FORM ONE KISWAHILI MIDTERM EXAMS

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

UPIMAJI WA KIDATO CHA KWANZA NUSU MUHULA

MACHI -2024

KISWAHILI

SEHEMU A: UFAHAMU

Alama 15

  1.      Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata

        UKIMWI ni upungufu wa kinga mwilini. Upungufu huu wa kinga mwilini husababishwa na aina ya virusi vinavyo shambulia chembechembe hai nyaupe zilizomo ndai ya damu. Chembechembe hizo nyeupe za damu ndizo zinazojenga kinga ya mwili dhidi ya majonjwa. Uharubifu wa chembechembe hizo baadaye hufikia kiwango ambacho huufanya mwili upoteze kinga yake dhidi ya maradhi. 

       Virusi hivyo vinashambulia chembechembe nyeupe ndani ya damu vimepewa jina la Virusi vya UKIMWI, Kwa kifupi (VVU). Katika mwili wa binadamu virusi hivi huishi katika majimaji ya mwilini.

      Virusi vya ukimwi sio UKIMWI, kuna tofauti kubwa kati ya mtu mwenye VVU na mgonjwa wa UKIMWI. Kama ilivyoelezwa VVU ni Virusi ambavyo hushambulia chembechembe hai nyeupe zinazojenga na kulinda mwili, lakini UKIMWI ni ile hali ya mtu kukosa kinga ya mwili kiasi kwamba akipata ugonjwa wowote, unamshambulia sana na haponi kwa haraka.

       Baada ya kuambukizwa mtu anaeza kuishi na VVU hata miaka kumi bila kuonyesha dalili yoyote ya ugojwa wa UKIMWI. Hivyo huezi kujua kama mtu ana VVU kwa kumangalia kwa macho tu. 

Maswali

  1.             Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyoisoma, kisichozidi maneno matano
  2.             Andika kirefu cha UKIMWI
  3.             Virisi vya UKIMWI vina madhara gani mwilini mwa binadamu?
  4.             Kuna tofauti gani kati ya UKIMWI na VVU?
  5.             Fafanua kazi ya chembechembe nyeupe za damu katika mwili wa binadamu.

SEHEMU B: SARUFI

Alama 30

2.  Elezea maana ya maneno yafuatayo

  1.             Nomino
  2.             Kitenzi
  3.             Kielezi
  4.             Kuvumishi
  5.             Kihisishi

3. Ainisha maneno yaliopigiwa mistari katika tungo zifuatazo.

  1.     Mti mkavu umekatwa
  2.  Banda la kuku limejengwa vibaya
  3.                         Wanafunzi  wangu wamefaulu mtihani
  4.                         Yule ni mwizi
  5.   Twiga hutembea kwa madaha

4.  Taja aina nne za sarufi

SEHEMU C: MAWASILIANO NA MATUMIZI YA LUGHA

Alama 30

5. Eleza madhara matano yatakayojitokeza endapo mtimiaji wa lugha hatatumia lugha fasaha

6. Kwa sentensi zifuatazo andika kweli au si kweli

  1.     Lugha ni kitambulisho muhimu cha jamii
  2.  Fani na maudhui ni anyanja kuu za lugha
  3.                         Umbo, sauti na mpangilio na maana ni tanzu ne za sarufi
  4.                         Mawasiliao ya binadami hutunia zaidi vyombo vya habari na simu tu
  5.   Lugha hubadilika kutokana  na mazingira

7. Maneno yafuatayo yana maana zaidi ya mbili kwa kila neno. Taja maaana mbili lwa kila neno

  1.     Tende
  2.  Paa
  3.                         Nyanya

8. Eleza faida nne za kutumia lugha fasaha

SEHEMU D: FASIHI KWA UJUMLA

Alama 10

9. Tegua Vitendawili vifuatavyo.

  1.                Gari langu halitumii mafuta
  2.                Napigwa faini kosa silijui
  3.                Kamba yangu ndefu lakini haifungi kuni
  4.                Ukiona njigi utazani njege na ukiona njege utazani njigi
  5.                Nyumba yangu ndogo lakini wapangaji wengi
  6.                Nasika mkeka lakini nalala chini
  7.                Kila aendako huacha alama
  8.                Nikimpiga mwanangu watu hucheka
  9.                Anatembea na nyumba yake
  10.                Nyumba yangu ina nguzo moja

