FORM FOUR KISWAHILI NECTA 2020

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA NUTIHANI LA TANZANIA

MTIHANI WA KUHITIMU KIDATO CHA NNE

021 KISWAHILI

(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

Muda: Saa 3 Mwaka: 2020

Maelekezo

l . Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).

2.Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali matatu (3) kutoka sehemu C.

3.Sehemu A ina alama kumi na tano (15), sehemu B alama arobaini (40) na sehemu C ina alama arobaini na tano (45).

4.Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.

5.Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.

6.Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi yajibu hilo katika kijitabu chako cha kujibia.

(i) Ni neno lipi linalotoa taarifa kuhusu nomino?

 1. Kitenzi
 2. Kielezi
 3. Kivumishi
 4. Kiwakilishi
 5. Kiunganishi
Choose Answer :


(ii)Katika lugha ya Kiswahili kuna aina ngapi za vitenzi?

 1. mbili
 2. tano
 3. Sita 
 4. tatu
 5. nne
Choose Answer :


(iii)Maneno yepi kati ya yafuatayo yametokana na lugha za Kibantu?

 1. Kitindamimba na bendera 
 2. Hela na mtutu
 3. Kitivo na ngeli 
 4. Godoro na sharubati
 5. Bunge na shule
Choose Answer :


(iv)Ni mambo gani muhimu ya kuzingatia katika kuteua maneno na miundo ya tungo wakati wa mazungumzo?

 1. Mada, muktadha na mazungumzo ya ana kwa ana.
 2. Mada, mazungumzo na uhusiano wa wazungumzaji.
 3. Mada, mzungumzaji na muktadha wa mazungumzo.
 4. Mada, mzungumzaji na uhusiano wa wazungumzaji.
 5.  Mada, muktadha na uhusiano wa wazungumzaji.
Choose Answer :


(v)Bainisha kauli inayoonesha dhima muhimu za vitendawili katika jamii:

 1. Kuhimiza umoja na ushirikiano.
 2. Kupanga watu katika marika yao.
 3. Kuchochea udadisi wa mambo.
 4. Kuchochea uwongo wa mambo.
 5. Kukosoa wadadisi wa mambo.
Choose Answer :


(vi)Njia mojawapo ya kuzuia utata katika lugha ya mazungumzo ni ipi kati ya zifuatazo?

 1. Kuepuka makosa ya kisarufi na kimantiki.
 2. Kutumia neno lenye maana zaidi ya moja.
 3. Kutumia kiwakilishi kiambata katika neno.
 4. Kuweka msisitizo au ufafanuzi zaidi.
 5. Kutumia mofimu sahihi za wakati.
Choose Answer :


(vii)”Waandishi wa fasihi huzungumzia watu wenye mienendo isiyokubalika katika jamii ili kukemea mienendo hiyo.” Katika tamthiliya ulizosoma, ni wahusika wepi kati ya wafuatao wana mienendo isiyokubalika?

 1. Joti, Ngoswe na Mama Furaha.
 2. Padri James, Ngoswe na Baba Anna.
 3. Mazoea, Mama Furaha na Joti.
 4. Ngoswe, Baba Anna na Suzi.
 5. Ngoswe, Joti na Padri James.
Choose Answer :


(viii)Kati ya sababu zifuatazo ni ipi si sahihi kuhusu matumizi ya kamusi?

 1. Kujifunza lugha ya kigeni.
 2. Kusanifisha maneno mapya.
 3. Kubaini kategoria ya neno.
 4. Kujua maana za maneno.
 5. Kujua tahajia za maneno.
Choose Answer :


(ix)Ni methali ipi inayokinzana na methali ''Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu?” 

 1. Manahodha wengi, chombo huenda mrama.
 2. Palipo na wengi, hapaharibiki neno.
 3. Haba na haba, hujaza kibaba.
 4. Kidole kimoja, hakivunji chawa. 
 5. Fimbo ya mnyonge, ni umoja.
Choose Answer :


(x)Bainisha sentensi ambatano yenye muundo wa sentensi changamano mbili kati ya sentensi zifuatazo:

 1. Gari lililomteka tumeliona na dereva aliyetekwa ameonekana.
 2. Mtoto aliyeumia jana amelazwa na mtoto mwingine hajitambui.
 3. Mpe haki yake yote ili nae akupe haki yako yote.
 4. Uchunguzi uliofanyika juzi umezaa matunda.
 5. Baba anataka kujenga nyumba lakini mama hataki kabisa.
Choose Answer :


2.Oanisha maana za vipera vya Fasihi Simulizi katika Safu A na dhana za Fasihi Simulizi zilizo katika Safu B; kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia.

Safu A

Safu B

(i)Sherehe au shughuli zinazofanywa na jamii katika kipindi maalumu cha mwaka.

(ii)Masimulizi ya mambo ya kishujaa ambayo mtu amewahi kuyafanya maishani mwake.

(iii)Maigizo mafupi yaliyojaa ucheshi na mzaha.

