FORM ONE HISTORIA MIDTERM EXAMS
OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

 MTIHANI WA ROBO MUHULA WA KIDATO CHA KWANZA

HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI

MUDA: SAA 2:30 MWAKA: 2026

MAELEKEZO

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C.
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A, B na C kwa wekevu na umakinifu.
  3. Sehemu A na ina jumla ya alama kumi na tano (15) na sehemu B inajumla ya alama sabini (70) na sehemu C ina alama 15.
  4. Zingatia maelekezo ya kila swali na kila sehemu
  5. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi za mtihani ulizopewa.
  6. Vifaa vyote vya mawasiliano na visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.

SEHEMU A (Alama 15) 

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika kipengele (i) mpaka cha (x) kisha andika herufi ya jibu sahihi katika sehemu ya karatasi ya mtihani uliyopewa

i. Somo la Historia ya Tanzania na Maadili linajumuisha dhana kuu ngapi?

  1. Moja
  2. Mbili
  3. Tatu
  4. Nne

ii. Historia inahusu mambo gani?

  1. Mambo ya sasa
  2. Mambo yaliyopita
  3. Mambo yajayo
  4. Mambo ya kubuni

iii. Ni kwa nini ni muhimu kujua historia yetu?

  1. Ili kuishi maisha ya anasa
  2. Ili kusafiri nchi za nje
  3. Ili kuelewa tulikotoka, tulipo, na tunakokwenda
  4. Ili kuwa maarufu

iv. Mabadiliko gani yamekuwa yakizingatiwa katika historia ya Tanzania?

  1. Mabadiliko ya hali ya hewa
  2. Mabadiliko ya teknolojia pekee
  3. Mabadiliko ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi
  4. Mabadiliko ya michezo

v. Maadili ni nini?

  1. Miongozo inayotawala tabia ya mtu na jamii
  2. Sheria za nchi
  3. Tamaduni za nchi za nje
  4. Mambo ya kidini tu

vi. Maadili yana umuhimu gani kwa taifa?

  1. Kujenga majivuno
  2. Kukuza uhasama
  3. Kutambulisha utu wetu, kujenga heshima, na kuleta maendeleo
  4. Kuleta machafuko 

vii. Somo la Historia ya Tanzania na Maadili linatusaidiaje?

  1. Kujenga chuki
  2. Kuelewa mila, desturi, na maadili ya jamii za Tanzania
  3. Kuiga tamaduni za kigeni
  4. Kuacha mila zetu 

viii. Ni nini umuhimu wa somo la Historia ya Tanzania na Maadili?

  1. Kujifunza lugha za kigeni
  2. Kujenga moyo wa kuipenda, kuilinda, na kuiheshimu nchi yetu
  3. Kusafiri duniani
  4. Kuwa na mali nyingi

ix. Somo la Historia ya Tanzania na Maadili linahusiana na masomo gani mengine?

  1. Jiografia, Hisabati, Kiswahili, Kiingereza, Chakula na Lishe, Sanaa na Michezo, Muziki, na Kilimo
  2. Fizikia na Kemia pekee
  3. Biashara na Ujasiriamali pekee
  4. Ufundi na Teknolojia pekee

x. Ni kwa nini maadili ni muhimu katika jamii?

  1. Huleta fujo
  2. Huleta ubaguzi
  3. Huleta amani, upendo, na maelewano
  4. Huleta vita

MAJIBU

i

ii

Iii

iv

v

vi

vii

viii

ix

x











2. Oanisha SAFU A kwa kutoa jibu sahihi kutoka katika SAFU B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika visanduku chini yake.

SAFU A

SAFU B

  1. Historia
  2. Maadili
  3. Jamii
  4. Ukoo
  5. Kabila


  1. A. Miongozo inayotawala tabia ya mtu na jamii 
  2. Mkusanyiko wa watu wenye uhusiano wa damu na asili moja
  3. Mambo au matukio yaliyopita yenye athari kubwa kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni
  4. Kitendo cha mtu binafsi, familia, kundi kubwa au jamii nzima kuondoka sehemu moja ya makazi na kwenda sehemu nyingine
  5. Kundi la watu wanaozungumza lugha moja na huwa na mila na desturi za aina moja
  6. Mkusanyiko wa watu kwa ujumla wake

MAJIBU

I

ii

iii

iv

v






SEHEMU B (Alama 70) 

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. Eleza ni kwa jinsi gani uhamiaji umechangia katika mabadiliko ya kijamii na kiuchumi katika jamii za Kitanzania?