SEHEMU E: UANDISHI WA INSHA / UTUNGAJI

Alama 15

10.  Mwandikie barua rafiki yako umwelezee hali halisi ya masomo ilivyo shuleni kwenu.

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 163  

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 163  

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA KUJIPIMA

KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA

MUDA : SAA 2:00

MAELEKEZO.

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B, C, D na E.
  2. Jibu maswali yote kama ilivyoelekezwa katika kila sehemu.
  3. Zingatia mwandiko mzuri, Mpangilio na usahihi wa majibu yako.
  4. Majibu yote yaandikwe kwenye karatasi za kujibia.

SEHEMU A UFAHAMU (Alama 10)

  1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kasha jibu maswali yafuatayo.

Aaah! Maskini ya Rabiee! Hii ndiyo nchi tuliyomo sisi!.  Nchi inayovuja jasho ,nchi masikini, nchi ambayo wanawake huvaa nguo _ _ _ _! Nchi ambayo wanawake huvaa nywele za maiti_ _ _Haya ndiyo maendeleo yetu_ _ _ _.

Haki na usawa katika nchi masikini ni ndoto. Wengi huamua kuwa mabubu mara tu deemokrasia inapopokonywa na watu wachache. Huu ni Unafiki mkubwa.Haki haipo nchini mwetu ila tu tumefumbwa macho, Tumekuwa Vipofu.

Mimi nimeamua kupambana, nitachukua panga_ _ _ nitachukua pinde _ _ _ nitachukua mishale _ _ _ nitapigana kufa na kupona. Nitapigania haki na usawa.Haki! Haki! Usawa Haki! Haki_ _ _ _ maana yake nini.

MASWALI

  1. Andika kichwa cha habari hii _______________________________________________________
  2. Je mwandishi analaani juu ya nini? __________________________________________________
  3. Taja matatizo manne ambayo mwandishi anayakemea
  1. _____________________________________________
  2. _____________________________________________
  3. _____________________________________________
  4. _____________________________________________

d) Haki na usawa vitapatikana kwa njia gani? ____________________________________________

e) Andika maana ya maneno yaliyopigiwa mstari.

 (a) Inapopokonywa.

 (b) Unafiki.

 (c) Vipofu.

SEHEMU B (Alama 30)

UTUMIZI WA LUGHA.

  1. Kwa kutumia mifano toa maana ya maneno yafuatayo.

(a) Kidahizo.   (b) Kitomeo.   (c) Kamusi.

(d) Lugha.   (e) Sherehe.

  1. (a) Kwa kutumia matumizi ya Kiswahili sanifu, sentensi zifuatazo zina makosa. Ziandikwe upya kwa ufasaha.

                    Kwa mfano

  • Kiti mkubwa amevunjika.

                            Usahihi- Kiti kikubwa kimevunjika.

  1. Chai imeingia nzi.
  2. Anakwenda baba kesho safari.
  3. Humwambiaga lakini haelewi.
  4. Ng’ombe zangu zimeibiwa.
  5. Daktari nina kifua sijalala usiku kucha.

(b)  Andika athari tano za kutotumia lugha kwa ufasaha.

  1. (a)  Taja matumizi matano(5) ya kamusi.

(b)  Kamusi hugawanyika katika sehemu ngapi? Zitaje.

(c)  Taja mambo mawili yanayopatikana katika utangulizi wa kamusi.

SEHEMU C:  (Alama 20)

SARUFI

  1. (a)  Kitenzi kikuu huweza kutumika sambamba na kitenzi kingine kukamilisha sentensi. Kwa kuandika upya sentensi katika karatasi uliyopewa, Bainisha vitenzi vilivyotumika katika sentensi zifuatazo.

