FORM ONE HISTORIA MIDTERM-2 EXAMS

Jina La Kamili ________________________________________

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA NUSU MUHULA

KIDATO CHA KWANZA

HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI

SAA: 2:30 September, 2026

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10).
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A B na C.
  3. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali.
  4. Simu za mikononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  5. Andika Jina lako kamili katika kila ukurasa wa mtihani.

SEHEMU A (ALAMA 15)

Jibu maswali yote kutoka sehemu hii

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele vyote (i) – (x) kisha andika herufi ya jibu hilo katika kisanduku cha kujibia ulichopewa.

(i) Godfrey ni mtoto mwenye maadili mazuri awapo nyumbani na shuleni. Ni tabia gani hatutegemei kuiona kwa Godfrey?

  1. Kuasaidia wenzake katika masomo
  2. Kuwasalimia wakubwa zake
  3. Kuvaa mavazi ya heshima
  4. Kutupa takataka barabarani

(ii) Utafiti wa kihistoria unaonesha chimbuko la wamasai ni wapi?

  1. Kusini mwa sudani
  2. Pwani ya Afrika mashariki
  3. Afrika ya magharibi
  4. Mwanzon mwa bonde la mto nile

(iii) Historia inaonesha jamii za Kitanzania zimeishi kwa amani toka enzi na enzi, hii ni kutokana na:

  1. Mabadiliko ya kisiasa
  2. Ushirikiano na mshikamano
  3. Ukosefu wa makaazi
  4. Vita vya kikabila.

(iv) Somo la historia ya Tanzania na maadili hufundisha kuhusu mwenendo wa shughuli za kiuchumi kama kilimo, utalii na uvuvi. Hii inaonesha uhusiano na somo gani?

  1. Kilimo
  2. Hisabati
  3. Jiografia
  4. Sayansi

(v) Nieneo gani kati ya haya yafuatayo ni sehemu ya urithi wa kihistoria na wakati huohuo ni urithi wa maliasili?

  1. Kalambo
  2. Amboni
  3. Kaole
  4. Engaruka

(vi) Ni namna gani jamii za Kitanzania zinaweza kuimarisha maadili ya ukarimu kwa wageni?

  1. Kwa kuwafukuza wageni kwa sababu ni mzigo
  2. Kwa kuwakaribisha wageni na kuwapa heshima na huduma bora
  3. Kwa kujitenga na wageni na kutowasaidia
  4. Kwa kuwazuia wageni kuingia nchini.

(vii) Watu wa jamii za asili za kitanzania walitumia bidhaa gani kutengeneza nguo?

  1. Majani ya miti na ukindu
  2. Vitambaa vya hariri na kaki
  3. Manyoya ya ndege, pamba na sufi
  4. Magome ya miti na Ngozi za wanyama

(viii) Kwa nini ni muhimu kwa mwanafunzi kuelewa historia ya Tanzania?

  1. Ili kujua matukio ya kihistoria ya mataifa mengine yanayofanana na historia ya taifa letu
  2. Ili kujua maadili ya mataifa mengine yanayohusiana na maadili ya taifa letu
  3. Ili kujua njia za kuepuka historia ya nchi yetu
  4. Ili kuelewa mabadiliko ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ya taifa letu.

(ix) Uhusiano kati ya historia ya Tanzania na maadili ni nini katika kujenga utambulisho wa taifa?

  1. Historia inatufundisha kuhusu matukio ya kisiasa tu
  2. Historia inasaidia kutambua na kuthamini maadili ya taifa
  3. Historia haihusiani na maadili
  4. Historia inajikita katika maadili ya watu wa mataifa mengine.

(x) Katika hali ya kushirikiana na kusaidiana, ni namna gani maadili yanaweza kuathiri ustawi wa jamii?

  1. Yanahamasisha ushirikiano, kusaidiana na kujenga jamii imara
  2. Yanazuia watu kusaidiana
  3. Yanachochea ubinafsi na kudumisha migawanyiko
  4. Yanachochea migogoro na kutokuwa na Amani

Majibu

i ii iii iv v vi vii viii ix x










2. Oanisha maelezo ya Orodha A na urithi wa kihistoria na wa asili katika Orodha B, kisha andika herufi ya jibu sahihi katika jedwali lililopo chini.

ORODHA A  ORODHA B
  1. Urithi wa asili.
  2. Mfano wa urithi wa kiutamaduni.
  3. Urithi usioshikika.
  4. Huthibitisha eneo kuwa urithi wa kiutamaduni na kiasili.
  5. Urithi unaoshikika.
  1. Mila na desturi
  2. Majengo
  3. Vyanzo vya maji
  4. Beid al Ajaib
  5. UNESCO
  6. Kutii sharia
  7. Wakichembe

Majibu

Orodha A i ii iii iv v
Orodha B




SEHEMU B (Alama 70)

Jibu maswali yote kutoka sehemu hii

3. Mulayka ni binti wa kisasa asiyeona umuhimu wowote wa kutunza vitu vilivyoachwa na jamii za kale wala kuiga mazuri yao kwani zama zao ni tofauti na zama hizi. Mfungue akili kwa kudokeza mambo matano yanayojumuisha urithi wa kihistoria katika jamii za watanzania ili asiwe na Imani potofu.

