FORM FOUR KISWAHILI MIDTERM EXAMS

JAMHURI YA MUNGANO WA TANZANIA

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

MTIHANI WA UPIMAJI – KISWAHILI

KIDATO CHA NNE- MACHI 2024

Muda : Saa 3

Maelekezo 

  1.         Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11).
  2.         Jibu maswali yote katika sehemu A na B, na maswali mawili (2) ktutoka sehemu C ambapo swali la tisa (9) ni la lazima.
  3.         Sehemu A ina alama kumi na sita (16), sehemu B alama hamsini na nne (54) na sehemu C ina alama thelathini (30)
  4.         Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
  5.         Vifaa vya mawasiliano na vitu visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  6.               Andika namba ya yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kujitabu  chako cha kujibia 

SEHEMU A (ALAMA 16)

  1.         Chagua herifi ya jibu sahihi katika kipengele cha (i-x) kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye karatasi ya kujibia.
  1.     Kikundi cha maneno kinachoonesha jambo lililotengwa na mtenda katika sentensi hujilikanaje
  1. Chagizo
  2.  Kitenzi
  3.  Kivumishi
  4. Shamirisho
  5.  Nomino
  1.  Viambishi vya O- rejeshi vya nomino “gari’ ni vipi kati ya vifuatavyo?
  1. O-YO
  2.  YE
  3.  LO-YO
  4. O-ZO
  5.  PO-YO
  1.                        Neno “Ngamia’  lipo katika ngeli ipi?
  1. I-ZI
  2.  YU-A-WA
  3.  KI-VI
  4. LI-YA
  5.  U-ZI
  1.                         Aina ipi ya maneno huyayanua zaidi kuhusu tendo au kivumishi kati ya haya yafuatayo?
  1. Kitenzi
  2.  Kihusishi
  3.  Kielezi
  4. Kiungaishi
  5.  Kiwakilishi
  1.   Ni neno lipi hufanya kazi na mofomo huru kati ya haya?
  1. Uji
  2.  Uzuri
  3.  Uchache
  4. Ufa
  5.  Mtoto
  1.                         Maneno yafuatayo yana maana zaidi ya moja ispokua:
  1. Ua
  2.  Kata
  3.  Paa
  4. Mbuzi
  5.  Nyau
  1.                      Katika neno ‘umempeleka” mofimu ipi inawakilisha kauli ya kutendea?
  1. –me-
  2.  –m-
  3.  –a-
  4. –e-
  5.  Pelek
  1.  Mbinu ya kufupisha maneno katika ushairi ili kupata ulinganifu wa mizani huitwaje?
  1. Tafsida
  2.  Inkisoni
  3.  Inkishafi
  4. Thathilitha
  5.  Ufupisho
  1.                         Kati ya zifuatazo, methali ipi ni tofauti na zingine?
  1. Ujanja mwingi mbele giza
  2.  Akili nyingi huondoa marifa
  3.  Mdharau bui huibuka yeye
  4. Ukupigao ndio ukufunzao
  5.  Mdharau mwiba, mguu huota tende
  1.   Ubainishaji wa maneno ya kuzua au yasiyo rasmi katika lugha huhusisha alama ipi ya uandishi kati yahizi?
  1. Mkato
  2.  Nukta
  3.  Mtajo
  4. Nukta- pacha
  5.  Nukta mkato.

 

  1.         Oanisha maelezo ya orogha A na yaliyopo katika Orodha B ili lipata maana kamili.

Orodha A

Orodha B

  1. Ngano
  2. Visakale
  3. Visasili
  4. Vigano
  5. mashairi
  1. Ni hadithi fupifupi za kuchekesha na kukejeli
  2. Ni hadithi zinazoelezea makosa na uovu wa watu fulani na kueleza maadili yanayofaa
  3. Ni hadithi ambazo husimulia kuhusu matukio ya kihistoria
  4. Ni hadithi ambazo husumulia asili ya watu, wanyama, miti na vitu visivyo na uhai
  5. Ni hadithi zinazotumia wahusika kama vile wanyama, miti na watu kuonya na kueleza kuhusu maisha
  6. Ni mpangilio maalumu wa maneno wenye ruwaza mahususi ya silabi na mkato.

