OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA ROBO MUHULA WA PILI KIDATO CHA TATU
021 KISWAHILI
(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)
Muda: Saa 3:00 Mwaka: 2026
Maelekezo
SEHEMU A (Alama 16)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
1. Katika vipengele (i) hadi (x), chagua herufi ya jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo katika kijitabu cha kujibia ulichopewa.
(i) Upatanisho wa kisarufi hutambulisha ngeli za nomino kwa kuzingatia viambishi awali vya maumbo ya:
(ii) ………………… ni tungo yenye neno moja au zaidi inayotoa taarifa fulani kwa kujikita katika neno kuu.
(iii) Obogo alifurahi alipopata maswali yote ya Kiswahili. Neno lililopigiwa mstari ni:
(iv) Kimapokeo, nomino inayojitokeza upande wa kiarifu inaitwa?
(v) “Kiswahili kilianzia kaskazini mashariki mwa Kenya”. Huu ni mtazamo unaoeleza chimbuko la Kiswahili kwa mujibu wa wataalamu wafuatao:
(vi) Lahaja ya kimtang’ata inazungumzwa wapi kati ya maeneo yafuatayo?
(vii) ………… ni kipengele kimojawapo katika fani ambacho humtofautisha mwandishi mmoja na mwingine.
(viii) Mashairi yenye mishororo miwili katika ubeti huitwa?
(ix) Ni tamathali ipi ya semi inayohusu ulinganishaji wa vitu tofauti bila ya kutumia maneno ya ulinganishaji au viunganishi?
(x) Ubantu wa lugha ya Kiswahili hudhihirika katika vipengele vifuatavyo isipokuwa:
2. Oanisha maelezo yaliyo katika orodha A na dhana husika katika orodha B kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi kisha uiandike katika kijitabu chako cha kujibia.
| ORODHA A | ORODHA B |
|
|
SEHEMU B (Alama 54)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
3. (a) Kila siku baba na mama wamekuwa wakigombana. Hali hii husababishwa na mama kushindwa kutumia lugha vizuri. Wewe kama mtoto msomi katika familia, eleza mambo matano (5) yanayomfanya mama kushindwa kuelewana na baba.
(b) Pwaguzi alimwambia Pwagu kuwa kiswahili ni kibantu. Pwagu alibisha na kudai kuwa Kiswahili ni kiarabu. Ungana na Pwaguzi kutetea hoja yake. Toa dondoo nne (4).
4. Kwa kutumia mifano, taja dhima sita (6) za viambishi awali.
5. Miongoni mwa mambo muhimu katika kuchochea maendeleo ya jamii ni kufahamu idadi ya watu katika jamii husika. Kwa kureja tamthilia ya “Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe”, onesha changamoto nne (4) walizokumbana nazo watu walioteuliwa kuendesha zoezi la sensa ya mwaka 2022 nchini Tanzania.
6. (a) Katika uandishi wa matangazo kuna mambo kadha wa kadha ya kuzingatia. Eleza mambo hayo kwa kutoa dondoo tano (5).
(b) Uongozi wa Kampuni ya Azam umetangaza kuwa kampuni inahitaji mwandishi bora wa matangazo ambaye atahusika kuandaa matangazo mbalimbali. Baada ya kuomba kazi iliyotangazwa umepewa jukumu la kuandaa tangazo kuhusu “Unga wa ngano wa Azam” kama kipimo cha kupata kazi. Onesha umahiri wako kuthibitisha kuwa utapata kazi hiyo.
7. (a) Uainishaji wa vipashio mbalimbali vinavyoijenga sentensi hufuata sheria inayohitaji mtiririko sahihi. Onesha mtiririko huo kwa kutoa hoja tano (5).
(b) Ainisha vipashio vinavyojenga sentensi hii “Anacheza”. Tumia mkabala wa kimapokeo.
8. “Ujio wa wageni nchini Tanzania ulididimiza maendeleo ya Kiswahili”. Kwa hoja sita (6), fafanua sababu zilizochangia kukua na kuenea kwa Kiswahili nchini Tanzania enzi za wajerumani.
