OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI BAADA YA MTIHANI WA UTAMIRIFU KIDATO CHA PILI
060 HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI
Masaa 2:30 Agosti 2026
MAELEKEZO
KWA MATUMIZI YA WATAHINI TU
| NAMBA YA SWALI | ALAMA | SAHIHI YA WATAHINI |
| 1 | ||
| 2 | ||
| 3 | ||
| 4 | ||
| 5 | ||
| 6 | ||
| 7 | ||
| 8 | ||
| 9 | ||
| 10 | ||
| JUMLA | ||
| SAHIHI YA WAHAKIKI | ||
SEHEMU A (ALAMA 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Katika kipengele (i) hadi (x) chagua herufi ya jibu sahihi, kisha andika herufi ya jibu hilo katika kisanduku ulichopewa.
i. Mwanafunzi mgeni wa kidato cha kwanza aitwae Meko ameshindwa kuelewa kwa undani maana ya neno “Historia ya Tanzania”. Mwalimu wa somo hilo Rashidi akakupa nafasi ya kumuelewesha kwa ufupi. Ipi kati ya maana zifuatazo utazizingatia wakati wa kumuelewesha?
ii. Salma anajivunia kuwa miongoni mwa wanafunzi wanaosoma somo la “Historia ya Tanzania na Maadili”, kwa kuwaelimisha kuwa na mapenzi na nchi yake. Kitendo hiki cha Salma kuipenda nchi yake kinajulikana kuwa ni?
iii. Wakati wa ufundishaji wa mada ya pili katika dhana ya jamii, Mwalimu Juma alisema “Ni mkusanyiko wa familia mbalimbali zenye uhusiano wa karibu”. Maana hii inashabihiana na ipi kati ya vipengele vifuatavyo?
iv. Katika kuhakikisha utunzwaji wa maeneo ya kihistoria duniani, Umoja wa Mataifa umeunda shirika linaloshughulikia utambuzi na upitishaji wa maeneo hayo kama Urithi wa Dunia na nchi husika. Lipi kati ya mashirika yafuatayo linajihusisha na masuala tajwa hapo juu?
v. Mila, desturi, lugha na ufundi ni kundi linalowakilisha urithi unaopatikana katika nchi ya Tanzania. Je, ni aina gani ya urithi?
vi. Katika hotuba yake juu ya ustawi wa maadili na maliasili za taifa, Waziri Mkuu alizungumzia majukumu yanayohusiana na uhifadhi na ulinzi wa urithi wa taifa na maadili. Unadhani ni nani hasa anayehusika na ulinzi huo kwa maendeleo ya taifa letu?
vii. Waarabu wa kwanza kuja Pwani ya Afrika walikuja kufanya biashara ya:
viii. Mfumo wa utawala wa Waingereza ulibadilika kutoka:
ix. Misingi mikuu ya maadili ya jamii za Kitanzania wakati wa ukoloni unaingia imejipambanua katika nyanja mbalimbali ikijumuisha vipengele vifuatavyo isipokuwa kipengele kimojawapo:-
x. Sababu zilizopelekea kushindwa kwa jamii nyingi za Kitanzania katika kupambana na ukoloni ni pamoja na:-
MAJIBU
| i | ii | iii | iv | v | vi | vii | viii | ix | x |
| . |
2. Oanisha vipengele vinavyoonesha kauli na kampeni za maraisi wa Tanzania katika vipindi mbalimbali juu ya mapambano dhidi ya rushwa na mmomonyoko wa maadili kutoka Orodha A na kundi husika kutoka Orodha B, kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kisanduku ulichopewa.
| ORODHA A | ORODHA B |
| i. African Association (AA) ii. Tanganyika African Association (TAA) iii. Afro-Shirazi Party (ASP) iv. Zanzibar and Pemba People’s Party (ZPPP) v. Zanzibar Nationalist Party (ZNP) | A. 1957 B. 1955 C. 1929 D. 1948 E. 1959 |
MAJIBU
| i | ii | iii | iv | v |
| . |
SEHEMU B (Alama 70)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
3. Kileo ni mwanafunzi wa kidato cha pili aliyeshindwa kuelewa athari mbalimbali za mifumo ya wakoloni katika maadili ya Kitanzania, muelezee athari zifuatazo:
4. Wanafunzi wa mkondo wa biashara wa shule ya sekondari Mawella walitakiwa kufanya utafiti kwa njia ya mtandao ili kubaini shughuli mbalimbali zilizofanywa na makundi ya jamii ya asili ya Kitanzania. Unadhani ni shughuli zipi walizibaini na kuzinukuu katika madaftari yao? Taja shughuli tano (5).
