KISWAHILI FORM ONE NEW NECTA FORMAT

LEARNING HUB.TZ

MTIHANI WA KUMALIZA MUHULA WA PILI

KISWAHILI KIDATO CHA KWANZA

JINA…………………………………………..DARASA……………………………MUDA: MASAA 2

 

MUDA: MASAA 2½

MAELEKEZO:

  1.                 Jibu maswali yote katika mtihani huu.
  2.                 Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali.

 

Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yafuatayo:

 

 Uharibifu wa mazingira umeenea katika maeneo mengi ya nch yetu kuanzia Kaskazini hadi Kusini, Mashariki hadi Magharibi. Watu wengi wametia pamba masikioni wanapoelezwa na serikali na taasisi zake juu ya kuharibu mazingira.

 Baadhi ya watendaji wa serikali wamekuwa wakipokea mlungula na kufumbia macho suala la uharibifu wa mazingira katika maeneo wanayofanya kazi.

 Baadhi ya shughuli za uharibifu wa mazingira zinazofanywa na watu katika nchi yetu ni uchomaji wa misitu, ukataji wa miti, uharibifu wa vyanzo vya mito, uchomaji wa mkaa, uingizaji wa mifugo katika maeneo yaliyotengwa kuhifadhi mazingira, utiririshaji wa maji taka kwenye mito, maziwa, bahari n.k.

 Madhara yanayopatikana kutokana na uharibifu wa mazingira ni pamoja na ukosefu wa mvua za kuaminika, magonjwa ya mlipuko hususani kipindupindu, taifodi na amweba, jangwa, kukauka kwa vyanzo vya mito n.k.

 Ushauri unatolewa kwa wananchi kutunza mazingira kwani mzaha mzaha hutumbua usaa.

 

MASWALI.

1. i) Eleza maana ya misemo ifuatayo katika kufungu hiki.

(a) Kutia pamba masikioni_____________________

(b) Kupokea mlungula________________________

(c) Mzaa mzaa hutumbua usaa__________________

     ii) Taja shughuli mbili zinazofanywa na watu kuharibu mazingira.

 1.________________________ 2._________________________

     iii) Taja madhara 4 (manne) ya kuharibu mazingira.

 1.________________________ 2._________________________

 3.________________________ 4._________________________

     iv) Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasiyozidi sitini (60).

 

2. Andika barua kwa Mkurugenzi mtendaji Shirika la chakula S.L. P 412 Dar es Salaam, ukimwomba kazi ya ukarani, elimu yako ni kidato cha sita, umri wako ni miaka 20. Jina lako liwe Amani Sana wa S.L.P 76 Mwanza.

3. (a) Kuna tofauti gani kati ya vihusishi na viunganishi, vihusishi na viwakilishi?

    (b) Taja aina za nomino unazozijua.

 

4. (a) Vipengele vifuatavyo vina umuhimu gani katika usimulizi?

 (i) Hadhira_______________________________________________

 (ii) Fanani________________________________________________

 (iii) Uwanja wa kutendea_______________________________________

    (b) Onyesha hatua za uandishi wa barua za kirafiki zisizopungua sita (6).

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

5. Jaza mchoro ufuatao kwa kuonyesha vipera vya tanzu za fasihi simulizi.

 

    FASIHI SIMULIZI

 

 

 

 

 

 

      

 

 

 

LEARNINGHUBTZ.COM.TZ Page 1

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZFORM ONE KISWAHILI MODAL SERIES 8

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256

   Click Here To Access You Scheme(ONLY IF YOU A HAVE CODE)