FORM FOUR KISWAHILI NECTA 2024

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

MTIHANI WA KUHITIMU KIDATO CHA INNE

021 KISWAHILI

(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

Muda: Saa 3 Mwaka: 2024

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11).
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B, na maswali mawili (2) kutoka sehemu C ambapo swali la tisa (9) ni la lazima.
  3. Sehemu A ina alama kumi na sita (16), sehemu B alama hamsini na nne (54) na sehemu C ina alama thelathini (30).
  4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
  5. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
  6. Vifaa vya mawasiliano na vitu visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  7. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 16)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

l . Katika kipengele (i) hadi (x), chagua herufi ya jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye kijitabu chako cha kujibia.

(i) Vifuatavyo ni vyanzo vya misimu, isipokuwa

  1. Tanakali sauti au milio 
  2. Sayansi na Teknolojia
  3. Shughuli maalumu 
  4. Utani katika jamii 
  5. Mabadiliko ya kihistoria
Choose Answer :


(ii) Neno lenye mofu ya mtendwa ni lipi kati ya haya?

  1. Aliyetembelea 
  2. Alimtembelea 
  3. Alivyotembea 
  4. Atakayetembea 
  5. Ametembea
Choose Answer :


(iii) Msaada wako umenifaa sana. Asante! Nena "Asante!" ni aina gani ya neno?

  1. Nomino 
  2. Kivumishi
  3. Kielezi
  4. Kitenzi 
  5. Kihisishi
Choose Answer :


(iv) Tamathali ipi ya semi hukipa kitu kisicho binadamu sifa ya ubinadamu?

  1. Taniaba 
  2. Tashihisi 
  3. Tashibiha
  4. Takriri 
  5. Tabaini
Choose Answer :


(v) "Wanafunzi wa Kidato cha Pili wamepigiwa ngoma." Kauli hii inaonesha hali gani?

  1. Kutendana 
  2. Kutendeka 
  3. Kutendewa
  4. Kutendwa 
  5. Kutendea
Choose Answer :


(vi) Tanzu sahihi za Fasihi simulizi ni zipi kati ya zifuatazo?

  1. Ngonjera, mashairi, nyimbo na tenzi
  2. Tarihi ngano, visasili na soga
  3. Semis hadithi, maigizo na ushairi
  4. Methali, misemo, nahau na vitendawili
  5. Michezo, vichekesho, majigambo na ngofijera
Choose Answer :


(vii) Mpangilio mzuri wa muundo wa insha ni upi?

  1. Kichwa, mwanzo, wazo na kiini 
  2. Mwanzo, kiini, hitimisho na wazo 
  3. Kichwa, wazo, hitimisho na kiini 
  4.  Kichwa, mwanzo, wazo na hitimisho 
  5. Kichwa, mwanzo, kiini na hitimisho
Choose Answer :


(viii) Kwa nini lugha ya mazungumzo ni halisi zaidi?

  1. Wahusika huwasiliana kwa simu
  2. Wahusika huwasiliana ana kwa ana
  3. Wahusika huwasiliana kwa mtandao
  4. Wahusika huwasiliana kwa barua
  5. Wahusika huwasiliana kwå barua pepe
Choose Answer :


(ix) Methali isiyosisitiza uvumilivu naji!ihada katika kazi ni ipi?

  1. Afiriti hafichiki 
  2. Mvumilivu hula mbivu 
  3. Acha koko uangue koma 
  4. Aali hupatikana kwa ghali 
  5. Abadi abadi kamba hukata jiwe
Choose Answer :


(x) Tungo ipi ina kiambishi rejeshi kati ya hizi?

  1. Anaondoka 
  2. Ameondoka 
  3. Aliondoshwa 
  4. Amejiondoa 
  5. Ameondokewa
Choose Answer :


2. Oanisha fasili za Vipera vya semi zilizopo katika Orodha A na Vipera husika kutoka Orodha B, kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia.

Orodha A

Orodha B

(i) Semi fupi Zinazoeleza kwa emuhtasari fikra au mafunzo mazito yaliyotokana na uzoefu wajamii.

(ii) Semi fupi za mafumbo zinazotumia lugha ya picha na zinazotolewa kwa hadhira zikieleza jambo lenye kuhitaji jibu.

(iii) Semi zilizojengwa kwa pichå kwa kutumia maneno ya kawaida lakini hutoa maana tofauti na maneno yaliyotumika.

(iv) Semi zenye maonyo au mawaidha ambazo maana zake za ndani zimefichika.

(v) Semi zenye picha za mafumbo zinazoonesha ukinzani wa fikra au matukio.

(vi) Semi zinazotumia picha, ishara na tamathali kueleza kitu au wazo kwa ufupi.

  1. Mafumbo
  2. Nahau
  3. Misemo
  4. Lakabu
  5. Vitendawili
  6. Mizungu
  7. Methali 
  8. Misimu

SEHEMU B (Alama 54)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

View Ans


3. (a) Kwa kutumia mifano, eleza jinsi vipengele vifuatavyo vinavyoweza kupotosha lengo la msemaji katika mazungumzo ya kila siku. 

(i) Matumizi ya msamiati usio sahihi

(ii) Matumizi ya miundo isiyo sahihi

(iii) Matumizi ya matamshi yasiyo sahihi

(iv) Kukosekana kwa mantiki katika tungo

View Ans


(b) Fasili kwa kifupi istilahi zifuafäzo kama zinavyotumika katika lugha ya Kiswahili.