5. Wananchi wa Tanganyika na Zanzibar walitumia mbinu mbalimbali za kudai uhuru, onesha mbinu tano (5) zilizotumika kupigania uhuru kutoka kwa wakoloni.
6. Jamii za Kitanzania imebeba zana ya kuwa na tabia. Ziainishe tabia tano (5) njema zinazofanywa na Watanzania:-
7. Chriss ni mwanafunzi wa chuo cha Oxford nchini Uingereza, anapenda umjulishe orodha ya urithi (5) wa dunia upatikanao Tanzania.
8. Mwalimu wa somo la Historia ya Tanzania alifundisha juu ya fursa zitokanazo na urithi wa jamii za Kitanzania ambapo alianisha mambo mbalimbali. Taja fursa tano (5).
9. Taja makundi makuu matano ya jamii za Kitanzania.
SEHEMU C (Alama 15)
Jibu swali la kumi (10).
10. Sokomoko ni kijana asiye na maadili katika jamii, wewe kama kijana mwenzake mfundishe juu ya faida ya maadili katika jamii, toa hoja sita (6).
FORM II HISTORIA EXAM SERIES 257
FORM II HISTORIA EXAM SERIES 257
OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA NUSU MUHULA KIDATO CHA PILI-AGOSTI
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI
MAELEKEZO
| NAMBA YA SWALI | ALAMA | SAINI YA MPIMAJI |
| 1. | ||
| 2. | ||
| 3. | ||
| 4. | ||
| 5. | ||
| 6. | ||
| 7. | ||
| 8. | ||
| 9. | ||
| 10. | ||
| JUMLA | ||
| SAHIHI YA MHAKIKI |
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
Katika vipengele (i) hadi (x), chagua herufi ya jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo katika kisanduku ulichopewa.
i) Jamii za asili za Tanzania zimegawanyika katika makundi makubwa manne. Kati ya makundi hayo, kundi moja linajihusisha zaidi na ufugaji kama sehemu ya utamaduni na maadili yao. Lipi kati ya makundi hayo linathibitisha ukweli huu wa kihistoria?
ii) Wakati wa utawala wa Wajerumani nchini Tanganyika, watawala hao walitumia mbinu mbalimbali za kuimarisha ukoloni. Ni ipi kati ya kauli zifuatazo inaelezea moja ya tabia ya utawala huo?
iii) Baada ya vita kuu ya kwanza ya Dunia, Ujerumani ilitimuliwa kuitawala Tanganyika. Ipi Athari ya mfumo wa kisiasa uliosababishwa na utawala wa Waingereza nchini Tanganyika?
iv) Katika ujenzi wa maadili miongoni mwa jamii za asili za Tanzania, mifumo mbali mbali ilitumika katika kuhakikisha kila Kundi linafikiwa. Ni mfumo gani ulitumika katika utoaji wa elimu kwa jamii za asili za Tanzania kabla ya ujio wa wakoloni?
v) Katika kipindi cha somo la Historia ya Tanzania na Maadili, mwalimu aliwaonyesha wanafunzi picha za majengo ya kale na sanaa za jadi. Vitu hivyo hutambulika kama?
vi) Misingi mikuu ya maadili ya jamii za Kitanzania wakati ukoloni unaingia umejipambanua katika nyanja mbalimbali ikijumuisha vipengele vifuatavyo isipokuwa kipengele kimojawapo:-
vii) Wakati wa utawala wa wakoloni kutoka Ulaya hasa Waingereza, walitoa elimu kwa baadhi ya wenyeji hapa Tanganyika. Hii ilikuwa na maana gani?
viii) Kama mwanafunzi wa kidato cha pili unafikiri ni upi Uhusiano kati ya Historia ya Tanzania na Maadili katika kujenga utambulisho wa taifa?