SEHEMU C (Alama 30)
Jibu maswali mawili (2) kutoka sehemu hii. Swali la tisa (9) ni la lazima
USHAIRI
Wasakatonge - M.s Khatibu (DUP)
Malenga Wapya - TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya Chekacheka - T. A Mvungi (EP & D Ltd)
RIWAYA
Takadini - Ben Hanson (MBS)
Watoto wa Maman’tilie - E. Mbogo (H.P)
Joka la Mdimu - A. J Safari (H.P)
TAMTHILIYA
Orodha - Steve Raynolds (MA)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. semzaba (ESC)
Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)
9. Washairi hupenda kutumia jazanda wakiwa na lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii. Thibitisha hilo kwa kutumia diwani mbili ulizosoa huku ukitoa hoja tatu (3) kwa kila moja.
10. Watanzania wa leo wangefaidika sana na tamthiliya kama wangekuwa na utamaduni wa kuzisoma. Thibitisha kauli hii kwa kutumia vitabu viwili kati ya vilivyotajwa hapo juu. Toa hoja tatu (3) kwa kila kitabu.
11. “Waandishi wa kazi za fasihi huibua migogoro mbalimbali na kupendekeza masuluhisho ili kuelimisha jamii husika. Thibitisha kauli hiyo kwa kutoa hoja tatu (3) kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.
FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 278
FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 278
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MITIHANI YA KUJIPIMA KWA SEKONDARI
MTIHANI WA NUSU MUHULA WA PILI
KISWAHILI KIDATO CHA TATU
MUDA: MASAA 3 AUG 2023
MAELEKEZO
1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C
2. Jibu maswali yote sehemu A na B na maswali 2 sehemu C
3. Zingatia maelekezo ya kila swali
SEHEMU A (ALAMA 16) JIBU MASWALI YOTE.
1. Chagua jibu sahihi katika vipengele (i-x) kisha andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi ya kujibia.
i. Huyu ni mwanafunzi hodari sana. Je “ni” ni aina gani ya neon.
a) Kitenzi shirikishi
b) Kiunganisha
c) Kitenzi kisaidizi
d) Kielezi cha wakati
ii. Njia ipi ni ya uhifadhi wa fasihi simulizi inayoweza kupokea mabadiliko kwa haraka kati ya hizi
a) Maandishi
b) Vinasa sauti
c) Kichwa (d)Kanda za video
iii. Tofauti ndogondogo zinazojitokeza katika lugha moja huitwa
a) Kimtang’ata
b) Lugha za kikanda
c) Lahaja
d) Kiimbo
iv. Wazo kuu la mtunzi katika kazi ya fasihi huitwa
a) Ujumbe
b) Dhamira
c) Falsafa
d) Mtazamo
v. -------------- ni maneno yasiyo sanifu yayozuka na kutoweka
a) Misimu
b) Rejesta
c) Msamiati
d) Kishazi tegemezi
vi. Kisawe cha neno umaskini
a) Ukwasi
b) Ubahili
c) Ujima
d) Ukata vii. Ni neno pamoja na taarifa zake kwenye kamusi huitwa
a) Kidahizo
b) Kitomeo
c) Msamiati
d) Muundo
viii. Utofauti wa kazi za kifasihi toka muandishi mmoja dhidi ya mwingine husababishwa na
a) Mtindo wa kazi
b) Dhamira za kazi za fasihi
c) Migogoro ya kazi husika
d) Muundo wa kazi ya fasihi
ix. Moja ya sifa kuu ya kirai ni
a) Kukaa sehemu yeyote katika sentensi
b) Hakina muundo wa kiima na kiarifu
c) Hutoa maana kamili
d) Huwa na muundo wa kiima na kiarifu
x. Neon lipi kati ya maneno haya linaweza kudokeza mtenda au mtendwa wa jambo
a) Kiunganishi
b) Kihisishi
c) Kielezi
d) Kivumishi
2. (a) Oanisha dhana katika orodha A kwa kuchagua herufi ya dhana husika kutoka orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika karatasi ya kujibia.
| ORODHA A | ORODHA B |
| I. Tungo shurutia II. Kosa la mpangilio mbaya wa viambishi III. Maneno yasiyo sanifu yanayozungumzwa na kikundi kidogo cha watu IV. Viambajengo vya sentensi V. Sehemu ya nchi kavu iliyochongoka na kuingia baharini VI. siataimba | A. Ghubu B. Mpegani C. Ukanushi D. Anampigia pasi E. Rasi F. Ukimwonw ndani ya gari utamlipia nauli G. Kiima na kiarifu H. Simo I. Misemo J. jakabu |
SEHEMU B (ALAMA 54)
3. Wewe ni mwanafunzi wa shule ya sekondari Mazinyungu iliyopo Morogoro.
Umepokea barua kutoka kaka yako aitwaye Amani Furaha anayeishi Tabora S.L.P 300 pamoja na kukujulia hali amekueleza vipi wanavyoendelea huko kwenu Tabora. Pia ametaka uwajulishe ni lini utakwenda huko Tabora. Kutokanaa na ratiba ya shule kukubana unatarajia kwenda utakapofunga shule mwezi Septemba mjulishe kwa kutumia simu ya maandishi jina lako liwe Tusekele Amani.