4. Jumanne alipokuwa akiangalia televisheni alivutiwa sana na kauli mbiu ya Safari channel inayosema “Tumerithishwa, tuwarithishe” lakini haoni faida ya kurithishwa urithi wa kihistoria. Muelekeze kwa kumuonyesha jinsi makundi yafuatayo yanavyoweza kufaidika na urithi wa kihistoria.

  1. Mtu binafsi (hoja moja)
  2. Jamii (hoja mbili)
  3. Taifa (hoja mbili)

5. Elimu nip ana sana. Mfumo wa elimu ya kijadi haukuwa na kwenda darasani wala kuvaa sare. Je ulijikita katika mambo gani?

6. Haijalishi nani anafanya nini, wapi na wakati gani katika Maisha atakuwa amegusa mfumo mmoja katika Maisha yaani kisiasa, kiuchumi au kijamii. Dhihirisha shughuli za kiuchumi zilizokuwa kabla ya ukoloni.

7. Kwa kutumia hoja tano, fafanua sifa za kuchaguliwa kiongozi katika jamii za wabantu

8. Ni dhahiri shahiri kwamba somo la historia na maadili ni geni kwa walio wengi wakiwemo wazazi wako. Wewe kama mmoja ya waliobahatika kusoma somo hili. Wafafanulie wazazi wako majukumu matano ya kiongozi katika jiamii za wabantu na wakichembe

9. Jamii zetu kwa sasa zimegubikwa na mambo mengi, changamoto mbalimbali zinawakabili wanajamii. Kwa kuzingatia hili, dokeza mambo Matano ambayo ni kikwazo katika ujenzi wa maadili mazuri katika jamii yako ya sasa.

SEHEMU C (Alama 15)

Jibu swali la kumi (10)

10. “Mja asili haachi asili, akiacha asili si mja asili”. Onesha kukubaliana na kauli hii kwa kuelezea hoja sita kuonyesha fursa zinazopatikana kutokana na urithi wa kiasili.

FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 289  

FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 289  

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA ROBO MUHULA AGOSTI

HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI

KIDATO CHA KWANZA 

MUDA: SAA 2:30 

MAAELEKEZO 1

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moaja(11)
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali mawili (2) kutoka sehemu C ambapo swali la tisa (9) ni la lazima
  3. Zingatia maelekezo ya kila sehemu ya kila swali

SEHEMU A (Alama 16)

1. Katika kipengele (i) hadi (x), chagua herufi ya jibu saahihi kisha andika herufi ya jibu sahihi.

i.   Jamii za asili ya Kitanzania zilihama kutoka eneo moja na kwenda eneo jingine kwa sababu:

  1. Kufuata wazazi wa asili yao. 
  2. Kufuata elimu ya jadi 
  3. kufuaata ardhi yenye rutuba
  4. kufanya biashara 

ii. Somo la historia a maadili limeundwa na dhana kuu mbili:

  1. Dhana ya Historia ya Tanzania na dhana ya maadili 
  2. Dhana ya makabila na dhana ya utamaduni 
  3. dhana ya jando na ya unyago
  4. dhana ya Sanaa na jamii 

iii. Uhusiano kati ya somo la historia na maadili na chakula na lishe ni:

  1. Kuelewa vyakula vya biashara na kula nyumbani 
  2. Kuelewa vyakula vya asili ya maji na ardhi. 
  3. kuelewa faida ya vyakula vya wanga.
  4. Kuelewa asili ya vyakula, mabadiliko ya mtindo ya kula katika jamii.

iv) jamii za wakushito zinahusisha makabila kama:

  1. Wazaramo na wandengereko 
  2. Wairaki na waburugi 
  3. wangindo na wamatumbi
  4. wachaga na wapare

v) “Rushwa ni adui mkubwa wa haki.Tusipoidhibiti itaangamiza taifa”Baadhi ya madhara ya rushwa ni:

  1. Kushuka kwa tija na fanisi wa taasisi 
  2. Kuapata huduma ya haraka 
  3. usawa na uhalali kupata huduma
  4. kuwajibika kutokana na hongo uliopata 

vi) kulikuwa na sifa maaalumu zilizozingatiwa ili mtu ateuliwe kuwa kiongozi wa ukoo.Miongoni mwa sifa hizo ni:

  1. Ujuzi wa uganga na ushujaa 
  2. Kumiliki wake wengi na mashamba 
  3. awe mkali na anaeogopwa
  4. awe na mali na mfanyabiashara 

vii) Mafunzo katika kujenga tabia njema yalisisitiza mambo yafuatayo:

  1. Kusisitiza kuheshimuu wazazi tu. 
  2. Kufanya kazi kwa maslahi binafsi. 
  3. uwaajibikaji,upendo na ujasiri
  4. kulima na kupika 

viii) Nini maana ya “Urithi wa jamii?”

