FORM TWO KISWAHILI MIDTERM EXAMS

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

UPIMAJI WA KIDATO CHA PILI NUSU MUHULA

MACHI -2024

KISWAHILI

SEHEMU A: UFAHAMU(Alama 15)

  1.      Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.

      Miaka ya hivi karibuni kumetokea ajali nyingi hapa duniani. Wengi tumesikia taarfa za ajali mbalimbali kutoka katika vyombo vya habari na baadhi yetu tumeshuhudia kwa macho yetu. Kila aliye sikia au kuona ajali hizo alivaa uso wa huzuni. Kwani nyingi zilikua za kutisha mno, wapo watu walio katika miguu, mikono  masikio na hata kunyofolewa macho na viungo vingine vya mwili. Ukiachilia mbali majeruhi na wale walionusurika, wapo Ndugu na marafiki zetu waliopotezxa maisha. Wengi tulipata machungu yaliokithiri, tulilia na kuwalaani wote tuliofikiria ndio waliosabaisha ajali hizo.

      Waliokufa katika ajali hizoni wadogowadogo watu wazima na hata vikongwe wanawake kwa wanaume. Kama ilivyo desturi kifo hakibagui na huvuna roho za watu wa umri na jinsia zote. Wazazi wengi wanaofariki katika ajali hizi huacha watoto ambao hawamo katika utaratibu wa kuendelea kielimu. Badala wanaingia katika kujitaftia ririki badala ya kujisomea. Watot wengi hufanya kazi ya kubeba mizigo, uvuvi kuchimba madini na migodibiashsara ndogondogo na hata kazi za nyumbani.

        Watoto hao walioachwa hukumbwa na matatizo mengi wafanyapo kazi katika sehemu hizo.kwakua wengi wao hawana upeo mkubwa wa mambo, hujikuta wakifanya kazi bila kufuata kanuni zaafya. Hali hiyo husababisha magonjwa kama kifua kikuu na hata kupata ajali mbaya, wafanyapo kazi migodini, ambazo zinaweza kusababish akifo au vilema vya maisha. Wengi huingizwa kwenye bishara za ukahaba na kupata mimba zisizitarajiwa tena katika umri mdogo. Wengine huambikzwa magonjwa kama UKIMWI.

          Pamoja na usemi wa ukweli kua “ Ajali haina kinga” Ajali nyingi zinazotokea zinatokana na makosa yetu wenyewe. Hizi tukiamua, tunaweza kuzizuia kwani penye nia pana njia. Hivyo hivyo suala la kuwapatia Elimu watoto  walioathirika na ajali liwe la kufa na kupona. Kama Taifa ni lazima tupige vita ajira kwa watoto, ikiwa kweli tunataka kwenda na wakati. Vinginevyo tutabaki nyuma.

1 (a) Andika herufi ya jibu sahihi

  1.     Mwandishi amesema kuwa wanaokufa katika ajali ni
  1. Watu wa aina zote
  2. Watoto wadogo
  3. Watu wazima
  4. Vikongwe, wanawake na wanaume
  1.  Ipi si kweli kuhusu maneno wanaoajiriwa watoto?
  1.    Kwenye machimbo ya madini
  2.    Kwenye biashara ndogondogo
  3.    Kazi za nyumba
  4.    Kwenye ofisi za serikali
  1.                        Ajira kwa watoto husababishwa na :-
  1.    Kutokuwepo na shule za kutosha
  2.       Vifo vya wazazi na ugumu wa maisha
  3.       Kampeni za vyama za siasa
  4.       Madeni ya nchi
  1.                         Ili watoto waweze kufanikiwa katika maisha yao ya baadaye ni lazima jamii:
  1.    Ipige vita rushwa
  2.    Ifuate sisa ya ujamaa na kujitegemea
  3.    Iwape watoto Elimu
  4.    Ijenge barabara nzuri
  1.   Moja ya haya yafuatayo sio ajali ya kujitakia :-
  1.    Gari kuanguka kutokana na mwendokasi
  2.    Kuzidisha uwezi wa uzito katika vyombo vya usafiri
  3.    Kuendesha vyombo vya usafiri pasipo kuzingatia sheria
  4.    Kuzuka kwa vimbunga vinavyoleta maafa makubwa
  1.                         Mwandishi anaamini kua tunaweza kuzuia ajali kwa
  1.    Kumwomba Mungu atuepushe na ajali hata kama atufuati kanuni na sheria
  2.    Kutoendesha magari katika barabara mbaya
  3.    Kuwa makini katika kuendesga vyombo vya usafiri
  4.    Kutowaruhusu wazazi wenye watoto kutumia vyombo vua usafiri

