FORM THREE KISWAHILI TERMINAL EXAMS

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA

NA SERIKALI ZA MITAA

JAMUHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA

MTIHANI WA MWISHO MUHULA

KIDATO CHA TATU

KISWAHILI 2023

Muda 2:30 

MAELEKEZO 

  1. Jibu maswali yote
  2. Mtihani huu una sehemu A. B na C (Jumla ya maswali 9)
  3. Simu za mkononi haziruhusiwi

SEHEMU A (15)

  1. Chagua herufi ya jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo katika sentensi (i) – (x)
  1. Pauka .............. Pakawa dhana hii hujihusisha katika aina gani ya vipera vya tanzu za fasihi simulizi?
  1. Tarihi
  2. Hadithi
  3. Vigano
  4. Ngano
  5. Masimulizi
  1. Maumbo ya mo, po, ye yanajulikana kama maumbo ya
  1. Mofimu
  2. Mofu
  3. O-rejeshi
  4. Fonimu
  5. Mofu huru
  1. Wataalamu wa simu ya lugha ya kiswahili wamekubaliana kwa dhana ya lugha imetoa fasili za kuzingatia isipokuwa
  1. Lugha ni kwa ajili ya binadamu
  2. Lugha ni sauti za nasibu
  3. Lugha ni mfumo maalumu
  4. Lugha hubadilika
  1. Nadharia gani? Yenye mashiko inayo chagua kunda asili y lugha ya kiswahili ni nini?
  1. Nadharia ya kibantu
  2. Nadharia ya kiarabu
  3. Nadharia ya kiajemi
  4. Nadharia ya kipijini na kikrio
  5. Nadharia ya kikongo
  1. Kipengele gani kinachohusu mjengo wa kazi za fasihi?
  1. Fani
  2. Maudhui
  3. Muundo
  4. Mtindo
  5. Fanani
  1. Mtoto wa muhammed Hussein alidondoka karibu na ukuta wa nyumba yao iliyojengwa kando ya barabara ya kuelekea kisutu. Maneno yaliyopigiwa mistari ni aina gani ya maneno
  1. Kihusishi
  2. Viunganishi
  3. Vielezi
  4. Vivumishi
  5. Vitenzi
  1. Shangazi yangu anapenda sana kurudia nomino katika muundo wa kiarifu anapokuwa akizungumza na wenzake, muundo huu hujulikana kama.
  1. Chagizo
  2. Yambua
  3. Kiyeyusho
  4. Hoponimu
  5. Shamilisho
  1. Neno nchi limeundwa na mfumo gani wa sauti?
  1. K + K + K + I
  2. I + I + I + K
  3. K + I + K + I
  4. K + K + K + K
  5. K + I
  1. Shamilisho katika uchanganuzi wa sentensi hutumia
  1. Kimapokeo
  2. Kimtindo
  3. Kisasa
  4. Kupatanisha
  5. Kisinteksia
  1. Mkazo katika mazungumzo ya kiswahili hutokea upande wa katika herufi ya?
  1. Upande wa kushoto herufi ya pili
  2. Upande wa kulia herufi ya kwanza
  3. Uoande wa juu herufi ya nne
  4. Upande wa chini herufi ya tano
  5. Upande wa kulia herufi ya tatu
  1.  

Kifungu A

Kifungu B

  1. Hadithi za kukejeli na kuchekesha
  2. Hadhithi za kuonya na maadili
  3. Hadithi za asili ya kitu (Umbo)
  4. Hadithi za matukio ya kihistoria
  5. Hadhithi za kuwaasa watoto juu ya maadili
  1. Ngano
  2. Visasili
  3. Soga
  4. Tarihi
  5.  
  6. Mizungu
  7. Vigano
  8. Lekebu
  9. Maghari
  10. Majigambo

 

SEHEMU B (ALAMA 55)

  1. Ni taarifa zipi zinazopatikana katika kiarifu hoja; kwa mfano
  2. Mtumiaji wa lugha ni bendera fuata upepo thibitisha kwa hoja nne (4)
  3. Bainisha mazingira manne ambapo O-rejeshi huweza kujipambania na kwa kila hoja tunga sentensi Moja
  4. Ondoa utata katika sentensi zifuatazo, kwa kutoa hoja mbili kwa kila sentensi
  1. Mtoto amelala na njaa
  2. Ana ametumwa na meshack
  3. Mwanafunzi amenunua mbuzi
  4. Kaka amekufa
  5. Ua limechanua
  1. (a)Wataalamu wa lugha ya kiswahili wanakubaliana kuwa kuna hatua za kuzifuata katika uchanganuzi wa sentensi ainishi hatua hizo hoja tano.

