?>
OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA MUHULA WA PILI MWEZI
SOMO: HISTORIA NA MAADILI YA TANZANIA DARASA: TATU
MUDA: SAA 1:00 SEHEMU
A: Chagua jibu sahihi zaidi na uandike herufi katika sehemu husika.
1. i. Ipi kati ya zifuatazo huonesha Amani na uhuru wa mtu na mali zake?
ii. Maadilia mazuri hufanya mtu kusaidia na ________________ watu.
iii. Mambo yafuatayo hupatikana kwenye mazingira ya nyumbani isipokuwa ______.
iv. Mtu mwenye mamlaka ya kufanya moja kwa moja na kusimamia wengine ni ______________.
v. Kujiunga na vyama na kikundi bila vikwazo nchini hujulikana kama ___________.
SEHEMU B:
2. Oanisha fungu A na Fungu B ili kupata maana sahihi iliyokusudiwa.
NA | KIFUNGU A | MAJIBU | KIFUNGU B |
i. | Mfano wa mawasiliano mabaya katika jamii | [ ] |
|
ii. | Kitendo cha kumdharau mtoto | [ ] | |
iii. | Njia inayotusaidia kushiriki katika kutatua matatizo ya wengine | [ ] | |
iv. | Kitu chochote kinachofaa kutokana na mazingira asili | [ ] | |
v. | Mwongoza na kanuni za maadili ambazo zinadhibiti tabia ya mtoto shuleni. | [ ] |
SEHEMU C:
3. Tumia maneno ya kwenye kisanduku kujaza nafasi zilizoachwa wazi.
Majukumu, uvumilivu, ustahimilivu, haki, uaminifu.
i. Kuwa mkweli na muwazi ________________________.
ii. Vitu ambavyo mtu anastahili na anapaswa kupewa ________________________.
iii. Uwezo wa kuishi na watu hata kama mnatofautiana kimawazo ______________________.
SEHEMU D:
4. Kamilisha jedwali lifuatalo na kujaza maana ya rangi za bendera ya Taifa
NA | RANGI YA BENDERA | MAANA YAKE |
i. | Kijani | |
ii. | Manjano | |
iii. | Samawati | |
iv. | Nyeusi | |
5. Angalia mchoro ufuatao kwa makini kisha jibu maswali yanayofuata
Maswali
i. Taja alama ya Taifa ambayo imeoneshwa hapo juu _________________________________________.
ii. Umuhimu wa alama hii ni _____________________________________________________________.
iii. Alama hii utaipata wapi mara nyingi? ____________________________________________________.
iv. Taja alama nyingine mbili za taifa ambazo unaziona hapo juu ______________________________ na _____________________________
6. Soma kifungu cha habari kwa makini kisha jibu maswali yafuatayo::
Ni muhimu sana kutunza mwili wako, akili na nafsi kila siku na sio tu wakati unaumwa. Hili linawezekana kwa kula vyema, kufanya mazoezi, kupunguza mawazo na kwenda mapumzikoni mwili unapohitajika. Mambo haya yatafanya ukae mwenye furaha, mwenye afya na mstahimilivu.
Maswali
i. Kifungu hiki kinahusu nini? ______________________________________________________.
ii. Njia tatu za kutunza miili yetu ni _________________________________________________, _________________________________ na ______________________________________.
iii. Taja vitu vitatu tunapaswa kuzingatia ili kuwa na afya.
(a) _______________________________________
(b) ________________________________________
(c) _______________________________________.
iv. Unafikiri nini kitatokea tukishindwa kutunza miili yetu? ___________________________________________.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZHISTORIA STANDARD THREE EXAM SERIES 114
OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MTAA
MTIHANI WA NUSU MUHULA AGOSTI 2025
MTIHANI WA DARASA LA III
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI
1. Andika herufi ya jibu sahihi kwenye mabano
(i). Elimu inayohusu matukio yaliyotokea nchini Tanzania tangu mwanzo wa maisha ya watu mpaka leo inaitwaje?
(ii). Kipi kati ya vitendo vifuatavyo ni kitendo cha maadili mema?
(iii). Mfululizo wa mambo yaliyotokea katika maisha yetu katika vipindi tofauti huitwaje?
(iv). Hayati John Pombe Magufuli alifariki tarehe 17 mwezi Machi 2021. Je, katika Maisha yetu hili ni tukio gani?
(v). Ipi ni faida mojawapo ya vitendo vya kimaadili?