                  Mfano

- Amina alikuwa anakula chakula kitamu.

      Ts       T

  1. Mgeni wangu amekwisha wasili.
  2. Amina hakutaka kumuhudhi.
  3. Mafundi wote wanashona viatu.
  4. Wataendelea kumsubiri hadi kesho.
  5. Gari lilikuwa limeharibikia mlimani Kitonga.

(b)   Ainisha maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo.

  1. Viti vizuri viwili vimevunjika.
  2. Ah! alitaka kuja shuleni.
  3. Wewe ndiye ndugu yangu.
  4. Wachezaji wote walifanya mazoezi ya viungo.
  5. Ndizi hizi zimeoza.
  1. (a)   Tunga sentensi moja kwa kila neno lililoandikwa kwa hati mcharazo.
  1. Vizuri kama kiwakilishi.
  2. Vizuri kama kivumishi.
  3. Vizuri kama kielezi.
  4. Mama kama Nomino.
  5. Mama kama kihisishi.

(b)  Tunga sentensi zenye miundo ifuatayo:-  kwa kupigia mstari sentensi hiyo kuonesha aina hizo 

        za maneno.

             Mfano:    N   +   T  +  E  =

                  Mama anapika jikoni.

        N         T        

  1. H  + N +  T +  E
  2. N  +  V  +  V +  TS  +  Ts  +  T
  3. W  +  t  +  N  +  V
  4. W  +  V + T
  5. T

SEHEMU D:  (Alama 30)

FASIHI    

  1. (a)  Sanaa ni nini?

(b)  Nakili kisha ukamilishe kielelezo kifuatacho.

(a)Fasihi ina dhima/kazi mbalimbali katika jamii. Taja tano (5) na uzieleze kwa ufupi.

(a)   Taja vipengele vitano (5) vinavyounda Fani katika kazi ya fasihi.

(b)   Taja vipengele vitano (5) vinavyounda Maudhui katika kazi ya fasihi.

SEHEMU E:    (Alama 10)

UTUNGAJI.

10.   Mwandikie barua rafiki yako umweleze kuhusu hali halisi ya masomo ilivyo shuleni kwenu. 

         zingatia taratibu za uandishi wa barua za kirafiki katika uandishi wako.

1

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 84  

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 84  

Nambari ya mtahiniwa...............................................

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MITIHANI YA KUJIPIMA KWA KIDATO CHA KWANZA

NUSU MUHULA WA KWANZA

2021-MACHI

MUDA SAA 2

Maelekezo.

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C Zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12)
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A and B na maswali matatu (3) kutoka sehemu C
  3. Sehemu A ina alama kumi na tano (15), sehemu B alama arobaini (40) na sehemu C INA ALAMA arobaini na tano (45).
  4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali.
  5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  6. Andika namba yako ya mtihani katka kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A ( Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

UFAHAMU

  1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali kwa kuandika hrufi ya jibu sahihi katika jedwali lilichorwa chini ya swali.

Watu wote walirudi makwao. Shida ilienea katika nchi ya Kufikirika. Watu walikuwa hawakufanya kazi kwa muda wa miaka sita mfululuzo kwa sababu wote walishughulika katika kutafuta tiba ya ugumba wa Mfalme na utasa wa Malkia. Hasara zilizotokea katika muda ule zilikuwa ni kubwa na nyingi; hata zilikuwa hazilingani na hasara zozote nyingine ambazo wato wa Kufikirika waliweza kukumbuka kuwa waliziona zamani katika nchi yao. Mashamba yalitupwa.  Mitambo, vinu na viwanda vilikuwa havina watu. Mazizi na maghala yalikuwa tupu kabisa.  Nusu ya sarafu na majohari katika hazina ilipotea. Kazi katika mashimo na nyingine zilifungwa. Waandishi walitupa chini kalamu zao na wanazuoni waliacha vitabu vyao wazi.