  1. Mali ya familia pekee 
  2. Mambo ya kisiasa tu 
  3. mila, desturi na tamaduni tunazorithi kutoka kwa wazee.
  4. shuguli za kibiashara.

ix) Maadili ya msingi katika jamii ni Pamoja na:

  1. Urafiki,wizi na heshima 
  2. Heshima,uaminifu na mshikamano. 
  3. Woga,upendeleo na bidi.
  4. Hasira,upendo na chuki

x) Mojawapo ya vyanzo vya Historia visivyoandikwaa ni:

  1. magazeti 
  2. Hati rasmi 
  3. mapokeo ya mdomo
  4. vitabu vya kumbukumbu

i

ii

iii

iv

v

vi

vii

viii

ix

x










.

2. Oanisha maelezo ya maneno kutoka kifungu A na maneno kutoka kifungu B kisha andika herufi ya jibu sahihi

KIFUNGU A

KIFUNGU B

  1. Uadilifu
  2. Utu
  3. Umoja
  4. Usawa
  5. Lugha ya taifa
  6. Uzalendo
  1. Kurahisisha mawasiliano ya watu wa taifa kwasababu inaunganisha watu wa Tanzania.
  2. Kuheshimiana na kujali hali za wengine kwa kuwasaidia na kutunza haki za binadamu.
  3. Unaonganisha watu wa Tanzania kutoka makabila,dini na utamaduni tofauti.
  4. Inahusu watu kuwa waaminifu na nidhamu.
  5. Watu wa Tanzania wanavyotambua haki za kila mtu mbele ya sheria
  6. Inahusu upendo wa watu kwa nchi yao

i

ii

iii

iv

v

vi






.

SEHEMU B (ALAMA 54)

Jibu maswali yote katika seehemu hii.

3. a) bainisha urithi wa asili uliopo maeneo unamoishi na taja manufaa ya urithi huo kwa jamii yako (hoja nne).

b) Urithi waa kihistoria ni eneo pana linalotoa na kazi kumnufaiisha mtu binafsi,jamii na taifa.Taja matumizi ya fursa hizo. (Hoja tano)

4. a) kabla kuingia ukoloni,jaamii za kitanzaniaa zilikuwa zinatumia mifumo maalumu kuelimisha watu. wake.bainisha malengo ya elimu kabla ya ukoloni (hoja nne) 

b) Taja tofauti kati ya jando na unyago. (Hoja tano)

5.a) Ni mambo gani mazuri yaliyopo katika mila ana desturi ya jamii za asili ambayo hayatiliwi mkazo kwa sasa?

b) utamaduni wa jamii za asili uliwandaa vijana kujitegemea kwa sababu ulitilia mkazo i. ii. iii.

6. Jamii za Wabantu,Wakushito,Wakichembe na Wanilo zilikuwa na desturi zilizolenga kukuza maadili katika Nyanja mbalimbali za Maisha yao.Taja malengo yaliojikita katika ujenzi wa maadili katika jamii.(hoja tano)

7. Tunapaswa kufahamu kuwa wajibu wa kulinda na kuifadhi maadili na urithi wa jamii ni jukumu la kila Mtanzania.thibitisha dai hili kwa kutaja matendo yanayokuza na kulinda maadili na urithi wa Tanzania.

8.Elezea maana ya istilahi zifuatazo:

  1. Urithi wa kihistoria
  2. Ol-Aiguanani
  3. Maadili
  4. Wakichembe
  5. Fursa
  6. matambiko

SEHEMU C (ALAMA 30)

Jibu maswali mawili (2) kutoka sehemu hii,swali la tisa (9) ni la lazima na kila swali lina alama 15.

9.Ukiwa kama mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule yako na mbobezi wa somo la Historia ya Tanzania na maadili Elezea tofaauti wa mfumo wa elimu ya jadi na mfumo wa elimu ya sasa.(hoja tano)

10. kumekuwepo na mmomomyoko wa maadili kwa jamii ya sasa kwa kiasi kikubwa hususani kwa vijana,Ungepewa nafasi ya kutoa maoni kuhusu maadili shuleni mambo gani ungependa yazingatiwe katika ujenzi wa maadili kwa vijana.elezea hoja tano(5) 11.elezea sababu za kujifunza somo la Historia ya Tanzania na maadili

FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 225  

FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 225  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256