(b)Changanua sentensi zifuatazo kwa njia ya ngoe kwa 

  1. Mwalimu mkorofi amefika darasa
  2. Mama anapika chakula na baba analima shamba

SEHEMU C (30)

  1. Jifanye wewe ni muhitimu wa kidato cha nne mwaka 2022 umeliona na kusoma tangazo katika gazeti la mambo leo andika barua kwa mkurugenzi wa kampuni faidika limited SLP 111 Mwanza ya kuomba nafasi SLP 100 Mtwara.
  2. Kwa mifano kumi anishi tofauti kati ya barua kirafiki na barua ya kikazi.

FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 133  

FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 133  

 

WIZARA YA ELIMU SAYASI NA TEKNOLOJIA

SHULE YA SEKONDARI KIZUKA

MTIHANI WA MUHULA WA KWANZA

KISWAHILI - KIDATO CHA TATU

Muda: Saa 2:30                    

 

MAELEKEZO

  1.                   Karatasi hii ina sehemu A, B, na C jumla ya maswali kumi na mbili (12).
  2.                   Jibu maswali yote kutoka sehemu A na B na maswali matatu kutoka sehemu C.
  3.                   Sehemu A ina alama kumi na tano (15),  sehemu B ina alama arobaini (40) na sehemu C ina alama arobaini na tano.
  4.                   Zingatia maagizo ya sehemu na ya kila swali.
  5.                   Andika majina yako yote matatu kwa usahihi katika karatasi ya kujibia.
  6.                   Udanganyifu wa aina yoyote hautakiwi kwenye chumba cha mtihani.

 

SEHEMU A (Alama 15) 

Jibu maswali yote kutoka sehemu hii

  1.                   Chagua herufi ya jibu sahihi katika kipengele (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu hilo katika karatasi yako ya kujibia.
  1. Neno linaloingizwa katika kamusi kwa wino ulio kolezwa, fasili, matamshi na aina ya neno kwa pamoja huitwa?
  1.              Kidalizo
  2.               Kitomeo
  3.              Istilahi
  4.             Kategoria
  5.               Fasili

 

  1. Ni sehemu ya neno isiyobadilika baada ya kuondolewa viambishi awali na tamati.
  1.              Shina
  2.               Kitenzi
  3.              Mzizi
  4.             Kiambishi tamati
  5.               Nomino

 

  1. Jambo gani muhimu huzingatiwa na mtunzi wa insha ya hoja?
  1.              Lugha yenye ukinzani
  2.               Lugha ya kisanaa
  3.              Lugha inayosifia
  4.             Lugha ya kufukirisha
  5.               Lugha isiyo na mvuto

 

 

  1. Zifuatzo ni njia za uundaji wa maneno isipokuwa moja wapo.
  1.              Ufupisho wa maneno
  2.               Ukatizaji
  3.              Kupachika maneno
  4.             Urudufishaji
  5.               Kuambatanisha katika mzizi wa neno

 

  1. Yafuatayo ni matumizi ya simu za maandishi isipokuwa moja wapo.
  1.              Kutoa taarifa juu ya vifo
  2.               Taarifa juu ya ugonjwa
  3.              Kutumia salamu
  4.             Taarifa juu ya kujiunga na shule
  5.               Taarifa ya kufaulu mtihani

 

  1. Ni namna ambavyo msanii hutunga kazi ya fasihi na kuipa sura ambayo kifani na maudhui na kutofautiana na mwandishi mwingine.
  1.              Mtindo
  2.               Muundo
  3.              Mandhari
  4.             Matumizi ya lugha
  5.               Fani