 

SEHEMU B

ALAMA 54

  1.         Andika methali inayohusiana na mambo yafuatayo.
  1.     Vidole vya binadamu
  2.  Ukulima
  3.                        Imani ya binadamu kwa Mungu
  4.                         Ulevi
  5.   Unyonge
  6.                         Mwizi
  1.         Andika sentensi zifuatazo katika hali timilifu
  1.     Petro huwatembelea wazazi wake
  2.  Mimi ninamshinda Asha kwa mbio
  3.                        Wewe ni abiria lazima ulipe nauli
  4.                         Mchezaji anarusha mpira
  5.   Mwalimu anafundisha somo la kiswahili
  1.         (a) bainisha dhima tano za viambishi katika lugha ya kiswahili

(b) bainisha mzizi katika maneno ya sentensi zifuatazo (vitenzi)

  1.     Mtoto anacheza mpira
  2.  Mzee amelala ndani
  3.                        Mimi sipendi utani
  4.                         Sote tumekula pipi
  1.         Eleza kazi za mofimu tegemezi zilizochorewa mstari katika maneno yafuatayo:
  1.             Hatutasaidiana
  2.             Kitoto
  3.             Akija
  4.             Nilikunywa
  5.             Hakumtaka
  6.             Ninalima
  1.         Andika Insha isiopungua maneno miambili kuhusu “UKIMWI”
  2.         Soma kifungu cha habari, kisha  jibu maswali yanayofuata

        “Ndugu wazazi kumbe safari yenu inahusu harusi ya Zaituni?”. Mkuu wa shule aliwauliza wazazi, “Ndiyo”, wazazi walijibu kwa pamoja bila aibu. “Inategemewa kufungwa lini”?. Mkuu aliendelea kuhoji.

        “Harusi hii ilikua ifanyike wakati Zaituni alipofika kidato cha nne, lakini Zaituni huyu ametufanyia uhuni na vituko visivyoelezeka. Nasi sasa tunachukiwa na kijiji kizaima na kudharauliwa na kila mtu. Hii imetuudhi sana, tumetungiwa nyimbo na kufanyiwa kila shutuma. Hatuna raha, hivyo tumeonelea bora tuje kukuomba umfukuze shule ili kiburi kimwishe. Nasi tupo tayari kukulipa kiasi chochote cha fedha ukitimiza haja yetu hii”.  Mzee Abdalah aluelezea. Muda wote huu mkuu wa shule alikua akimtazama mzee kwa chati sana. Kisha akauliza swali la kuchochea zaidi “ Zaituni ana kiburi kumbe?”

         Mama Zaituni hakutaka hilo limpite, himahima akatoa maelezo yake  “ Mama wee, Zaituni usimwone hiivi, Zaituni manangu hataki kufuata utamaduni wetu wa kuoelewa. Zaituni ati achague mchumba mwenyewe, ati mahari haioni kama ni kitu cha msingi. Kiburi hicho kinatokana na Elimu mliyompa”. Mtoto sasa ameharibika, anafanya apendavyo. Hii Elimu gani isiyojali adabu wala utii? Mama Zaituni alimaliza huku jasho na machozi yanamtoka.

          Hapa mkuu wa shule aliona kwanza awaelimishe kabla hajawatolea kauli ya mwisho. Alikwisha tambua kwamba wazazi wa Zaituni walikua wameachwa nuuma na wakati. Kila upya wa mawazo waliuita kiburi. 

 

Maswali

  1.             Wazazi wa Zaituni walikwenda shule kufanya nini?
  2.             Wazazi walisema kuwa Zaituni amefanya kosa gani?
  3.             Eleza mgogoro mkuu uliopo kati ya Zaituni na wazazi wake
  4.             Fupusha habari hio kwa maneno yasiyopungua 50 na yasiozidi 60.

SEHEMU C

ALAMA 30

Jibu maswali mawili kutoka katika sehemu hii

ORODHA YA VITABU.

USHAIRI. 

