FORM TWO KISWAHILI NECTA 2006

KISWAHILI 2006

SEHEMU A UFAHAMU

1. Soma kifungu cha habari kifuatacho, kisha jibu maswali.

"Naomba mia, naomba hela ya kula, shikamoo! Mzazi leo nimelala nikihesabu mapaa na mitambaa panya. Naomba msaada! Nisaidieee " Hayo ndiyo maneno yanayotawala kundi ambalo linaendelea kuwa kubwa la kizazi cha leo. Kundi hilo limesahaulika kana kwamba jamii haioni Ni lugha inayosikika na inayoendelea kuenea katika miji mikubwa kwa midogo, na sehemu mbalimball zenye mkusanyiko wa watu. Ukitaka kujua ni nani wanaotoa kilio hicho kila kukicha, basi siku moja ubahatike kukutana na mtoto mmojawapo kati ya kundi la "watoto wa mitaani" utayaamini hayo yanayosemwa.

Hali hiyo waliyonayo siyo kwamba wameitaka iwasibu, la hasha! Imewapata kutokana na mlolongo wa mambo yanayochangia half hiyo kutokea; kuyaeleza yote mengine nitayatia chumvi, lakini umasikini kutamalaki katika familia zetu ni mojawapo. Aidha uzazi usiotarajiwa, na pengine katika umri mdogo, ukosefu wa elimu, kuvunjika kwa ndoa na kubwa zaidi gonjwa la UKIMWI lililotapakaa nalo limeongezea tatizo hili kuwa kubwa.

Kilio cha kundi hilo kingesikilizwa, kungekuwa na ahueni, lakini wapi? Watoto hao wanaambulia kubakwa na kulawitiwa. Tiba zenyewe hawapati, na kuhusu elimu, kwao inakuwa ni njozi na ni vigumu kutekelezwa. Hatimaye, kundi hilo linapokosa matumaini, basi madawa ya kulevya, pombe na wizi vinakuwa ndilo kimbilio lao.

Kila mwananchi, wewe na mimi tunapowaona wahusika hao, tunamtupia fulani mpira huo, kwamba ndiye mwenye uwezo na wajibu wa kumiliki tatizo hilo. Kasumba hiyo haiwezi kumaliza janga hilo. Hatuna budi wote tuliokusanyika kwenye kona tuone kama kila mmoja wetu anawajibika kuiondoa hatari hii. Kukaa pembeni na kubaki kuoneshea kidole na kukandia wengine to ati fulani ndiye mwenye jukumu la kutunza kundi hilo, si sahihi. Hivi ndivyo tusemavyo eti, "Serikali ndiyo yenye jukumu hilo". Lakini serikali ni pamoja na sisi sote. Waswahili husema,"Mchelea mwana kulia, mwishoni utalia wewe".

MASWALI

(i) Andika kichwa cha habari kisichozo zidi maneno matatu

View Ans


(ii) Mwandishi anasema ukitaka kuamini yanayosemwa ufanye nini?

View Ans


(iii) Taja jambo kubwa moja ambalo limeonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa tatizo analolizungumzia mwandishi.

View Ans


(iv) Ni maeneo gani ambamo kundi la watu hao huonekana?

View Ans


(v) Watoto hao wa mitaani walishakata tamaa ya maisha na kukimbilia kwenye nini?

View Ans


(vi) Mwandishi ana maana gani anaposema, "Kukaa pembeni na kuoneshea kidole na kukandia wengine"?

View Ans


(vii) Eleza maana za maneno yafuatayo jinsi yalivyotumiwa katika habari hii.

  • Ahueni
  • Njozi
  • Mpira
  • Wajibu
  • Chumvi
View Ans


(viii) Taja funzo moja unalolipata kutokana na habari hii.

View Ans


(ix) Andika ufupisho wa habari hii usiozidi maneno sitini (60). 

View Ans


SEHEMU B

LUGHA KWA UJUMLA NA UTUMIZI WAKE

2. (a) Taja kazi nne (4) za lugha katika jamii.

View Ans


(b) Ni mazingira gani ambamo rejesta zifuatazo hutumika?