 

  1. Ni aina ya ngeli ambayo huchukuwa upatanisho wa umoja na wingi wa sentesi na kujumuisha viumbe kama wanyama, binadamu, ndege na wadudu.
  1.              Ki-vi
  2.               Yu-A –WA
  3.              Li-YA
  4.             U-I
  5.               I-ZI

 

  1. Ni neno au mapangilio wa maneno ambao hudokeza taarifa fulani ambayo inaweza kuwa kamili au isiyo kamili.
  1.              Kishazi
  2.               Tungo
  3.              Sentensi
  4.             Neno
  5.               Kirai

 

  1. Ni aina ya sentensi inayoundwa na kishanzi tegemezi kimoja au zaidi au kishazi huru kimoja au zaidi
  1.              Sentensi huru
  2.               Sentensi changamano
  3.              Sentensi ambatano
  4.             Sentensi shurutia
  5.               Sentensi sahili

 

  1.             Ni mwana ushahidi wa kihistoria juu ya chimbuko la lugha ya kiswahili na alipata kuandika kuwa Zanzibar ni kivutio chenye ukubwa wa mzunguko wa maili 200 za mraba na wana utawala wao wa kifalme na watu hawalipi kodi.
  1.              Marco-polo
  2.               Al Idris
  3.              Al- Masoud
  4.             Morce
  5.               Historia ya mji wa Kilwa

 

 

  1.               Orodhesha maana za tamathali za semi na maneno mbalimbali katika Orodha A na B kisha andika herufi ya jibu sahihi.

ORODHA  A

ORODHA B

  1. Uhaishwaji wa kitu kisicho binadamu kupewa uwezo wa kutenda kama binadamu.
  2. Nihadithi zinazosimulia matukio ya kihistoria yaliyopita yanaweza kuwa ya kweli au ya kubuni.
  3. Ni aina ya lahaja iliyozungumzwa Tanga.
  4. Ni kipashio kidogo cha sarufi chenye kutoa taarifa kamili au isiyo kamili.
  5. Ushangaaji wa jambo fulani aghalabu huambatana na alama ya mshangao.
  6.  
  1.              Tashihisi
  2.               Kimtang’ata
  3.              Tarihi
  4.             Kingozi
  5.               Tashititi
  6.               Mofimu
  7.              Viambishi
  8.             Nidaa

 

 

 

SEHEMU B (Alama 40)

SARUFI, UTUMIZI WA LUGHA, MAENDELEO YA KISWAHILI

Jibu maswali yote katika sehemu hii

 

  1.               Andika tofauti nne (4) kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi.

 

  1.               Tunga sentensi au tungo moja kwa kila kipengele (i) – (iv) ukizingatia viambajengo vya kila kipengele.

 

  1.               Kisha tegemezi + kishazi huru
  2.             Kishazi huru
  3.          Kishazi tegemezi
  4.          Kishazi huru + kishazi huru

 

 

  1.               (a) Toa maana mbili za maneno yafuatayo:-
  1.               Paa             (ii) Mbuzi  (iii) Kanga   (iv)  Tai     (v) Kata

 

 

  1.               Kwa kutumia nomino zifuatazo tunga sentensi zenye upatanisho wa kisarufi na ukionyesha O-rejeshi kwa kupigia mstari chini yake.
  1.               Kalamu   (ii) Kiti     (iii) Ukuta (iv) Sufuria.

 

  1.               Kiswahili ni kibantu “thibitisha kwa kutumia vigezo vya kiisimu na kwa mifano

 

  1.               Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yafuatayo:-

 

Huwezi kuwazuaia, waliokubaliana

Mimi wananitumia, wapate kuelewana,

Kanuni wazingatia, ili kuwasiliana,

Sauti zangu nasibu, hakuna wa kukanusha

 

Mfumo wangu makini, Sauiti kupangilia,

Maneno kuyatumia, yenye mpangilio sawa,

Sentensi kuzitumia, mawazo kupangilia,

Sauti zangu nasibu, hakuna wa kukanusha

 

 

 

 

MASWALI

  1.               Mwandishi anazungumzia nini katika shairi ulilosoma?
  2.             Ni nini walikubalina kuwasiliana kwa hicho alichokizungumzia mwandishi katika ubeti wa pili?
  3.          Ni mambo gani matatu yaliyojumuishwa na mwandishi katika mfumo wa jambo analolizungumzia?
  4.          Unafikiri kwa nini mstari wa mwisho wa kila beti umerudiwa na mwandishi?

