FORM SIX KISWAHILI NECTA 2010

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL ADVANCED CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION EXAMINATION

121/1 KISWAHILI 1

(Kwa Watahiniwa Walioko Shuleni tuu)

Muda: Saa 3 Jumatatu, 08 Februari 2010 asubuhi

Maelekezo

1. Karatasi hii ina maswali kumi na tatu (13) katika sehemu A, B, C, D na E.

2. Jibu maswali tano (5) kwa kuchagua swali moja kutoka kila sehemu.

3. Kila sehemu ina alama ishirini (20).

4. Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani.

5. Vikokotozi haviruhusiwi ndani ya chumba cha mtihani.

6. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A

HISTORIA

1.Eleza ubora na udhaifu wa nadharia za asili ya Kiswahili zilizotolewa na wanaisimu wafuatao.

(a) Askofu Edward Steere

(b) Dkt. R. Reuch

(c) Dkt Meinhoffna Dkt. Rohl

(d) Prof. Malcolm Guthrie

View Ans


2."Uhai na maendeleo ya Kiswahili nchini Tanzania umekumbwa na changamoto nyingi." Jadili changamoto tatu (3) kuthibitisha kauli hiyo.

View Ans


3. Eleza sifa tano (5) zinazokifanya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha za kimataifa.

View Ans


SEHEMU B

SARUFI

4. Eleza njia tano (5) zitumiwazo kuunda maneno katika Kiswahili na toa mifano mitano (5) kwa kila njia kuthibitisha hoja zako.

View Ans


5. Fafanua kwa kutumia mifano mitano (5) kuonesha jinsi viwakilishi vinavyofanya kazi ya viambishi.

View Ans


6. Eleza mfanano na tofauti iliyopo katika aina za sentensi zifuatazo:

(a) Sahili

(b) Tat-a

(c) Shurutia

(d) Changamano Ambatano

View Ans


SEHEMU C

MATUMIZI YA LUGHA

7. "Msamiati wa lugha yoyote wapaswa kukuzwa. "Thibitisha hoja hii kwa mifano mitano (5) ukitumia lugha ya Kiswahili.

View Ans


8. Fafanua sababu tatu (3) za utata katika tungo.

View Ans


9. Fafanua mambo matano (5) ambayo hutawala mtindo wa lugha.

View Ans


SEHEMU D

UTUNCAJI

10. Andika insha ya wasifu wa kisanaa yenye maneno yasiyozidi mia nne (400) na yasiyopungua mia tatu (300) juu ya mandhari ya shule yako.

View Ans


11. Andika insha ya maneno yasiyozidi mia nne (400) na yasiyopungua mia tatu (300) juu ya Uchaguzi wa Taifa mwaka 2010.

View Ans


12. Jifanye wewe ni mfanyabiashara wa kuuza magari. Andika barua rasmi ya biashara. Jina lako liwe Dokta Gadi Virani, S.L.P. 155, Mabatini, Mwanza.

View Ans


SEHEMU E

UFAHAMU

13. Soma habari ifuatayo kwa makini kisha jibu maswali yanayofuata.

Hapo zamani za kale kulikuwa na mvuvi ambaye aliishi na mkewe katika kibanda kibovu karibu na ufukwe wa bahari. Siku moja wakati akivua samaki kwa ndoano, alimwona samaki mmoja mkubwa sana wa ajabu!

Samaki yule alimrarai mvuvi huku akilia na kusema: "Tafadhali, tafadhali, naomba uniache niishi. Mimi si samaki bali ni Mwana wa Mfalme nirudishe baharini na uniruhusu niende.

Kusikia vile, yule mvuvi akajibu: "Ooh! usiseme maneno mengi; sina haja na samaki anayezungumza, kwa hiyo nenda zako mapema iwezekanavyo." Akamnasua na kumrudisha baharini aliporudi nyumbani na kumweleza mkewe kuhusu mkasa ule, mkewe alikuja juu na kumwuliza mumewe, kwanini alimwachia bila kumwomba lolote mwana yule wa kifalme?

"Hapana." Yule mvuvi alijibu, "Kwani ningeomba nini?" Akauliza. Kusikia hivyo, mkewe akajibu kwa mshangao, "Ah! sisi tunaishi katika kibanda hiki kibovu; kwanini hujamwomba atusaidie nyumba?

Yule mvuvi alienda moja kwa moja hadi ufukweni na kuanza kuita kwa sauti! "Ewe Bwana wa bahari, njoo unisikilize; mke wangu amenituma nije nikuombe msaada wa nyumba"

Mara yule samaki akajitokeza na kumwamuru arejee mara moja nyumbani. Mvuvi alipofika nyumbani alimkuta mkewe katika nyumba nzuri ndogo, iliyokuwa na bustani nzuri ya maua yenye rihi ya kupendeza na matunda matamu; huku kuku na mabata wakiranda huku na kule. Furaha ikapasua anga za maisha yao.

Lakini baada ya majuma mawili mke wa mvuvi alianza kunyong'onyea, na siku moja akapasua jipu: "Kajumba haka hakatoshi na hata kabustani tuliko nako ni kidogo. Nenda basi kamwambie yule samaki atupatiekasri.

Baada ya kusikia hayo, mvuvi alimsihi sana mkewe ili waridhike na walichokuwa nacho na kwenda tena kuomba kwa samaki si jambo jema kwani huenda kungemchukiza. Lakini mkewe alimshinikiza aende kwa samaki na mvuvi alienda shingo upande. Moyo wake ulikuwa mzito kwani alijua samaki hatafurahia ombi hilo. Hata hivyo samaki aliridhia ombi lile la mke wa mvuvi. Wakapata kasri kubwa lililokuwa na watumishi wa kila fani na waaminifu; samani za ajabu na bustani kubwa iliyojaa kila aina ya wanyama na ndege. Mvuvi akaamini kwamba yeye na mkewe wataishi kwa furaha kwa siku zote za maisha yao.

Walipoamka, mkewe akaja na ombi jipya. Alimtaka mumewe akamwombe samiki ili wao ndio wawe mfalme na malkia wa nchi ile. Baada ya kumwona mumewe anasita, akamwambia "kama wewe hutaki kuwa mfalme, mimi nitakuwa mfalme - nenda kamwambie samaki.

Samaki alipopewa rai hiyo, alitekeleza mke wa mvuvi akawa mfalme! Hata hivyo, mfalme huyo hakuridhika. Sasa akataka awe mtawala wa watawala wote. Hapo mumewe alikataa kwenda kwa samaki kuwasilisha ombi hilo. Lakini mkewe akamwambia, "Mimi ndiye mfalme na wewe ni mtumwa wangu tu. Tekeleza ninalokuamuru." Hata alipopata kuwa mtawala wa watawala, mke wa mvuvi hakuridhika. Sasa akataka mamlaka yakuamuru jua liwake na mwezi ung'are.

Samaki alipopewa ombi hilo alijibu kwa maneno machache "Rudi nyumbani, katika kibanda chenu kikuu kuu." Na huko ndiko wanakoishi hadi leo.

MASWALI

(a) Andika kichwa cha habari hii kwa maneno yasiyozidi manne (4).

(b) Eleza maana ya maneno yaliyokolezwa wino.

(c) Mvuvi na mkewe walikuwa na wasifu wa ndani aina gani?

(d) Ungekuwa wewe ndiye mvuvi, ungetekelezaje lile ombi la mwisho?

(e) Andika ufupisho wa habari uliyosoma kwa maneno yasiyopungua mia moja na sabini (170).

View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256