4. Kw kutoa hoja nne na mifano eleze jinsi matumizi ya picha na michoro yanavyosaidia matumizi ya kamusi.
5. (a) toa dhana ya sentensi
(b) sentensi za Kiswahili hujipambaua kwa sifa zake (taja 3).
(c) changanua sentensi zifuatazo kwa mkabala wa kimuundo na kimapokeo
(i) watu wote walimsikilza Rais (kwa njia ya matawi)
(ii) wao wanaimba lakini sis tuanacheza ngoma (kwa njia ya jedwali)
6. (a) nini maana ya mzizi wa neon
(b) Onesha mizizi ya maneno yafatayo
(i) Salisha
(ii) Onesha
(iii) Onyana
(iv) Mpiganaji
(c) Eleza maana ya istilahi zifuatazo
(i) Sarufi
(ii) Kitomeo
(iii) Lugha
(iv) Kielezi
7. Kwa kutumia mifano toshelezi toa uthibitisho wa kiisimu wa Kiswahili ni kibantu.
8. Kwa kuzingatia maumbo ya umoja na wingi tunga sentensi mbili kwa kila ngeli zifuatazo
(a) YU-A-WA
(b) KI-VI
(c) U-ZI
(d) I-ZI
(e)LI-YA.
SEHEMU C (ALAMA 30)
JIBU MASWALI MAWILI KUTOKA SEHEMU HII
9. Ujio wa waarabu ulisaidia sana kukuza lugha ya Kiswahili. Thibitisha kauli hii kwa hoja zisizopungua nne (4).
10. Wanaisimu huona kuwa fasihi simulizi ni bora kuliko fasihi andishi. Kwa kutumia hoja tano (5) thibitisha ukweli huu.
11. Methali zinafunza na zinaweza kupotosha jamii zisipotumika kwa ukamilifu kwwa kutumia methali tano (5) thibitisha kila moja inayoweza kufunza na kupotosha.
FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 148
FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 148
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
KIDATO CHA TATU 2021
MSIMBO: 021 KISWAHILI
MUDA: SAA 3:00 AUG 2021
MAELEKEZO
SEHEMU A {Alama 15 }
Jibu maswali yote
| ORODHA A | ORODHA B |
|
|
SEHEMU B (Alama 40)
Chanjo haipatikani Ulaya hakukaliki,
Tiba haijulikani, Dunia haifurukutu,
Korona ni maafa kujikinga lazima,
Mafua, homa kupanda utaona uki”gugo”,
China mpaka mpanda, korona haina vigo,
Korona ina maafa kujikinga lazima
Karantini kwa wotee, makapera wameoa,
Mabinti wasiopenzini, huu msimu wa ndoa
Korona ina maafa kujinginga lazima
Wanandoa walishane penzi bila taabu,
Nao wapenzi wachanga, wasubiri janga lipite
Korona ina maafa kujikinga lazima
Elimu tazingatia Wizara wanakumbushia,
Tunawe yetu mikono, epuka msongamano
Koroana ina maafa kujikinga lazima
MASWALI
SEHEMU C (Alama 45)
Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii
ORODHA YA VITABU
USHAURI
Wasakatonge - M.s Khatibu (DUP)
Malenga wapya - Takiluki (DUP)
Mashairi ya chekacheka - T. A Mvungi (EP & D. LTD)
RIWAYA
Takadini - Benj. Hanson (MBS)
Watoto wa mama ntiliye - E. Mbogo (H.P)
Joka la mdimu - A.J Safari (H.P)
TAMTHILIYA
Orodha Steven Reynolds (MA)
Ngoswe penzi kitovu cha uzembe -E. semzaba
Kilio chetu -Medical Aid foundation
Page 1 of 4
FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 65
FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 65
THE PRESIDENT'S OFFICE
MINISTRY OF REGIONAL GOVERNMENT AND LOCAL GOVERNMENT
AUGUST-SEPTEMBER EXAMINATION SERIES
KISWAHILI FORM-3
2020
TIME: 2:30 HRS
Maelekezo
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo katika kijitabu chako cha kujibia.
