FORM THREE KISWAHILI MIDTERM EXAMS

JAMHURI YA MUNGANO WA TANZANIA

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

MTIHANI WA UPIMAJI – KISWAHILI

KIDATO CHA TATU- MARCHI 2024

Muda : Saa 3

Maelekezo 

  1.         Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11).
  2.         Jibu maswali yote katika sehemu A na B, na maswali mawili (2) ktutoka sehemu C ambapo swali la tisa (9) ni la lazima.
  3.         Sehemu A ina alama kumi na sita (16), sehemu B alama hamsini na nne (54) na sehemu C ina alama thelathini (30)
  4.         Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
  5.         Vifaa vya mawasiliano na vitu visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  6.         Andika namba ya yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kujitabu  chako cha kujibia 

SEHEMU A (ALAMA 16)

  1.         Chagua jibu sahihi katika maswali yafuatayo;
  1.  Mende anapenda kula uchafu . neno Mende lipo katika ngeli ipi;
  1.    Ki-vi
  2.    U –i
  3.    A- wa
  4.    Ku
  5.    Li-ya
  1.  ......................... mna watu wengi
  1.    Aliingia
  2.    Alipoingia
  3.    Alikoingia
  4.    Alivyoingia
  5.    Alimoingia
  1.   Neno papai linaingia katika ngeli ya
  1.    Li-ya
  2.    Yu-a-wa
  3.    Pa- mu- ku
  4.    Ki-vi
  5.    U-i

 

  1.                         “Shangazi yupo shambani mwake “ kifungu hili kipo katika ngeli gani:-
  1.    Pa-mu-ku
  2.    Yu-a-wa
  3.    U-zi
  4.    U-ya
  5.    Li-ya
  1.   Ni ipi sababbu miojawapo ya kutumia kugha kulingana na muktadha?
  1.    Kusuka kwa matukio mbalimbali
  2.    Kuendana na Sayansi na technologia
  3.    Kumudu shughuli inayofanyika
  4.    Kupamba mazungumzo
  5.    Kuwezesha mawasiliano
  1.               Katika neno wanakula mzizi wa neno ni:
  1.    Kul
  2.    Kula
  3.    –l-
  4.    Nak
  5.    Ku
  1.                      Visasili ni mojawapoya vipera vya hadithi ambavyo hueleza kuhusu:
  1.    Matukio ya kihistoria
  2.    Makosa na uovu wa watu
  3.    Kuonya kuhusu maisha
  4.    Asili ya vitu kama vile milima, mito, wanyana n.k
  1.  Neno linaloingizwa katika kamusi kwa wino uliokolezwa, fasili, matamshi na aina ya neno kwa pamoja huitwa
  1.    Kidahizo
  2.    Kitomeo
  3.    Istilahi
  4.    Fasihi
  1.                         Neno lipi kati ya yafuatayo ni mofimu honi?
  1.    Chai
  2.    Kula
  3.    Imba
  4.    Ruka
  5.     Lala
  1.   Katika sababu zifuatazo ni ipi si sahihi kuhusu kamusi?
  1.    Kujifunza lugha ya kigeni
  2.    Kujua maana ya neno
  3.    Kujua tahajia ya neno
  4.    Kusanifisha maneno mapya

 

  1.         Oanisha dhana zlizopo katika Orodha A na zilizopo katika orodha B , kukamilisha mana kamili

ORODHA A

ORODHA B

(i)    Mwanafunzi aliyepewa zawadi jana asimame

  1. Kirai
  2. Kishazi tegemezi
  3. Shamirisho
  4. Kirai kielezi
  5. Chagizo
  6. Sentensi changamano
  7. Kirai nomino
  8. Prediketa

(ii) Huundwa na vitenzi vyenye O-rejeshi

(iii)                       Sehemu ya kiarifu ilyokaliwa na nomino

(iv)                        Neno au mpangilio wa neno wenye neno kuu moja

(v)  “Mwenye duka” ni muundo wa

(vi)                        Sehemu ya kiarifu inayokaliwa na kienzi

 

 

SEHEMU B

ALAMA 54

  1.         (a) Kwa kutumia mifano, fafanua taarifa nne za kisarufi zilizopo katika viambishi awali na vitrnzi vya kiswahili

(b) Nominisha vitenzi vifuatavyo

  1.     Pata
  2.  Jenga
  3.                        Fundisha
  4.                         Panda
  5.   Chuja
  1.         (a) Fafanua njia tatu (3) za uundaji wa misimu kwa kutumia mifano.