Nchi ambayo zamani ilikuwa ya shibe, utajiri, nguo, tafriji na neema zote sasa ilikuwa imegeuka nchi ya njaa; umasikini na uhitaji wa kila namna ulikuwa mbele ya watu. Maisha haya mapya yalisumbua watu sana hata yakawa hayavumiliki. Afya ya watu ilitishwa na maradhi. Vifo vilitokea kwa wingi mno.  Shida hii ilipaswa kuzuiwa au Wafikirika wote wangalipanguswa katika uso wa ardhi, ilikuwa ni wajibu wa kila mtu kutenda awezavyo kujisaidia mwenyewe, watoto wake nan chi yake. Basi baada ya marejeo kila mtu alijitia katika kazi yake kwa bidii zote.

Isipokuwa watoto, Wafikirika wote walikuwa wana desturi ya kufanya kazi kwa muda mwingi kuliko watu wote katika mataifa mengine ya dunia. Muda wa kufanya kazi katika nchi yao ulikuwa ni saa kumi na mbili. Saa mbili zilitumiwa kwa maburudisho katika michezo saa mbili nyingine zilikuwa ni za mapumziko na saa nane ni za kulala katika kila saa ishirini nan ne au siku moja.  Vitanda vilikuwa havina watu juu baada ya muda wa saa nane za kulala isipokuwa wagonjwa na watoto wadogo wadogo tu. Kama si kwa sababu ya faida ya afya hata saa nane za kulala zingalipunguzwa kuwa saa saba au sita tu. Shauri la kupunguza wakati wa kulala lilipelekwa mbele ya madiwani wan chi ya Kufikirika na wasimamizi wa kazi. Lilikubaliwa na halmshauri ndogo lakini halikufaulu katika halmashauri kuu kwa sababu ilidhaniwa kuwa hofu ya hatari juu ya maisha itakuwa kubwa sana. Kwa hivi halikupata idhini ya serikali.  Wafikirika walikuwa na umoja madhubuti ambao ulisimama imara mbele ya machafuko yoyot. Shauri moja jema lilikubaliwa na kushangiliwa na wot na baya lilikataliwa na kila mtu.

Wafikirika waliweza kufanya kazi bora na za kuajabisha mno wakati wa mataifa mengine walipokuwa wamo katika usingizi, uvivu, anasa au uzembe. Kutwa walikuwa katika kazi na katika fikira za kujistawisha. Mtu ambay hafanyi kazi kwa muda wa saa kumi na mbili alikuwa na aibu kwa mwenziwe; hasara kwa serikali na kwake mwenyewe. Kumwita mtu mvivu katika Kufikirika ilikuwa si dhihaka ya kusameheka ila hatia kubwa mno kwa sababu nchi hiyo haikuwa na mtu mvitu hata mmoja. Kwa sheria za Kufikirika uvivu ulikuwa una tafsiri ya wizi wa wakati.  Mwizi wa wakati alipatilizwa kwa adhabu ngumu sawa na mwizi wa mali au kitu kingine. Kazi kubwa, ngumu na nzito kwa watu wa Kufikirika zilikuwa ni sawa sawa kabisa na mabandia ya mchezo kwa watoto wadogo. Ari ya kila mtu ilikuwa ni kutenda tendo kubwa na lililo bora kuliko mwingine. Hii ni desturi inayodumu hata sasa katika nchi ya Kufikirika

MASWALI;