(iv)Sadaka itolewayo kwa miungu au mahoka.

(v)Masihara wanayofanyiana wanajamii wakati wa shida na raha.

 1. Utani
 2. Matambiko
 3. Miviga
 4. Harusi
 5. Ngoma
 6. Majigambo
 7. Vichekesho
View Ans


SEHEMU B (Alama 40)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3.Ainisha maneno yaliyokolezwa wino katika tungo zifuatazo: 

(i) Wangapi waliondoka mapema leo?

(ii)Wachezaji wangapi watashiriki kwenye mechi ya kwanza?

(iii)Wanangu wapendwa niwaeleze mara ngapi mpate kunielewa?

(iv)Wawakilishi wote waliunga mkono hoja ya mbunge wa Kusini Unguja.

View Ans


4.Eleza kwa ufupi mazingira manne ambayo kielezi huweza kujipambanua, kisha tunga sentensi moja kwa kila aina ya mazingira.

View Ans


5.Eleza maana mbili kwa kila tungo zifuatazo: 

(a) Mama anaota.

(b)Tafadhali nipe sahani ya kulia.

(c)Vijakazi wanalima barabara.

(d)Amekanyaga mtoto.

View Ans


6.Kwa kutumia mifano kutoka katika riwaya ya Takadini iliyoandikwa na Ben J. Hanson (MBS), eleza kwa kifupi madhara manne yanayoweza kutokea katika jamii iwapo itaendekeza mila potofu ya kuwabagua walemavu wa ngozi.

View Ans


7. Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata katika kijitabu cha kujibia.

Chawa huyo ni kinyozi, mtia wembe kichwani, 

Ndiye huharibu ngozi, anapokata fashini,

Chawa ni huyo mkazi, uliyenaye jirani,

Usimdhanie mbuzi, huyo yuko majanini,

Wala usidhani funzi, umuonaye shambani,

Hawa hawana ujuzi, wa kukunyoa mtani,

Panapouma ufizi, sumu hutoka kinywani, 

Wapi hutokea nzi, kama si pako chooni,

Chawa aliye kichwani, ni huyo kinyozi wako.


Chawa unapomuona, upesi muweke dole,

Usimwache kunona, mpaka azue kelele,

Jitahidi kumbana, akatokomee mbele,

Ukimwacha kutuna, atakutia upele,

Usije kula dona, na kutafuta mchele,

Chawa usimpe jina, abaki akutawale,

Ukianza kujikuna, mtafute kwenye nywele,

Na nguoni hujibana, mkame kama nyenyele, 

Chawa aliye kichwani, ni huyo kinyozi wako.

Maswali

(a) Kwa kutumia mfano, fafanua mtindo uliotumika katika shairi hili kwa kutoa hoja mbili. 

(b) Mwandishi anamaanisha nini anaposema, "Chawa unapomuona, upesi muweke dole?"

(c)Eleza kwa ufupi kuhusu mtazamo wa mtunzi wa shairi hili.

(d)(i) Andika methali moja inayosadifu shairi hili.

(ii) Kwa kutumia maneno yako eleza jinsi shairi hili linavyoendana na maisha halisi ya jamii zetu.

View Ans


8.(a) Eleza kwa kifupi tofauti ya msingi kati ya barua ya mwaliko na tangazo.

View Ans


(b) Andika tangazo la kumtafuta ndugu yako wa kiume anayeitwa Masana Madale ambaye amepotea.

View Ans


SEHEMU C (Alama 45)

Jibu maswali matatu (3) kutoka katika sehemu hii.

9.Kwa kutumia aina nne za vyombo vya habari vilivyopo nchini hivi sasa, onesha mchango wa kila kimoja katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili.

ORODHA VA VITABU

USHAIRI

Wasakatonge M.S. Khatibu (DUP)

Malenga Wapya TAKILUKI (DUP) 

Mashairi ya Chekacheka TA. Mvungi (EP & D. LTD)

RIWAYA

Takadini Ben J. Hanson (MBS)

Watoto wa Mama N'tilic E. Mbogo (H.P)

Joka la Mdimu AJ .Safari (H.P.)

TAMTHILIYA

Orodha Steve Reynolds (MA)

Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe E. Semzaba (ESC)

Kilio Chetu Medical Aid Foundation (TPH

View Ans


10. Kauli za washairi ni nyenzo muhimu katika ujenzi wa jamii bora. Thibitisha usemi huu kwa kutumia hoja tatu kwa kila kitabu kutoka katika diwani mbili ulizozisoma.

View Ans


I I . "Jamii ya kitanzania inakabili'.va na matatizo mbalimbali ya kijamii yanayokwamisha maendeleo.” Thibitisha kauli hii k',va kutoa hoja tatu kwa kila riwaya kati ya riwaya mbili ulizosoma.

View Ans


12. "Waandishi wa kazi ya fasihi hulenga kulcta mabadiliko katika yale wanayoyaandika.” Kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma, tetea kauli hii kwa kutumia hoja tatu kutoka katika kila kitabu.

View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256