ix) Jamii za asili za Tanzania, zimehusiana na jamii nyingine kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni jambo ambalo limepelekea matokeo hasi na chanya. Kama mwanafunzi wa kidato cha pili, unafikiri ni ipi jamii ya kwanza kutoka Ulaya kufika eneo la Pwani ya Tanzania karne ya 15?
x) “Ni matokeo ya matumizi ya sayansi katika kubuni zana au vifaa mbali mbali ili kurahisisha utendaji” sentensi hii inatoa maelezo juu ya kitu gani kati ya mambo yafuatayo?
Majibu
| i | ii | iii | iv | v | vi | vii | viii | ix | x |
| . |
2. Oanisha maelezo ya ORODHA A na maneno katika ORODHA B, kisha andika herufi ya jibu sahihi katika jedwali lililopo chini.
| ORODHA A | ORODHA B |
| i. Kugawanywa kwa bara la Afrika miongoni mwa mataifa ya Ulaya. ii. Utawala wa wajerumani katika jamii za kitanzania. iii. Utawala wa kiuwakala katika jamii za kitanzania. iv. Mkataba wa Heligoland. v. Wamisionari wa kwanza wa madhehebu ya kikristo katika jamii ya kitanzania | A. 1885-1919 B. Ludwig Krapf na Johan Rebman C. 1884-1885 D. Wajerumani. E. Waingereza F. 1890 G. Carl Peters na Johan Rebman |
Majibu
| Orodha A | i | ii | iii | iv | v |
| Orodha B |
SEHEMU B (Alama 70)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
3. Wakoloni walipofika nchini Tanzania, walikuta watanzania wanamaadili yao. Kama mwanafunzi wa kidato cha pili, taja na elezea ni maadili yapi yaliyodumishwa wakati na baada ya ujio wa wakoloni? (hoja tano)
4. Tumia hoja tano, elezea Athari za kiuchumi zilizotokana na uhusiano wa jamii za asili za Tanzania na jamii za Mashariki ya kati kabla ya ujio wa wakoloni kutoka Ulaya magharibi.
5. Katika mabadiliko muhimu miongoni mwa jamii za asili za Tanzania ni ugunduzi wa chuma. Tumia hoja tano, Elezea athari zilizotokea kutokana na ugunduzi huo, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.
6. Kwa kutumia hoja tano, elezea ni kwa namna gani Mifumo ya kisiasa na kiuchumi kabla ya ukoloni ilichangia kwa kiasi kikubwa kujenga maadili ya jamii za kitanzania kabla ya ukoloni.
7. Kwa kutumia mifano, taja na eleza mbinu tano zilizotumiwa na Wajerumani katika kuanzisha utawala wa kikoloni eneo la Tanzania mwishoni mwa karne ya 19.
8. Tanzania ni nchi yenye utajiri mkubwa wa urithi wa asili kama vile Bahari, Misitu, Mbuga za Wanyama na Mlima Kilimanjaro. Kwa kutumia hoja tano, taja na eleza fursa zitokanazo na uwepo wa urithi huo.
9. Kama mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye uelewa juu ya utawala wa wakoloni chini Tanzania, elezea sababu tano zilizopelekea jamii za asili za Tanzania kupinga ujio wa wakoloni.
SEHEMU C (Alama 15)
Jibu swali la kumi.
10. “Rushwa ni adui mkubwa wa haki. Tusipoidhibiti itaangamiza taifa” Mwalimu J.K. Nyerere (1965). Kama mwanafunzi wa kidato cha pili, tumia hoja tano elezea mbinu za kupambana na rushwa.