i

ii

iii

iv

v

vi

(b) Eleza maana ya misemo ifuatayo kama ilivyotumika habari uliyoisoma

  1.     Alivaa uso wa huzuni
  2.  Liwe la kufa na kupona
  3.         Penye nia pana njia

(c) Andika kichwa cha habari kisichozidi maneno matatu

  1.         Andika ufupisho wa habari hii usiozidi maneno sitini (60)

SEHEMU B: SARUFI

ALAMA 20

  1.         (a)Nyumbua maneno yafuatayo lwa kutumia kauli ya kutendesha
  1.     Lima
  2.  Imba
  3.                        Piga
  4.                         Fyeka
  5.   Ita

                (b) Unda nomino moja tuu kutokana na kila kitenzi katika vitenzi vifuatavyo.

  1.     Lea
  2.  Nyoa
  3.                        Pika
  4.                         Cheza
  5.   Soma
  1.         Bainisha aina ya nomino zifuatazo .

Mfano Mayai – Nomino ya kawaida

  1.     Papai
  2.  Mungu
  3.                        Arusha
  4.                         Upepo
  5.   Jumamosi

SEHEMU C: MAWASILIANO NA UTIMIZI WA LUGHA.

ALAMA 20

  1.         Onesha rejesta zifuatazo hutumika katika mazingira gani?
  1.     Mimi wali kuku, huyu wali maharage na pale ng’ombe
  2.  Zuia babu kula hivyo vichwa
  3.                        Napenda kujibu swali la nyongeza la mheshimiwa kama ifuatavvo
  4.                         Ndugu Matata, unahukumiwa kwa kosa la jinai la kuiba mali ya umma
  5.   Jipatie mahitaji ya jikoni, nyanya , vitunguu, karoti, pilipili, na ndimu , vyote vipo
  1.         Bainisha sifa tano za misimu
  2.         Fafanua tofauti tano za lugha ya kimaandishi na lugha ya kimazungumzo

SEHEMU D: FASIHI KWA UJUMLA

ALAMA 30

  1.         Kamilisha methali zifuatazo
  1.             Hakuna masika....................................................................
  2.             Mchinga mwiko ..................................................................
  3.             Chanda chema ...................................................................
  4.             Asiyefunzwa na mamaye ...................................................
  5.             Dalili ya mvua ....................................................................
  1.          
  1.             Taja vipera vitano vya ushairi
  2.             Taja njia tano zakuhifdhi kazi za fashi simulizi
  3.             Taja dhima tano za hadithi

SEHEMU E: UANDISHI WA INSHA/ UTUNGAJI

ALAMA 15

  1.    Kwa kingatia hoja tano(5) andika insha isiyopungua maneno 100 ma isiyosodo maneno 150 kuhusu athari za ugojwa wa Corona [Covid 19]

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 169  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 169  

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA KUJIPIMA

KISWAHILI KIDATO CHA PILI

021                                                                         

MUDA: SAA 2:30                                                       MACHI- 2022

image

Maelekezo

1.      Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E.

2.      Jibu maswali yote.

3.      Fuata maelekezo ya kila swali.

4.      Majibu yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa.

5.      Majibu yote yaandikwe kwa wino wa bluu au mweusi

6.      Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.

7.      Andika Namba yako ya Mtihani upande wa juu kulia wa kila ukurasa wa karatasi yako.

KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU

NAMBA YA SWALI

ALAMA

SAINI YA MTAHINI

1

2

3

4

5

6

7

8

9

10

JUMLA

SAINI YA MHAKIKI

SEHEMU A: (Alama 15) UFAHAMU

1. Soma kwa makini shairi lifuatalo, kisha jibu maswali yanayofuata:

Shime basi waungwana, Umoja kutekeleza,

Mabibi hadi Mabwana, harambe nguvu kukoza,

Mpaka wetu vijana, tusije tukalegeza,

Nchi inayopendeza, ni watu kusikilizana.

Watu wakishikamana, hata amani huwepo,

Mambo kukubaliana, ndipo waendeleapo, Viongozi pia kutuna, kazi yao inyookapo, Nchi inayopendeza, ni watu kusikilizana.

Kaditama kwelezana, hapo basi nanyamaza,

La zaidi sina tena, ni hayo niloeleza, Basi shime kuungana, usawa kutekeleza,

Nchi inayopendeza, ni watu kusikilizana.

Maswali:

(i)         Pendekeza kichwa cha habari kisichozidi maneno matano.

 (ii)      Shairi hili linahusu nini? 

(iii)    Waungwana ni watu wa aina gani.

