JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI MUHULA WA KWANZA KIDATO CHA PILI
060 HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI
Muda: Masaa 2:30 Mei 2026
MAELEKEZO
SEHEMU A (ALAMA 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
1. Chagua jibu sahihi katika vipengele (i) – (x) kisha andika herufi ya jibu sahihi kwenye jedwali ulilopewa hapo chini.
i. Mzee Mpenda Ukweli alitaka kujua ni kwanini wanafunzi katika shule za Tanzania wanasoma somo la Historia ya Tanzania. Alipowauliza kidato cha pili walimpa jibu lifuatalo:
ii. Mwanafunzi Juhudi alisoma kuhusu vyama vya ushirika vya wakulima vilivyo anzishwa kabla ya uhuru. Je vyama hivyo vilikua na lengo gani?
iii. Katika makundi ya jamii za asili zaTanzania, ni kundi moja tu ambao ndio wazawa wa Tanzania waliokutwa na jamii nyingine. Kundi hilo ni:
iv. Msichana aitwaye Elizabeth aliambiwa na mwalimu ataje vitendo vyenye maadili ambavyo hutendwa na wanafunzi wenzake awapo shuleni. Majibu aliyotoa ni haya yafuatayo isipokuwa:
v. Kwa mujibu wa wanafalsafa mbalimbali, neno 'Jamii' lina maana gani?
vi. Mkutano wa kimataifa uliofanyika nchini Ujeruman katika mji wa Berlin mwaka 1884-1885 ukiongozwa na Otto Von Bismark ulifanyika kwa lengo gani?
vii. Ni aina gani ya elimu ilikuwa ikitolewa katika jamii za Kitanzania kabla ya ujio wa kikoloni?
viii. Wakati Wajerumani na Waingereza wanaitawala Afrika mashariki walitoa huduma ya elimu kwa waafrika. Hii ilikua na maana gani?
ix. Ashura anawadharau wenzake kwasababu wanatoka familia masikini. Kitendo cha Ashura kuwa na tabia hii kinakiuka maadili yapi kati ya haya yafuatayo?
x.…..ni hali ya mtu au nchi kuamua na kufanya mambo yake bila kuingiliwa na mtu au taifa lolote.
Majibu
| i | ii | iii | iv | v | vi | vii | viii | ix | x |
| . |
2. Oanisha maelezo yaliyopo katika Orodha Ana dhana zilizopo katika Orodha Bkwa kuandika herufi ya jibu sahihi.
| Orodha A | Orodha B |
|
|
Majibu
| Orodha A | i | ii | iii | iv | v |
| Orodha B |
SEHEMU B (ALAMA 70)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
3. a) Eleza maana ya dhana “Mfumo wa ukoo”
b) Taja na eleza kwa kifupi sifa kuu nne (04) zilizozingatiwa ili mtu ateuliwe kuwa kiongozi wa ukoo.
4. Ujenzi wa maadili katika jamii sio tukio la siku moja bali kuna mifumo mbalimbali ya kijamii inayosaidia. Fafanua mifumo ya kijamii inayohusika kujenga maadili kabla ya ujio wa wakoloni katika jamii za kitanzania
5. Tunapaswa kufahamu kuwa ujio wa wakoloni uliathiri nyanja nyingi katika jamii za kitanzania hivyo jamii nyingi za kiafrika zilipinga ili kuhifadhi na kulinda maadili, uchumi, utawala na tamaduni zao. Eleza sababu zilizosababisha mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
6. Jamii za asili ya kitanzania zilihama kutoka sehemu na kwenda maeneo mengine kutokana na sababu mbalimbali. Mueleweshe mwanafunzi wa kidato cha kwanza sababu hizo. Hoja tano
7. Ukiwa kama mwanafunzi wa kidato cha pili na mbobezi wa somo la Historia ya Tanzania na Maadili. Elezea utofauti wa mfumo wa elimu ya jadi na mfumo wa elimu ya sasa. Hoja tano
8. Katika mapambano dhidi ya uvamizi wa wakoloni, jamii za Kitanzania zililenga kulinda maadili yao. Bainisha maadili ya jamii za kitanzania yaliyodumu licha ya ushawishi wa utawala wa kikoloni kuyafuta. Hoja tano.
9. Taja na eleza kifupi mbinu zilizotumika kudai uhuru wa Tanganyika na Zanzibar katika kipindi cha kwanza kwanzia mwaka1900 mpaka 1944. Hoja tano (05)
SEHEMU C (ALAMA 15)
Jibu swali namba 10
10. Tanzania ina utajiri mkubwa wa urithi wa asili, ambao huwapa manufaa makubwa wanajamii na Taifa kwa ujumla. Waeleweshe watanzania umuhimu huo kwa kutumia aina mbalimbali za urithi wa asili
FORM TWO HISTORIA EXAM SERIES 253
FORM TWO HISTORIA EXAM SERIES 253