i. ______________________________________________________________________ 

ii. ________________________________________________________________________ 

iii. ________________________________________________________________________ 

iv. ________________________________________________________________________ 

v. ________________________________________________________________________

4. Tanzania ina takribani makabila mia moja na ishirini na kila kabila lina utamaduni wake wa asili pamoja na mila na desturi zake . Taja makabila manne makuu yanayopatikana Tanzania, na utaje asili ya kila kabila.

i. ________________________________________________________________________ 

ii. ________________________________________________________________________ 

iii. ________________________________________________________________________ 

iv. ________________________________________________________________________ 

v. ________________________________________________________________________

5. Watanzania wengi katika jamii ya leo tumetokana na wabantu kwani lugha nyingi za makabila nchini Tanzania hufanana matamshi pia hata maana. Eleza kwa kutoa mifano mitano (05) shughuli za kiuchumi na kijamii za jamii za Kibantu.

i. ________________________________________________________________________ 

ii. ________________________________________________________________________ 

iii. ________________________________________________________________________ 

iv. ________________________________________________________________________ 

v. ________________________________________________________________________

6. Kwa kutoa mifano dhabiti eleza uhusiano kati ya somo la Historia ya Tanzania na Maadili na masomo mengine kama vile

i) Jiografia ________________________________________________________________________ ________________________________________________________________________ 

________________________________________________________________________ 

ii)Hisabati. ________________________________________________________________________ ________________________________________________________________________

________________________________________________________________________

7. Taja baadhi ya mambo yanayozingatiwa katika historia ya Tanzania.

i. __________________________________________________________________ 

ii. __________________________________________________________________ 

iii. __________________________________________________________________ 

iv. __________________________________________________________________ 

v. __________________________________________________________________

8. Jamii huusisha watu wa sehemu tofauti tofauti kwakulijua hilo, wewe ukiwa kama mwanafunzi wa kidato cha kwanza fafanua dhana ya jamii na vipengele vyake.

i. __________________________________________________________________ 

ii. __________________________________________________________________ 

iii. __________________________________________________________________ 

iv. __________________________________________________________________ 

v. __________________________________________________________________

9. a) Nini maana ya maadili

________________________________________________________________________ ________________________________________________________________________

________________________________________________________________________

b) Toa faida (04) nne za maadili katika taifa la Tanzania

i. __________________________________________________________________ 

ii. __________________________________________________________________ 

iii. __________________________________________________________________ 

iv. __________________________________________________________________

SEHEMU C (Alama 15)

Jibu swali namba 10

10. Shule ya Sekondari ‘’KATWE’’ kulikua na mgongano baina ya wanafunzi wa kidato cha kwanza ‘’a’’ wakidai kwamba somo la historia ya Tanzania na maadili halina faida kwao huku kidato cha kwanza ‘’b’’ hawajui somo linahusu nini kabisa. Wewe ukiwa kama mtaalamu wa historia na maswala ya utamaduni wasaidie wanafunzi wa kidato cha kwanza ‘’a’’ na ‘’b’’ katika shule ya ‘’KATWE’’ kujua umuhimu wa somo hilo.

FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 240  

FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 240  

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA KUMALIZA NUSU MUHULA KIDATO CHA KWANZA

HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI 2025

MUDA 2:30

MAELEKEZO

1. Karatasi hii Ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi 10

2. Jibu maswali yote kwenye nafasi ulizopewa 

3. Sehemu A na C Zina alama kumi na Tano (15) Kila na sehemu B Ina alama sabini (70)

4. Zingatia maelezo ya Kila sehemu na ya Kila swali 

5. Andika jina lako juu ya karatasi hii.

 

SEHEMU A. Alama 15

1. Chagua jibu sahihi kutoka machuguzi uliopewa kwa vipengele (i)- (x) kasha andika jibu lake katika nafasi uliopewa.

i) Somo la historia ya Tanzania na maadili linaundwa na dhana kuu mbili nazo ni

  1. Historia ya Tanzania na maadili
  2. Historia kuhusu mambo au matukio yaliyopita
  3. Historia ya Tanzania na Tehama
  4. Historia ya Tanzania na utu

 ii) Ni miongozo inayotawala tabia na matendo ya mtu mmoja mmoja au jamii kwa ujumla. dhana hii imebebwa na neno

  1. Maadili
  2. Huruma
  3. Tanzania
  4. Historia

iii) Neno maadili linapotumika huweza pia kuashiria au kuimarisha Tunu za jamii au taifa ni zipi Kati ya zifuatazo

