FORM TWO KISWAHILI NECTA 2013

SEHEMU A

1. Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata.

Ukisimama hadharani kuzungumzia suala la haki za wanaume, watu wengi watakuona mwendawazimu, lakini wanaume wanazo -12n_raniot, kadhaa. Ni siri iliyofichuka sasa kuwa ni zamu ya wanaume kunyanyaswa kama walivyonyanyaswa wanawake.

Kwa miongu miwili ya mwisho wa karne ya ishirini, dunia nzima imekuwa katika za kutetea haki za wanawake hususan watoto wa kike. Ni kweli kuwa mtoto wa kike amekuwa akidunishwa na kudhulumiwa na mifumo ya kitamaduni, kisiasa na kiuchumi iliyokosa mashiko.

Wasichana walitumbukia kwenye ghilba za ndoa za mapema katika umri mdogo, hawakupata fursa ya kwenda shule, walikeketwa na kufanyiwa dhuluma nyingine kadha wa kadha. Kutokana na hali hii, mtoto wa kiume amekuwa akifurahia hadhi ya kuzaliwa akiwa mvulana, kwamba ndiye anayefaa zaidi ya msichana. Si ajabu mzee mmoja kumuoza bintiye iii mahari itakayopatikana ilipe karo ya kaka yake anayesoma. Kikao kikuu cha haki za wanawake kule Beijing China cha mwaka 1985, ni mojawapo ya vikao vilivyomulika zaidi haki za wanawake.

Mashirika yasiyo ya kiserikali, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, serikali mbalimbali na hata makampuni yaliunga mkono harakati za kupigana na adui mmoja "kukosekana kwa usawa wa ". Lengo lilikuwa ni kumkweza msichana iii afike alipokuwa mvulana. Misaada ikatolewa, miradi ikaanzishwa, shule zikajengwa, mashirika ya kidini yakaibuka, mikopo ikatolewa na vyote vilimlenga huyo msichana aliyekuwa na mahitaji makubwa ya haki. Msichana akakwenA; kwa kiasi kikubwa, akakikwea kizingiti.

Hatari ya harabi hizi, ni kuelemea upande wa jinsia ya kike zaidi na kusahau wanaume. Wanaume pia wanahitaji kupewa fursa na haki sawa kama wanawake. Tatizo la ajira kwa watoto hususan wa kiume waishio katika mazingira magumu na hatarishi linaongezeka nchini. Visa vya wizi, uharibifu wa mali na mauaji ya watu wasio na hatia vimezidi, aghalabu vijana ndio hutumiwa zaidi na watu wenye pesa kufanya uhalifu huo. Wapo ambao hawaendi shule wamegeukia dawa za kulevya, wanaitwa "mateja". Jitihada za dhati lazima zifanyike kuliokoa kundi hilo.

 MASWALI

 1. Andika kichwa cha habari kinachofaa kwa habari hii (maneno yasizidi matano)
 2. Je, tatizo kuu linalozungumziwa katika habari uliyoisoma hapo ni lipi?
 3. Taja vitendo viwili vya unyanyaswaji walivyofanyiwa wasichana kulingana na habari uliyosoma.
 4. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika habari uliyosoma.

(i) Changamoto ................ (ii) Jinsia ....... 

(iii) Kukweza ......... (iv) Harakati ..... 

(v) Miongo........ 

(e) Andika ufupisho wa habari hiyo kwa maneno yasiyopungua 40 na yasiyozidi 80.

View Ans


SEHEMU B: UTUMIZI WA LUGHA NA USAHIHI WA UANDISHI

2. (a) Oanisha Orodha A na kujenga dhana sahihi. Onesha majibu yako kwa kutumia kisanduku ulichopewa. Namba (i) umepewa kama mfano.

Orodha A

Orodha B

(i) Huonesha mpangilio wa maneno ya lugha ki­alfabeti, maana zake, jinsi yanavyoandikwa na kutamkwa.

(ii) Lugha ya mazungumzo na Lugha ya maandishi.

(iii) Maneneo ambayo si sanifu yanayotumiwa na watu wachache wenye utamaduni mmoja.

(iv) Mazungumzo au majibizano ya kupokezana baina ya watu wawili au zaidi.

(v) Mtindo wa lugha kulingana na muktadha na kusudi la mazungumzo.

(vi) Taaluma inayohusu mpangilio wa maneno katika tungo.

 1. Dayalojia
 2. Kamusi
 3. Kidahizo
 4. Misimu
 5. Rejesta
 6. Sarufi Maumbo
 7. Sarufi Miundo
 8. Semi
 9. Tanzu za Lugha
View Ans


(b) Chunguza mazungumzo yafuatayo kisha jaza sehemu zilizoachwa wazi. 

Mchuuzi: Karibu mteja, mali mpya imengia leo leo. Kuangalia ni bure 

Mteja: Viatu vya wanafunzi unauzaje?