FORM II HISTORIA EXAM SERIES 256
FORM II HISTORIA EXAM SERIES 256
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI MUHULA WA KWANZA KIDATO CHA PILI
060 HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI
Muda: Masaa 2:30 Mei 2026
MAELEKEZO
SEHEMU A (ALAMA 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
1. Chagua jibu sahihi katika vipengele (i) – (x) kisha andika herufi ya jibu sahihi kwenye jedwali ulilopewa hapo chini.
i. Mzee Mpenda Ukweli alitaka kujua ni kwanini wanafunzi katika shule za Tanzania wanasoma somo la Historia ya Tanzania. Alipowauliza kidato cha pili walimpa jibu lifuatalo:
ii. Mwanafunzi Juhudi alisoma kuhusu vyama vya ushirika vya wakulima vilivyo anzishwa kabla ya uhuru. Je vyama hivyo vilikua na lengo gani?
iii. Katika makundi ya jamii za asili zaTanzania, ni kundi moja tu ambao ndio wazawa wa Tanzania waliokutwa na jamii nyingine. Kundi hilo ni:
iv. Msichana aitwaye Elizabeth aliambiwa na mwalimu ataje vitendo vyenye maadili ambavyo hutendwa na wanafunzi wenzake awapo shuleni. Majibu aliyotoa ni haya yafuatayo isipokuwa:
v. Kwa mujibu wa wanafalsafa mbalimbali, neno 'Jamii' lina maana gani?
vi. Mkutano wa kimataifa uliofanyika nchini Ujeruman katika mji wa Berlin mwaka 1884-1885 ukiongozwa na Otto Von Bismark ulifanyika kwa lengo gani?
vii. Ni aina gani ya elimu ilikuwa ikitolewa katika jamii za Kitanzania kabla ya ujio wa kikoloni?
viii. Wakati Wajerumani na Waingereza wanaitawala Afrika mashariki walitoa huduma ya elimu kwa waafrika. Hii ilikua na maana gani?
ix. Ashura anawadharau wenzake kwasababu wanatoka familia masikini. Kitendo cha Ashura kuwa na tabia hii kinakiuka maadili yapi kati ya haya yafuatayo?
x.…..ni hali ya mtu au nchi kuamua na kufanya mambo yake bila kuingiliwa na mtu au taifa lolote.
Majibu
| i | ii | iii | iv | v | vi | vii | viii | ix | x |
| . |
2. Oanisha maelezo yaliyopo katika Orodha Ana dhana zilizopo katika Orodha Bkwa kuandika herufi ya jibu sahihi.
| Orodha A | Orodha B |
|
|
Majibu
| Orodha A | i | ii | iii | iv | v |
| Orodha B |
SEHEMU B (ALAMA 70)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
3. a) Eleza maana ya dhana “Mfumo wa ukoo”
b) Taja na eleza kwa kifupi sifa kuu nne (04) zilizozingatiwa ili mtu ateuliwe kuwa kiongozi wa ukoo.
4. Ujenzi wa maadili katika jamii sio tukio la siku moja bali kuna mifumo mbalimbali ya kijamii inayosaidia. Fafanua mifumo ya kijamii inayohusika kujenga maadili kabla ya ujio wa wakoloni katika jamii za kitanzania
5. Tunapaswa kufahamu kuwa ujio wa wakoloni uliathiri nyanja nyingi katika jamii za kitanzania hivyo jamii nyingi za kiafrika zilipinga ili kuhifadhi na kulinda maadili, uchumi, utawala na tamaduni zao. Eleza sababu zilizosababisha mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
6. Jamii za asili ya kitanzania zilihama kutoka sehemu na kwenda maeneo mengine kutokana na sababu mbalimbali. Mueleweshe mwanafunzi wa kidato cha kwanza sababu hizo. Hoja tano
7. Ukiwa kama mwanafunzi wa kidato cha pili na mbobezi wa somo la Historia ya Tanzania na Maadili. Elezea utofauti wa mfumo wa elimu ya jadi na mfumo wa elimu ya sasa. Hoja tano
8. Katika mapambano dhidi ya uvamizi wa wakoloni, jamii za Kitanzania zililenga kulinda maadili yao. Bainisha maadili ya jamii za kitanzania yaliyodumu licha ya ushawishi wa utawala wa kikoloni kuyafuta. Hoja tano.
