JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU-TAMISEMI
MTIHANI WA MUHULA WA KWANZA KIDATO CHA TATU MEI
MSIMBO: 015 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU
Muda: Saa 3
MAELEKEZO
SEHEMU A (Alama 16)
Jibu maswali yote kutoka katika sehemu hii
1. Katika kipengele (i) – (x) chagua jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye karatasi ya kujibia.
(i) “Amemfundisha mwanadamu mambo aliyokuwa hayajui.” (96:5). Aya hii inathibitisha kitu gani?
(ii) Firauni katika Maisha yake alikuwa akikanusha uwepo wa Allah (S.W), lakini siku alipokuwa anazamishwa baharini akakiri uwepo wake. Ni jambo gani lilimfanya kutambua hilo?
(iii)Watu wa Nabii Lut (A.S) waliangamizwa kutokana na maovu mbalimbali. Maovu gani utakayowakataza watu wa jamii yako ili wasikutwe na yaliyowakuta watu hawa?
(vii) Ukiwa unaongoza swala ya maiti unatakiwa ufanye nini baada ya kumswalia Mtume Muhammad (S.A.W)?
(viii) Umemkuta rafiki yako ameghadhibika kiasi cha kutaka kumdhuru aliyemghadhibisha. Utamsihi afanye nini ili aondokane na hali hiyo?
(ix) Ikiwa umemkuta mtu anayejuta kwa kuua bila ya kukusudia utamshauri afanye nini kwa mujibu wa Uislamu?
(x) Wakati gani Ijtihad inatumika kama msingi wa sheria ya Kiislamu?
| ORODHA A | ORODHA B |
|
|
SEHEMU B (Alama 54)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
3. Katika kongamano la wazazi Sheikh Mundele alitakiwa kuwasilisha mada ya malezi ya Watoto kimaadili. Bainisha dondoo tatu atakazoweza kuzitumia Sheikh huyu katika kufikisha mada yake hii.
4. Uislamu baada ya kuenea na kuongoza sehemu mbali mbali, ilikuwa ndio mwanzo wa kukomesha biashara ya utumwa na kumkomboa mwanaadamu kiutu, (kiroho), kifikra na kisaikolojia. Thibitisha kauli hii kwa kutumia hoja sita.
5. Maisha ya furaha na amani ya kweli hupatikana kwa kusimama misingi ya haki na Uadilifu katika jamii. Bainisha misingi hiyo kwa kutumia hoja tatu.
6. ‘Kwa hakika Kitabu cha Qur’an hakikaribiwi na batili mbele yake wala nyuma yake.’Kwa mujibu wa kauli hii, toa tofauti tatu kati ya Qur’an na Vitabu vilivyotangulia.
7. “Kwa hakika shirki ni dhulma kubwa” Qur’an (31:13). Kutokana na aya hii, onesha kina cha uovu wa shirki kwa mwenye kushirikisha.
8. Suala la kuamini kuwepo Mwenyezi Mungu si la ububusa na kufuata mkumbo, bali linahitaji ushahidi na dalili. Thibitisha kauli hii kwa kutoa sababu kuu sita.
SEHEMU C (Alama 30)
Jibu maswali mawili tu katika sehemu hii
9. Utafiti uliofanyika katika maeneo mbalimbali umebaini kuwa wapo Waislamu wanaoswali lakini bado wanashiriki katika kufanya maovu mbalimbali. Wewe kama mtaalamu wa Elimu ya Dini ya Kiislamu bainisha sababu tano zinazoweza kupelekea hali hii ili watu wachukue tahadhari na kuiepuka.
10. Katika hukumu za Kiislamu baada ya Qur’an kigezo kinachofuata ni Hadith sahihi za Mtume Muhammad (S.A.W). Wabainishie watu wa Msikitini kwako sifa tano zinazoitofautisha na aina nyingine za kigezo cha usahihi ili watu waweze kufanyia kazi mafundisho yaliyo sahihi tu.
