KISWAHILI FORM THREE NEW NECTA FORMAT

THE PRESIDENT'S OFFICE

MINISTRY OF REGIONAL GOVERNMENT AND LOCAL GOVERNMENT

AUGUST-SEPTEMBER   EXAMINATION SERIES

KISWAHILI  FORM-3

2020

TIME: 2:30 HRS

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali matatu (3) kutoka sehemu C.
  3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali.
  4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  5. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo katika kijitabu chako cha kujibia.

(i) Neno lipi kati ya maneno haya linaweza kudokeza mtenda au mtendwa?

  1. Kiunganishi   
  2. Kivumishi
  3. Kihisishi 
  4. Kiwakilishi 
  5. Kielezi

(ii) Shamba letu li kubwa neno “Li” ni aina gani ya neno? 

  1. Kiwakilishi 
  2. Kielezi 
  3. Kivumishi 
  4. Kiunganishi 
  5. Kitenzi kishirikishi

     (iii) Lugha fasaha hufuata taratibu za lugha, taratibu hizo ni pamoja na 

A       fonolojia, mofolojia, semantiki na sintaksia

B        maana, matamshi, muundo na maumbo

C        maana, matamshi, muundo na mantiki

D        kiimbo, shada, mkazo na toni

E.       fonolojia, mkazo, shada na semantiki

(iv) Kamati ya lugha ya Afrika ya Mashariki (the interteritorial Swahili language committee) iliteua lahaja moja na kuisanifisha, lahaja hiyo ilikuwa ni

A         kimvita             

 B       kiunguja

C         kimtang’ata       

D        kisiu

E         kivumba

(v). Watoto hawa wanacheza vizuri neno “Vizuri” ni aina gani ya neno? 

  1. Kivumishi 
  2. Kielezi 
  3. Kiwakilishi 
  4. Kivumishi cha sifa 
  5. Kihisishi 

 

(vi) Kiswahili ni kibantu kwa kuwa:- 

  1. Kinaongewa na wabantu wengi 
  2. Ni lugha ya Taifa 
  3. Kina maneno mengi ya kibantu 
  4. Kimethibitishwa kiisimu na kihistoria 
  5. Wasomi wengi wamethibitisha hivyo.  


(vii) Ni jambo gani linalodhihirisha upekee wa kazi fulani ya kifasihi? 

  1. Muundo 
  2. Mtindo 
  3. Wahusika 
  4. Jina la mtunzi  
  5. Jina la kazi husika 


(vii) Ipi ni fasili sahihi kuhusu tungo? 

  1. Maneno yanayoonesha uhusiano baina ya neno moja na jingine. 
  2. Kipashio kidogo katika lugha kinachotumika kama dhana ya kuchambulia lugha Fulani. 
  3. Matokeo ya kuweka na kupanga pamoja vipashio sahili ili kujenga vipashio vikubwa zaidi. 
  4. Kipashi cha kimuundo chenye neno moja na kuendelea 
  5. Maneno yenye kutoa maana kamili


(viii) Nini maana ya sentensi sahili. 

  1. Ni sentensi yenye kishazi kuu kimoja au zaidi pamoja na kishazi tegemezi.
  2. Ni sentensi yenye kishazi huru 
  3. Ni sentensi yenye kuonesha masharti 
  4. Ni sentensi yenye maana nyingi 
  5. Ni sentensi yenye vishazi vingi 


(ix) Zifuatazo ni sifa za pijini isipokuwa 

A.      Pijini huwa na maneno kutoka lugha mbili au zaidi

B.      Pijini hutokea kurahisisha mawasiliano baina ya watu ambao kila mmoja 

         ana lugha yake

C.      Miundo ya maneno na tungo katika pijini imerahisishwa ili kukidhi 

         mawasiliano

   D.     Pijini haina msamiati mwa kutosha, hivyo wazungumzaji hutumia sana 

        ishara

  E.    Pijini ina watu ambao kwao hiyo ni lugha yao ya kwanza


2. Katika kila sentensi uliyopewa, orodhesha vishazi huru katika Safu A na vishazi tegemezi katika safu B.
(a) Ngoma hailii vizuri kwa kuwa imepasuka.
(b) Watoto walioandikishwa watakuja kesho.
(c) Kiongozi atakayefunga mkutano amepelekewa taarifa.
(d) Mtawatambua walio wasikivu.
 (e)       Kitabu ulichopewa kina kurasa nyingi. 