9. Taja na eleza kifupi mbinu zilizotumika kudai uhuru wa Tanganyika na Zanzibar katika kipindi cha kwanza kwanzia mwaka1900 mpaka 1944. Hoja tano (05)
SEHEMU C (ALAMA 15)
Jibu swali namba 10
10. Tanzania ina utajiri mkubwa wa urithi wa asili, ambao huwapa manufaa makubwa wanajamii na Taifa kwa ujumla. Waeleweshe watanzania umuhimu huo kwa kutumia aina mbalimbali za urithi wa asili
FORM II HISTORIA EXAM SERIES 253
FORM II HISTORIA EXAM SERIES 253
Namba Ya Upimaji___________________________
OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA NUSU MUHULA - MACHI
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI KIDATO CHA PILI
MUDA : Masaa 2:30
MAELEKEZO
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika kipengele (i) mpaka cha (x) kisha andika herufi ya jibu sahihi katika sehemu ya karatasi ya mtihani uliyopewa
i. Katika somo la Historia ya Tanzania na Maadili neno Ukoloni lina maana gani?
ii. Ukoloni ulitokana na kustawi kwa mfumo wa ubepari. Mfumo huu wa ubepariulifikia hatua gani huko Ulayamagharibi hadi kuwalazimuwakolonikuvuka mipaka ya nchi zao ili kutafutarasilimali na masoko mapya za bidhaa zao?
iii. Mapinduzi ya viwanda katika nchi za ulayamagharibiyalisababisha ongezeko la mahitaji mbalimbali kama ifuatavyo isipokuwa
iv. Mwarabu wa kwanza kutawala kwa pamoja dola za Omani na Zanzibar kuanzia mwaka 1800 hadi 1856 baada ya kufarikialijulikana kama ……
v. Ukoloni ulishamiribarani Afrika katika karne za…….
vi. Katika utawala wa Kijerumani, koloni la Tanganyika lilijulikana kwa jina la…
vii. Ni mkataba gani wa amani wa mwaka 1919 ulioamuru kwamba makoloni yote yaloyokuwa ya
Wajerumaniyakabidhiwe kwa mataifayaliyoshinda vita kuu ya kwanza ya Dunia?
viii. Shughuli za biashara wakati wa utawala wa Waingerezazilifanywa na watu wa jamii ya Kiasia hasa Waarabu na Wahindi pamoja na…….;
ix. Mabadiliko ya kisiasa wakati wa utawala wa Waingerezayalihusisha pia kuanzishwa kwa mfumo wa matumizi ya utawala wa kiuwakala. Utawala huu ulianzishwa mwaka 1926 na Gavana wa kiingerezaaliyejulikana kwa jina la.;
x. Katika utawala wa Waingerezakuliundwashirikisho la machifu, kwa kila kabila kumteuachifummoja kuwa kiongozi mwandamizi wa wengine. ChifuFundikiraaliteuliwa kuongoza machifu wa.?
MAJIBU:
| i | ii | iii | iv | v | vi | vii | viii | ix | x |
| . |
2. Oanisha SAFU A kwa kutoajibu sahihi kutoka katika SAFU B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika visanduku chini yake.
| SAFU A | SAFU B |
| i. Tanganyikailiwekwa rasmikwenye utawala wa waingereza ii. walitumiamfumo wa kiuwakala katika utawala wao iii. Maarufu kwa biasharaya watumwa iv. Ujerumani ilichukua rasmi mamlaka ya kiutawala Africa ya Mashariki v. Mwinyi mkuu |
|
MAJIBU:
| i | ii | iii | iv | v |
| . |
SEHEMU B (Alama 70)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
3. Ukuaji wa mfumo wa ubepari hadi kufikia ubeberu katika robo ya mwisho ya karne ya 19 uliambatana na mapinduzi ya viwanda katika nchi za ulayamagharibi. Kwa hoja tano eleza mahitaji yaliyosababishwa na mapinduzi ya viwanda huko ulaya
4. Wakoloniwalitumia mbinu mbalimbali kuanzisha na kuimarisha tawala zao barani Afrika. Kwa hoja tano eleza mbinu zilizotumika kuanzisha na kuimarisha utawala wa kikoloni katika jamii za Kitanzania.
5. SultaniSeyyidSaid bin Sultan alihamisha makazi yake kutoka Omani kuja Zanzibar mwaka 1840. Kwahoja tano eleza sababu za kiongozi huyo wa utawala wa Waarabukuhamisha makazi yake kuja Zanzibar.