 (iv)     Nini maana ya kaditama?

 (v)       Kiitikio cha shiri hili ni kipi?

2. Fupisha shairi ulilosoma kwa maneno yasiyozidi arobaini (40).

SEHEMU B: (Alama 20)

SARUFI

3.(a) Tumia mzizi wa kitenzi – IMB – Kunyumbulisha maneno katika hali zifuatazo kwa  kupigia mstari kinyumbulishi hicho kinachoonesha kazi (hali) hiyo.

                (i)       Hali ya urejeshi  .......................................................................................

               (ii)      Njeo..........................................................................................................

   (iii)     Hali ya ukanushi nafsi ya tatu umoja.....................................................

 (iv)       Hali ya kutendwa..................................................................................

 (v)        Hali ya kutendeka..................................................................................

   (b)    Ainisha maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo:

(i)                 Samia anasoma vizuri   ____________________________________________

(ii)              Vizuri vinaliwa na matajiri    _______________________________________

(iii)            Vyombo vizuri vimenunuliwa  ______________________________________

(iv)             Huyu ni mkorofi.  _______________________________________________

(v)               Baba na mama wanapendana sana ___________________________________

4.  (a) (i)          Nini maana ya mofimu?

 (ii)       Ubainishaji wa mofimu huzingatia mambo kadhaa. Taja mambo manne (4) yanayomwezesha mtumiaji wa lugha kubainisha mofimu.

(b) Mzee Kimbo alinunua kamusi na kumpatia binti yake aitwaye Fatma. Binti yule alipoifungua ndani ile Kamusi aliona picha na michoro mingi katika sehemu mbalimbali ya ile Kamusi. Akamuuliza baba yake, ‘Kwani hizi picha na michoro ina kazi gani? Mbona kama zinajaza tu nafasi na kuifanya Kamusi iwe kubwa na nzito? Inanipa kazi kuibeba!! Msaidie Mzee Kimbo kujibu swali hilo kwa kutoa hoja tano za kumuelewesha binti yake.

_____________________________________________________________________

SEHEMU C: (Alama 20)

MAWASILIANO NA MATUMIZI YA LUGHA

5.        (a)      Nini maana ya lugha fasaha?

_________________________________________________________________

_________________________________________________________________

_________________________________________________________________

(b)      Onesha madhara manne (04) yanayoweza kutokea endapo mtumiaji wa lugha  hatatumia lugha fasaha.

6.        Baini makosa katika sentensi zifuatazo kwa kupigia mstari, kisha ziandike vizuri         kuepuka makosa hayo.

(a)   Duka la madawa limefungwa.

____________________________________________________________________

(b)   Chai imeingia nzi.

____________________________________________________________________

(c)   Sisi wote tulikusanyika uwanjani.

____________________________________________________________________

(d)   Nyinyi mnapenda kula matunda?

____________________________________________________________________

(e)   Hakuna mtu yoyote aliyechelewa kufika.

____________________________________________________________________

SEHEMU D: (Alama 30)

FASIHI KWA UJUMLA

7.      Tungo zifuatazo zinafanana vipera mbalimbali vya tanzu za fasihi simulizi. Baini vipera hivyo katika kila tungo zifuatazo:

(a)   Kuku wangu katagia mibani _____________________________________________

(b)   Aso hili ana lile  _______________________________________________________

(c)   Nitasikiliza nikusikie kukusikia nitasikia kwa kusikia sauti yako 

      ____________________________________________________________________

(d)   Mchuma janga hula na wa kwao

___________________________________________________________________________

(e)   Papai limevia nyumbani lakini siwezi kulila

____________________________________________________________________

8.      Baadhi ya watu hudai kuwa utungaji wa majigambo ni mgumu sana lakini kutunga majigambo si jambo gumu asilani.

Thibitisha kauli hii kwa kuandika kanuni tano (5) za kuzingatia katika uandishi wa majigambo.

(i)     ____________________________________________________________________

___________________________________________________________________________ _______

(ii)  __________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________

(iii)                        __________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________ ________

(iv) __________________________________________________________________________

___________________________________________________________________________

(v)____________________________________________________________________________

__________

_____________________________________________________________________________ ____

9.      Wewe ni mwanafunzi wa Kidato cha Pili ambaye una rafiki wa Kidato cha kwanza. Rafiki yako amekuomba umfafanulie maana ya maneno yafuatayo ili aweze kuelewa zaidi, kwani darasani hakuelewa vizuri. Msaidie rafiki yako kwa kumfafanulia maneno yafuatayo:

(i)     Vichekesho ___________________________________________________________

_______________________________________________________________________________ ________

(ii)  Mtindo ______________________________________________________________

_______________________________________________________________________________ ________

(iii)                        Lakabu_______________________________________________________________ ______________________________________________________________________________

(iv)Soga ________________________________________________________________

_______________________________________________________________________________ ________

(v)   Dhamira _____________________________________________________________

_______________________________________________________________________________ ________

SEHEMU E: (Alama 15) UANDISHI/UTUNGAJI

10. Wewe ni mwanafunzi wa kidato cha Pili, ukiwa likizo kijijini kwenu Mafyati kilichopo Wilaya ya Nachingwea S.L.P. 99 Nachingwea, serikali ya kijiji imeandaa sherehe ya makaribisho ya mwenge. Katika sherehe hiyo miongoni mwa wanaotarajiwa kualikwa ni pamoja na Mkuu wa Mkoa. Kwa niaba ya serikali ya kijiji, Andika barua ya kumualika kiongozi huyo katika sherehe hiyo. Anuani ya Mkuu wa Mkoa ni S.L.P. 602, Lindi. Jina lako liwe HALIM SAID au HALIMA SAID.

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 91  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 91  

Nambari ya Mtahiniwa.....................................................

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MITIHANI YA KUJIPIMA KWA KIDATO CHA PILI

NUSU MUHULA WA KWANZA

2021-MACHI

MUDA SAA 3

Maelekezo.

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C Zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12)
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A and B na maswali matatu (3) kutoka sehemu C
  3. Sehemu A ina alama kumi na tano (15), sehemu B alama arobaini (40) na sehemu C INA ALAMA arobaini na tano (45).
  4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali.
  5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  6. Andika namba yako ya mtihani katka kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A ( Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

  1. Soma habari hii na kisha jibu maswali yafuatayo hapa chini;

Giza totoro jukwaani. Sauti ya mtoto aliaye na mshichana anamwongoa kwa wimbo.

“Oowa Oowa mtoto Oowa

Usilie mtoto usilie

Mama kaenda kazini O-owa

Baba kaenda kazini O-owa

Kukuletea haluwa O-owa

Owa Owa mtoto.....

Mara kwawaka umeme na fujo yaanza. Mayowe ya wanawake wanaoomboleza kwa kelele sana na kwa sauti ya kusikitisha sana. Taa zaanza kuwaka polepole na wanawake watatu wanapanda jukwaani polepole. Wawili wanapiga mayowe sana na kulia kwa kwikwi. Mmoja wa hao asikitisha sana maana ni mtoto mbichi wa kama miaka 16 hivi ana mimba na amevaa matambara; mikono kichwani akilia sana. Wa pili ana mtoto mchanga mkononi aliyfunikwa vizuri – mama huyu pia amevaa vizuri lakini analia kwa uchungu. Wa tatu anayepanda jukwaani mbele ana mtoto mgongoni, kitunga kikukuu-kuu alichojiangika begani na tita la kuni kichwani.  Amelemewa sana na mizigo hiyo. Yeye halii lakini anaonyesha huzuni na ananungunika. Mara kwa mara awatazama hao wawili waliao na kusema huku waliao wakipunguza mayowe – asema huku akitua tita la kuni na kitunga.

(kwikwi zangungua)

MKE III: Basi wanangu basi, subira huvuta heri. 

Tulieni msijighasi epukeni shari. 

Shikeni ngao, msi, mjitetee mjisetiri. 

Ajifanyao, jabari sawia mwondoeni.

    (kwikwi)

(huku akifutafuta machozi)

MKE II Subira huvuta heri, walishasema wahenga 

Kwetu ilileta shari, kamwe haikutukinga. 

Na waliao majabari, vipi tutawapinga?

 Dunia hii ya mawi, dunia ya wanaume

MKE III Juhusi huleta pato, na penye nia njia 

Shupaeni mpate pito, mpate mnayoania. 

Futeni yenu majuto, msigange yalopita.

Yalopita si ndwele, gangeni yanayokuja.

MKE I (Akifutafuta machozi)

 Tugange yanayokuja, si ndwele yaliyopita. 

Ela bado yanakuja, ya mbele hayajapita.  

Yafuliza moja moja yaja yakitusuta. 

Kwenye dunia ya wawi, dunia ya wanaume

MKE III Fungateni masombo, tayari kupia vita. 

Ondoeni ulimbo, ambao unawavuta 

mwende charazwa fimbo, hayo myakatae kata

Mnyakue wenu uhuru, mpate kunufaika

 MKE II Tawezaje nufaika, uhuru kuunyakua?