 

 

SEHEMU C (Alama 45)

Jibu maswali matatu (3) tu katika sehemu hii, swali la kumi (10) ni la lazima

  1.               Bi. Hilda alimweleza Bw. Agustino kuwa insha za kisanaa na insha za kiada ni sawa na ndugu wa tumbo moja, Japo kuwa Bw. Agustino hakukubaliana na maoni yake Bi. Hilda. Je wewe kama mwanafunzi mzuri ungetumia hoja gani kumuunga mkono Bw. Agustino? Toa hoja sita (6) zinazothibitisha kama kweli umemuunga mkono Bw. Agustino.

 

  1.          Bw. Lugusi alimweleza Bw. Asheri kuwa waandishi wa kazi za kifasihi hawajafanikiwa kuonesha ufaafu wowote ule wa kimaudhui katika kazi zao, ingawa Bw. Asheri alimkatalia kata kata Bw. Lugusi kutokana na uneni wake alionena. Je wewe kama mwanafunzi uliyefundishwa darasani na ulielewa ungetumia hoja zipi ili umuunge mkono Bw. Asheri. Toa hoja tatu (3) kwa kila diwani.

 

  1.          Bi. Isabela alimweza Bi Theresia Mushi kuwa mapenzi hayana upofu wowote ule miongoni mwa wanajamii. Ingawa Bi. Theresia Mushi hakukubalina na usemi alionena Bi. Isabela. Je wewe kama msomi mzuri wa kazi za fasihi andishi ungetumia hoja zipi ili uweze kumuunga mkono Bi. Theresia Mushi? Toa hoja tatu (3) kwa kila riwaya.

 

  1.          Bw. Mbuya alimfahamisha Bw. Mkway kuwa uwepo wa misigano katika kazi za kifasihi hakuwezi kung’amua malengo makuu ya waandishi asilia. Ingawa Bw. Mkway hakumkubalia Bw. Mbuya kutokana na usemi wake, je wewe kama mwanafunzi uliyemesoma tasnia hii ya fasihi kwa muda mrefu ungetumia hoja zipi ili umuunge mkono Bw. Mkway? Toa hoja tatu (3) kwa kila tamthilia.

 

 

 

 

FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 131  

FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 131  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

KISWAHILI KIDATO CHA TATU

MUDA: SAA 3:00        MAY  2022

 

MAELEKEZO

  1.                Karatasi hii ina sehemu A, B, na C, zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12)
  2.                Jibu maswali yote kama ilivyoelekezwa katika kila sehemu. A na B maswali matatu kutoka sehemu C
  3.                Sehemu A ina alama kumi natano (15), sehemu B alama arobaini (40) na sehemu C ina alama arobaini na tano (45)
  4.                Zingatia mwandiko mzuri, Mpangilio na usahihi wa majibu yako.
  5.                Majibu yote yaandikwe kwenye karatasi za kujibia.

 

 