  1. Irabu 
  2. Kiimbo
  3. Konsonanti 
  4. Lafudhi 
  5. Mkazo
View Ans


4. Ujio wa Waarabu, Wajerumani na Waingereza ulikuwa na mchango mkubwa katika kukuza na kueneza Lugha ya Kiswahili nchini Tanzania kabla ya uhuru. Eleza umuhimu wao kwa kutoa hoja mbili kwa kila taifa.

View Ans


5. (a) Kwa kutoa mfano mmoja kwa kila neno, fafanua istilahi zifuatazo kama zinavyotumika katika kamusi ya Kiswahili Sanifu. 

  1. Homonimu
  2. Sinonimu
  3. Kategoria
  4. Kisawe
View Ans


(b) Bainisha aina za maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo:

(i) Nguo yoyote fupi ni marufuku.

(ii) Amina ndiye mwanangu.

(iii) Alisoma kwa bidii japokuwa alifeli.

(iv) Afadhali! mwalimu amerudi nyumba. 

(v) Walianguka kizembe.

View Ans


6. Kwa kutumia hoja şita, fafanua mafanikio sita ya Kamati ya Lugha ya Afrika Mashariki ya mwaka 1930 katika kusimamia usanifishaji wa lugha ya Kiswahili.

View Ans


7. Fafanua mambo tisa ya muhimu ya kuzingatia katika uandishi wa dayalojia.

View Ans


8. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.

Kulikuwa na kiongozi mmoja maarufu aliyekuwa amebobea na kusifika sana katika ukanda wenye misitu minene. Siku zote alikuwa anasisitiza umuhimu wa kupanda miti kabla ya kukata miti. Aidha, kila mara alikuwa anawahamasisha watu juu ya umuhimu wa kupanda miti kuzunguka maeneo yao yote kwa kuamini kuwa akiba haiozi.

Siku moja alialikwa katika shule ya Sekondari Twaweza kuhudhuria mahafali ya kuhitimu Kidato cha Nne. Kabla ya shamrashamra kuanza, alihakikisha kwanza miti inapandwa katika eneo lote la kuzunguka shule. Katika wosia Wake, aliwashawishi wanafunzi kuwa mabalozi wa upandaji miti, utunzaji miti na usafi. Aliwasisitiza kuwa safi kwani usafi ndiyo njia pekee ya kulinda afya zao kwa kuwa afya njema ni mtaji wa mafanikio yao. Vilevile, alikemea vikali tabia ya kutiririsha maji machafu, kutupa takataka ovyo na kujisaidia sehemu zisizostahili.

Aliwasihi wahitimu kuwa, miongoni mwao watapatikana viongozi ambao watakuwa na moyo wa kuendeleza kazi ambayo viongozi waliokuwepo waliithamini sana. Hii itasaidia kuinusuru nchi yetu isije ikavamiwa na madhara ya jangwa baada ya kipindi si kirefu. Ukataji wa miti holela huathiri uoto wa asili, kufukuza mvua na kukaribisha ukame.

Aliendelea kueleza kuwa, hatuna budi kuelewa kwamba ukosefu wa mvua siku zote ndicho chanzo kikuu cha madhila kwa binadamu, wanyama wa mwituni, wanyama wafugwao na hata wadudu na mimea Pia. Kila mmoja akikariri kauli mbiu panda miti kata mti tutakwepa ukame. Hivyo, kila mwanajamii. anapaswa kuienzi kwa dhati kabisa kauli mbiu hii kwani mchelea nzwana kulia, hulia yeye.

Maswali

(a) Andika kichwa cha habari hii kwa maneno matatu.

(b) Eleza maana ya methali zifuatazo kama zilivyotumika katika habari uliyosoma.

  1. Akiba haiozi.
  2. Mchelea mwana kulia, hulia yeye.

(c) Kutokana na habari uliyosoma, taja athari mbili za kukosa mvua kwa binadamu, wanyama, wadudu na mimea.

(d) Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasiyopungua sitini na yasiyozidi sabini.

SEHEMU C (Alama 30)

Jibu maswali mawili (2) kutoka katika sehemu hii. Swali la tisa (9) ni la lazima na kila swali lina alama 15.

ORODHA YA VITABU

USHAIRI

  • Wasakatonge  - M. S. Khatibu (DUP)
  • Malenga Wapya  - TAKILUKI (DUP) 
  • Mashairi ya Chekacheka  - T. A. Mvungi (EP & D. LTD)

RIWAYA

  • Takadini - Ben J. Hanson (MBS)
  • Watoto wa Mama N'tilie  - E. Mbogo (H. P)
  • Joka la Mdimu  - A. J. Safari (H. P.)

TAMTHILIYA

  • Orodha - Steve Reynolds (MA)
  • Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba (ESC)
  • Kilio Chetu - Medical Aid Foundation (TPH)
View Ans


9. Kwa kutoa hoja mbili na mifano, eleza namna jina la kitabu linavyosadifu yaliyomo katika diwani mbili ulizosoma.

View Ans


10. "Mapenzi ya dhati huleta faraja miongoni mwa wanajamii." Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu kutoka katika kila riwaya kati ya riwaya mbili ulizosoma.

View Ans


11. Kwa kutumia hoja tatu kwa kila kitabu katika tamthiliya mbili ulizosoma, eleza namna wasanii walivyotumia dhamira mbalimbali ili kuakisi jamii ya leo.

View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256