  • Kaa chini, simama juu, mbele tembea..........
  • Bwana alitoa na Bwana ametwaa. .........
  • Haloo, leo mzigo mzito, meli imesheheni kweli..........
  • Yule ticha mnoko sana, ngoja nitampa sulubu. .........
  • Mpambe mwanao kwa shilingi mia mbili, baba mpambe mkeo kwa mia tatu.
View Ans


(c) Onesha kosa la kisarufi katika sentensi zifuatazo, kisha uziandike kwa usahihi.

  • Enyi ndugu zangu samahanini kwa makosa niliyowatendea.

Kosa: . . . . . . ..

Usahihi: ......

  • Wakati huu utakuwa aidha nyumbani au kazini.

Kosa: . . . . . . ..

Usahihi: ......

  • Nyinyi nyote njooni hapa 

Kosa: . . . . . . ..

Usahihi: ......

  • Asha anasambaza vitabu mashuleni.

Kosa: ......

Usahihi: ....

  • Kwa mapungufu tuliyoona hatuna budi kufanya kazi kwa bidii.

Kosa: ......

Usahihi: ......

View Ans


SEHEMU C

SARUFI

3. (a) Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali.

Marafiki ni muhimu sana kwa kila mwanadamu. Hawa wanahitajika ili kutuondolea ukiwa na kuleta faraja. Marafiki hupatikana mahali popote, shuleni, kazini, nyumbani na safarini. Wapo marafiki walio wema na wengine wabaya. Tunatakiwa tuchague wale walio wema lakini tusiwachukie walio wabaya.

Swali: Kutokana na habari uliyosoma, andika maneno mawili kwa kila kundi la maneno lililoorodheshwa.

  • Nomino
  • Vitenzi
  • Vielezi
  • Vivumishi
  • Viunganishi
View Ans


(b) Panga maneno yafuatayo kama yatakavyokuwa katika kamusi:

Kafeli, Tosha, Zaituni, Zainabu, Buriani, Roho, Paroko, Kaheshimu.

View Ans


(c) Eleza dhima za mofimu zilizopigiwa mstari katika maneno yafuatayo:

  1. Sitaki ..........................
  2. Amekiondoa .....................
  3. Wamejiua ........................
  4. Umesoma........................
  5. Mazungumzo......................
View Ans


(d) Nyumbua maneno yafutayo katika kauli za kutendeka, kutendea, kutendwa.

MANENO

KUTENDEKA

KUTENDEA

KUTENDWA

Fyeka




Vunja




Lipa




Tesa




View Ans


SEHEMU D 
UTUNGAJI

4. Soma simu ya maandishi ifuatayo kisha uandike majibu kwa simu ya maandishi ukieleza kuwa hutaweza kwenda haraka kwa sababu uko kwenye kipindi cha mtihani.

BAHATI KAZI SLP 74 IRINGA MAMA MGONJWA NJOO HARAKA WARIDI.

Kwa kujibu tumia jina na anwani ifuatayo - Waridi Kazi, S.L.P 18 Same. Simu hiyo isizidi maneno kumi (10).

View Ans


5.(a)(i) Ili fasihi simulizi iweze kuwasilishwa, inahitaji mambo makuu matano(5), ambayo ni . .. . . . . . .

View Ans


(ii) Taja vipengele vitano(5) viundavyo fani katika kazi ya fasihi

View Ans


(b) Zifuatazo ni njia zinazotumiwa katika kuhifadhi fasihi simulizi. Onesha faida moja na hasara moja kwa kila njia.

NJIA FAIDA HASARA
(i) Kichwani(Akilini)

(ii) Maandishi

(iii) Sinema

(iv) Kanda za vinasa sauti

(v) Picha

View Ans


(c) Andika kipera cha fasihi simulizi kinacholingana na maelezo yaliyotolewa

  • Maneno ya mzaha na ucheshi yanayoongelewa kati ya mtu na mtu, kabila na kabila na ukoo na ukoo
  • Sala au ibada inayo wasilishwa kwa Mungu au miungu ikiambatanishwa na sadaka kwaajili ya kuomba uponyaji, kukinga magonjwa, majanga ya njaa na ukame
  • Semi zinazozunguka katika jamii kwa kutaka kueleza hali na matukio mbalimbali yanayo tokea kwa wakati huo
  • Semi fupi zenye mafunzo zinazo hitaji majibu
  • Hadith fupi zinazosimulia asili ya watu, wanyama na vitu visivyo hai
View Ans


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256