Wasakatonge – M.S. Khatibu (DUP)

Malenga Wapya – TAKILUKI (DUP)

Mashairi ya ChekaCheka T.A. Mvungi (EP&D LTD)

 

RIWAYA

Takadini – Ben J Henson (MBS)

Watoto wa Mama Ntilie – E. Mbogo (H.P)

Joka la Mdimu – A. J. Safari (H.P )

 

TAMTHILIYA

Orodha – Stebe Reynolds (M.A)

Kilio Chetu – Medical Aid Foundation (TPH)

Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe – E. Semzaba (ESC)

  1.         “Jamii ya watanzania kwa sas inaongozwa na wanawake katika sekta mbalimbali” kwa kutumia Riwanya mbili ulizosoma eleza nafasi ya mwanamke katika jamii, toa hoja tatu kwa kila RIWAYA.
  2.         Wahusika ni kipengele kimoja wapo cha umbo la nje la kazi ya fasihi. Kwa kutimia mhusika mmoja kutoka kila kitabu onesha ujumbe unaowasilishwa na waandishi wa tamthiliya kuoitia matendo yao ( hoja tatu kutoka kila kitabu)
  3.    Mshairi ni kama taa imulikayo gizani ili kufuchua kilkichojifcha. Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kutoa hoja tatu kutoka kila diwani kati ya mbili ulizosoma.

 

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 181  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 181  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA KIDATO CHA NNE

021 KISWAHILI

MUDA: SAA 3:00 MACHI : 2023

MAELEZO

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C.
  2. Jibu maswali yote kutoka sehemu A, B na chagua maswali matatu kutoka sehemu C.
  3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na kila swali.
  4. Andika kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au nyeusi.
  5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyo ruhusiwa kwenye chumba cha mtihani haviruhusiwi.
  6. Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa karatasi yako ya kujibia.

SEHEMU A (alama 15)

Jibu Maswali yote Katika sehemu hii

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu hilo katika karatasi ya kujibia.

(i) Neno lipi kati ya maneno haya linaweza kudokeza hisia za mtenda au mtendwa

  1. Kiunganishi
  2. Kivumishi
  3. Kihisishi
  4. Kielezi
  5. Kiwakilishi

(ii) Lahaja ya kimtang’ata huongelewa sehemu gani ya Pwani ya A.Mashariki?

  1. Kaskazini mwa Pwani ya Tanga.
  2. Kisiwa cha Unguja.
  3. Kisiwa cha Mafia.
  4. Pwani ya Somalia
  5. Kisiwa cha Lamu

(iii) Kategoria ya kisarufi inayowakilisha wakati katika kitenzi.

  1. Leksimu
  2. Kiambishi awali
  3. Shina
  4. Mtendewa/mtendwa
  5. Njeo

(iv) Zifuatazo ni dhima za picha na mchoro katika kamusi isipokuwa ipi?

  1. Huvuta umakini wa mtumiaji kamusi.
  2. Huwawezesha watumiaji kamusi kuunda dhana ya jambo.
  3. Maumbo hunata katika kumbukumbu za watumiaji.
  4. Huchafua kamusi na kuifanya ichukize kwa watumiaji.
  5. Huwawezesha watumiaji kamusi kuona mfanano

(v) Ipi ni maana ya nahau “mbiu ya mgambo” kati ya maana hizi hapa chini.

  1. Tia aibu
  2. Tangazo maalumu
  3. Fanya Tashtiti
  4. Mluzi wa mgambo
  5. Sare za mgambo

(vi) Upi ni mzizi wa neno anakula?

  1. Kul
  2. La
  3. L
  4. Kula
  5. a

(vii) Mama Zita anakuja” Tungo hii ni tata, utata huo umesababishwa na nini?

  1. “Msamiati” mama kuwa na maana zaidi ya moja.
  2. Matumizi yasiyo kuwa bayana ya viunganishi na vihusishi.
  3. Matumizi ya lugha ya kifasihi.
  4. Kutozingatia taratibu za uandishi.
  5. Kosa la upatanishi wa kisarufi.

(viii) Kwa vipi ngonjera ni igizo?

  1. Ina urari wa vina na mizani.
  2. Inaimbika
  3. Inahusu utendaji
  4. Hufanyika mbele ya jukwaa
  5. Inahusisha wahusika binadamu.