 

3. Taja aina za sentensi zifuatazo kisha eleza muundo ujengao kila sentensi.

  1. Maisha ni safari ndefu.
  2. Ukisoma kwa bidii utafaulu kwa kiwango cha juu.
  3. Mtoto aliyelazwa hospitalini ameruhusiwa kwenda nyumbani.
  4. Nitakuja leo ingawa nitachelewa sana.
  5. Alinunua madaftari lakini kitabu cha Kiswahili alipewa na mwalimu.

4. Andika maneno matano ambayo yameundwa kutokana na kufananisha sauti. Kwa kila neno tunga sentensi moja.

5. Eleza dhima za mofimu "li" kama ilivyotumika katika sentensi zifuatazo:

  1. Shamba letu li kubwa sana.
  2. Wlishelewa kurudi.
  3. Tunalifuatilia.
  4. Limeharibika.
  5. Shikilia.

6. Andika sentensi zifuatazo katika hali ya ukanushi:

  1. Ameshiba sana.
  2. Watoto wengi wanaogelea.
  3. Mvua ilinyesha kwa wingi sana.
  4. Kijana anakula chakula kingi.
  5. Mimi nasoma polepole.

7. Bainisha mzizi wa asili kwa kila neno katika maneno yafuatayo:

  1. Anawaandikisha
  2. Mkimbizi
  3. Mlaji
  4. Muumbaji
  5. Nisingelipenda
  6. Kuburudika
  7. Sadifu
  8. Aliokota
  9. Walichopoka
  10. Kipambanuliwe

1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:

Karibu masikio ya watu wa mahali pengi yalijaa habari za Karama na mashtaka yake. Umaarufu wake wa ghafla ulizungumzwa karibu na mbali. Mtu yeyote wa desturi anapozuka katika umaarufu, huyavuta masikio na macho ya watu wengi kwa sababu jambo kama hili hutokea nadra sana kwa watu ambao bahati mbaya imeshughulika kuwaweka nyuma. Kwa hiyo, siku ya tatu ya baraza ilihudhuriwa na mfalme, watu wenye vyeo mbalimbali, pamoja na nusu moja ya umati mkubwa wa Kusadikika. Fikra zilizochanganyika ziliushika umati huu. Baadhi ya watu walimwajabia Karama wakamhesabu kama mtu bora wa karne yao. Hawa walitumaini ataokoka lakini wengine waliwaza kuwa Karama alikuwa kama mjinga aliyekuwa akicheza na hatari kubwa iliyofunua taya mbele yake.

Waliokuwa wakimtazamia kuokoka walikuwa na wasiwasi wao; na wale waliokuwa wakimtazamia kuanguka walikuwa na fadhaa yao. Walakini hapana mtu hata mmoja aliyepata kulisema wazo lake.

Bila ya kujua alivyoajabiwa Karama aliendelea kusema mbele ya baraza, “Watu wanaoteswa ndio wanaoyajua mateso yao.” Kusadikika ilikuwa chini ya mateso makubwa sana. Maisha yao yalizungukwa na maradhi na mauti, uadui usiokwisha, nchi iliyokaribia kugeuka jangwa na mwamba na madhila mengine mazito yaliyowakabili watu. Wanakusadikika walitaka faraja katika mateso haya. Kila jitihada ilijaribiwa ili kuirekebisha saa ya maendeleo ya nchi, lakini mara kwa mara majira yake yalirudishwa nyuma. Kama hili lilifanywa kwa makosa ama kwa makusudi ni siri iliyo ng’ambo ya fahamu zangu hata sasa. Lakini kama siri njema hufichika, ile iliyo mbaya haifichiki hata kidogo. Uchaguzi wa wajumbe ulikuwako lakini hathibitisho ya matokeo ya ujumbe hayakupatikana.

Kusadikika iliishi kuona mjumbe baada ya mjumbe kuadhiriwa na kuadhibiwa vibaya. Kama washauri hawakudhuriwa na hili lakini watu wengine walidhuriwa sana. Kazi njema za wajumbe wawili zilipotea bure. Manung’uniko ya lawama hii yalikuwa katika hewa yote ya Kusadikika.

