na uiandike katika kisanduku ulichopewa
(i). Mtu anayeongoza meli na kuifikisha mahali inapohitajika huitwa
(ii) Sentensi hii ipo katika wakati gani? "Mtoto hakula chakula"
(iii). "Chungu cha shangazi yangu ni kizuri" wingi wa sentensi hii ni..
(iv) Taja neno moja linalo beba maneno haya, mfenesi, mpera, mkomamanga, mpapai.
(v) Neno "shaghalabaghala" lina silabi ngapP
SEHEMU C (Alama 10)
3. Andika jibu sahihi kwa maswali yafuatayo:
(i). Andika methali inayofanana na "Jungu kuu halikosi ukoko."
(ii) Utatumia methali gani kumuonya mtu anayependa kuuliza sana maswali ili kuelewajambo?
(iii) Nini maana ya methali "Haba na haba hujaza kibaba?"
(iv) Baada ya kikao cha familia na wana ukoo tulimaliza msiba na kuanza safari. Ni nahau gani inafaa kwa maelezo haya?
(v) Ni kitendawili gani ambacho jibu lake ni MBARIKA?
4. Andika sentensi zifuatazo kwa usahihi. Hakikisha unaweka alama sahihi za uandishi na herufi kubwa.
(i) atu anaishi mkoa wa arusha
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
(ii). wanafunzi walitembelea mbuga za wanyama za mikumi manyara, na tarangire
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
(iii) lo mtoto ameanguka
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
(iv). shambani kwa babu kuna mazao gani
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
(v). shangazi alisema karibu mpwa wangu
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
SEHEMU E (Alama10)
UFAHAMU
5. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata kwa kuandika jibu sahihi katika nafasi iliyoachwa wazi.
Siku ya Jumatatu, Imani aliamka asubuhi na mapema kwenda shuleni. Njiani alikuta ajali ya mtu aliyeanguka na baiskeli. Alipoangalia kando ya barabara, alimuona mtu amelala chini. Alipoangalia pembeni yake, aliona tenga la nyanya na baiskeli. Usukani na gurudumu la mbele la baiskeli vilikuwa vimepinda. Baadhi ya nyanya zilizokuwa kwenye tenga nyingine zilikuwa zimesambaa barabarani. Imani alimuuliza kijana aliyeitwa Bakari, "Kaka kumetokea nini hapa?"
Yule kijana akamjibu. "Kumetokea ajali, mwendesha baiskeli nmeteleza na kuanguka" Imani alisikitika sana. Akauliza tena, "Je, ameumia?" Yule kijana akamjibu, "Sina uhakika ila amepoteza fahamu". Imani akauliza tena, "Mbona hamumpeleki hospitali?" yule kijana akajibu, "Ajali imetokea sasa hivi"
Imani aliendelea na safari ya kuelekea shuleni. Mbele kidogo alikutana na mwendesha pikipiki. Alimsimamisha na kumwueleza kuhusu mwendesha baiskeli aliyepata ajali. Akamuomba kama anaweza kwenda kumsaidia. Yule mwendesha pikipiki alikubali kwenda kumchukua na kumpeleka hospitali.
MASWALI
(i). Nani aliamka mapema kwenda shuleni
(ii). Ajali iliyotokea barabarani ilikuwa ni ya nini?
(iii). Nani aliulizwa na Imani kuhusu kilichotokea
(iv). Je. Imani ni mwanafunzi mwenye tabia gani
(v). Nani aliyemsaidia mwendesha baiskeli na kumpeleka hospitali
STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 6
STANDARD FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 6