11. Eleza kwa hoja tano kwanini Khalifa Uthman bin Affan (r.a) alinakili upya Quran kutoka kwenye Msahafu wa Mtume(s.a.w) baada ya kufariki kwake.
FORM THREE EDK EXAM SERIES 276
FORM THREE EDK EXAM SERIES 276
OFISI YA WAZIRI MKUU-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA MUHULA KIDATO CHA TATU
ELIMU YA DINI YA KIISLAMU
MUDA: SAA3:00 MEI 2026
SEHEMU A (ALAMA 20)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1.Chagua herufi ya jibu sahihi kisha andika katika kisanduku (i)sanda ya watoto wadogo wakike na wakiume ambao hawajafikia baleghe ina majamvi mangapi? ni
(ii)Uislamu ndio dini ya pekee inayostahiki kuchaguliwa na kufuatwa kama mwongozo sahihi wa maisha na watu kwa sababu?
(iii)Zifuatazo ni aina za shirki isipokuwa.
(iv)mojawapo ya kazi za malaika ni ......
(v)Zaburi ni kitabu alichoteremshiwa nabii......
(vi)mambo anayo fanyiwa mtu mara baada kufa ni..........
(vii)Mtu aliyeelimika anatofautiana vipi na yule ambaye hajaelimika?.
(viii)Kwa mujibu wa uislamu ,kwanini haiwezekani mtu kuishi bila kuwa na dini?.
(ix).Njia ipi inakamilisha kupatikana kwa jitihaad kama msingi wa sheria za kiislamu.
(x) Ni yapi makusudio ya kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan?
2.Oanisha sentensi katika orodha A na maneno katika orodha B kisha jaza herufi yake katika karatasi ya kujibia.
| Orodha A. | Orodha B |
| (i)kutembea baina ya vilima viwili vya saffa na marwa mara saba. (ii)Kuwatii kwa kufuata maamurisho yao na kuacha makatazo yao na kuacha makatazo yao katika kila kipengele cha maisha ya kibinafsi na kijamii. (iii).Shafii ,Abuhanifa ,Ahmed bin Hambal na Malik. (iv).Wala siabudu mnachokiabudu ,wala nyinyi hamuabudu ninaye mwabudu . (v).Kuzunguka kaa'ba mara saba. (vi).Huyu ni yule ambaye ananyanyasa yatima ,wala hajihimizi yeye wala wengine katika kuwalisha masikini. |
|
SEHEMU B. (Alama 64).
jibu maswali yote katika sehemu hii
3.(a)Tofautisha elimu yenye manufaa na elimu isiyo na manufaa.
(b)kwanini uisilamu umeipa elimu nafasi ya kwanza? toa hoja tatu
4.Kwanini uislamu ndio dini pekee inayostahiki kuchaguliwa na kufuatwa kama mwongozo sahihi wa maisha. toa hoja tano
5.Mwanadamu pamoja na ujuzi alionao hawezi kujiundia mfumo (dini)sahihi wa maisha .Thibitisha kauli hii kwa hoja tano.
6.Ainisha matunda yatakayopatikana kwa uislamu kusimama na kuongoza maisha jamii. toa hoja nne tu.
7.Bainisha dalili tano zinazothibitisha uwepo wa Allah (s.w) pasina shaka yeyote.
8. (a).Taja sifa tano za malaika wa Allah(s.w).
(b).Bainisha kazi tatu za malaika wa Allah (s.w).
SEHEMU C (ALAMA 20)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
9."Mungu hayupo kwasababu milango ya fahamu haitambui " hii ni kauli ya Charles Darwin na wenzake juu ya kupinga uwepo wa mungu muumba.Onyesha madai yao na madhaifu ya kila dai.
10. Suala la kuamini kuwepo Allah (s.w) si la kibubusa na kufuata mkumbo bali linahitaji ushahidi na dalili za kielimu .Thibitisha kauli hii kwa kutoa sababu kuu tano.
FORM THREE EDK EXAM SERIES 275
FORM THREE EDK EXAM SERIES 275