(ix) Kifungu cha maneno ambacho hujibu maswali ya ziada kuhusu tendo katika sentensi huitwa. _______________

  1. Kiigizi
  2. Kirai Nomino
  3. Tungo
  4. Kirai kielezi
  5. Kikundi kivumishi

(x) Ili mzungumzaji wa lugha aweze kuwasiliana kwa usahihi anahitaji mambo manne ambayo ni _______________

  1. Mahusiano ya wahusika, muundo, mahali, lengo
  2. Lengo, mada, mandhari, umbo
  3. Mahali, mada, muda, wahusika
  4. Mada, mandhari, lengo,uhusiano wa wahusika
  5. Maudhui, lengo, mada, maana.

2. Oanisha dhana zilizo katika orodha A kwa kuchagua herufi ya dhana husika katika Orodha B. kisha andika herufi husika katika karatasi ya majibu.

ORODHA A

ORODHA B

(i) Hatua ya kwanza ya uchanganuzi wa sentensi

(ii) Kanda

(iii) Shamirisho

(iv) Mofimu ni kiambishi

(v) Wingi wa shule

  1. Sentensi nyofu
  2. Ni kipatanisho cha kiarifu
  3. Shule
  4. Kuainisha maneno ya sentensi
  5. Mashule
  6. Neno tata
  7. Itakaliwa na maneno ya vitenzi
  8. Kuanisha aina ya sentensi
  9. Usemi huu ni sahihi


SEHEMU B. (Alama 40)

Jibu maswali yote

3. Uteuzi mzuri wa maneno ni lazima uzingatie unaongea nini unaongea na nani? unaongea wapi? Na kwa nini? Eleza kwa ufupi hoja nne.

4. Andika methali inayohusiana na mambo yafuatayo.

  1. Vidole vya binadamu
  2. Ukulima
  3. Imani ya binadamu kwa Mungu
  4. Ulevi

5. (a) Sentensi zifuatazo zinamakosa kisarufi ziandikwe upya kwa usahihi.

  1. Huyu hapaendi ugovi
  2. Mafanikio alidondoka pale wakati anamkimbia
  3. Mtoto angepelekwa hospitalini mapema angelipona
  4. Mzee Peko alichinja mbuzi zake zote

(b) Kwa kutumia mifano, andika miundo mine (4) ya sentensi shurutia.

6. Wewe na msaidizi wako mmehudhuria kikao cha kupanga mahafali ya kumaliza kidato cha nne. Andika kumbukumbu ya kikao kilichofanyika katika shule kilichokuwa na wajumbe nane.

7. Ukuaji na ueneaji wa lugha ya Kiswahili, umepitia vipindi vingi tofauti, fafanua kwa mifano mambo manne (4) yaliosaidia kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili baada ya uhuru.

8. Soma kifungu cha habari kisha jibu maswali yafuatayo:

Nchi ya Tanzania hufanya uchaguzi wake kila baada ya miaka mitano, uchaguzi mkuu huhusisha uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani. Octoba 2020 watanzania wote walikuwa katika pilikapilika za kuwapata viongozi wa kuwawakilisha katika matatizo yao.

Mtanzania aliyekuwa huru kuchagua viongozi wake alitakiwa kutimiza masharti yafuatayo:-

Awe amejiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, awe na umri wa miaka kumi na nane na kuendelea, awe raia wa Tanzania na awe na akili timamu.

Uchaguzi ulifanyika kwa amani, wananchi waliweza kuelemishwa kupitia vyombo vya habari kama redio, magazeti, Runinga pamoja na majarida. Kwa kutumia vyombo hivyo vya habari zilifika sehemu zote za nchi yaani mijini na vijijini, kila mtanzania alijua uchaguzi ni muhimu kwake kwani hutupatia viongozi bora kuendeleza demokrasia, kuleta mabadiliko nchini na kutatua migogoro mbalimabli katika jamii pamoja na kuondoa ubaguzi. Watanzania tushikamane kuendeleza amani nchini.

MASWALI:

  1. Pendekeza kichwa cha habari kifaacho kwa habari hiyo.
  2. Uchaguzi hufanyika kila baada ya miaka mingapi hapa Tanzania?
  3. Taja sifa tatu za mtu anaetakiwa kupiga kura.
  4. Unafikiri uchaguzi una umuhimu? Kama ndio au hapana toa hoja tatu.