  1. Kichwa cha habari kinachofaa kwa habari hii ni;
  1. Kufikirika     d) Maisha ni shida
  2. Kilimo katika nchi ya kufikirika e) Maisha mapya yenye faraja
  3. Magtokeo ya kutofanya kazi
  1. Wananchi wa Kufikirika waliacha kufanya kazi kwa muda mrefu kwa sababu;
  1. Walikuwa wamechoka  
  2. Walipewa likizo    
  3. Mfalme wao alikuwa mgonjwa
  4. Malkia alikuwa mgonjwa
  5. Walikuwa wanatafuta tiba ya Mfalme wako na mke wake
  1. Mwandishi anasema “shida hii ilipaswa kuzuiwa au Wafikirika wote wangalipanguswa katika uso wa ardhi” ana maana kuwa;
  1. Watalazwa ardhini   d) Watavuna mazao bora
  2. Wangekufa    e) Watawajibika ipaswavyo kwa mfalme wao
  3. Watalima mazo mengi
  1. Wananchi wa Kufikirika waliipenda kazi kuliko usingizi kwa sababu:
  1. Muda wao mwingi waliutumia kufanya kazi
  2. Ilikubaliwa na halmashauri yao
  3. Waliamriwa hivyo na serikali yao
  4. Waliogopa machafuko
  5. Walikuwa tayari kupunguza muda wao wa kulala kufikia sass aba usiku au sita kwa siku.
  1. Shauri la kuongeza saa za kufanya kazi ililipelekwa mbele ya madiwa na hawa;
  1. Walikubaliana na pendekezo hili
  2. Walipinga muswada huo
  3. Walikubaliana lakini wakalipeleka mbele kwa uamuzi
  4. Walifurahi bila kutoa uamuzi
  5. Waliwafukuza walioleta pendekezo hilo.
  1. Mwandishi anasema usingizi unamsaidia Mwanakufikirika kuwa;
  1. Mpiganaji bora    d) Mnyonge
  2. Mfanyakazi mwenye uchovu  e) Mkulima hodari
  3. Mwananchi mwenye afya bora
  1. Mwandishi anaposema “Umoja madhubuti uliosimama imara” ana maana ya;
  1. Umoja sharti usimame  d) Kupata idhini ya serikali
  2. Umoja usiotetereka  e) Umoja ni dhihaka inayosamehewa
  3. Umoja si nguvu
  1. Asiyefanya kazi katiak nchi ya Kufikirika alifananishwa na;
  1. Jangili     d) Mpenda anasa
  2. Mvivu wa kutupwa   e) Mzemb e
  3. Mwizi wa mali au kitu chochote
  1. Mwandishi anaposema “anapatilizwa” ana maana kuwa
  1. Anafanya jambo   d) anapokewa
  2. Anahukumiwa   e) anabatizwa
  3. Anasamehewa
  1. Juhudi ya kutokubali kushindwa bali kufanikiwa ilioneshwa na kila Mwanakufikirika kwa;
  1. Kufanya kazi kila siku
  2. Kutumia muda wao kuburudika
  3. Kupenda michezo
  4. Kufanya kila jambo vizuri zaidi kuliko Mwanakufikirika mwingine
  5. Kuwa mabandia wa michezo

MAJIBU

i

ii

iii

iv

v

vi

vii

viii

ix

x

SEHEMU B (ALAMA 25)

  1. (a) Andika neno lenye kosa katika tungo zifuatazo:

Mfano: 

  1. Mama anakaa au huoni:

Kosa.  Anakaa

  1. Juma anapanga nyumbani

Kosa......................................................................

  1. Mama anasomaga kitabu

Kosa......................................................................

  1. Daktari ameniunga mkono wangu wote

Kosa........................................................................

  1. Mwalimu anapiga kula kumchagua Raisi

Kosa.......................................................................

  1. Kyama chetu cha Mapinduzi kimeshindwa

Kosa..........................................................................

  1. Mtoto anariaria nini? Hapa sipendi mimi

Kosa,........................................................................

 (b)Taja nchi tano unazozifahamu zinatumia lugha ya Kiswahili;

  1. .....................................................................................
  2. ....................................................................................
  3. ....................................................................................
  4. ....................................................................................
  5. ....................................................................................

(c) Ukioanisha Orodha A na orodha B utapata muunganiko ulio sahihi. Andika herufi inayoleta usahihi ikioanishwa Orodha A na Orodha B.

