OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA KUMALIZA MUHULA KIDATO CHA KWANZA
KISWAHILI
MUDA: SAA 2:30HRS MEI: 2025
MAELEZO
Karatasi hii inajumuisha sehemu A, B, na C.
Jibu maswali yote katika sehemu A, B na C.
Jibu maswali yote katika nafasi uliyoachiwa.
Simu za mkononi, vikokotoo na nyenzo zozote za kompyuta haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.
Maandishi yote lazima yawe katika kalamu ya mpira ya bluu/mweusi isipokuwa michoro ambayo lazima iwe kwenye penseli.
Andika nambari yako ya mtihani kwenye kona ya juu kulia ya kila ukurasa.
SEHEMU A (ALAMA 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
(i) Ipi kati ya Tungo zifutazo si dhima ya lugha katika mawasiliano?
Kutambulisha utamaduni
Kutumia mpangilio maalumu wa sauti
Kuunganisha watu
Kurithisha amali za jamii
Kupashana habari
(ii) Vipengele vipi vya lugha kati ya vifuatavyo hubainisha utamaduni wa Mtanzania?
Unasibu, salamu, mavazi
Vyakula, kilimo, mavazi
Nyimbo, unasibu, mavazi
Salamu, mavazi, vyakula
Mavazi, unasibu, vyakula
(iii) Ni jambo gani muhimu katika kufasili lugha kati ya mambo yafuatayo?
Mfumo wa sauti za nasibu
Mfumo wa kutamka
Mfumo wa kuwasiliana
Mfumo wa kuelezea matukio
Mfumo wa mazungumzo ya kawaida
(iv) Ipi kati ya zifuatazo ni sababu ya kuzingatia lugha na utamaduni wake?
Kuweza kutamka kwa usahihi
Kuweza kuwasiliana kwa usahihi
Kuweza kutamka lafudhi yake kwa usahihi
Kuweza kuburudika vizuri
Kuweza kuunganisha watu
(v) Ipi kati ya zifuatazo ni fursa itokanayo na lugha ya Kiswahili?
Kuwatambulisha watu
Kuwafundisha watu wa mataifa mbalimbali
Kurithisha amali za jamii
Kuburudisha jamii
Kuwakusanya watu katika jamii
(vi) Kumbo na Kapelo walikuwa wanabishana kuhusu muundo wa sentensi. “ Mimi nitafua na wewe utaosha vyombo”. Upi ni muundo sahihi wa sentensi hiyo?
E T U W T N
W T U W T E
W T U W T N
V T U W T E
N T U W T N
(vii) Ipi si dhima mojawapo ya kiimbo kati ya hizi zifuatazo?
Kubadili maana ya neno
Kuuliza swali
Kusisitiza jambo
Kuonesha hisia
Kubadili maana ya tungo
(viii) “Mama alinunua vyombo vizuri. Vizuri vyote viliwekwa kabatini. Mimi nilivipanga vizuri”. Katika mfuatano wa sentensi hizo, neno vizuri limetumikaje?
Kiwakilishi, kivumishi, kielezi
Kivumishi, kielezi, kiwakilishi
Kielezi, kivumishi, kiwakilishi
kiwakilishi, kielezi, kivumishi
Kivumishi, kiwakilishi, kielezi
(ix) Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo ina makosa ya kimatamshi?
Kaka amefua nguo
Osha sahani uliyolia chakula
Suedi amenunua kanga
Eva amenunua kanga
Joni amempigia mpila Asha
(x) Upi si umuhimu wa kuzingatia ushikamani wa sentensi katika aya?
Kuleta maana ya sentensi katika aya
KUfanya aya iwe ndefu
Kuleta uhusiano wa kimaana
Kuonesha ushikamani wa kimawazo
Kuleta mtiririko wa mwanzo
2. Oanisha dhana zilizopo katika Orodha A na maelezo yaliyopo katika Orodha B kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.
Orodha A
Orodha B
(i) Utambulisho wa jamii
(ii) Tafsida
(iii) Utamaduni
(iv) Lugha
(v) Mawasiliano
Tamathali ya semi inayoficha au kupunguza ukali wa neno.