SEHEMU ‘C’ Alama (45)

Jibu maswali matatu tu kutoka sehemu hii

9. Umealikwa kwenda kuelimisha jamii yako juu ya “madhara ya mapenzi katka umri mdogo”. Tunga mchezo mfupi wa kuigiza usiozidi maneno (300) mia tatu kuhusu mada hiyo.

ORODHA YA VITABU

 USHAIRI

  • Wasakatonge -M.S. Khatibu (DUP)
  • Malenga Wapya -TAKILUKI (DUP)
  • Mashairi ya Chekacheka-T.A Mvungi (EP & DLTP)

RIWAYA

  • Takadini-Ben Hanson (M.B. S)
  • Watoto wa Mama Ntilie-E. Mbogo (H.P)
  • Joka La Mdimu-A.J. Safari (H.P)

TAMTHILIA

  • Orodha - Steven Raymond (M.A)
  • Ngoswe penzi kitovu cha uzembe-E. Semzaba (E.S.C)
  • Kilio chetu -Medical Aid Foundation (F.P.H)

10. Mashairi siku zote hukemea uonevu katika jamii. Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja 3 kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili ulizo soma.

11. Kwa kutumia riwaya mbili ulizosoma, fafanua namna ambavyo waaandishi wametumia kipengele cha mtindo kuumba kazi zao. Eleza hoja tatu kwa kila kitabu.

12. Kwa kutumia hoja tatu kutoka kwa kila tamthiliya kutoka katika tamthiliya mbili ulizosoma. Jadili kufaulu kwa mwandishi katika kipengele cha matumizi ya lugha.

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 138  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 138  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA KIDATO CHA NNE

021                        KISWAHILI

MUDA: SAA 3:00                                                     APRILI: 2022

 

MAELEKEZO

1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, na D

2. Zingatia maagizo ya kila sehemu na kila swali.

3. Majibu yote yaandikwe kwa wino wa bluu au mweusi.

4. Jibu maswali yote katika sehemu A, B, C na maswali matatu sehemu D, swali la tisa ni lazima.

 

SEHEMU A (Alama 10)

1.Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herefu ya jibu hilo.

i) Ni jambo gani linalodhihirisha umbo la nje ya kazi ya fasihi?

  1. Muundo
  2. Jina la kitabu
  3. Fani
  4. Mtindo.

ii) Ni sehemu ya neno ambayo huweza kutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu moja la sauti.

  1.  Irabu
  2. Konsonati
  3. Mofu
  4. Silabi

iii) leta wali kuku.hii ni aina gani ya rejista?

A. Rejesta ya Hotolini

B. Rejesta ya Hospitalin

C. Rejesta ya Mtaani

D. Rejista ya Shambani

iv) Ipi maana inayoelekeana na methali hii? ‘chanda chema huvikwa pete’

  1. Mwanamke mrembo
  2. Mtoto wa kike mwenye tabia njema hupendwa
  3. Mtoto mzuri huvaa nguo zikampendeza
  4. Bibi harusi

v) ..........ni hadithi zinazozungumzia matukio ya kihistoriya.

  1.  Ngano
  2.  Tarihi
  3.  Visasili
  4.  Soga

vi) Mara nyingi fasihi simulizi huzingatia uwepo wa;

  1.  Fanani Na Hadhira
  2.  Mtunzi
  3.  Fanani
  4.  Hadhira

vii)Upi ni mzizi wa neno anakula?

  1. Kul
  2. La
  3. L
  4. Akul

viii)Ni jambo gani linalodhihirisha upekee wa kazi Fulani ya kifasihi?

  1.  Muundo wa kazi husika
  2.  Wahusika wa kazi husika
  3.  Mtindo wa kazi husika
  4.  Jina la kazi husika

ix) Neno lipi kati ya maneno haya linaweza kudokeza mtenda au mtendwa?

  1. Kiunganishi
  2. Kihisishi
  3. Kielezi
  4. Kiwakilishi

x) Ni sifa ipi haitofautishi fasihi simulizi na fasihi andishi?

