FORM TWO KISWAHILI NECTA 2015

2015 - KISWAHILI

SEHEMU A

UFAHAMU

1. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:

Wakati wa ukoloni mabepari wa Kijerumani walianzisha kilimo cha pamba huko Kusini mwa Tanzani. Waliwalazimisha Wamatumbi kufanya kazi katika mashamba yao. Pamba iliyopatikana ilipelekwa Ujerumani. Kama anavyosema kibarua mmoja aliyeteswa na mabepari hao, "Wakati wa kilimo kulikuwa na dhiki sana. Sisi vibarua tuliokamatwa tulikaa mstari wa mbele, tukilima. Nyuma yetu kuliwa namnyapara,kazi yake kutupiga kwa mijeledi. Nyuma ya mnyapara alikuwepo jumbe, na kila jumbe alisimama nyuma ya watu hamsini. Na nyuma ya majumbe alisimama Bwana Kinoo mwenyewe. Lo! Hapo shuhudia kifo."

Mjerumani alipofika nchini akaamrisha Wamatumbi kulipa kodi. Watu walimjibu, "Hudai kitu. Hatuna deni kwako. Ikiwa wewe mgeni unataka kukaa nchi hii basi ni lazima wewe utuombe sisi. Na Sisi tutakuambia utoe sadaka kwa Miungu wetu. Wewe utatoa chochote na Sisi tutaifanyia karamu Miungu kwa niaba yako; tutakupa ardhi na wewe utakuwa na mahali pa kukaa. Lakini siyo Sisi wenyeji tukupe wewe sadaka. Hilo haliwezekani hata kidogo".

Juu ya dhiki zote walizopata yaani dhiki ya njaa, dhiki ya maonevu, dhiki ya kulimishwa na kupigwa, watu walistahimili wakavumilia kwa sababu hawakuweza kupigana, kwani hawakuwa na umoja. Vilevile walijua kuwa nguvu ya Mjerumani ilikuwa kubwa. Wakangoja.

Katika mwaka wa 1904 akaja mtume, jina lake Kinjeketile. Karibu na kwao Ngarambe kulikuwa na bwawa la maji katika kijito cha Mto Rufiji. Kinjeketile alipandwa na pepo aitwaye Hongo, aliyekuwa akikaa katika bwawa hilo.

Kinjeketile aliwafundisha Waafrika maana ya umoja. akawapa moyo kwa nguvu ya maji. Waafrika wakawa na umoja na nguvu. Watu wengi waliosikia jina lake walikuja kumuunga mkono.

MASWALI

(a)Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari uliyosoma kisichozidi maneno matano.

(b) Eleza wazo kuu linalojitokeza katika habari uliyoisoma.

(c) Ni mambo gani yanayothibitisha kwamba ni kweli Wamatumbi waliteswa? Taja mambo matatu.

(d) Toa maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu cha habari ulichosoma.

(i)Mnyapara ....

(ii)Mijeledi .........

(iii) Walistahimili .....

(iv) Sadaka ... ... ...

(v) Mtume . . . . . . . . .

(e)Ni mambo gani mawili unayojifunza kutokana na habari hii?

(f)Fupisha aya ya kwanza hadi ya tatu kwa maneno yasiyozidi 40.

View Ans


SEHEMU B

UTUMIZI WA LUCHA NA USAHIHI WA MAANDISHI

2. (a) Kwa kauli zifuatazo andikaKweli kwa kauli iliyo sahihi au Si Kweli kwa kauli isiyo sahihi.

(i)Kazi ya fasihi ni moja tu na ni ile ya kuelimisha jamii ........

(ii)Kiunganishi ni neno ambalo huunganisha dhana mbili tu.

(iii)Elekeza, shikilia, shikamana, maelekezo, mshikamano, tolewa, nitakutolea, ondokeni ni maneno yaliyoundwa kutokana na mnyumbuliko .........

(iv)Methali ni usemi wenye pande mbili .........

(v)Kitendawili ni aina ya fumbo lisilotumia lugha ya picha lakini hudai jibu .

(b)Andika tungo zifuatazo kwa usahihi:

(i)Mwalimu mkuu amewakilisha mada katika mkutano.

(ii)Nilikwenda mjini nikamkutana Maria.

(iii)Habarini zenu mabibi na maBwana.

(iv)Kila siku nafanyaga kazi.

(v)Kwa kuwa sina gari nitakwenda na miguu.

(c)Andika mifano ya kauli zinazoonesha muktadha wa rejesta zifuatazo:

(i)Hotelini ... ... ... 

(ii) Mahakamani ............