Hueleza mambo yatokanayo na utamaduni wa Mtanzania.
Upashanaji wa habari au taarifa kwa njia ya mazungumzo, maandishi na ishara.
Makubaliano ya pamoja baina ya wazungumzaji.
Mwenendo wa maisha unaohusisha asili, mila na desturi na jadi unaotumika katika jamii fulani.
Hueleza sifa bainifu za jamii fulani.
Mfumo wa sauti za nasibu unaotumia maneno yanayosemwa na binadamu ambao huwawezesha watu wa jamii fulani kuwasiliana.
SEHEMU B. ALAMA 70.
JIBU MASWALI YOTE
3. Eleza umuhimu wa kulinda na kuheshimu utamaduni wa Kitanzania.
4. Bainisha maneno yenye makosa ya kimatamshi katika sentensi zifuatazo kwa kuyapigia mstari, kisha andika sentensi hizo kwa usahihi.
Mwanafunzi anayejitambua hapendagi mzaha katika masomo.
Shule yetu ina vifaa vya samani.
Mti uliokuwa kalibu na bustani ya maua umeanguka.
Mzee Kiza amedhuru mbuga za wanyama.
5. Matumizi ya kiimbo husaidia kubainisha lengo la mzungumzaji. Fafanua malengo ya mzungumzaji katika sentensi zifuatazo:
Mwanafunzi anasoma kwa bidii.
Mwanafunzi, soma kwa bidii.
Mwanafunzi anasoma kwa bidii?
Mwanafunzi anasoma kwa bidii!
6. Kamilisha sentensi zifuatazo kwa kutumia maneno uliyopewa katika kisanduku.
gari, mwema, wao, shambani, ili, aisee, katika, si, pikipiki, kwa
Mwanafunzi anatakiwa kusoma vitabu vingi................kupata maarifa.
..................lake limeharibika.
Mtoto....................huwaheshimu watu wote.
...............wamemaliza kazi yao kwa wakati.
Mkulima amepanda mazao mengi..................
...............! Kijana huyu anajituma sana.
Maki........................mtundu.
Babu anapenda kupumzika.......................bustani ya maua.
7. Utata usababishwa na mambo mengi. Toa maana mbili katika maneno yafuatayo na weka mfano mmoja kwa kila maana.
Kanga
Ua
Pamba
Mbuzi
Kata
8. Badilisha nomino zifuatazo kuwa vitenzi
Wimbo
Umbo
Kilio
Mtoro
Mlo
9. Kwa kuzingatia lafudhi na matamshi sahihi, bainisha maneno yenye makossa katika sentensi zifuatazo
Nimepata ujumbe wa simu wenye taarifa mbaya _______________
Ntoto wangu anaumwa ____________
Rafiki yangu naja ______________
Ama kweri elimu haina mwisho ________________
Kurara badara ya kutafuta kazi ya kufanya kunasababisha maisha kuwa magumu _________________
10. Wananchi wa kijiji cha Fungafunga wanasifika kwa utaalamu wa kuchonga vinyago kutokanana na uwepo wa misitu katika kijiji cha Fungafunga. Ukiwa kama Afisa misitu tumia hoja sita (6) kuwaeleza wananchi wa kijiji cha Fungafunga kuhusu umuhimu wa misitu kwa kutunga insha isiyozidi maneno 250 .
Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani
SEHEMU A (Alama 30)
Chagua herufi ya jibu sahihi miongoni mwa majibu kisha andika herufi ya jibu hilo
Asha ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Iringa sauti zake hazina maana anapoziunuma hujumuisha kama?
Lugha ya maneno
Lugha ya kiswahili
Lugha ya Ishara
Lugha ya mazungumzo
Kila mwandishi huwa na ufundi wake katika utunzi wa kazi za fasihi zake je? Jambo gani ambalo hutofautiana maandishi Janeth na Mwandishi Simba katika utuzi wa kazi zao
Mwandiko
Mtindo
Muundo
Lugha
Mwalimu wa somo la kiswahili huwa anatufundisha kando ya daraja letu. Neno lililopigiea mstari ni gani ya maneno aina gani ya maneno?