  1. Ukubwa
  2. Uwasilishwaji
  3. Uhifadhi
  4. Ueneaji 

 

SEHEMU B (Alama 5)

 

2. Oanisha sentensi za kifungu A, kwa kuchagua jibu sahihi katika kifungu B, andika jibu lako kwa usahihi katika kisanduku ulichopewa hapo chini;

 

 KIFUNGU A

KIFUNGU B

  1. Huonesha mpangilio wa maneno kialfabeti,jinsi yanavyoandikwa kutamkwa na maana zake.
  2. Mjengo au umbo la kazi ya fasihi.
  3. Maneno yasiyo sanifu yanayozungumzwa na kikundi kidogo cha watu.
  4. Taauluma inayoshughulikia maumbo au mjengo wa maneno katika tungo.
  5. Ni mtindo wa lugha inayozungumzwa kulingana na muktadha na kusudi maalum.

 

 

 

  1.         Tanzu za fasihi.

 

  1.         Rejesta.

 

  1.         Misimo.

 

  1.         Sarufi maumbo.

 

  1.         Misimu.

 

  1.          Mofimu.

 

  1.         Muundo.

 

  1.         Nomino.

 

  1.          Kamusi.

 

 

KIFUNGU: A

I

II

III

IV

V

KIFUNGU B

 

 

 

 

 

 


 

 

SEHEMU C: ALAMA 40

Jibu maswali yote katika sehemu hii

 

3. Eleza maana ya kielezi kwa kutoa mfano wa sentensi moja.

4. Kwa kila tungo uliyopewa pigia mstari kielezi na kisha taja ni kielezi cha aina gani? 

i) Darasani kuna utulivu mkubwa.

     ii) Wanafunzi wanaimba kimasihara.

     iii) Mwalimu amerudi tena.

     iv)  Nitaondoka wiki ijayo.    

5. Toa maana tano (5) za neno “Kibao” kisha tunga sentensi moja kwa kila maana ulitoa.

6.Taja njia nne (4) zitumikazo kuunda misamiati na utoe mfano kwa kila njia. 

7. Taja aina mbili za Mashairi na maana zake. 

8. Soma shairi lifuatalo kisha jibu sehemu hii.

Utu wa binadamu, ni kama yai na kuku,

Utu niile nidhamu, mola aliyo mtunuku,

Ubinadamu ni damu, ya utu wa kila siku,

Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake.

 

Yeyote mwanadamu, ana asili ya mtu,

Yaani kwenye yake damu, hakikosi hiki kitu,

Utu sifa maalum, ya mtu kuitwa mtu,

Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake.

 

Utu ni kiumbe hai, tunacho chaonekana,

Utu kamwe haudai, tabia ya kujivuna,

Utu ni ule uhai, ushikao uungwana.

Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake

 

Utu unayo aibu, na tabia ya muhali,

Utu huenda na jibu, kila imani na ukweli,

Utuwe hauna tabu, tabia ya ujalili,

Utu wowote wa mtu, ni kuwajali wenzake.

 

 

MASWALI

  1. Pendekeza kichwa cha shairi ulilosoma
  2. Eleza maana ya maneno yaliyopigiwa mstari kama yalivyotumika katika shairi ulilosoma.
  1. Kukhuluku
  2. Uungwana
  3. ujalili.
  4. Muhali.
  1.  Mwandishi anasisitiza nini katika utanzu huu wa shairi
  2. Onesha muundo na mtindo uliotumika katika shairi hili.
  3. Umepata ujumbe gani katika shairi hili? Toa hoja mbili.

 

SEHEMU D (Alama 45)

 

Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii swali la 9 ni lazima

9. Ukiwa kiongozi wa michezo katika shule ya Sekondari Kizota S L P 30 Dodoma, andika barua kwa mkuu wako wa shule  kupitia kwa mwalimu wa michezo kuomba kuongezewa siku za michezo  shuleni. jina lako liwe Siku njema Afya.

 

10 “Msanii ni kinda la jamii husika anayoandika kuihusu jamii hiyo”. Jadili kauli hii kwa kutumia hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili zilizoorodheshwa.

 

11. “Wahusika katika kazi za fasihi ni mfano wa kuigwa na jamii kwa tabia na matendo yao”. Thibitisha kauli hii kwa kutumia hoja tatu kwa kila mhusika kutoka katika tamthilliya mbili zilizoorodheshwa.

12.Elimu ni ufunguo wa maisha. Fafanua kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu kati ya vitabu viwili vya riwaya vilivyoorodheshwa.

