JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA NflTIHAN1 LA TANZANIA MTIHANI WA KUHITIMU KIDATO CHA NNE
021 KISWAHILI
(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)
Muda: Saa 3 Mwaka: 2023
Maelekezo
Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11).
Jibu maswali yote katika sehemu A na B, na maswali mawili (2) kutoka sehemu C ambapo swali la tisa (9) ni la lazima.
Sehemu A ina alama kumi na sita (16), sehemu B alama hamsini na nne (54) na sehemu C ina alama thelathini (30).
Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
Vifaa vya mawasiliano na vitu visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.
SEHEMU A (Alama 16)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
Kalika kipengele (i) - (x), chagua jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye kijitabu chako cha kujibia.
(i) Katika masimulizi ya hadithi, maana sahihi ya soga ni ipi?
Hadithi ndefu zinazohusu binadamu.
Hadithi zinazohusu binadamu na wanyama.
Hadithi fupi za kuchekesha na kukejeli.
Hadithi fupi zinazoelezea makosa au uovu.
Hadithi ndefu za kubuni na zinazochekesha.
Choose Answer :
(ii) Kati ya methali zifuatazo, ipi ina maana tofauti na zingine?
Ujanja mwingi mbele giza.
Akili nyingi huondoa maarifa.
Mdharau biu huibuka yeye.
Ukupigao ndio ukufunzao.
Mdharau mwiba, mguu huota tende.
Choose Answer :
(iii) "Kiangazi kiliunguza kikaunguza Hatimaye, mwaka elfu moja mia tisa hamsini na sita mvua zikaanza ijapokuwa kwa maringo.” Usimulizi huu ni aina gani ya hadithi?
Visasili
Vigano
Soga
Ngano
Tarihi
Choose Answer :
(iv) "Papai limeiva nyumbani lakini nashindwa kuliła.” Kauli hii inawakilisha aina gani ya semi'?
Methali
Mizungu
Nahau
Kitendawili
Misemo
Choose Answer :
(v) Mbinu ya kufupisha maneno katika ushairi ili kupała ulinganifu wa mizani huitwaje'?
Tasfida
Tathilitha
Inkisari
Ufupisho
Inkishafi
Choose Answer :
(vi) Ubainishaji wa maneno ya kuzua au yasiyo rasmi katika lugha huhusisha alama ipi ya uandishi kati ya hizi?
Mkato
Nukta-pacha
Nukta
Nukta-mkato
Mtajo
Choose Answer :
(vii) Kati ya maneno yafuatayo, neno lipi haliundwi kwa mbinu ya mwambatano?
Batamzinga
Barabara
Jotoridi
Chajio
Deltao
Choose Answer :
(viii) Maneno yafuatayo yana maana zaidi ya moja isipokuwa
Ua
Mbuzi
Kata
Nyau
Paa
Choose Answer :
(ix) Katika neno 'umempelekea' mofimu ipi inawakilisha kauli ya kutendea?
me-
-e-
-m-
-pelek-
-a
Choose Answer :
(x) Kulingana na chimbuko la Kiswahili, lahaja ya Kijomvu ilizungumzwa maeneo gani?
Kaskazini mwa Tanga
Kusini mwa Somalia
Kisiwa cha Mafia
Sehemu ya Malindi
Kisiwa cha Pemba
Choose Answer :
2. Oanisha tungo tata zilizopo katika Orodha A na chanzo cha utata huo kutoka Orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia.
8. Soma kwa umakini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.
Mchezo wa jana wa mpira wa miguu ulikuwa patashika nguo kuchanika. Katika kutupia macho wachezaji wa Tunisia, ni dhahiri kuwa mtazamaji yeyote angeweza kutabiri kuwa wachezaji gani wangejipatia ushindi. Wachezaji wa Tunisia walionekana kuwa majitu ya miraba minne na hivyo kutabiriwa kuwa washindi wa mchezo huo. Kwa siku za nyuma, wachezaji wa timu ya Tanzania waliweza kwenda sare na timu ya Tunisia kwa kipindi chote cha mchezo na pengine hawakuweza kupata ushindi kabisa. Kutokana na hilo, hofu kubwa ilitanda miongoni mwa Watanzania lavani siku hiyo huenda historia ikajirudia ya kufungwa au kutoka sare. Kipenga kilipolia wachezaji wa pande zote mbili walijitupa uwanjani wakionesha utanashati na manjonjo mengi huku wakipiga mazoezi ya hapa na pale. Watu walipowashangilia kwa hoi hoi na vifijo waliongeza madaha yao. Haukupita muda mrefu walitengana na kila mmoja alikwenda katika sehemu yake na mara kipenga cha kuashiria mpira kuanza kikapigwa. Naam, ilianza vuta nikuvute, kila mmoja akiwania kuanza kuufumania mlango wa mpinzani wake. Kukuru kakara hiyo iliendelea hadi mwisho '*va kipindi cha kwanza ambapo hakuna aliyefanikiwa kugusa nyavu za mwenzie. Kwa kipindi hiki chote timu ya Tanzania ilionekana kupiga moyo konde na kuwania ushindi. Wachezaji wa Tunisia nao waliapa kutoshindwa kuwatoa Watanzania kama walivyotazamia.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila mchezaji kujihami dhidi ya adui yake ili mradi kila mmoja apate nafasi ya kuutundika mpira wavuni. Hata hivyo wachezaji wengi wa pande zote walionekana kulowa kwa kutoelewa nini kitatokea mbele yao baada ya dakika arobaini na tano zilizofuatia.
Muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza, timu ya Tunisia iliona lango la timu ya Tanzania na kujiandikia bao la kwanza. Uwanja mzima ulipooza kwa upande wa Watanzania lakini Watunisia walionekana kufunguka nyuso zao kwa bashasha. Waswahili wanasema, "Mungu si Athumani.” Hivyo, ilipotimia dakika ya themanini ya mchezo, Mohamedi Kajole alipata nafasi nzuri, akautoma mkwaju mkali kinywani mwa lango la Tunisia na kuiandikia timu ya Tanzania goli la kusawazisha. Nderemo, shangwe, vifijo na vigelegele vilitawala uwanjani kwa kuwa Kajole aliwatoa Watanzania aibu katika kiwanja cha nyumbani.
Mchezo ulikuwa kama umepata mvuto na ari mpya kwa wachezaji wa Tanzania ambao walionekana kuwa na kasi kubwa katika kupasiana mpira. Wachezaji wa Tunisia walianza kuhangaika uwanjani wakijua kuwa ushindi karibu utatoweka mikononi mwao. Mashabiki wa Tanzania nao walishika kasi katika kushangilia timu yao.
Harakati hizo zilizaa matunda katika dakika ya themanini na tisa pale Kassim Kapombe alipoipatia timu yake ya Tanzania goli la ushindi. Vifijo, hoi hoi na shangwe zilitawala uwanjani kwa upande wa Watanzania. Lakini mambo hayakuwa mazuri kwa upande wa timu ya Tunisia kwani walichokitegemea hawakukipata. Hadi mwisho wa mchezo huu, Tanzania iliibuka kidedea kwa mabao mawili dhidi ya bao moja la Tunisia.
Maswali
(a) Pendekeza kichwa kifaacho kwa habari uliyosoma.
(b) Eleza mawazo waliyokuwa nayo watazamaji wengi kabla ya kuanza kwa mpira.
(c) Eleza maana ya misemo ifuatayo kama ilivyotumika katika kifungu cha habari.
Patashika nguo kuchanika.
Walipiga moyo konde.
Mungu si Athumani.
Waliibuka kidedea.
Walishika kasi.
(d) Watunisia walikuwa na hali gani baada ya kufungwa goli la pili'?
(e) Fupisha habari hii kwa maneno yasiyopungua mia moja (100) na yasiyozidi mia na tano (105).
Jibu maswali mawili (2) kutoka sehemu hii. Swali la tisa (9) ni la Iazima.
ORODHA YA VITABU
USHAIRI
Wasakatonge M.S. Khatibu (DUP)
Malenga Wapya TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya Chekacheka T.A. Mvungi (EP & D. LTD)
RIWAYA
Takadini Ben J. Hanson (MBS)
Watoto wa Mama N'tilie E. Mbogo (H .P)
Joka la Mdimu A. J. Safari (H. P)
TAMTHILIYA
Orodha Steve Reynolds (MA)
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe E. (ESC)
Kilio Chetu Medical Aid Foundation (TPH)
9. "Lugha ni nyenzo muhimu katika kutoa mafunzo kwa jamii.” Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kutumia vipengele vitatu vya lugha kwa kila kitabu kutoka katika diwani mbili ulizosoma.
10. "Mhusika hawezi kuwa kamili katika kazi ya fasihi bila kubeba kikamilifu mavvazo ya mwandishi." Chagua mhusika mmoja kwa kila kitabu, kisha onesha namna kila mmoja alivyowasilisha mawazo matatu ya mwandishi kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.
11. "Mara zote wasanii wa tamthiliya huonesha mikakati ya kupambana na changamoto zilizopo katika jamii." Onesha mikakati mitatu iliyotolewa na wasanii kwa kila kitabu kutoka katika tamthiliya mbili ulizosoma.