(iii) Dukani .............

(iv) Darasani . . . . . . . . .

(v)Hospitalini ................

View Ans


SEHEMU C

SARUFI

3. (a) Nyumbua maneno yafuatayo na kuunda maneno manne kwa kila neno:

(i) Angalia ... ... ...

(ii)Chukua ...............

(iii)Oga ... ... ...

(iv)Kata . . ................

(v)Omba ... ... ..........

(b) Tumia maneno yafuatayo kama nomino na utunge sentensi moja kwa kila neno:

(i) Starehe . ..............

(ii) Ukweli .........

(iii)Utaalamu ...... .. 

 (iv) Umoja ... ... ...

(v) Uzembe ...........

(vi) Ukarimu .... .....

(viii) Upweke .. .....

(vii) Ushujaa . .........

(ix) Upendo ... ... ...    

(x) Furaha . .............

(c) Kitenzi kikuu huweza kutumika sambamba na kitenzi kingine kukamilisha sentensi. Katika sentensi zifuatazo bainisha vitenzi vilivyotumika. Sentensi ya kwanza ni mfano:

(i) Aliyekuja atasafiri kesho.

(ii) Mgeni wangu amekwisha kuwasili.

(iii) Amina hakutaka kumuudhi.

(iv)Mafundi wangali wanashona viatu.

(v)Wataendelea kumsubiri hadi kesho.

(vi) Gari lilikuwa limeharibika mlimani Kitonga

View Ans


SEHEMU D

FASIHI SIMULIZI

4. (a) Eleza kwa kifupi maana ya dhana zifuatazo:

(i) Shairi .............

(ii)Vichekesho ... ... ...

(iii)Ngonjera ... ......

(iv)Visasili .............

(v) Mapingiti ..............

(b) Jaza nafasi iliyoachwa wazi kukamilisha methali zifuatazo:

(i) Samaki mkunje ........................

(ii) ............njaa mwana malegeza. 

(iii) ..........hutanda na kuyeyuka. 

(iv)  Ajidhaniaye kasimama .........

 (v) ...........usiilalie mlango wazi.

 (c) Soma shairi lifuatalo kisha jibu maswali yanayofuata:

Mwanafunzi ikibali, mbeleya wako mwalimu.

Katika siku si mbali, utakuwa aalimu,

Kujitia baradhuli, baadaye ulaumu,

Mbeleya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali.

Usijifanye kiburi, kujifanya chakaramu,

Hiyo wanaita shari, ndaniyake ina sumu,

Hivi hauna habari, heshima kitu adimu,

Mbeleya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali.

Katika hii sayari, namba moja ni elimu,

Usiipate sufuri, kisha hapo ulaumu,

Maisha haya safari, mwana kitu adimu,

Mbeleya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali.

Ni walezi mashuhuri, hivyo wana umuhimu, 

Wameishika nambari, kutokana na kalamu, 

Usimwendeshe chuchuri, uidumishe nidhamu, 

Mbeleya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali.

Mwalimu baba na mama, hilo wazi ufahamu,

Hivyo tazama ndarama, zisisababishe-ghamu, 

Neno hili ni la zama, shika nakupajukumu,

Mbeleya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali.

Sitapenda kukuchosha, kwa mengi kukushutumu,

Nakutakia maisha,ya shuleyenye utamu,

Ili upate bashasha,na mema kutakadamu,

Mbeleya wako mwalimu, mwanafunzi ikibali.

MASWALI

(i)Mtunzi wa shairi hili anatoa ujumbe gani?

(ii)Ni mambo gani matatu ambayo mwanafunzi unatakiwa kuyaepuka kama yalivyoelezwa katika shairi ulilosoma?

(iii) Bainisha kituo bahari katika shairi ulilosoma.

(iv)Bainisha vina vya kati na vya mwisho vya shairi ulilosoma.

(v)Mshairi ana maana gani anaposema, Neno hili ni la zama, shika nakupa jukumu.”

(vi) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi ulilosoma:

 • Ikibali ..... ... .
 •  Baradhuli ...........
 • Kutakadamu .........
 •  Chuchuri .........
 • Bashasha .........
 • View Ans


  SEHEMU E

  UANDISHI WA INSHA/UTUNGAJI. 

  Unatarajia kwenda kumtembelea shangazi yako aitwaye Nakijwa aishiye Ikwiriri Rufiji. Andika barua kwa shangazi kumjulisha makusudio yako. Jina lako liwe Jaja Okwi, Shule ya Sekondari Ndorwe, S.L.P 1534. Kilomeni. Mwanga.

  View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256