Kiunganishi
Kielezi
Kutokana na wataalamu wa lugha ya kiswahili katika fasihi la neno wanakubaliana kuwa lugha ni sauti za nasibu kwa nini?
Lugha ni nyenzo ya mawasiliano
Binadamu huchagua lugha ya kuongea
Hakuna tofauti kati ya kiwe na kirejelewe
Majibu yote hayo ni sahihi
Ni utaratibu wa kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti wakati wa mazungumzaji
Kiimbo
Lafidhi
Mkazo
Nyimbo
Kaka mkuu wa shule yetu alituelekeza kuwa chura katika ngozi yake ina mabaka mabaka pia hupendwa kuishi majini kuliko nchi kavu. Je hiyo ni hadhithi zinazohusu?
Visasili
Vigano
Ngano
Tarihi
Ni umbo la ndani la kazi ya fasihi ambalo hueleza Msanii kwa yale yote aliyokusudia katika kazi yake.
Fani
Dhamira
Mtindo
Maudhui
Dhana gani ya mtu wa kaskazini na nyanda za juu kusini, hudokeza utambulisho wa maneno yanayotoka?
Sauti
Lafudhi
Matamshi
Silabi
Othuman anaishi tanga. Neno Tanga ni aina gani ya neno?
Neno sikukuu limeundwa na silabi ngapi?
8
5
4
3
Misamiati iayoingizwa katika kamusi na kukolezwa wino, pia kutoa taarifa ya msamiati hiyo kama vile aina ya neno, asili na namna neno linavyoandikwa.
Kitomeo
Kidahiao
Sampuli
Kisevo
Oanishi sentensi zenye matumizi ya vielezi katika Orodha A na aina ya vielezi katika Orodha B. Kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.
Orodha A
Orodha B
Daktari amenishauri ninywe daiwa kutwa mara tano
Mchezaji wa timu yetu alipiga mpira chini
Kaka mfupi amepita polepole
Mimi sijawahi kusherekea mahafali tangu mwaka jana
Kitenzi cha mujibu
Kitenzi cha namna
Kitenzi cha wakati
Kitenzi cha mahali
Kitenzi cha idadi
SEHEMU B (ALAMA )50
Panga maneno kama kwenye kamusi na toa maana na tunga sentinsi kwa kila neno.
Ua
Panga
Chizi
Baba
Panda
Fasihi maana ya misamiati ifuatayo
Maghani
Fanani
Lugha
Sanda
Kamusi
(a)Ainisha tanzu za fasihi simulizi
(i) _______________(ii) _______________
(iii) ______________(iv) _______________
(b) Kwa kila tanzu tajwa hapo juu bainisha tanzu hizo za fasihi simulizi, zimejengwa na vipera vipi? Kwa kila tanzu ainisha hoja tano.
SEHEMU C (ALAMA) 20
(a) Toa maana ya Soga
(b) Jifanye wewe ni kiongozi wa michezo katika shule yenu, umechaguliwa kishiriki mashindano ya utungaji wa hadithi shindano linahusu sungura na fisi yenye maneno thamanini tu (80) Andika soga yenye maneno themanini tu (80)
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA
MUDA: SAA 2:00 2022
MAELEKEZO.
Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E.
Jibu maswali yote kama ilivyoelekezwa katika kila sehemu.
Zingatia mwandiko mzuri, Mpangilio na usahihi wa majibu yako.
Majibu yote yaandikwe kwenye karatasi za kujibia.
SEHEMU A UFAHAMU (Alama 10)
Soma kifungu cha habari kifuatacho kasha jibu maswali yafuatayo.
Aaah! Maskini ya Rabiee! Hii ndiyo nchi tuliyomo sisi!.Nchi inayovuja jasho ,nchi masikini, nchi ambayo wanawake huvaa nguo _ _ _ _! Nchi ambayo wanawake huvaa nywele za maiti_ _ _Haya ndiyo maendeleo yetu_ _ _ _.
Haki na usawa katika nchi masikini ni ndoto. Wengi huamua kuwa mabubu mara tu deemokrasia inapopokonywa na watu wachache. Huu ni Unafiki mkubwa.Haki haipo nchini mwetu ila tu tumefumbwa macho, Tumekuwa Vipofu.