Il’hali twahangaika, kila kipembe kufukuta

Ili tupate kupika, wanetu wapate kua

Nasi twazidi konga, kunyonywa na kunyanyaswa?

MKE III Hayo msiyakubali, kuwa ni yenu jaala

Maisha muyamikie, fanyeni hala hala

Utumwa muuondoe, nao wapige lahaula

Wakose wa kunyonya, wakome kuwanyanyasa

 MKE I  Mama hebu nisikiza, name nataka kusema

   Kabla ya kuwachagiza nao wapate kukoma

   Kwanza tutajiuliza, yetu hali kuisoma

   Tujielezee vyema, ulivyo unyonge wetu.

 MKE II Kiko kingine kipenge’ lazima tuufahamu

   Uovu pia unyonge, wa wetu mahasimu

   Ndipo nao tujikinge, pas na kujihujumu

   Bila hayo kuyajua, kamwe hautafaulu.

 MKE III Yafuteni machozi, muweze tena kucheka,

   Kicheko ambukizi, nipate name kucheka

   Nipate maliwazi, niweze kufuhahika.

   Pigeni mioyo konde, mpate wenu uhuru.

 MKE I + II (Waangaliana kutabasamu na kusema pamoja......)

   Haki tutapigania, hadi mwisho wa malimwengu

   Vipi wao wamilkia, raha za ulimwengu

   Dini na pia sheria, mrututu twala uchungu

   Patupu twaambulia ila tabu na dhiki?

   (kwa sauti ya juu)

   Tumechoka, tumechoka, mzigo huu kuubeba

   Nao sasa twawatwika, vijana na kina baba

   Wapate nao kuchoka wajue tabu kubeba

   Huku ukitukanwa, kunyonywa na kunyanyaswa

   Mizigo tuliyopewa, haya yetu maumbile

   Siyo ya kuongezewa, vibaya itukalile

   Miamba, wana kuzaliwa, miezi ya uwele

   Si mchezo, si masikhara, ni mzigo mzito kubeba

   (Kwa Kelele)

   Wanawake tuungane, mabibi tuungani

   Haki zetu kuzidai, tusikubali kunyonywa

   Dunia haiwi yao tuka.........

 MKE III (Akiwakadiza)

   Basi basi wangu

   Anzeni jitegemea, muondoe kupuuzwa

   Muweze jifurahisha msiwe mkigandamizwa

   Msikubali kunyanyaswa, kuonewa (Kwa sauti)

 MKE I  (Akiwasogelea watazamaji)

   Nanyi wake wenzangu, amkeni msidanganywe

   Fikirini malimwengu, jitokezeni munene

   Vueni haya,  machungu, tuungane tupigane

   Uhuru wetu na haki, lazima tutazipata

       -TUTAZINYAKUA.

 MKE II Ole wenu waume, myanyasao wake zetu

   Mlio mapaka shume, itafika zamu yenu

   Mshike jembe kiume, kuauni mama zenu

   Mlowanyonya bila haya, karne nenda

   Karne rudi AMKENI MJITEGEMEE

 MKE I + II Hatutakubali tena, kunyonywa twawaapia

   Tuliponynywa sana, na mkoloni mlaaniwa

   Pamoja tulipigana, uhuru kunyakuliwa

   Leo tumepata uhuru, imekuaje mtuangamize

   ONDOENI WENU UBEBERU

   Ikiwa mumekubali, kiuchumi kutawaliwa

   Kwetu sis ni muhali, na nyinyi kuumbuliwa 

   Mliofanywa mafahali, gumba wasothaminiwa

   Wakoloni wawanyonye, nanyi mutunyonye sis?

   KATU HATUNYONYWI MARADUFU

   Vueni wenu ugumba, na ubeberu uacheni

   Dua sote twaomba, uchumi tufanikisheni

   Watoto tunaoumba, waishi stareheni

   Pamoja tushikamane, Kujenga dunia bora

   TUUNGANI KATIKA USAWA

   Njia panda tumefika, ya mababu, ya kisasa

   Yetu twataka kufyeka, maana twacha visa

   Vya fisi mhadithika, tuepuke lake kosa

   Waume tushikamane, kujenga dunia bora

   TUUNGANE KATIKA USAWA.

MASWALI

  1. (a) Taja na onesha kwa mifano dhamiri 3 zilizojitokeza

(b)Onesha mgogoro uliopo katika habari hii

 (c) Eleza kwa ufupi ujumbe wa mwandishi

  1. (a) Kwa mifano dhahiri elezea vipengele viwili vya matumizi ya lugha

(b) Onesha aina mbili za maleba yaliyotumika.

