FORM SIX KISWAHILI NECTA 2014

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL 
ADVANCED CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION 
EXAMINATION  

121/1 KISWAHILI 1

(Kwa Watahiniwa Walioko Shuleni na Wasiokuwa Shuleni)

Muda: Saa 3 Jumatatu, 04 Mei 2014 asubuhi

Maelekezo

1. Karatasi hii ina maswali kumi (10) katika sehemu A, B, C, D na E.

2. Jibu maswali saba (7) kwa kuzingatia maelekezo kutoka katika kila sehemu.

3. Kila sehemu ina alama ishirini (20).

4. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani. 

5. Vikokotozi haviruhusiwi ndani ya chumba cha mtihani.  

6. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A

UFAHAMU

1. Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:

Mwelekeo wa watu umekuwa ama kikwazo au motisha katika matumizi ya Kiswahili hapa Tanzania. Kabla na baada ya uhuru, watu wengi walikiona Kiswahili kuwa duni sana. Wengi walipima elimu ya mtu kutokana na ujuzi wake wa Kiingereza. Kama mtu aliweza kuzungumza, kusoma na kuandika Kiingereza vizuri, basi mtu huyo alichukuliwa kwamba ameelimika sana. Asiyejua Kiingereza alionekana duni na wala hakuweza kuaminika kwamba ana elimu. Kasumba hii ya kukipa hadhi Kiingereza ilidunisha hadhi ya Kiswahili na wala watu wengi hawakuona umuhimu wa kukijua vilivyo. Isitoshe, hata katika kupata kazi mbalimbali mwenye ujuzi wa Kiingereza alifikiriwa kwanza, na hivyo ikaonekana kuwa lugha hiyo ndiyo ufunguo wa ufanisi katika maisha.

Matumizi ya Kiswahili yalijitokeza sana miongoni mwa wakazi wa mjini. Jambo hili lilidhihirika katika kukitumia zaidi kwenye shughuli zao za kila Siku majumbani na kwingineko, kama vile sokoni au kwenye matamasha ya michezo. Lakini kwa bahati mbaya wakazi wa mjini katika enzi hizo za kabla ya uhuru na hata miaka michache baada ya uhuru hawakuwa wengi sana ukilinganisha na wakazi wa vijijini. Wakazi wa vijijini walipenda zaidi lugha za makabila, Kiswahili walikitumia tu pale ilipobidi kutumika na hivyo, walionekana kuwa wamepitwa na wakati.

Athari ya kuamini zaidi katika ujuzi wa Kiingereza kuliko ujuzi wa Kiswahili inapatikana hasa miongoni mwa wananchi waliopata elimu ya sekondari. Kabla ya uhuru na miaka michache baada ya uhuru, wengi kati yao hadi leo, hawaamini kwamba lugha ya Kiswahili inaweza kutumiwa kama lugha ya kufundishia masomo mbalimbali tangu elimu ya msingi hadi elimu ya juu. Wao huona msamiati wa Kiswahili haujitoshelezi kumudu dhana na minyambuliko ya kisayansi. Kwa kawaida watu wa aina hii lugha ya kigeni wanayoijua ni Kiingereza tu na hivyo, hukiona kimekamilika kwa vile wao hudhani hakikuathiriwa na lugha nyinginezo.

Kwa upande wa kujitosheleza katika msamiati wa dhana na minyumbuliko ya sayansi, hali halisi iliyopo ni kwamba msamiati wa kisayansi ni wa kimataifa. Mfaransa, Mwingereza, Mjerumani na Mrusi hutumia neno lile lile ila atalitohoa kusudi lilingane na matamshi ya lugha yake. Hakuna sababu kwa nini Kiswahili kisifuate utaratibu huu kadiri inavyowezekana badala ya kila mara kutaka kuunda neno jipya kabisa.

Kwa vile lugha iliyo hai hukua na ikipanuka, jambo litakiwalo ni mwelekeo unaofaa miongoni mwa watumiaji. Kinachotakiwa ni ujenzi wa matumizi bora na kuhimiza matumizi hayo. Tukijenga mwelekeo ufaao na kuzingatia muundo wa lugha hii kifani na kisarufi, basi tutakuwa tumejitahidi kutekeleza wajibu wetu wa kuiendeleza lugha yetu ya taifa, ambayo inaanza kuwa lugha ya kimataifa.

MASWALI

(a) Eleza maana ya vifungu vya maneno vifuatavyo kama vilivyotumika katika habari uliyosoma:

(i) Mwenye ujuzi wa Kiingereza alifikiriwa kwanza. 

(ii) Ufunguo wa ufanisi katika maisha.

(b) Taja faida tano zitakazopatikana endapo Kiswahili kitatumika kama lugha ya kufundishia na kujifunzia kuanzia ngazi ya elimu ya msingi hadi elimu ya juu.

(c) Kwa mujibu wa habari uliyosoma unafikiri kwa nini watu hawakithamini Kiswahili? Toa sababu moja ya msingi.

(d) Andika kichwa cha habari uliyosoma kwa maneno yasiyozidi matano.

View Ans


2. Fupisha habari uliyoisoma kwa maneno yasiyozidi mia moja na ishirini (120).

View Ans


SEHEMU B

MATUMIZI YA SARUFI NA UTUMIZI WA LUGHA

3. Chambua na fafanua kazi ya kila mofimu katika maneno yafuatayo:

(a) Sikukukumbuka

(b) Tulililia

(c) Unavyocheza

(d) Hakukitaka

View Ans


4. Kwa kutumia mifano, fafanua mambo matano yanayoweza kusababisha mabadiliko katika matumizi ya lugha.

View Ans


5. Kwa kutumia mifano onesha tofauti tano za kimuundo zilizopo kati ya sentensi sahili na sentensi ambatano.

View Ans


6. Toa maana tano za neno panga na kila maana tunga sentensi moja ukionesha jinsi neno hilo linavyotumika.

View Ans


SEHEMU C

UTUNCAJI

7. Andika barua kwa meneja wa kampuni ya uchapaji vitabu iitwayo Juhudi na Maarifa, S.L.P 3030 Nyikani, kuomba nafasi ya ajira ya Mhariri Mkuu. Jina lako liwe Kazi Njema wa S.L.P 2011 Bondeni.

View Ans


SEHEMU D

MAENDELEO YA KISWAHILI

8.Kwa kutumia mifano, eleza mambo matano yaliyokwamisha kukua na kuenea kwa Kiswahili nchini Kenya kabla ya uhuru.

View Ans


9."Wataalamu wa lugha wanakubaliana kuwa Kiswahili ni Kibantu." Unga mkono dai hilo kwa kutumia hoja tano za kiisimu.


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256