ORODHA A

ORODHA B

  1. Barua pepe
  2. Irabu
  3. Lugha ya mazungumzo
  4. Kiswahili
  5. Anakula
  1. Kitenzi
  2. Njia ya mawasiliano
  3. Sauti
  4. Maumbo
  5. Tanzania
  6. Lugha inayotumika Zanzibar
  7. Aina ya lugha ya Kiswahili
  8. Hutumia mdomo katika matumizi yake

MAJIBU

Orodha A

i

ii

iii

iv

v

Orodha B

 (d) Kuna Irabu ngapi katika maneno yafuatayo;

 Mfano

  1. Anasoma

Irabu 2

  1. Atacheza

Irabu ...........................................

  1. Palilia

Irabu............................................

  1. Sambamba

Irabu.............................................

  1. Katisheni

Irabu............................................

  1. Amesomoa

Irabu............................................

 (e) Panga majina yafuatayo kwa mtiririko unaotakiwa;

  1. Zawadi
  2. Juma
  3. Annarose
  4. Matayo
  5. Kalamu

Andika kwa mpangilio mzuri

  1. .....................................................................
  2. .....................................................................
  3. .....................................................................
  4. .....................................................................
  5. ....................................................................

SEHEMU C (ALAMA 15)

SARUFI

  1. (a) Pigia msitari vivumishi katika maneno yafuatayo;
  1. Mtu huyu anaimba vizuri
  2. Wale wanacheza mpira mzuri
  3. Yeye ni mchawi katika kijiji hiki
  4. Wale wa shangazi wamefaulu

(b) Taja aina za vitenzi

  1. .........................................................................
  2. .........................................................................
  3. ...........................................................................
  4. ..........................................................................

(c) Tunga sentensi kwa kutumia

N + T

W +V + T + E

T

SEHEMU D (ALAMA 40)

FASIHI KWA UJUMLA

  1. (a) Katika Orodha A kuna methali zinazofanana na methali za orodha B.  chagua methali za Orodha B zinazofanana na Orodha A na kisha kujaza herufi katika kisanduku hapo chini.

ORODHA A

  1. Mtoto umleavvyo ndivyo akuavyo
  2. Usipo ziba ufa utajenga ukuta
  3. Haraka haraka haina Baraka
  4. Kujikwaa sio kuanguka bali ni kwenda mbele
  5. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu

ORODHA B

  1. Siko la kufa halisikii dawa
  2. Samaki mkunje anali mbichi
  3. Bandu bandu humaliza gogo
  4. Polepole ndio mwendo
  5. Kufa kufaana
  6. Kukopa harusi kulipa matanga
  7. Kukosea njia ndio kujua njia

MAJIBU

Orodha A

i

ii

iii

iv

v

Orodha B

(b) Taja aina tano za wanyama zinazoweza kutumika katika kazi ya fasihi mara kwa mara zaidi kwenye hadithi.

  1. .........................................................................................
  2. .........................................................................................
  3. .........................................................................................
  4. .........................................................................................
  5. ..........................................................................................

(c) Katika habari ifuatayo taja methali tano (5) zilizotumika.

Wanadamu huwa kwenye mambo mengi magumu sana lakini wali deni mchuzi karadha na hivyo mafanikio yatakuwepo. Kadhalika Mungu hufufua mfu kitangani kwani bila yeye tusingeweza sisi wanadamu. Mungu ni mtoa hukumu, mauti ni faradhi, ni lazima wote tupite huko. Mkono mtupu haulambwi lakini kwa maneno hayo hayana nafasi katika utukufu wa Mungu. Tunapaswa kupambana na maisha na mwisho tufanikiwe na si kutoa lawama tu kwani mlevi si mnywa tembo hata mla mali hulewa. Tusiende mienendo isiyo  mizuri.

  1. ...........................................................................................................
  2. ...........................................................................................................
  3. ...........................................................................................................
  4. ........................................................................................................
  5. .......................................................................................................

(d) Taja nyenzo tano zinazotumika katika uchongoji

  1. ..............................................................................
  2. .............................................................................
  3. .............................................................................
  4. .............................................................................
  5. .............................................................................

(e) Andika habari kuhusu historia ya maisha yako;

....................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

1 | Page

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 52  

FORM ONE KISWAHILI EXAM SERIES 52  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256