SEHEMU B

UTUMIZI WA LUGHA NA USAHIHI WA MAANDISHI

  1. (a) Eleza maana ya kielezi kwa kutoa mfano wa sentensi moja.

.................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

(b) Kwa kila tungo uliyopewa pigia mstari kielelezi na kisha taja ni cha aina gani

  1. Darasani kuna utulivu mkubwa
  2. Wanafunzi wanaimba kimasihara
  3. Mwalimu amerudi tena
  4. Nitaondoka wiki inayokuja

(c) Fafanua utata uliopo katika sentensi zifuatazo:

  1. Mama anafurahia pango

................................................................................................................................................................................................................................

  1. Mwalimu analima barabara

................................................................................................................................................................................................................................

  1. Alimpigia ngoma

  1. Baba anaunda

  1. Tafadhali nipe sahani ya kulia

................................................................................................................................................................................................................................

  1. (a) Mnyumbuliko ni nini

........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

(b) Kwa kutumia mifano, taja dhima nne za mnyumbuliko katika lugha ya Kiswahili;

........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

(c) Taja kazi nne za lugha katika jamii

  1. ................................................................................................................
  2. ................................................................................................................
  3. ...............................................................................................................
  4. ................................................................................................................

SEHEMU C

SARUFI

  1. (a) Eleza dhima za mofimu zilizopigwa mstari katika maneno yafuatayo:

Sitaki:.....................................................................................................

Amekiondoa.............................................................................................

Wamejiua.................................................................................................

Umesoma..................................................................................................

Mazungumzo.............................................................................................

(b) Eleza maana ya utilahi zifuatazo;

  1. Uambishaji.....................................................................................
  2. Mzizi...............................................................................................
  3. Sarufi.............................................................................................
  4. Kiimbo.............................................................................................
  5. Kitendawili.......................................................................................
  1. (a) eleza njia tano za uundaji wa maneno ya Kiswahili kwa kutoa mfano mmoja kwa kila njia.
  1. ..............................................................................................................
  2. ..............................................................................................................
  3. ..............................................................................................................
  4. ................................................................................................................
  5. ...............................................................................................................

(b) Nyambua maneno yafuatayo katika kauli ya kutendeka

  1. Imba........................................................................................................
  2. Lima........................................................................................................
  3. Oga.........................................................................................................
  4. Piga..........................................................................................................
  5. Soma.......................................................................................................

SEHEMU D

FASIHI KWA UJUMLA

  1. (a) Taja sifa tano (5) za fasihi simulizi;
  1. ..............................................................................................................
  2. ..............................................................................................................
  3. ..............................................................................................................
  4. ................................................................................................................
  5. ...............................................................................................................

(b) Taja vipengele vitano (5) vinavyounda fani katika kazi ya fasihi;

  1. ..............................................................................................................
  2. ..............................................................................................................
  3. ..............................................................................................................
  4. ................................................................................................................
  5. ...............................................................................................................
  1. (a) Makazi ni njia mojawapo za uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi. Taja njia tano za uhifadhi kwa kazi za fasihi.
  1. ..............................................................................................................
  2. ..............................................................................................................
  3. ..............................................................................................................
  4. ................................................................................................................
  5. ...............................................................................................................

(b) Fasihi ina umuhimu gani kwa jamii. Taja

SEHEMU E

UTUNGAJI/UANDISHI

  1. Kwa kutumia mchoro taja sehemu au muundo wa barua ya kikazi.

..................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

1 | Page

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 52  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 52  

MTIHANI WA NUSU MUHULA KISWAHILI KIDATO CHA PILI

MUDA : SAA 2:00       APRIL, 2020

MAELEKEZO:

  • Mtihani huu una sehemu A,B,C,D na E.
  • Jibu maswali yote katika sehemu zote
  • Majibu yote yaandike kwenye nafsi zilizowekwa.

SEHEMU A :UFAHAMU

1. Soma kifungu cha habari kifuatacho, kasha jibu maswali yanayofuata, kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.

Afrika ni bara tajiri lenye rasilimali nyingi na adhimu. Utajiri wa bara hilo hauendani na utajiri wa wenyeji wa bara hilo, yaani waafrika. Yapo mambo mengi yanayosababisha mambo mbalimbali yaende ndivyo sivyo. Yapo ya kihistoria, kiuchumi, kisiasa na kiutawala.

