JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI
021 KISWAHILI
Muda: 2:30 Mwaka : 2022
Maelekezo
Karatasi hii ina sehemu A, B, na C zenye jumla ya maswali kumi (10)
Jibu maswali yote katika sehemu A na B na swali moja (1) kutoka sehemu C.
Sehemu A na C zina alama kumi na tano (15) kila moja na sehemu B ina alama sabini (70)
Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa
Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi
Vifaa vyote vya mawasiliano visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha upimaji.
Andika Namba yako ya Upimaji katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia
KWA MATUMIZI YA MPIMAJI TUU
NAMBA YA SWALI
ALAMA
SAHIHI YA MPIMAJI
1.
2.
3.
4.
5.
6.
7.
8.
9.
10.
JUMLA
SAHIHI YA MHAKIKI
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Katika vipengele (i) hadi (x) chagua herufi ya jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo katika kisanduku ulichopewa.
(i) Seti ipi ni sahihi kuhusu vipengele vya fani katika fasihi simulizi?
Dhamira, migogoro, mtindo na mafunzo.
Ujumbe, matumizi ya lugha, wahusika, mtindo na muundo
Wahusika, matumizi ya lugha, muundo, mtindo na mandhari
Migogoro, ujumbe, wahusika, mafunzo na mtindo.
Choose Answer :
(ii) Ni muundo upi wa ushairi wa fasihi simulizi unaundwa na mistari/mishororo mitano?
Sabilia
Takhmisa
Tathmisa
Tathilitha
Choose Answer :
(iii) Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia yana athari chanya na hasi katika ukuaji wa fasihi simulizi. Zipi ni athari hasi zinazoikabili fasihi simulizi?
Hupunguza hadhi na ubora wa kazi fasihi
Huhifadhi kazi za fasihi simulizi kwa muda mrefu.
Huboresha uwasilishaji wa kazi za fasihi simulizi
Hutunza kiini au maana ya ujumbe wa fasihi simulizi
Choose Answer :
(iv) Sababu zifuatazo husababishwa kutokea kwa utata katika tungo, isipokuwa:
Neno kuwa na maana zaidi ya moja
Kuzingatia taratibu za uandishi
Kutumia maneno yenye maana ya picha
Kutotamka neno ulilokusudia kwa usahihi
Choose Answer :
(v) Juma huimba vizuri sana. Nneo linalopigiwa msitari linafanya kazi ya aina ipi ya neno?
Kielezi
Kivumishi
Kitenzi
kihisishi
Choose Answer :
(vi) Wewe na rafiki yako mmepewa kazi ya kubainisha sentensi yenye vivumishi vya a-unganifu katika tungo. Je ni sentensi ipi katika ya zifuatazo itakuwa sahihi?
Juma anacheza kwa madoido
Halima mrefu amefika
Abdul na Zuberi wameondoka jana
Janeth wa Dodoma ameingia darasani
Choose Answer :
(vii) Kati ya kanuni zifuatazo mojawapo si sahihi kuhusu usimulizi wa matukio
Kutamka matamshi kwa usahihi
Mpangilio mzuri wa mawazo
Kujua muundo wa matukio kwa usahihi
Choose Answer :
(viii) Kati ya alama zifuatazo, alama ipi hutumika badala ya kiunganishi cha kuunga tungo mbili
Nukta (.)
Nukta pacha (:)
Mkato (,)
Alama ya mshangao (!)
Choose Answer :
(ix) Ipi ni dhima sahihi ya kutumia picha na michoro katika kamusi?
Hufanya kamusi kutambulika kwa haraka
Hufanya kamusi kupendwa na wasomaji
Hupunguza umakini na idadi ya watumiaji
Husaidia wasomaji kuwa na kumbukumbu
Choose Answer :
(x) Ipi ni maana sahihi ya shina la neno kati ya zifuatazo?
Sehemu ya neno yenye mzizi na viambishi awali na tamani
Sehemu ya neno yenye mzizi na viambishi awali pekee
Sehemu ya neno yenye mzizi na viambishi tamati pekee
Sehemu ya neno yenye mzizi na kiambishi tamati vijenzi.
Choose Answer :
2. Oanisha dhima za nyimbo za fasihi simulizi zilizo katika Orodha A na aina za nyimbo kutoka Orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kisanduku ulichopewa.
3. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Baba mmoja aliishi na mkewe na mwanae wa pekee wa kike. Baba huyu alikuwa mtu wa kufuata maadili, mila na desturi za kiafrika. Alitamani kila mmoja ndani ya nyumba aishi maisha ya kimalaika. Hakupenda mtu yeyote kwenda kinyume na mawazo yake ili maisha yake yasiende mrama., hasa mwanae aliyekuwa mboni ya jicho lake.
Binti yule akawa mtoto wa getikali, hakuna cha disko wala ufukweni, mama yake naye hakuruhusiwa kujipamba kiasi ch kupitiliza, ikiwemo kusuka nywele kwa mitindo ya kisasa. Mama na binti yake walilazimika kutii kwa kumuogopa baba yule wa miraba minne, mwenye kuongea kwa mrindimo.
Siku moja binti yake aliwazua, akabaini kwamba pale nyumbani hapakuwa na maisha anayoyahitaji, akaamua kufanya uamuzi mbaya wa kutoroka usiku. Baba na mama hawakujua mtoto alikokwenda. Mama akashikwa na kihoro akaumwa sana hatimaye umauti ukamfika.
Baba alisikitika sana, akatafakari na kutafakari, hatimaye akagundua kuwa msimamo wake haukuwa sahihi na kwamba alitakiwa kupokea mawazo na kusikiliza ushauri toka kwa wengine. Vilevile akagundua kuwa hakuna mtu aliyemkamilifu kwan binadamu wote tuna upungufu.
Maswali
(a) Pendekeza kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma kisichozidi maneno matano.
(b) Eleza maana ya maneno/vifungu vya maneno vifuatavyo kama vilivyotumika katika habari uliyosoma.