(i) Neno lipi kati ya maneno haya linaweza kudokeza mtenda au mtendwa?
(ii) Shamba letu li kubwa neno “Li” ni aina gani ya neno?
A fonolojia, mofolojia, semantiki na sintaksia
B maana, matamshi, muundo na maumbo
C maana, matamshi, muundo na mantiki
D kiimbo, shada, mkazo na toni
E. fonolojia, mkazo, shada na semantiki
(iv) Kamati ya lugha ya Afrika ya Mashariki (the interteritorial Swahili language committee) iliteua lahaja moja na kuisanifisha, lahaja hiyo ilikuwa ni
A kimvita
B kiunguja
C kimtang’ata
D kisiu
E kivumba
(v). Watoto hawa wanacheza vizuri neno “Vizuri” ni aina gani ya neno?
(vi) Kiswahili ni kibantu kwa kuwa:-
(vii) Ni jambo gani linalodhihirisha upekee wa kazi fulani ya kifasihi?
(vii) Ipi ni fasili sahihi kuhusu tungo?
(viii) Nini maana ya sentensi sahili.
(ix) Zifuatazo ni sifa za pijini isipokuwa
A. Pijini huwa na maneno kutoka lugha mbili au zaidi
B. Pijini hutokea kurahisisha mawasiliano baina ya watu ambao kila mmoja
ana lugha yake
C. Miundo ya maneno na tungo katika pijini imerahisishwa ili kukidhi
mawasiliano
D. Pijini haina msamiati mwa kutosha, hivyo wazungumzaji hutumia sana
ishara
E. Pijini ina watu ambao kwao hiyo ni lugha yao ya kwanza
2. Katika kila sentensi uliyopewa, orodhesha vishazi huru katika Safu A na vishazi tegemezi katika safu B.
(a) Ngoma hailii vizuri kwa kuwa imepasuka.
(b) Watoto walioandikishwa watakuja kesho.
(c) Kiongozi atakayefunga mkutano amepelekewa taarifa.
(d) Mtawatambua walio wasikivu.
(e) Kitabu ulichopewa kina kurasa nyingi.
3. Taja aina za sentensi zifuatazo kisha eleza muundo ujengao kila sentensi.
4. Andika maneno matano ambayo yameundwa kutokana na kufananisha sauti. Kwa kila neno tunga sentensi moja.
5. Eleza dhima za mofimu "li" kama ilivyotumika katika sentensi zifuatazo:
6. Andika sentensi zifuatazo katika hali ya ukanushi:
7. Bainisha mzizi wa asili kwa kila neno katika maneno yafuatayo:
1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Karibu masikio ya watu wa mahali pengi yalijaa habari za Karama na mashtaka yake. Umaarufu wake wa ghafla ulizungumzwa karibu na mbali. Mtu yeyote wa desturi anapozuka katika umaarufu, huyavuta masikio na macho ya watu wengi kwa sababu jambo kama hili hutokea nadra sana kwa watu ambao bahati mbaya imeshughulika kuwaweka nyuma. Kwa hiyo, siku ya tatu ya baraza ilihudhuriwa na mfalme, watu wenye vyeo mbalimbali, pamoja na nusu moja ya umati mkubwa wa Kusadikika. Fikra zilizochanganyika ziliushika umati huu. Baadhi ya watu walimwajabia Karama wakamhesabu kama mtu bora wa karne yao. Hawa walitumaini ataokoka lakini wengine waliwaza kuwa Karama alikuwa kama mjinga aliyekuwa akicheza na hatari kubwa iliyofunua taya mbele yake.
Waliokuwa wakimtazamia kuokoka walikuwa na wasiwasi wao; na wale waliokuwa wakimtazamia kuanguka walikuwa na fadhaa yao. Walakini hapana mtu hata mmoja aliyepata kulisema wazo lake.
Bila ya kujua alivyoajabiwa Karama aliendelea kusema mbele ya baraza, “Watu wanaoteswa ndio wanaoyajua mateso yao.” Kusadikika ilikuwa chini ya mateso makubwa sana. Maisha yao yalizungukwa na maradhi na mauti, uadui usiokwisha, nchi iliyokaribia kugeuka jangwa na mwamba na madhila mengine mazito yaliyowakabili watu. Wanakusadikika walitaka faraja katika mateso haya. Kila jitihada ilijaribiwa ili kuirekebisha saa ya maendeleo ya nchi, lakini mara kwa mara majira yake yalirudishwa nyuma. Kama hili lilifanywa kwa makosa ama kwa makusudi ni siri iliyo ng’ambo ya fahamu zangu hata sasa. Lakini kama siri njema hufichika, ile iliyo mbaya haifichiki hata kidogo. Uchaguzi wa wajumbe ulikuwako lakini hathibitisho ya matokeo ya ujumbe hayakupatikana.