Nchi mbalimbali za kiafrika hukabiliwa na majanga lukuki . majanga hayo tunaweza kuyagawa katika aina kuu mbili, nayo ni majanga ya asili na “majanga watu”. Majanga ya asili ni kama vile tetemeko la ardhi, mafuriko, ukame, mlipuko wa volcano na vimbunga. Majanga haya hutokana na nguvu za asili za dunia ambazo zipo juu ya uwezo wa binadamu. Aidha, “majanga watu” ni kama vile rushwa, matumizi mabaya ya madaraka, upendeleo, ufujaji wa mali ya umma, matumizi mabaya ya rasilimali za nchi, wivu, choyo na ubinafsi.

Haya yote uwepo wake hutokana na harakati za binadamu katika jamii husika. Kuna watu katika mfumo wa serikali hufumba macho na kuyaziba masikio ili wasione na kusikiliza kilio cha walalahoi. Kati ya watu hao likuki nchini, anajitokeza shujaa mwokozi. Shujaa huyu anaizunguka nchi yake nzima kujinadi kuwa yeye ni mzalendo,atawatoa kutoka nchi dhalimu na kuwavusha kwenye bahari ya misukosuko na mazila mengi hadi kwenye nchi tulivu ya asili na maziwa. Sauti kali inamtoka, ikipasua miamba na kuvunja kila aina ya hofu na uovu wa maneno. Sauti ilijipenyeza masikioni hadi mioyo ya wanajamii kote nchini. Wananchi wake wakampenda na kujipatia tumaini jipya. Hivyo, basi kwa kutumia “vichinjio” vyao wakakata shauri kumpa nafasi ili hatamu aishike. Ama kweli, tabia ni kama ngozi ya mwili, haibadiliki.

Maswali 

(i) Kichwa cha habari chafaa kuwa:- 

A. Utajiri wa Afrika 

B. Uongozi mbaya Afrika 

C. Uchumi wa nchi za Afrika 

D. Rasilimali za Taifa 

(ii) Majanga watu yanaweza kuwakilishwa na:- 

A. Rushwa na mafuriko

B. Ufisadi na ubinafsi

C. Uchoyo na Kimbunga 

D. Ukabila na volcano.

(iii) Majanga ya asili katika jamii ni kama vile:- 

A. Radi na mafuriko   B. Tetemeko la ardhi na ufisadi

C. Kimbunga na ukabila  D. Choyo na wivu. 

(iv) Neno walala hoi lina maana gani kama lilivyo tumika kwenye habari? 

A. Watu wliochoka sana 

B. Watu wanaolala wakiwa hoi 

C. watu maskini wa kipato cha chini 

D. Watu walioumia sana 

(v) Rasilimali za nchi ni kama vile 

A. Misitu ina wanyamapori

B. Gesi asilia na majengo 

C. Hifadhi za taifa na viwanda 

D. Madini na biashara

(vi) Kulifumbia macho jambo maana yake ni:- 

A. Kufumba macho 

B. kuliziba jambo Fulani 

C. Kutoliona jambo Fulani 

D. Kupuuza na kutolizingatia jambo Fulani.

(vii) Shujaa kujinadi kuwa yeye ni mzalendo; maana yake ni:-

A. mgombea wa nafasi ya uongozi kuwa mzalendo

B. shujaa kuwa na uzalendo wa kweli katika jamii 

C. Mgombea nafasi ya uongozi kuwashawishi wananchi ili wamchague ili apambanie hali zao nay a nchi 

D. Shujaa kujinadi kwa mbwembwe na maneno mengi ya ushawishi

(viii) Baadhi ya wanajamii waliopewa dhamana ya kuongoza jamii zao wanalaumiwa kwa:- 

A. Kutenda kinyumbe na ahadi walizotoa 

B. Kuwa wazalendo na wapambanaji.

C. Kuanguka nchi nzima kujinadi 

D. Kupenda nchi na jamii yao 

(x) Mwandishi anatuambia nini katika habari hii?

 A. Majanga watu ni mengi sana.

 B. Viongozi wajinadi nchi nzima ili wapewe fursa. 

 C. Bara la Afrika lina rasilimali nyingi.

 D. Ili kujenga jamii mpya na bara ni lazima kuyaondoa majanga watu 

(x) Bahari ya misukosuko na madhila mengi kama ilivyotumika kwenye habari, maana yake ni:- 

A. Nchi zenye matatizo na mahangaiko mengi 

B. Nchi yenye bahari nyingi 

C. Nchi yenye faida nyingi 

D. Nchi yenye rasilimali mbalimbali.

Andika ufupisho wa habari ulivyoisoma kwa maneno kati ya 50 na 70.

……………………………………………………………………………………………………………………………………….

………………………………………………………………………………………………………………………………………..

…………………………………………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………………………………………...

SEHEMU B:20%

UTUMIZI WA LUGHA NA USAHIHI WA MAANDISHI.