Mchuuzi: . . . . . . . . . . . . . . . 

Mteja: . . . . . . . . . . . . . . . 

Mchuuzi: . . . . . . . . . . . . . . . . 

Mteja: . . . . . . . . . . . . . . . 

Mchuuzi: . . . . . . . . . . . . . . . 

Mteja: Ninazo hizo to ndugu yangu.

Mchuuzi: Basi lete, nipate hata nauli ya kurudia.

View Ans


(c) Sentensi zifuatazo ni tata. Toa maana mbili kwa kila sentensi iii kuthibitisha utata huo.

 1. Amempigia nini? ... 
 2. Ameiba kanga 
 3. Ukipita sokoni njoo na nyanya 
 4. Dada, una ua? .. 
 5. He ni nyumba ya wageni.. 
View Ans


3. (a) Bainisha aina za maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo. Sentensi ya kwanza ni mfano:

 1. Viti vizuri vimepangwa vizuri sana.
 2. Jumba lilikuwa Jimepasuka kuta zake mara tano.
 3. Ah! Mwenzetu ameumia.
 4. Wale wali wa Liwale wamefika.
 5. Nitasafiri ingawa sijajiandaa.
View Ans


 (b) Chunguza jedwali lifuatalo kwa makini kisha jaza sehemu zilizoachwa wazi.

NENO Mzizi Kauli Ya Kutendeana Kauli Ya Kutendwa
Kusema  . . . . . . . . . . .  . . . . . . . . . .  . . . . . . . . 
 . . . . . . .  . . . . . . . . . .. Kupigana  . . . . . . . .
Kuomba  . . . . . . . . . .  Kuombana  . . . . . . . .
 . . . . . . . . Andik  . . . . . . Kundikwa
View Ans


(c) Kamusi ina mambo makuu mawili ambayo ni Kidahizo na Kitomeo. Taja taarifa tano zinazopatikana kwenye kitomeo.

View Ans


SEHEMU D : FASIHI SIMULIZI

4. (a) Katika kuumba sanaa, kuna nyenzo mbalimbali zinazotumika ili kutofautisha maumbo/sanaa hizo. Kwa kutumia mchoro ufuatao, taja matawi ya sanaa unayoyafahamu.

View Ans


(b) Andika methali au nahau moja inayoelezea uhalisia wa tabia za watu za kila siku katika maisha yao kama zilivyotajwa katika jedwali lifuatalo:

Aina Ya Tabia Methali au Nahau Inayo husika
(i) Uchoyo
(ii) Uvivu wa kuishi na kutegemea mali au hali ya ndugu
(iii) Kusema sana au kuzungumza kulinganisha na wanakikundi hicho (Kutawa mazungumzo)
(iv) Kutoa au kupekea rushwa
(v) Kulea watoto katika malezi yasiyo faa kwa kuogopa kuwa wataumia. Hatimaye wanafikia kusababisha hasara kwa wazazi.

 1.  . . . . . . . . . . .
 2. . . . . . . . . . . .
 3.  
 4. . . . . . . . . . . .
 5. . . . . . . . . . . .
View Ans


(c) Soma utungo ufuatao kisha hakiki maudhui yake

Nakuona waduwaa, 

Maisha kuyashangaa, 

Husuda zimekujaa, 

Kuhusudu walojaa,

Siharakishe maisha, 

nawe una fungu lako.

Ubado ni mwanafunzi, 

Usiingiwe simanzi,

Ruka vikwazo vya pumzi,

Uipambe yako enzi,

Maisha safari ndefu, 

kutembea usichoke.

Soma bado endelea, 

Sicheze pate potea, 

Muda ukishatimia, 

Maisha tafurahisha, 

Usiache kutegua, kwa kutegemea tega.

Punguza haraka zako, 

Badilisha mwendo wako, 

Subira ni chombo chako, T

akutwisha kwenye fuko,

Usisahu usemi, subira yavuta heri.

MASWAL1

 1. Nini dhamira ya mtunzi wa utungo huu?
 2. Mtunzi wa utungo huu anakerwa na kitu gani?
 3. Taja ujumbe mmoja anaotoa mtunzi wa utungo huu.
 4. Mtunzi wa utungo huu anaamini nini kuhusu maisha ya mtu?
 5. Elezea fundisho moja unalolipata baada ya kusoma utungo huu. 
View Ans


SEHEMU E : UANDISHI WA INSHA/UTUt4GAJI

5. Wewe ni miongoni mwa Watanzania wanaopenda kuishi maisha marefu, hivyo unakerwa sana na tatizo la ajali za barabarani. Andika barua kwenye gazeti la Uhuru ukipendekeza kwa serikali hatua gani zichukuliwe iii kuthibiti ajali za barabarani. Toa hoja tatu tu.

View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256