2. Oanisha fungu A na fungu B ili kupata maana kamili
Fungu A | Fungu B |
(i). Tukio la kihistoria [ ] (ii). Kumpa pole rafiki yako aliyejikwaa [ ] (iii). Kufanya kazi kwa ushirikiano [ ] (iv). Kusema uongo [ ] | A. Tendo la huruma B. Tendo lisilo la maadili C. Uhusiano mwema D. Mwaka wa kuzaliwa |
3. Jaza nafasi zilizo wazi kwa kuchagua neno kwenye mabano
(i). Kusaidiana katika jamii huleta ................................................. (umoja na mshikamano/chuki)
(ii). Kusalimia wakubwa ni tendo la ........................................................................... (adabu/huruma)
(iii). Kupigana shuleni ni tendo la ............................................................................... (upendo/ukatili)
(iv). Historia huelezea matukio ............................................................................ (yajayo/yaliyopita)
4. Chunguza matendo kwenye jedwali lifuatalo kisha weka alama ya vema (√) kwenye sehemu inayohusika kuainisha kama ni tendo linalofaa au lisilofaa.
Tendo | Tendo linalofaa | Tendo lisilofaa |
(i). Kuwasalimia wazazi |
|
|
(ii). Kuiba matunda |
|
|
(iii). Kuomba msamaha unapokosea |
|
|
(iv). Kutukana wenzako |
|
|
5. Soma habari kisha jibu maswali
Vyanzo vya taarifa za Historia ya Tanzania ni vitu mbalimbali vinavyotuwezesha kupata taarifa za matukio yaliyowahi kitokea hapa nchini. Vyanzo hivyo ni kama kusikiliza masimulizi, kusoma vitabu na makumbusho ya Taifa. Vyombo vya habari na tovuti vinaweza pia kuwa ni vyanzo vya kupata taarifa za kihistoria. Vyanzo vya taarifa ya Historia ya Tanzania hutusaidia kupata taarifa za matukio yaliyowahi kutokea katika nchi yetu. Mfano wa tukio la kihistoria ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao ulifanyika tarehe 26 Aprili 1964.
MASWALI
(i). Je, ni upi umuhimu wa vyanzo vya taarifa za historia ya Tanzania? . . . . . . . . . . . . ...
(ii). Chanzo cha taarifa za historia ya Tanzania ambacho huhusisha mazungumzo ya mdomo kinaitwajwe? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...
(iii).Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulifanyika lini? . . . . . . . . . . . . . . . . . . ... . . .
(iv). Taja vyanzo viwili tu vya historia ya Tanzania.
(i) . . . . . . . . . .. . .. ii. . . . . . . . . . .....
6. Tizama picha ifuatayo, kisha jibu maswali
|
(i).Picha hiyo inaonesha mazingira ya wapi? . . . . . . . . . . . . . . . ...
(ii).Je, ni akina nani unawaona kwenye picha hiyo? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .
(iii).Hao Watoto unaowaona kwenye picha wamesimama. Unadhani kwanini wamesimama? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...
(iv).Unafikiri tendo wanalolitenda kwa kusimama ni la heshima au dharau? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..
LEARNINGHUBTZ.CO.TZHISTORIA STANDARD THREE EXAM SERIES 102
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA KUJIPIMA KWA SHULE ZA MSINGI
MACHI 2025
DARASA LA TATU HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI
2. Andika majibu matendo yasiyofaa au yanayofaa
i. Kutokupenda kufanya kazi
ii. Kuwahi shuleni
iii. Kuchelewa kurudi nyumbani
iv. Kutoroka shuleni
v. Kuwasaidia wasiojiweza
3. Toa majibu katika maswali yafuatayo
i. Historia ya Tanzania ni elimu kuhusu matukio yaliyojitokea nchini
ii. Maadili ni nini? ……………………….
iii. Historia inaweza kuhusu maisha yetu binafsi, familia au ………………
iv. Raisi wa awamu ya pili wa Jamuhuri ya muungano alikuwa anaitwa…………
v. Kuwasaidia mzigo watu wazee ni miongoni mwa matendo katika jamii ………………..
SEHEMU B: 4. JIBU NDIYO AU HAPANA
i. Kuwathamini na kuwalea wazee ni matendo ya kimaadili
ii. Kuwaheshimu watu waliokuzidi umru sio jambo la kimaadili
iii. Kusema ukweli ni jambo la kimaadili
iv. Sehemu mojawapo ya vyanzo vya historia ya Tanzania ni makumbusho ya taifa
v. Kuwanyanganya na kuwadhalilisha ni jambo la kimaadili
LEARNINGHUBTZ.CO.TZHISTORIA STANDARD THREE EXAM SERIES 99