 

ORODHA YA VITABU

USHAIRI

Wasakatonge                                                     M.S. Khatibu (DUP)

Malenga Wapya                                                TAKILUKI (DUP)

Mashairi ya Chekacheka                                   T.A.Mvungi (EP & D.LT.D)

RIWAYA

Takadini                                                            Ben J. Hanson (Mbs)

Watoto Wa Mama N’tilie                                   E. Mbogo (H.P)

Joka La Mdimu                                                   A.J.Safari (H.P)

TAMTILIYA

Orodha                                                             Steve Reynolds (Ma)

Ngoswe Penzi Kitovu Cha Uzembe                   E.Semzaba    (Esc)

Kilio Chetu                                                       Medical Aid Foundation (Tph)

 

 

1

 

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 80  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 80  

OFISI YA RAIS

WIZARA YA ELIMU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA NUSU MUHULU- MACHI-2020

            KISWAHILI

SEHEMU A (Alama 10)

UFAHAMU

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata;

Nchi yetu ya Tanzania imejulikana sana kutokana na mazingira yake yanayowavutia watalii. Hali yake ya hewa ni nzuri na yenye kutamanika. Mvua yake si nyingi na haichukizi bali ni ya rasharasha na tena ni ya hapa na pale. Majira yenyewe ya masika ni mafupi sana na hayana baridi kama huko ulaya.

Kitu hasa kinachowavutia watalii kutembelea nchi yetu ni pwani zetu ambazo zina mchanga mweupe na laini. Mchanga wenyewe hauna matope wala uchafu wowote. Kandokando ya pwani hizo kuna vichaka vyenye miti yenye rangi ya chanikiwiti na maua ya sampuli nyingi ya kutamanisha. Maua hayo yapo ya rangi nyekundu na vilevile hunukia vizuri, ama huweza kuwa na rangi ya manjano na kisha yakawa mviringo.

Kando kidogo unaweza kuona mawe makubwa yenye mapango makubwa meusi ambamo wanyama wakubwa na wakali kama chui huishi. Pengine hata wanyama wa kuchekesha na hata watundu kama tumbili na kima huonekana humo.

Pembezoni, ambapo ni nje ya pwani zetu, kuna mashamba yenye mimea ya rangi ya kijani ikinawiri hasa wakati wa masika. Kipindi hiki wakulima nao huwa wanajishughulisha na matayarisho pamoja na maendeleo ya kazi zao za kila siku. Baadhi yao hupenda kufanya kazi huku wamevaa majoho marefu meupe au pengine shuka za kaniki zilizochakaa. Aidha, wengine hawajishughulishi kamwe na mambo ya mavazi kwani wao huvaa vikoi vikuukuu na vilivyokwajuka, bila kujali wapita njia.

Zaidi ya pwani zetu, watalii huvutiwa sana na mbuga zetu za wanyama wa porini. Wengi wa wanyama katika mbuga zetu huwa na ngozi zenye madoa ya rangi za kuvutia. Pengine hata maungo yao huwa ya kutisha na yasiyokuwa ya kawaida. Mathalani ukimwona kifaru, utadhani amekasirika na kwamba anataka kukurarua vipande vipande. Simba naye anajulikana kwa makucha yake marefu ya kutisha. Kiboko kwa upande wake, anajulikana kwa unene wake. Tumbo lake ni kubwa la kuchekesha kwani kila umwonapo utadhani matumbo yataporomoka dakika yoyote.

Basi mambo kama hayo na mengine mengi, ndiyo yanayowavutia watalii kuja kwetu. Watalii hawa ambao wengine kati yao ni warefu na pia wachangamfu lakini wapo walio wembamba na wepesi katika kuipanda milima yetu. Hata hivyo, wapo pia wazee vikongwe wenye ari na nguvu katika kuipanda milima hiyo. Wote hawa wanakuwa na hamu ya kutembelea vivutio vyetu. Baada ya kutembelea sehemu mbalimbali, hurudi kwao na furaha isiyo kipimo huku wakituachia fedha nyingi za kigeni.