Kusadikika iliishi kuona mjumbe baada ya mjumbe kuadhiriwa na kuadhibiwa vibaya. Kama washauri hawakudhuriwa na hili lakini watu wengine walidhuriwa sana. Kazi njema za wajumbe wawili zilipotea bure. Manung’uniko ya lawama hii yalikuwa katika hewa yote ya Kusadikika.
Hili lilipotokea serikali iliombwa ima faima kufanya ujumbe mwingine. Basi mjumbe wa tatu alitakikana ajitolee mwenyewe kwa ujumbe wa Kusini. Wito wa mjumbe wa tatu uliitikiwa na Kabuli; mtu mwenye busara, haya na mcheshi. Yeye alipatikana upesi kabisa kuliko ilivyokuwa kwa mara ya pili na ya kwanza. Misiba ya Buruhani na Fadhili ilikuwa mikubwa ya kutosha kuikongoa mioyo ya bidii katika bawaba zake. Kabuli aliyajua haya yote lakini alikuwa mtu wa moyo wa namna nyingine kabisa. Alikuwa na bidii kubwa kama ile ya siafu athubutiye kukivuka kijito kwa daraja iliyofanywa kwa maiti ya siafu wengine walioelea majini huko na huko. Maji yalijulikana kuwa na asili ya rutuba, mvuke na umeme. Nguvu nyingine za namna mbalimbali zipo pia katika maji. Kama siafu mdudu mdogo na kipofu wakati mwingine haogopi kuzikabili nguvu hizo pamoja na hatari zake kwa sababu njema, basi ni dhahiri kuwa viongozi wa wanadamu wanapoteswa bure bidii za wafuasi wao hutanuka ajabu.
Hapana tishio liwezalo kuukomesha mwendo huu. Kwa hakika utafululiza kuwako duniani mpaka mateso yakome kabisa, na labda wakati huo dunia hii itakuwa njema kama itamaniwavyo kuwa.
Buruhani na Fadhili walitoa sadaka zao bora ili kuyahimiza majilio ya wakati uliotakikana sana. Kabuli aliwaona watu wawili hawa kama wafadhili wakubwa wa ulimwengu. Alitaka kuwa mshirika wao kwa thamani yoyote ya maisha yake.
Kama ilijulikanavyo, Kusini na upande wa dunia yatokako matufani makubwa na baridi kali sana. Kabuli aliyakabili mashaka haya bila ya kigeugeu. Naam, alikuwa kama mtu aliyekuwa akinywa uchungu bila ya kigegezi. Mara mbili alikamatwa akafanywa mahabusu.
Maswali
(a) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu cha habari:
(b) Eleza mchanganyiko wa fikira walizonazo wana wa Kusadikika kuhusu Karama.
(c) Kwanini bidii ya mjumbe wa Kusini imelinganishwa na bidii ya siafu? Toa sababu mbili.
(d) Ujumbe wa mwandishi wa kifungu hiki unahusu nini?
SEHEMU C (Alama 45)
Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii.
8. Andika insha isiyozidi maneno mia tatu (300) na isiyopungua mia mbili na hamsini (250) kuhusu faida za televisheni kwa jamii.
ORODHA YA VITABU USHAIRI
Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP)
Malenga Wapya - TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya Chekacheka - T.A. Mvungi (EP & D.LTD)
RIWAYA
Takadini - Ben J. Hanson (MBS)
Watoto wa Maman’tilie - E. Mbogo (H.P)
Joka la Mdimu - A.J. Safari (H.P)
TAMTHILIYA
Orodha - Steve Reynolds (MA)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)
Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)
10. "Fasihi ya Kiswahili imemweka mwanamke katika hadhi tofauti tofauti." Thibitisha usemi huu kwa kutumia hoja tatu kwa kila riwaya kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.
11. (a) Vigano ni nini?
(b) Tunga vigano kwa kutumia methali isemayo "Umdhaniaye siye kumbe ndiye!"
FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 28
FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 28