FORM FOUR EDK TERMINAL EXAMS

OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA NUSU MUHULA - KIDATO CHA NNE 

015 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU 

(Kwa watahiniwa walioko na wasiokuwa shuleni)

Maelekezo

  1. Kratasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11).
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali mawili (2) kutoka sehemu C.
  3. Sehemu A ina alama kumi na sita (16), sehemu B alama hamsini na nne (54) na sehemu C ina alama thelathini (30).
  4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
  5. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
  6. Vifaa vya mawasiliano na vitu visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  7. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa karatasi zako za kujibia.

SEHEMU A (Alama 16)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Katika kipengele (i) – (x), chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake katika kijitabu chako cha kujibia.

i) Kwanini Waislamu wa leo wanapaswa kuipa elimu kipaumbele?

  1. Wapate kuitumia kutafuta riziki ya halali
  2. Ndio nyenzo kuu ya kuwa khalifa wa kweli
  3. Waweze kushiriki kwenye mambo ya kielimu
  4. Wawe wengi katika nafasi za kazi serikalini
  5. Kuleta ushindani na wawe wasio waislamu

ii) Umeombwa kuwaelezea wanafunzi wenzio kuhusu historia ya madhehebu ya Ki-Fiqh. Utachagua yapi kati ya haya kutekeleza jambo hilo?

  1. Ahlus Sunnah Wal Jamaa 
  2. Shia, Ibadh na Sunni 
  3. Hanbaliyah na Hanafiyah
  4. Salafus Swaleh na Bakwata
  5. Ahmadiyah na Ismailiyah

iii) Kosa gani walilofanya watu wa Madyan tu ambalo hadi sasa linafanywa?

  1. Kupunguza vipimo 
  2. Kufanya ufisadi 
  3. Uharamia njiani
  4. Uzinifu na ufuska 
  5. Kiburi na majivuno

iv) Mwalimu amekusimamisha useme ulichojifunza kutokana na maandalizi ya kimafunzo ya Mtume wa mwisho. Utasema lipi kati ya haya yafuatayo?

  1. Umuhimu wa Hadith za Mtume 
  2. Umuhimu wa historia 
  3. Nafasi ya dua katika Da’wa
  4. Ukombozi wa fikra kwa vijana
  5. Nafasi ya swala za Usiku

v) Bwana Mbundu ni mwanasayansi anayetaka kuanzisha mfumo wa maisha utakaowasaidia watu wote kuishi kwa raha kwa kutumia ujuzi wake, lakini akaambiwa hawezi kufanya hivyo. Kwanini bwana huyu asiweze?

  1. Kuna tafiti za kisayansi hajazikamilisha
  2. Nyenzo atakazozitumia haziwezi kumsaidia
  3. Hawezi kukubaliwa na wanasayansi wengine
  4. Anahitaji ujuzi mwingine baada ya huu alionao
  5. Anahitaji kushirikiana na wenzake na si peke yake

vi) Kwa ujumla kanuni zinazotumika kuweka sheria za Kiislamu hujulikana kwa jina gani?

  1. Usuul Thalathah 
  2. Usuul Hadith 
  3. Usuul Sunnah
  4. Usuul Fiqh 
  5. Usuul Ibada

vii) Bwana Ngugu ametokewa na jambo fulani mchana wa Ramadhani lakini

akaambiwa funga yake haijaharibika. Bwana huyu ametokewa na nini?

  1. Kutia nia ya kula tu
  2. Kunyweshwa dawa 
  3. Kutokwa na manii
  4. Kutapishwa na daktari 
  5. Kutia nia ya kunywa tu.

viii) Muandaaji wa sanda ya mtoto wa kike anapaswa kuzingatia jambo gani kati ya haya?

  1. Jinsia ya mtoto aliyefariki
  2. Kuwa na vipande vitano
  3. wepesi na aina ya kitambaa
  4. Kuwa na vipande vitatu
  5. Masharti na nguzo za sanda

(ix) imageNuun Sakna ) ((ن au (Tan wiin) inapokutana na Qaaf yenye fat-ha inapatikana hukumu gani?