SEHEMU A

Jibu maswali yote katika sehemu hii

  1.                Chagua herufi ya jibu sahihi katika kipengtele cha (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi ya kujibia
  1. Lugha huweza kuchukua maneno kutoka katika lugha za asili, baini maneno hayo katika orodha ifuatayo;
  1.              Bendera na meza
  2.               Bunge na shule
  3.               Hela na mtutu
  4.              Godoro na sharubati
  5.               Kitivo na ngeli
  1. Ipi ni aina ya tungo ambayo muudo wake una kitenzi ndani yake? Kitenzi hiko huweza kutoa taarifa kamili au isiyo kamili.
  1.              Kishazi
  2.               Kirai
  3.               Shamirisho
  4.              Yambwa
  5.               Sentensi
  1. Katika neon wanaimba, kuna viambishi vingapi?
  1.              4
  2.               8
  3.               3
  4.              5
  5.               6
  1. Ni mchakato wa uundaji wa maneno kwa kupachika viambishi kabla na baada ya mzizi wa neno.
  1.              Utohoaji
  2.               Uambishaji
  3.               Mnyambuliko
  4.              Uambatishaji
  5.               Urudufishaji
  1. Kitomeo huweza kuwa na taarifa kadha wa kadha. Je ipi kati ya zifuatazo si taarifa sahihi inayopatikana katika kitomeo?
  1.              Wingi wa neon
  2.               Aina ya neno
  3.               Mfano wa matumizi
  4.              Asili ya neno
  5.               Mnyumbuliko wa maneno
  1. Katika maneno choka na chako ni mbinu gani imetumika katika kuunda maneni hayo?
  1.              Uradidi
  2.               Uambishaji
  3.               Uhulutishaji
  4.              Mpangilio tofauti wa vitamkwa
  5.               unyumbulishaji
  1. Vipashio vya lugha hupangwa kidarajia kuanzia kidogo kwenda kikubwa katika mpangilio huo ni kipashio kipi kikubwa cha lugha?
  1.              Kirai
  2.               Neno
  3.               Sentensi
  4.              Kishazi
  5.               Sauti
  1. Kutokana na kigezo cha tabia muhusika JOTI ni aina gani ya mhusika?
  1.              Mhusika shida
  2.               Mhusika bapa
  3.               Mhusika foili
  4.              Mhusika mkuu
  5.               Mhusika duara
  1. Waingereza wanakumbukwa kwa mchango wao mkubwa kwa kufanya jambo moja la pekee tofauti na Waarabu na Waingereza katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili enzi za utawala wao, jambo gani hilo.
  1.              Kutoa elimu kwa lugha ya Kiswahili
  2.               Kusafirisha manamba kutoka sehemu mbalimbali na kuwa fundisha Kiswahili
  3.               Kuteua lahaja ya kiunguja na kuisanifisha
  4.              kuhimizA matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ofisi zao
  5.               kuchapisha kamusi mbalimbali za lugha ya kiswahili
  1. Ipi ni maana ya nahau “Uso mkavu”
  1.              Uso usio na mafuta
  2.               Uso usio na nuru
  3.               Uso usio na haya
  4.              Uso usio na shukurani
  5.               Uso wenye mabaka mabaka
  1.                Oanisha maana ya dhana zilizo katika ORODHA A kwa kuchangua herufi ya dhana husika katika ORODHA B

ORODHA A

ORODHA B

  1.                  Ngeli
  2.                Sentensi
  3.             Nomino za pekee
  4.              Neno lenye mofimu nne
  5.                Kiambishi cha nafsi ya pili wingi
  1.              Pangani, Asha, Usingizi na John
  2.               Anayesinzia ni mvivu
  3.               Chaki
  4.              PAMUKU
  5.               Wanaimba
  6.                Mnaimba
  7.              Mtoto
  8.              Chai
  9.                 Kariakoo, Tanga, Iringa na Ali
  10.                 Wewe ni mvivu

 

SEHEMU B (Alama 40)

Jibu maswali yote ya sehemu hii kwa kuzingatia maelekezo ya kila swali.

 

  1.                Taja mambo manne (4) yakuzingatia katika uandishi wa kumbukumbu za mikutano
  2.                Badili vishazi tegemezi vifuatavyo kuwa vishazi huru
  1.                  Mtoto aliyelia jana usiku
  2.                Kazi zinazofanywa
  3.             Jambo litakalomsumbua
  4.              Kitabu kinachosomwa
  1.                Kwa mwanafunzi anayeijua vizuri sarufi ya lugha ya Kiswahili ni rahisi kutambua makossa yanayotokea katika lugha. Kwa hoja nne (4) na mifano fafanua makossa ya kisarifi yanayojitokeza katika utumiaji wa lugha kwa mwanafunzi wa kitanzania.
  2.                Ainisha sentensi zifuatazo, kisha toa sababu moja (1) yaa uainishaji huo kwa kila sentensi.
  1.                  Mkate uliotupatia umeharibika
  2.                Sanga alikuwa amelala
  3.             Aliadhibiwa kwa kuwa alifanya makossa
  4.              Mwalimu akirudi tutaendelea na somo
  1.                “Licha ya lugha ya Kiswahili kuteuliwa kuwa lugha ya Taifa la Tanzania, bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali kwa sasa” Onesha ukweli wa kauli hiyo kwa hoja nne (4)
  2.                Vifuatavyo ni vipera vya tanzu za fasi simulizi. Onesha tofauti iliyopo baina ya jozi za vipera hivyo
  1.                  Visakale na visasili
  2.                Ngonjera na majingambo
  3.             Mizungu na misemo
  4.              Wimbo na utenzi