Mimi nimeamua kupambana, nitachukua panga_ _ _ nitachukua pinde _ _ _ nitachukua mishale _ _ _ nitapigana kufa na kupona. Nitapigania haki na usawa.Haki! Haki! Usawa Haki! Haki_ _ _ _ maana yake nini.
MASWALI
Andika kichwa cha habari hii _______________________________________________
Je mwandishi analaani juu ya nini? ______________________________________
Taja matatizo manne ambayo mwandishi anayakemea
_____________________________________________
_____________________________________________
_____________________________________________
_____________________________________________
d)Haki na usawa vitapatikana kwa njia gani? ______________________________
e)Andika maana ya maneno yaliyopigiwa mstari.
Inapopokonywa.
Unafiki.
Vipofu.
SEHEMU B (Alama 30)
UTUMIZI WA LUGHA.
Kwa kutumia mifano toa maana ya maneno yafuatayo.
Kidahizo.
Kitomeo.
Kamusi.
Lugha.
Sherehe
(a) Kwa kutumia matumizi ya Kiswahili sanifu, sentensi zifuatazo zina makosa. Ziandikwe upya kwa ufasaha.
Kwa mfano
Kiti mkubwa amevunjika.
Usahihi- Kiti kikubwa kimevunjika.
Chai imeingia nzi.
Anakwenda baba kesho safari.
Humwambiaga lakini haelewi.
Ng’ombe zangu zimeibiwa.
Daktari nina kifua sijalala usiku kucha.
(b)Andika athari tano za kutotumia lugha kwa ufasaha.
(a) Taja matumizi Matano (5) ya kamusi.
(b)Kamusi hugawanyika katika sehemu ngapi? Zitaje.
(c)Taja mambo mawili yanayopatikana katika utangulizi wa kamusi.
SEHEMU C: (Alama 20)
SARUFI
(a) Kitenzi kikuu huweza kutumika sambamba na kitenzi kingine kukamilisha sentensi. Kwa kuandika upya sentensi katika karatasi uliyopewa, Bainisha vitenzi vilivyotumika katika sentensi zifuatazo.
Mfano
- Amina alikuwaanakula chakula kitamu.
TsT
Mgeni wangu amekwisha wasili.
Amina hakutaka kumuhudhi.
Mafundi wote wanashona viatu.
Wataendelea kumsubiri hadi kesho.
Gari lilikuwa limeharibikia mlimani Kitonga.
(b)Ainisha maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo.
Viti vizuri viwili vimevunjika.
Ah! alitaka kuja shuleni.
Wewe ndiye ndugu yangu.
Wachezaji wote walifanya mazoezi ya viungo.
Ndizi hizi zimeoza.
(a) Tunga sentensi moja kwa kila neno lililoandikwa kwa hati mcharazo.
Vizuri kama kiwakilishi.
Vizuri kama kivumishi.
Vizuri kama kielezi.
Mama kama Nomino.
Mama kama kihisishi.
(b)Tunga sentensi zenye miundo ifuatayo:-kwa kupigia mstari sentensi hiyo kuonesha aina hizo
za maneno.
Mfano:N+T + E =
Mamaanapikajikoni.
NTE
H + N + T + E
N + V + V + TS + Ts + T
W + t + N + V
W + V + T
T
SEHEMU D: (Alama 30)
FASIHI
(a) Sanaa ni nini?
(b)Nakili kisha ukamilishe kielelezo kifuatacho.
(a)Fasihi ina dhima/kazi mbalimbali katika jamii. Taja tano (5) na uzieleze kwa ufupi.
(a)Taja vipengele vitano (5) vinavyounda Fani katika kazi ya fasihi.
(b)Taja vipengele vitano (5) vinavyounda Maudhui katika kazi ya fasihi.
SEHEMU E: (Alama 10)
UTUNGAJI.
10.Mwandikie barua rafiki yako umweleze kuhusu hali halisi ya masomo ilivyo shuleni kwenu.
zingatia taratibu za uandishi wa barua za kirafiki katika uandishi wako.