(b) Taja misimu minne iliyozuka kipindi cha serikalli ya awamu ya tano

  1.         Katika sentensi zifuatazo, onesha matumizi ya mofimu “ki”
  1.     Ukimwona atakueleza
  2.  Alikua akilia  gari lilipogonga mti
  3.                        Amevaa kifalme
  4.                         Mtoto anakimbia
  5.   Kikombe kimevunjika
  6.                         Amechukua kimoja tuu
  1.         Bainisha O- rejejeshi katika sentensi zifuatazo.
  1.     Mtu anayekunon’goneza aje apa
  2.  Mti ukioanguka umevunja nyumba lakini hakuna watu waliojeruhiwa
  3.                        Panga lililopotea limepatikana
  4.                         Kitabu alichookota ni cha kwangu
  5.   Vitabu vilivyosomwa ni vile vilivyotolewa na waziri wa Elimu
  6.                         Mahali alipolala mbuzi pamevamiwa na siafu
  1.         Andika simu ya maneno kwa mjomba wako kuhusu kuomba pesa ya safari ya kwenda hifadhi ya wanyama Tarangire . Jina lako liwe Mitomingi wa S.L.P. 37, huko Kibaha ,Mkoa wa Dar-es-Salaam . ( maneno tisa 9)
  2.         Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali.

         Ili kuondoa utat wa maneno sanaa na fasihi, inafaa kuyaeleza maneno hayo kwa uwazi zaidi. Sanaa imeelezwa kuwa ni uzuri ulio katika umbo lililosanifiwa. Fasihi ni sehemu ya uzuri huo. Katika fasihi kuna uzuri wa kifasihi, huitwa  fani na jambo lisemwalo huitwa maudhui. Fasihi lazima iwe na sehemu hizi mbili. Ikikosekana moja wapo, kazi haiwi ya kifasihi.

           Mtunzi wa kazi ya fasihi huwa na jambo kusema na namna ya kulisema. Kwa hiyo,ana dhamira na anatumia ufundi wa maneno mbalimbali kufikisha dhamira yake.

           Kazi ya fasihi inaweza kuwa na upungufu kutokana na upotofu wa fani au maudhui. Maudhui yanajengwa na dhamira, ujumbe, maadili, falsafa, na maranyingine suluhisho. Dhamira ya mtunzi ikiwa potofu au haikubaliki katika jamii, inapunguza uzuri wa kazi yake.

 

Maswali 

  1.     Kwa mujibu wa habari hii nini maana ya fasihi
  2.  Eleza tofauti kati ya sanaa na fasihi
  3.                        Mtunzi anaposema kazi ya fasihi inaweza kua na upungufu kutokana na upotofu wa fani na maudhui, ana maana gani?
  4.                         Eleza umuhimu wa sanaa katika fasihi
  5.   Fafanua imuhimu wa  fani na maudhui katika fasihi.

 

SEHEMU E

ALAMA  30

 

Jibu maswali mawili kutoka sehemu hii

 

  1.         “Fasihi ni chombo cha kufundishia maisha”. Jadili ukweli wa kauli hii kwa kutumia hoja sita.
  2.    Fasihi simulizi ndio fasihi ya awali iliyoanza wakati binadamu alipoanza kutumia lugha. Mara kwa mara inapowasilishwa ka hadhira huchukua sifa muhimu kadhaa ambazo si rahisi kuzipata katika fasihi andishi. Thibitisha iweli huu kwa hoja sita.
  3.    (a) Unaelewa nini kuhusu mashairi ya kimapokeo ?

(b) Kwa kutumia mifano kuntu, fafanua vipengele saba vya kuzingatia wakati wa kutunga shairi la kimapokeo.

FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 164  

FORM THREE KISWAHILI EXAM SERIES 164  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256