 

Maswali

  1. Andika kichwa cha habari hii kisichozidi maneno manne.
  2. Taja dhamira kuu inayotokana na habari hii
  3. Mwandishi anatoa ushahidi gani kuthibitisha kuwa nchi yetu ina vivutio vingi vya utalii?
  4. “ wenyeji wan chi yetu ya Tanzania nao ni sehemu ya vivutio vya utalii” Thibitisha kauli hii kwa mujibu wa habari uliosoma.
  5. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu cha habari;
  1. Chanikiwiti
  2. Vilivyokwajuka

2. Fupisha habari ulioisoma kwa maneno yasiozidi arobaini (40)

 

 

SEHEMU B (Alama 25)

 

SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA

 

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

 

 

3. (a) Eleza maana ya utohoaji.

    (b) Maneno yafuatayo yametoholewa kutoka lugha gani.

  1. Picha
  2. Duka
  3. Shule
  4. Rehema
  5. Shati
  6. Trekta
  7. Ikulu
  8. Bunge
  9. Achali

 

4.  Taja aina za sentensi zifuatazo kisha eleza muundo ujengao kila sentensi.

  1. Maisha ni safari ndefu
  2. Ukisoma kwa bidiii utafaulu kwa kiwango cha juu.
  3. Mtoto aliyelazwa hospitalini ameruhusiwa kwenda nyumbani.
  4. Nitakuja leo ingawa nitachelewa sana.
  5. Alinunua madaftari lakini kitabu cha Kiswahili alipewa na mwalimu.

 

5. (a) Eleza maana ya urejeshi katika kitenzi.

    (b) Tunga sentensi tatu zinazoonesha urejeshi wa:

  1. Mtenda nafsi ya tatu umoja.
  2. Mtendwa (idadi – wingi)
  3. Mtenda (kitu)

 

6. Bainisha tabia za maumbo yaliyokolezwa wino katika vitenzi ulivyopewa.

  1. Futa ubao
  2. Hutafaulu mtihani
  3. Ametualika
  4. Mtoto hulia mara nyingi
  5. Yeye ni mwalimu
  6. Mgonjwa amejilaza chini
  7. Wanavisoma vitabu vyao
  8. Paka amepigwa
  9. Mti umekatika.

 

7. (a) Eleza maana na dhima ya kiunganishi katika sentensi.

    (b) Tunga sentensi mbili kwa kila kiunganishi kifuatacho;

  1. Kwa sababu
  2. Kama
  3. Ingawa
  4. Lakini

 

 

 

8.  Jifanye kuwa mfanyabiashara wa mchele na unataka kuitangaza biashara yako nje na ndani ya nchi. Andika tangazo kuhusu biashara hiyo na jina lako liwe Pera Mlavi.

 

 

SEHEMU C. (Alama 45)

 

FASIHI KWA UJUMLA

 

Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii. 

 

 

ORODHA YA VITABU:

 

USHAIRI

Wasakatonge                                                                         -                       M.S. Khatiby (DUP)

Malenga Wapya                                                                    -                       TAKILUKI (DUP)

Mashairi ya ChekaCheka                                                    -                       T.A. Mvungi (EP & D. LTD)

 

 

RIWAYA

Takadini                                                                                 -                       Ben J. Hanson (MBS)

Watoto wa Mama N’tilie                                                      -                       E. Mbogo (H.P)

Joka la Mdimu                                                                      -                       A.J. Safari (H.P)

 

 

TAMTHILIYA

Orodha                                                                                   -                       Steve Reynolds (MA)

Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe                                      -                       E. Semzaba (ESC)

Kilio chetu                                                                              -                       Medical Aid Foundation (TPH)

 

 

 

9. “Waandishi wa tamthiliya wameshindwa kufikisha ujumbe kwa jamii iliyokusudiwa.” Kanusha kauli hii kwa kutumia hoja tatu kwa kila kitabu kotoka katika tamthiliya mbili ulizosoma.

 

10. “Mshairi ni mwalimu wa viongozi wa nchi.” Jadili kauli hii kwa kutoa hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili ilizosoma.

 

11. Kwa kutumia hoja tatu kwa kila tamthiliya kutoka katika tamthiliya mbili ulizosoma, jadili kufaulu kwa waandishi katika kipengele cha utumizi wa tamathali za semi.

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 4  

FORM FOUR KISWAHILI EXAM SERIES 4  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256