JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI
021 KISWAHILI
Muda: 2:30 Mwaka: 2023
Maelekezo
Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenyejumla ya maswali kumi (10).
Jibu maswali yote kwenye nafasi ulizopewa.
Sehemu A na C zina alama kumi na tano (15) kila moja na sehemu B ina alama sabini (70).
Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
Vifaa vyote vya mawasiliano visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha upimaji.
Andika Namba yako ya Upimaji katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia.
KWA MATUMIZI YA MPIMAJI TUU
NAMBA YA SWALI
ALAMA
SAHIHI YA MPIMAJI
1.
2.
3.
4.
5.
6.
7.
8.
9.
10.
JUMLA
SAHIHI YA MHAKIKI
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Katika vipengele (i) hadi (x), chagua herufi ya jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo katika kisanduku ulichopewa.
(i) Ni methali ipi inayofanana na methali inayosema, "Mtaka cha uvunguni Sharti ainame”?
Ujanja mwingi mbele giza.
Mjumbe hauawi.
Akili nyingi huondoa maarifa.
Atangae sana na jua hujua.
Choose Answer :
(ii) Bainisha ubora wa kuhifadhi kazi za fasihi kwa kutumia njia ya picha na vinasa sauti.
Fanani na hadhira huonana ana kwa ana.
Wasanii huonekana dhahiri.
Huwa na gharama ya kumiliki.
Huweza kupotea na kutopatikana tena.
Choose Answer :
(iii) Mwalimu aliwaagiza wanafunzi wawili wajibizane kishairil mbele ya wenzao darasani. Ni kipera kipi kinawakilisha walichofanya wanafunzi hao?
Ngonjera
Majigambo
Kichekesho
Igizo
Choose Answer :
(iv) Sentensi ipi kati ya zifuatazo imeundwa kwa kitenzi kishirikishi?
Tanzania ilikuwa inapendeza toka zamani.
Watoto wanalima shamba dogo sana.
Watu wa mjini si wengi kama wa vijijini.
Mto mdogo umejaa majani mengi.
Choose Answer :
(v) Sauti ya lugha inayotamkwa bila kuwapo na kizuizi chochote kwenye mkondo wa hewa huitwaje?
Silabu
Irabu
Konsonanti
Mkazo
Choose Answer :
(vi) Mojawapo ya alama za uandishi ni nukta. Kazi ya alama hiyo ni ipi katika sentensi?
Kukariri au kurudia maneno yaliyosemwa.
Kuonesha sentensi imefikia mwisho na imekamilika.
Kubainisha sehemu mbili za sentensi zilizo kinyume.
Kuashiria maneno yaliyo kwenye orodha.
Choose Answer :
(vii) Mwalimu aliwataka wanafunzi kuchambua neno "anacheza” na kuonesha viambishi vyake. Uchambuzi upi unaonesha mpangalio sahihi wa viambishi?
Kiambishi awali ni a-, -na- na kiambishi tamati ni —a
Kiambishi awali ni —a na kiambishi tamati ni —na
Kiambishi awali ni —na- na tamati ni a-
Kiambishi awali ni —na- na chez na tamati ni a-
Choose Answer :
(viii) Kisawe cha neno "jokofu” ni kipi kati ya hivi?
Jiko
Tanuru
Friji
Stovu
Choose Answer :
(ix) Aina ipi ya kamusi hutumia lugha mbili?
Wahidiya
Thaniya
Mahuluti
Rubaia
Choose Answer :
(x) Maelezo yapi yanafafanua kwa usahihi dhana ya mofimu?
Kipashio kinachojitosheleza kileksika au kisarufi.
Kipashio kinachojitosheleza kimuundo au kileksika.
Kipashio kinachojitosheleza kimuundo au kisarufi.
Kipashio kinachounda msamiati au maneno.
Choose Answer :
p>2. Oanisha maana za tanzu za fasihi simulizi zilizopo katika Orodha A na tanzu husika kutoka Orodha B, kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kisanduku ulichopewa.
Orodha A
Orodha B
Tungo yenye mpangilio mzuri wa silabi na lugha ya mkato.
Tungo zenye muundo wa mashairi ya kimapokeo.
Maigizo yanayohusu mambo mbalimbali ya kishujaa.
Tungo zenye mpangilio wa silabi zinazolingana kwa kila mstari.
Mpangilio wa maneno unaoambatana na utendaji wa wahusika.
3. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Ulimwengu ni sawa na kitabu kikubwa ambacho juu ya ukubwa wote kurasa zake ni mbili, nazo ni furaha na huzuni. Mwanadamu katika safari yake ya maisha hapa duniani, hana budi kusoma kurasa zote mbili. Kwa mujibu wa maumbile, kila mwanadamu angependelea sana kudumu na ukurasa wa furaha, lakini matarajio haya hayapati kuwatokea waombaji. Badala yake huletewa kurasa hizo mbili kwa zamu. Ni dhahiri kwamba sisi sote tunajua kwamba kurasa hizi hazikwepeki na hatuna budi tuzisome.
Kama tulivyokuwa na majaliwa ya namna mbalimbali, imedhihirika kwamba kuna wengine wamejaliwa kusoma ukurasa wa furaha kwa muda mrefu kuliko kusoma wa huzuni. Pia kuna wale ambao kujaliwa kwao kumewafungulia ukurasa ule wa pili wa kusoma kwa muda mrefu zaidi kuliko wa kwanza. Tena, hapana shaka kwamba wapo waliojaliwa kupata huku na huku, sawasawa. Hivyo kila mmoja hana budi kuonja kurasa zote mbili.
Endapo kungetokea nafasi ya kuchagua ukurasa uupendao kusoma, bila shaka kila mmoja wetu angechagua ukurasa wa furaha. Lakini uchaguzi huu usingekuwa na tija kwa sababu watu wa kundi hili wangejua kwamba duniani kuna furaha tu na hakuna ambaye angeweza kuwarudi wanapofanya kufuru. Aidha, wasingewafikiria wenzao wenye huzuni na kuwafariji. Vilevile kama mmojawapo angekosea akachagua huzuni tu, pia angejihisi kuwa ni mnyonge sana katika jamii kwa sababu yeye angeishi maisha yaliyogubikwa na huzuni tu, wala furaha isingepata nafasi katika maisha yake.
Hali kama hii ingeleta watu kubaguana na kutosaidiana asilani, kusingekuwa na watu rahimu. Kwani, mwenye furaha angehisi nini mpaka amsaidie mwenye huzuni? Furaha na huzuni vinashabihiana katika maisha ya binadamu, utajiona una huzuni kwa sababu huna furaha, hivyo hivyo kwa mwenye furaha. Kauli mbiu ni kwamba "furaha na huzuni ni sehemu ya maisha" kubali matokeo ya hali ya maisha inayojitokeza.
Maswali
(a) Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma kisichozidi maneno matano
(b) Kwa nini mwandishi anasisitiza umuhimu wa kila mmoja kusoma kurasa zote mbili za kitabu9
(c) Eleza maana ya maneno kama yalivyotumika katika kifungu cha habari ulichosoma.
10.Umepata matatizo ya kiafya hivyo unahitaji kwenda kutibiwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma. Andika barua kwa Mkuu wa Shule kuomba ruhusa ya siku mbili. jina lako liwe Juhudi Sabuni na anuani iwe Shule ya Sekondari Tegemeo, S.L.P 130, Dodoma.