Hili lilipotokea serikali iliombwa ima faima kufanya ujumbe mwingine. Basi mjumbe wa tatu alitakikana ajitolee mwenyewe kwa ujumbe wa Kusini. Wito wa mjumbe wa tatu uliitikiwa na Kabuli; mtu mwenye busara, haya na mcheshi. Yeye alipatikana upesi kabisa kuliko ilivyokuwa kwa mara ya pili na ya kwanza. Misiba ya Buruhani na Fadhili ilikuwa mikubwa ya kutosha kuikongoa mioyo ya bidii katika bawaba zake. Kabuli aliyajua haya yote lakini alikuwa mtu wa moyo wa namna nyingine kabisa. Alikuwa na bidii kubwa kama ile ya siafu athubutiye kukivuka kijito kwa daraja iliyofanywa kwa maiti ya siafu wengine walioelea majini huko na huko. Maji yalijulikana kuwa na asili ya rutuba, mvuke na umeme. Nguvu nyingine za namna mbalimbali zipo pia katika maji. Kama siafu mdudu mdogo na kipofu wakati mwingine haogopi kuzikabili nguvu hizo pamoja na hatari zake kwa sababu njema, basi ni dhahiri kuwa viongozi wa wanadamu wanapoteswa bure bidii za wafuasi wao hutanuka ajabu.

Hapana tishio liwezalo kuukomesha mwendo huu. Kwa hakika utafululiza kuwako duniani mpaka mateso yakome kabisa, na labda wakati huo dunia hii itakuwa njema kama itamaniwavyo kuwa.

Buruhani na Fadhili walitoa sadaka zao bora ili kuyahimiza majilio ya wakati uliotakikana sana. Kabuli aliwaona watu wawili hawa kama wafadhili wakubwa wa ulimwengu. Alitaka kuwa mshirika wao kwa thamani yoyote ya maisha yake.

Kama ilijulikanavyo, Kusini na upande wa dunia yatokako matufani makubwa na baridi kali sana. Kabuli aliyakabili mashaka haya bila ya kigeugeu. Naam, alikuwa kama mtu aliyekuwa akinywa uchungu bila ya kigegezi. Mara mbili alikamatwa akafanywa mahabusu.

Maswali

(a) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu cha habari:

  1. Fadhaa
  2. Madhila
  3. Kuadhiriwa
  4. Ima faima
  5. Kigeugeu
  6.  Kigegezi.

(b) Eleza mchanganyiko wa fikira walizonazo wana wa Kusadikika kuhusu Karama.

(c) Kwanini bidii ya mjumbe wa Kusini imelinganishwa na bidii ya siafu? Toa sababu mbili.

(d) Ujumbe wa mwandishi wa kifungu hiki unahusu nini?

SEHEMU C (Alama 45)

Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii.

8. Andika insha isiyozidi maneno mia tatu (300) na isiyopungua mia mbili na hamsini (250) kuhusu faida za televisheni kwa jamii.

ORODHA YA VITABU USHAIRI

Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP)

Malenga   Wapya - TAKILUKI (DUP)

Mashairi   ya   Chekacheka - T.A. Mvungi (EP & D.LTD)

RIWAYA

Takadini - Ben J. Hanson (MBS)

Watoto   wa   Maman’tilie - E. Mbogo (H.P)

Joka   la   Mdimu - A.J. Safari (H.P)

TAMTHILIYA

Orodha - Steve Reynolds (MA)

Ngoswe Penzi Kitovu   cha   Uzembe - E. Semzaba (ESC)

Kilio   Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)

10. "Fasihi ya Kiswahili imemweka mwanamke katika hadhi tofauti tofauti." Thibitisha usemi huu kwa kutumia hoja tatu kwa kila riwaya kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.

11. (a) Vigano ni nini?

(b) Tunga vigano kwa kutumia methali isemayo "Umdhaniaye siye kumbe ndiye!"

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM THREE KISWAHILI MODAL SERIES 21

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

   Click Here To Access You Scheme(ONLY IF YOU A HAVE CODE)