  1. Uhuru na Amani
  2. Amani na furaha
  3. Furaha na unyenyekevu
  4. Unyenyekevu na upendo

vi) Tunaweza kuwakaribisha wageni kwa furaha na kuwapa heshima kubwa ikiwa pamoja na kukirimiwa kwa 

  1. Chakula na malazi
  2. Chakula na malezi
  3. Chakula na kuoga
  4. Chakula na heshima

v) Mazingira ya kiliografia yanaweza kuathiri shughuli za binadamu kama vile 

  1. Biashara,utamaduni,kilimo na uhamaji wa watu
  2. Biashara,uchumi,siasa, na mazingira
  3. Uchumi,jamii,uvuvi, na uwindaji
  4. Uwindaji,ukusanyaji,ulinzi na mazingira

vi) Kwa kutumia uchambuzi wa makabila Tanzania ni nchi yenye makundi ya makabila yote yanayopatikana barani Afrika makundi hayo ni

  1. Wabantu ,wakichembe,wakushito na wanilo
  2. Wabantu,wangoni,wamakonde na wazaramo
  3. Wakichembe,Wabantu,wahaya na wanyakyusa
  4. Wanilo,wakushito,wakichembe,na wapemba

vii) Kihistoria kundi kubwa la tatu la watanzania ambalo ni jamii ya wafugaji walioingia nchini Tanzania wakitokea kusini mwa sudani ni 

  1. Wabantu
  2. Wanilo
  3. Wakushito
  4. Wakichembe

viii) Jamii za wakushito zinahusisha makabila kama 

  1. Wairaki,wagorowa, na waburugi
  2. Wamasai,wapare na Wairaki
  3. Wameru,Wamasai na Hadzabe
  4. Hadzabe,Tindiga, na Wairaki

ix) Kwa hapa Tanzania jamii za Wanilo ni kama 

  1. Wamasai,wajaluo, na wadatoga
  2. Wamasai Wairaki, na wadatoga
  3. Wadatoga,wajaluo na Hadzabe
  4. Hadzabe,Tindiga na Wairaki

x) Morani ni kundirika katika jamii ya kimasai la vijana wenye umri Kati ya miaka

A) 18 na 35

B)18 na 40

C)18 na 60

D) 18 na 80

 

2. OANISHA JIBU LA ORODHA 'A' NA JIBU LA ORODHA 'B'

ORODHA A

ORODHA B

  1.                     Wakichembe
  2.                   Wanilo
  3.                 Wabantu
  4.                 Mitala

 

  1. Hutumia lugha ya kugongagonga ulimi
  2. Wairaki na wagorowa
  3. Wadatoga na Wamasai
  4. Wahadimu,watumbatu na wapemba
  5. Ndoa za wake wengi

 

 

SEHEMU B. Alama 70

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. Mkude ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya wavulana buingu . Ameshindwa kuelewa maana ya maneno yafuatayo kwenye somo la historia ya Tanzania na maadili. Msaidie kumuelezea maana ya maneno hayo.

a) Tunu za taifa

b) maadili

c) Jiografia

d) Jamii

e) wajibu

4. Ukiwa kama mwanafunzi wa kidato cha kwanza mkondo A waelezee wanafunzi wenzako umuhimu wa kuwa na maadili katika jamii na taifa kwa ujumla.

5.Warioba ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza alichaguliwa na jamii yake kuelezea namna ambavyo vijana wanaweza kujengwa kwa kuwa na tabia njema. Msaidie warioba katika kuwaeleza vijana vitu vinavyojenga tabia njema katika jamii zetu nukta Tano.

6. Ukiwa Kama mwanafunzi kutoka shule ya sekondari chekeleni. waelezee wanafunzi wenzio kwanini jamii za Asili ya kitanzania zilihama kutoka eneo Moja kwenda eneo jingine nukta Tano

7. Kwa kutumia nukta Tano tofautisha jamii za Asili za wakichembe na jamii za Asili za kibantu.

8. Kwa kumtumia mtaalamu "EMILE DURKHEIM" (1884) Toa dhana ya neno 'Jamii'

9. Eleza Tofauti iliyopo Kati ya maadili yaliyojengwa katika jamii za Asili na jamii za sasa za kitanzania

SEHEMU C Alama 15

Jibu swali la kumi

Bainisha changamoto za kukuza maadili katika jamii unamoishi na Kisha toa mapendekezo ya jinsi ya kuzitatua.

 

 

FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 201  

FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 201  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256