3. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Miti ina faida nyingi sana katika maisha ya binadamu. Nchi isiyo na miti ni sawa na mtu atembeaye bila kuvaa nguo. Ipo miti ya asili na mingine ni ya kupandwa, yote hiyo ina faida lukuki kwa maisha ya binadamu.
Ongezeko la watu duniani na kutokuwa na nishati mbadala kama vile gesi na umeme hasa sehemu za vijijini kumesababisha matumizi lufufu ya kuni na mkaa. Matumizi haya yametokana na ukosefu wa elimu ya utunzaji wa mazingira. Hali hii imesababisha jangwa kwa kuwa waswahili husema, "chovya chovya humaliza buyu la asali.'
Miti ina faida kadhaa katika maisha ya kiumbe yeyote duniani. Miti hutupatia hewa safi tunayoivuta kila sekunde ya uhai wetu, kutengenezea fanicha, kutupatia matunda ili kutukinga na magonjwa na harufu ya miti ni dawa dhidi ya maadui mbalimbali kama vile nyoka.
Ukataji miti ovyo una madhara kama vile ukame, mmomonyoko wa udongo, uhaba wa hewa safi ya oksijeni na athari nyingine nyingi zinazoondoa uwepo wa viumbe hai na viumbe visivyo hai.
Kwa sasa serikali yetu imeanzisha kampeni mbalimbali za kulinda mazingira kama vile, "kata mti panda mti", "mti wa milenia" na "mtu mmoja miti mingi." Kampeni hizo hutolewa katika redio, runinga na vyombo vingine vya habari. Ni jukumu la kila mtu kuitunza na kuilinda misitu yetu.
Maswali:
(a) Kutokana na habari uliyosoma;
Andika kichwa cha habari kwa maneno yasiyozidi matano.
Unafikiri kwa nini kumekuwa na wimbi kubwa la ukataji wa miti?
Bainisha matumizi manne ya miti.
(b) Kulingana na habari uliyosoma, kampeni mbalimbali zinazotolewa katika vyombo vya habari Zina umuhimu gani katika jamii?
(c) Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasiyopungua 60 na yasiyozidi 70.
Mada iliyo moyoni, hii ninawaletea, Watoto wa mitaani, mada nimeshafungua, Wanapata mitihani, katika hii dunia, Nawaonea huruma, imewatupa dunia.
Wanashinda jalalani, hayo ndiyo mazoea, Umkute kituoni, anaomba abiria, Ni njaa mwake tumboni, ndiyo inamsumbua, Ataomba kwa imani, huku anakulilia.
Wapo pia maaluni, vibaya wamezoea, Hawaombi wala nini, kazi yao kukwapua, Husimama vituoni, abiria kuvizia, Abiria wanalia, kila kitu kimekombwa.
Twajenga taifa gani, watoto kuachilia? Wazurure mitaani, na sisi twachekelea, Tunadhania utani, na mwishowe tutalia, Kwani mzaha mzaha, huutumbua usaha.
Maswali
(a) Bainisha;
(i) Muundo wa shairi:
(ii)Mtindo wa shairi:
(b) Eleza dhamira ya mwandishi katika ubeti wa pili.
(c) Eleza kwa kifupi ujumbe wa shairi hili.
(d) Toa methali nyingine moja yenye maana sawa na methali "Mzaha mzaha, hutumbua usaha" kama ilivyotumika katika shairi.
(e) Andika kichwa cha habari cha shairi hili kisichozidi maneno matano na kisichopungua maneno matatu.
10. Badili barua ifuatayo kuwa simu ya maandishi kwa kutumia maneno yasiyozidi kumi (10).
Shule ya Sekondari Busega,
S.L.P 1010,
KASULU.
10/11/2015.
Mpendwa kaka Haruna Mashaka, kwanza shikamoo!
Habari za hapo nyumbani? Wazazi wetu na wengine wote huko hawajambo? Mimi huku shuleni sijambo naendelea vizuri na masomo yangu.
Dhumuni la barua hii ni kukufahamisha kuwa nilipokuwa safarini kutoka nyumbani kuja shuleni, kwa bahati mbaya niliibiwa fedha za karo ya shule ulizonipa, hivyo bado nadaiwa karo ya shule. Tafadhali kaka nisamehe kwa usumbufu ninaokusababishia, nitumie fedha zingine kwa ajili ya karo ya shule.