JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA, MTIHANI WA KUHITMU KIDATO CHA NNE
021 KISWAHILI
(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)
Muda: Saa 3 Mwaka 2021
Maelekezo
- Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).
- Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali matatu (3) kutoka sehemu C.
- Sehemu A ina alama kumi na tano (15), sehemu B alama arobaini (40) na sehemu C ina alama arobaini na tano (45).
- Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
- Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
- Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x). kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye kijitabu chako cha kujibia.
(i) İpi ni seti sahihi ya vipera vya semi?
- Methali, mizungu na maghani
- Soga, nyimbo na nahau
- Misemo, mafumbo na vigano
- Mafumbo, soga na maghani
- Nahau, vitendawili na mizungu
Choose Answer :
(ii) Dhima kuu ya misimu katika lugha ni ipi?
- Kuunda mizizi ya maneno.
- Kuficha jambo kwa wasiohusika.
- Kuongeza ukali wa maneno.
- Kutambulisha aina za maneno.
- Kupatanisha maneno.
Choose Answer :
(iii) Bainisha sentensi yenye muundo wa kiwakilishi + kirai vumishi + kitenzi kikuu + kirai nomino:
- Sisi sote tulicheza vizuri sana.
- Mimi na yeye hatuelewani hata kidogo.
- Wao hawataki tuimbe nyimbo zetu.
- Wale wote wanapenda muziki.
- Ninyi nyote tunawapenda sana.
Choose Answer :
(iv) Njia ipi ya uhifadhi wa fasihi simulizi inayowcza kupokea mabadiliko kwa haraka kati ya hizi?
- Maandishi
- Kichwa
- Vinasa sauti
- Kanda za video
- Kompyuta
Choose Answer :
(v) "Ni budi nisome kwa bidii ili nifaulu mtihani wangu.” Yapi ni masahihisho sahihi ya sentensi hii?
- Nina budi kusoma kwa bidii ili nifaulu mtihani wangu.
- Sio budi kusoma kwa bidii ili nifaulu mtihani wangu.
- Sina budi kusoma kwa bidii ili nifaulu mtihani wangu.
- Sitakiwi kusoma kwa bidii ili nifaulu mtihani
- Sio lazima kusoma kwa bidii ili nifaulu mtihani wangu.
Choose Answer :
(vi) "Kutwa mara tatu; asubuhi, mchana na jioni." Dhima ya muundo wa mazungumzo haya ni ipi?
- Kupunguza ukali v„ra mazungumzo.
- Kufupisha urefu wa mazungumzo.
- Kupamba lugha ya mazungumzo.
- Kuonesha msisitizo wa mazungumzo.
- Kukidhi haja ya mazungumzo.
Choose Answer :
(vii) "Juma anaendesha baiskeli yake polepole." Kiarifu cha sentensi hii kimejengwa na mfuatano upi wa viambajengo?
- Kiima, chagizo na shamirisho
- Kitenzi kishirikishi, shamirisho na chagizo
- Kiarifu, kiima na chagizo
- Shamirisho, chagizo na kitenzi kikuu
- Kitenzi kikuu, shamirisho na chagizo
Choose Answer :
(viii) Fungu la sauti zinazotokea katikati au mwishoni mwa kila mstari wa ushairi huitwaje?
- Vina
- Vituo
- Mizani
- Silabi
- Mistari
Choose Answer :
(ix) Mambo muhimu ya kuzingatiwa katika uandishi wa tangazo la biashara ni yapi kati ya haya?
- Aina ya bidhaa na idadi ya wateja.
- Kichwa cha tangazo na bei ya kila bidhaa.
- Aina na kichwa cha tangazo la bidhaa.
- Aina ya bidhaa na bei ya kila moja.
- Kichwa cha tangazo na lengo lake.
Choose Answer :
(x) Ni kauli ipi iliyotumika katika uundaji wa neno "nitamfitinia"?
- kutenda
- kutendana
- kutendea
- kutendeana
- kutendewa
Choose Answer :