 

SEHEMU C (Alama 45)

Jibu maswali matatu (3) kutoka sehemu hii

 

  1.                Anna ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kibo. Alikutwa na simu licha ya katazo la serekali na shule kuwa hairuhusiwi mwanafunzi kumiliki simu akiwa shuleni. Baada ya kukutwa na simu hiyo alihojiwa na mwalimu wa nidhamu. Kwa kutumia ukurasa mmoja na nusu (11/2) andika namna mazungumzo yao yalivyokuwa. 

 

FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 90  

FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 90  

  OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA KWANZA

KIDATO CHA TATU

021KISWAHILI

(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

MUDA: SAA 3 MEI 2021


Maelekezo

1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).

2. Jibu maswali yote kutoka sehemu A, Bna chagua maswali matatu (03)kutoka sehemu C.

3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na kila swali.

4.Andika kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au nyeusi

5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa haziruhusiwikatika chumba cha mtihani.

6. Andika namba yako ya mtihani katika kila karatasi yako ya kujibia.

  1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele i-x kisha andika herufi ya jibu sahih katika kisanduku.
  1.  Ni neno lipi linalotoa taarifa kuhusu Nomino?

A: Kitenzi  B: Kielezi  C: Kivumishi

D: Kiwakilishi  E: Kiunganishi

(ii) Katika lugha ya Kiswahili kuna aina ngapi za Vitenzi.

 A: Mbili  B: Tano  C: Sita

 D: Tatu  E: Nne

(iii) Maneno yapi kati ya haya yafuatayo yametokana na lugha ya Kibantu.

  A: Kitindamimba ba bendera   B: Hela za mtoto

  C: Kitivo na ngeli    D: Godoro na sharubati

  E: Bunge na Shule

(iv) Ni mambo gani muhimu ya kuzingatia katika kuteua maneno na miundo 

    ya tungo wakati wa mazungumzo.

   A: Mada, muktadhia wa mazungumzo ya aina kwa nia

    B: Mada, mazungumzo na uhusiano wa wazungumzaji

   C: Mada, mzungumzaji na muktadha wa mazungumzo 

   D: Mada, mzungumzaji na uhusiano wa wazungumzaji

   E: Mada, muktadha na uhusiano wa wazungumzaji.

(v)  Bainisha kauli unayoonyesha dhima muhimu za vitendawili katika jamii za 

    vitendawili katika jamii.

     A. Kuhimiza umoja na mshikamano.

    B. Kupanga watu katika marika yao.

    C. Kuchochea udadisi wa mambo

  D. Kuchochea uwongo wa mambo.

  E. Kukosoa wadadisi wa mambo.

(vi) Njia mojawapo ya kuzuia utata katika lugha ya mazungumzo ni ipi kati ya zifuatazo?

 A. Kuepuka makosa ya kisarufi na kimantiki

 B. Kutumia neno lenye maana zaidi ya moja 

 C. Kutumia kiwakilishi kiambata katika neno 

 D. Kuweka msisitizo au ufafanuzi zaidi

 E. Kutumia misimu sahihi za wakati.

(vii) ‘’Wanafasihi hutumia wahusika wenye mienendo hiyo’’ katika tamthiliya ulizosoma, ni wahusika wapi kati ya wafuatao wana mienendo isiyokubalika?