  1. Iq-lab 
  2. Idh-har 
  3. Id-gham 
  4. Ish-mam 
  5. Ikh-fau

x) Bwana Ng’ombo anamiliki mbuzi na mbuzi 40. Baada ya kupinduka mwaka nini anapaswa kutoa kama Zakat katika hiki alichonacho?

  1. Mbuzi mmoja 
  2. Kondoo na mbuzi watatu 
  3. Kondoo mmoja wa miaka miwili
  4. Ndama mmoja
  5. Kondoo na mbuzi mmoja.

2. Oanisha maelezo ya shahada yaliyo katika Oradha A na aina za shahada zilizo katika Orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihih katika kijitabu chako cha kujibia.

ORODHA A

ORODHA B

  1. Kuishi kwa kufuata Qur’an na Sunnah.
  2. Kitambulisho cha Muislamu aliye sahihi.
  3. Hudhihirisha ualimu wa Mtume wa mwisho.
  4. Hupatikana kwa aliye na mapenzi ya dhati ya Allah na Mtume wake.
  5. Kuishi kwa kumtii Allah daima.
  6. Hupatikana faida ya kujua walioongezeka katika Dini ya Allah.
  1. Shahada ya moyoni
  2. Shahada ya matamshi
  3. Shahada ya kwanza
  4. Shahada ya kusilimu
  5. Shahada mbili
  6. Shahada ya ahadi
  7. Shahada ya matendo
  8. Shahada ya pili

SEHEMU B (ALAMA 54)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

Jibu maswali yote katika sehemu hii. Andika majibu yako kwa ufupi na ufasaha.

3. Wewe kama Muislamu unapaswa kuvifanyia nini viungo vyako vifuatavyo? 

  1. a) Kiwiliwili
  2. b) Mdomo na ulimi
  3. c) Mikono na miguu

4. Tumia hoja tatu kuwafafanulia wanajamii wa mtaani kwako ni kwa namna gani mahari inaweza kushusha hadhi ya mwanamke?

5. Umekutana na vijana watatu wanaotetea sheria zilizotungwa kwenye mabunge mbalimbali kuwa hazina kasoro.

  1. a) Waeleweshe vijana hawa chimbuko la sheria wanazozitetea.
  2. b) Tumia hoja nne kukosoa msimamo wao huu.

6. Wayahudi walifanya jitihada kubwa ya kuuzima Uislamu Madinah kwa kufanya vitimbi mbalimbali dhidi ya Dola na Waislamu. Wewe kama khatibu wa Ijumaa wafahamishe Waumini wa msikitini hapo mambo sita hayo ili waweze kuchukua tahadhari na wanaofanana na hao.

7. Umekaribishwa katika mjadala wa wasioamini siku ya mwisho kwa kutoa hoja zao mbalimbali. Wathibitishie ulazima wa kuwepo siku hiyo kwa kuwabainishia hoja tatu ili waondokane na fikra yao hiyo potofu.

8. Katika jamii ya Waislamu wapo watu wasiokubali ukhalifa wa Khalifa wa kwanza kwa kutokana na mitazamo tofauti juu ya uchaguzi wake. Tumia hoja mbili madhubuti kuwafafanulia waislamu hao mitazamo hiyo ili wasije kuingia kwenye makosa.

SEHEMU C (Alama 30)

Jibu maswali mawili (2) kutoka sehemu hii

9. Miongoni mwa hoja wanazozitumia wasio waislamu katika kuichafua Qur’an ni kudai kuwa ni kitabu cha mashairi ya Mtume Muhammad (Sallallahu Alayhi Wasallam). Toa hoja nne kuwadhihirishia watu hawa kuwa wanachokidai si sahihi.

10. Umealikwa kutoa semina kwa mahujaji watarajiwa juu ya utekelezaji wa ibada ya Hijjah. Waambie namna watakavyoweza kufikia kumpenda Allah kikwelikweli kwa kupitia utekelezaji wa ibada hiyo? (Hoja tano)

11. Mwalimu ameingia darasani kufundisha usahihi wa hadith za Mtume Muhammad (Sallallahu Alayhi Wasallam) kwa kuangalia matini yake. Atatumia hoja gani kuelezea mada hii? (Hoja tano)

FORM FOUR EDK EXAM SERIES 244  

FORM FOUR EDK EXAM SERIES 244  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256