Eleza umuhimu na kutumia lugha fasaha

(i) ………………………………………………………………………………………………………………………………..

(ii) ……………………………………………… ………………………… ………………………………………...

(iii) ………………………………… ………………………………… ………………………………………..

(iv) …………………………………… ………………………………… ………………………………...

(v) ……………………………… …………………………………………… ……………………………….

Eleza kwa mifano dhima tano (5) muhimu za lugha katika mawasiliano.

(i) ……………………………………… ……………………………… ……………………………… ……

(ii) ……………………………… ………………………………… ……………………………………

(iii) …………………………………… ………………………… …………………………………

(iv) ……………………………………… ………………………………… ……………………………………………

(v) …………………………… ……………………………………… ………… ……………………………

(a) Tambulisha maeneo ya asili wanayotoka wazungumzaji wa Lugha zifuatazo:-

(i) Aisee chalii wangu twende zetu ngarenaro.

………………………………………………………………………………………………………………………………

(ii) Chamaki nchanga kimbanika njuli chana

 ………………………………………………………………………………………………………………..

(iii) Aroo nenda nenda kure karare

 …………………………………………………………………………………………………………………

(iv) Aise Mangi siku hisi biashara ni mbaya ni mbaya kweli

 …………………………………………………………………………………………………………………

(v) Mwe! Mihogo imecheleza balaha shambani 

 …………………………………………………………………………………………………………………

  (b) Tambulisha itaofa wa wazungumzaji wa lugha zifuatazo:-

 (i) Mtoto yako inaishi fashi gani?

  ……………………………………………………………………………………………………………………

 (ii). Am ! am ! sisi iko kuja Tansazia mara kwa mara 

  ……………………………………………………………………………………………………………………

 (iii) Bibi yangu inaishi na nyanya yangu kule Kaunti. 

  ……………………………………………………………………………………………………………………

 (v) Chijana vuipi? Jikaza Chiume 

  ……………………………………………………………………………………………………………………

SEHEMU C: 25%

SARUFI.

taja aina za maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo:

(i) Amina ndiye aliyeleta hii zawadi

 ………………………………………………………………………………………………………………………………

(ii) Kuimba kwake kumemfurahisha Kasisi 

 ………………………………………………………………………………………………………………………………

(iii) Chumbani kumevurujika 

 ………………………………………………………………………………………………………………………………

(iv) Nenda nje ukapunge hewa 

 ……………………………………………………………………………………………………………………………..

(v) Hata wewe umekosea 

 …………………………………………………………………………………………………………………………….

Toa maana ya maneno yafuatayo na kasha kila neno ulitungie sentenzi moja.

(i) Vipukusi.

 ………………………………………………………………………………………………………………………………

 ………………………………………………………………………………………………………………………………

 ………………………………………………………………………………………………………………………………

(ii) Barakoa 

……………………………………………………………………………………………………………………………..

 ………………………………………………………………………………………………………………………………

 ………………………………………………………………………………………………………………………………

(iii) Kiwiko 

 ………………………………………………………………………………………………………………………………

 ………………………………………………………………………………………………………………………………

 ………………………………………………………………………………………………………………………………

(iv) Corona 

 ………………………………………………………………………………………………………………………………

 ………………………………………………………………………………………………………………………………

 ………………………………………………………………………………………………………………………………

(v) Karantini 

 ………………………………………………………………………………………………………………………………

 ………………………………………………………………………………………………………………………………

 ………………………………………………………………………………………………………………………………

Eleza kwa mifano dhima tano za mofimu:

  1. ……………………………………………………………………………………………………………………
  2. ……………………………………………………………………………………………………………………
  3. ……………………………………………………………………………………………………………………
  4. ……………………………………………………………………………………………………………………
  5. ……………………………………………………………………………………………………………………

SEHEMU D:

FASIHI SIMULIZI 15%

Eleza sifa tano bainifu za fasihi simulizi.

  1. ……………………………………………………………………………………………………………………
  2. ……………………………………………………………………………………………………………………
  3. ……………………………………………………………………………………………………………………
  4. ……………………………………………………………………………………………………………………
  5. ……………………………………………………………………………………………………………………

SEHEMU E:15%

UANDISHI.

Andika barua kwa mdogo wako anayeishi Mwanza na umwelezee tahadhari ya kupambambana na homa kali ya mapafu ya “Covid 19”. Anuani yako ni, S.L.P 120, Tanga na anuani ya mdogo wako ni S.L.P 112, Mwanza.

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 10  

FORM TWO KISWAHILI EXAM SERIES 10  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256