 A. Joti, Ngoswe na Mama Furaha

 B. Padri James, Ngoswe na Baba Anna.

 C. Mazoea, Mama Furaha na Joti

 D. Ngoswe, Baba Anna na Suzi

 E. Ngoswe, Joti na Padri Jamaes

(viii) Kati ya sababu zifuatazo ni ipi si sahihi kuhusu matumizi ya Kamusi?

 A. Kujifunza Lugha ya Kigeni

 B. Kusanifisha maneno mapya

 C. Kubaini kategoria ya neno

 D. Kujua maana za maneno

 E. Kujua tahajia za maneno.

(ix) Ni methali ipi inayokinzana na methali ‘’Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.’’

 A. Manahodha wengi, chombo huenda mrama.

 B. Palipo na wengi, hapaharibiki neno

 C. Haba na haba, hujaza kibaba.

 D. Kidole kimoja, hakivunji chawa

 E. Fimbo ya mnyonge, ni umoja 

(x) Upachikaji wa Viambishi katika mzizi wa neno huitwaje?

 A. Mnyambuliko  B. Utohoaji  C. Uambishaji

 D. Viambishi   E. Kukopa maneno  

  1. Oanisha maana za maneno kutoka orodha A kwa kubainisha dhama zilizoko katika

Orodha B na uandike herufi ya jibu sahihi pembeni na swali.

ORODHAA

ORODHAB

(i) Tungo shurutia ukwasi

A. Rejesta ya Tanga

(ii) Kimtang’ata

B. Angeliniita ningeitika

(iii) Malaika, Shetani, Mzimu

C. Lahaja ya Kiswahili

(iv) Juzi asubuhi

D. Nomino za mguso


E. Njeo ya ya wakati wa mazoea


F. Nomino za dhahania


G. Kirai kielezi


H. Utajiri

SEHEMU B: (ALAMA 40)

Jibu maswali yote kutoka sehemu hii

  1. Bainisha mzizi asilia kwa kila neno katika maneno yafuatayo.

(a) Anawaandikisha

(b) Mkimbizi

(c) Mlaji

(d) Muumbaji

(e) Nisingelipenda

(f) Kuburudika

(g) Sadifu

(h) Aliokota

(i) Walichopoka

(j) Kipambanuliwe.

  1. Bainisha matumizi mbalimbali ya ‘’KWA’’ katika sentensi zifuatazo

(a) Amejificha kwa kuwa hapendi anione

(b) Kukataa kwa Mwajuma kumesababisha matatizo mengi.

(c) Amelima shamba kwa jembe

(d) Ameenda kwa Mwalimu

(e) Amesafiri kwa ndege

  1. Kwa kutumia mfano taja njia tano za uundaji wa maneno.
  2. Toa maana mbili katika tungo tata zifuatazo?

(a) Pili alimwandikia barua Asha

(b) Wizi wa Silaha umeongezeka

(c) Mwalimu ameijia fedha yake

(d) Mtoto amelalia uji

(e) Mama amenuena Mbuzi

  1. Taja mambo matano ya kuzingatia wakati wa utunzi wa Insha na ueleze umuhimu wa kila jambo.
  2. Eleza tofauti za msingi tano, zilizopo baina ya varua ya kikazi na barua za kindugu.

SEHEMU C: (ALAMA 45)

Jibu maswali matatu tu toka sehemu hii

  1. Eleza sababu tano zilizosaidia kuenezza Kiswahili wakati wa utawala wa Wajerumani.
  2. Fasihi ni Chuo chenye kufundisha kila mwanajamii husika. Thibitisha hoja hiyo kwa kutumia vitabu viwili vya riwaya ulivyosoma. Toa hoja tatu kwa kila Kitabu.
  3. Mashairi huburudisha na kuliwaza pale yanapoimbwa au kusomwa lakini nayatoa mafunzo mazuri sana kwa jamii husika. Jadili kauli hii kwa kutumia Diwani mbili ulizosoma. Toa hoja nne kutoka kila diwani.
  4. Siku zote katika jamii, migogoro ndiyo inayoibua dhamira mbalimbali. Thibitisha dai hili kwa kutumia tamthiliya mbili ulizozisoma ukitoa hoja tano kwa kila kitabu.

1

FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 55  

FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 55  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256