FORM TWO KISWAHILI NECTA 2017

2017 - KISWAHILI

SEHEMU A

UFAHAMU

    1.  Soma kifungu cha habari kifuatachokisha jibu maswali yanayofuata.

Tafiti zilizofanyika zinaoneshakuwa asilimia 60 ya raia wa mataifa yanayoendelea wanaishi katika hali ya umasikini. Kwa mujibu wa maelezo ya tafiti za Umoja wa Mataifa, watu masikini pato lao ni chini ya dola moja kwa siku. Uchumi wa mataifa hayo hutegemea sana kilimo ambacho huendeshwa kwa kutegemea mvua, ambayo kwa bahati mbaya mara kwa mara huwa adimu.

Yapo mataifa ambayo yametatua tatizo la ukosefu wa mvua kwa kutumia miradi ya umwagiliaji maji kutoka katika mito na maziwa. Miradi hii huhakikisha kuwa harakati za kilimo hazitegemei mvua pekee. Suala la umwagiliaji linahitaji uwekezaji mzuri na utengaji wa kasma ili kugharamia miradi yenyewe ambayo inaweza kuwa ghali. Uwekezaji huu unaweza kuwapo ikiwa viongozi wataweka msisitizo katika miradi husika.

Katika mataifa mengine kuna juhudi za kuhakikisha kuwa maji ya mvua yanahifadhiwa katika njia ifaayo kwa matumizi ya nyumbani na hata katika umwagiliaji mashambani. Maji hayo yanaweza kuhifadhiwa kwa utengenezaji wa mabwawa. Isitoshe uchimbaji wa visima vya maji unaweza kusaidia Pia.

Licha ya kuwa maji yatokanayo na visima hayawezi kutumika katika umwagiliaji kwa kiwango cha juu, maji hayo yanaweza kutumika katika kilimo cha bustani. Kilimo cha namna hii kinaweza kupunguza adha maisha kwa wananchi.

Maswali

(a)     Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma kisichozidi maneno matano.

(b)    Kwa mujibu wa habari uliyosoma unadhani ni kwa nini kilimo cha umwagiliaji ni cha uhakika?

(c)     Taja njia tatu zinazotumiwa na baadhi ya nchi zinazoendelea katika kutatua tatizo la uhaba wa mvua.

(d)    Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu cha habari ulichosoma:

(i)Adimu

(ii)Kasma

(iii) Ghali

(iv)Adha

View Ans


2. Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasiyopungua hamsini (50) na yasiyozidi sitini (60)

View Ans


SEHEMU B

SARUFI

3.         Eleza dhima mbili kwa kila mofimu iliyopigiwa mstari 

(a) Mama atakuja kesho.

(b)      Mti umeanguka.

(c)       Mwalimu alimfundisha Juma.

(d)      Ninakupenda.

(e)       Sitakuja shuleni kesho.

View Ans


4.         Panga maneno yafuatayo kama yanavyotakiwa kuwa kwenye kamusi.

(a)       Duwaa

(b)      Chichiri

(c)       Adhabu

(d)      Kidahizo

(e)       Faladi 

(f)      Chege

(g)     Kitomeo

(h)     Dabiri    

(i)     Anzali

(j)      Fanusi

View Ans


SEHEMU C

MAWASILIANO NA UTUMIZI WA LUGHA

5.         Eleza kwa kifupi dhima tano za lugha katika jamii.

View Ans


6.         (a) Eleza maana ya misimu katika lugha ya Kiswahili.

            (b) Fafanua sifa nne za misimu.

View Ans


SEHEMU D

FASIHI KWA UJUMLA

7.         (a) Tengua vitendawili vifuatavyo:

(i) Nasuka mkeka lakini nalala Chini ...... ......... 

(ii) Kila aendapo huacha alama .........................

(iii)Nikimpiga mwanangu watu hucheza .......

(iv)Anatembea na nyumba yake .....................

(v)Nyumba yangu ina nguzo moja . ..... . ...... .. 

(b)      Kamilisha methali zifuatazo:

(i)Vita vya panzi ....... ........„......... ....... ...... ............ 

(ii) Hakuna marefu ......... .............. ...... ..... . ...... . ...... 

(iii) Siri ya mtungi ........... . ....................

(iv)Baniani mbaya ......................... . .......

(v)Mgaagaa na upwa ... ...... ...... ....... ...................

View Ans


8. Fafanua vipengele vifuatavyo vya fani:

(a) Mandhari

(b) Wahusika

Fanani

(d) Hadhira

(e) Muundo

View Ans


9.  Eleza kufanana na kutokufanana kwa vipera vifuatavyo vya fasihi simulizi.

Toa hoja moja katika kufanana na hoja moja katika kutofautiana.

 (a) Vitendawili na methali

(i) Kufanana ..... ...... . .

(ii) Kutofautiana ... . .....

(b)      Majigambo na ngonjera

(i)Kufanana . ...... ......

(ii)Kutofautiana ..... ....

(c)   Misemo na nahau

(i)Kufanana ... ...... .. 

(ii)Kutofautiana . ........

(d)  Utenzi na shairi

(i)Kufanana .............

(ii)Kutofautiana ... ......

(d) Michezo ya jukwaani na vichekesho

(i)Kufanana ....... ......

(ii)Kutofautiana ...... ...

View Ans


SEHEMU D

UANDISHI WA INSHA/UTUNGAJI

10. Kwa maneno yasiyopungua 150 na yasiyozidi 200, andika insha kuhusu Umuhimu wa Misitu katika Jamii kwa kutumia hoja nne.

View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256