6. Mifumo ya kisiasa na kiuchumi ilikuwa na mchango mkubwa sana katika kukuza maadili ya jamii za asili ya Tanzania, unadhani ni ipi michango ya mifumo hiyo ya kisiasa na kiuchumi katika jamii za asili ya Tanzania.
7. Wakoloniwalijenga njia za uchukuzi na mawasiliano kama vile barabara, reli na bandari. Kwa hoja tano (5) eleza umuhimu wa miundombinu hiyo katika shughuli za serikali za kikoloni
8. Wanafunzi wa shule ya sekondari Kwadoe walitakiwa kufanya utafiti kwa njia ya mtandao ili kubaini tunu mbalimbali za taifa, unadhani ni tunu zipi hizo walizobaini na kuziandika katika ripoti yao.
9. Mabadiliko ya kijamii katika utawala wa Wajerumani na Waingerezayalijikita Zaidi katika utoaji wa huduma za msingi kama elimu, afya, maji, umeme na miundombinu, lengo ni kurahisisha utekelezaji wa malengo ya kikoloni. Kwa hoja tano (5) eleza sifa za elimu ya kikoloni wakati wa utawala wa Wajerumani
SEHEMU C (Alama 15)
Jibu swali namba 10
10. Mchango wa ukoloni katika uhusiano wa Tanzania na mataifayaliyoitawala ni mkubwa sana kwani ulileta mabadiliko mengi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii katika jamii za kitanzania. kwa hoja sita eleza athari hasizilizotokana na utawala wa kikoloni katika jamii za kitanzania
FORM II HISTORIA EXAM SERIES 229
FORM II HISTORIA EXAM SERIES 229
OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA NUSU MUHULA - MACHI 2026
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI KIDATO CHA PILI
MUDA : Masaa 2:30 Machi 2026
MAELEKEZO
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Kwa kila moja ya vipengee (i)–(x), chagua jibu sahihi kutoka katika mapendekezo yaliyotolewa na andika herufi yake kwenye kisanduku kilichotolewa.
(i) Historia ya Tanzania ni mfululizo wa matukio ya
(ii) Maadili ya Kitanzania yanatokana na
(iii) Makundi makuu manne ya jamii za Kitanzania ni
(iv) Moja ya athari za ukoloni katika maadili ya Kitanzania ni
(v) Ukoloni ulianza kwa nguvu kubwa nchini Tanganyika mwaka
(vi) Sababu kuu ya ukoloni ilikuwa
(vii) Moja ya maadili yaliyoharibiwa na ukoloni ni
(viii) Jamii za Kitanzania zilipinga ukoloni kwa sababu
(ix) Maadili ya Kitanzania yanachangia
(x) Ukoloni ulileta mfumo mpya wa maadili unaoitwa
2. Oanisha vipengee kutoka ORODHA A na maelezo yanayolingana kutoka ORODHA B. ORODHA A ina vipengee vitano (i-v) vinavyohusu sababu kuu za ukoloni wa Kitanzania, na ORODHA B ina vipengee saba (A-G) vinavyotoa maelezo au mifano yanayohusiana.
| ORODHA A | ORODHA B |
| (i) Kustawi kwa Ubepari na Ubeberu Ulaya Magharibi (Karne ya 19) (ii) Mahitaji ya Malighafi kwa Viwanda vya Ulaya (iii) Hitaji la Masoko Mapya na Maeneo ya Uwekezaji Mitaji (iv) Ushindani wa Kisiasa na Kijeshi kati ya Mataifa ya Ulaya (v) Kueneza Dini ya Kikristo |
|
SEHEMU B (Alama 40)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
3. Eleza kwa ufupi maana ya maneno yafuatayo:
4. Toa mifano minne ya makundi ya jamii za Kitanzania na asili zao.
5. Eleza sababu nne kuu za kuanza kwa ukoloni nchini Tanganyika.
6. Eleza athari tano za ukoloni katika maadili ya jamii za Kitanzania.
7. Thibitisha kwa hoja tano kwamba ukoloni ulidhoofisha maadili ya umoja na ushirikiano wa jadi.
8. Eleza umuhimu wa maadili ya Kitanzania katika kujenga taifa lenye mshikamano (hoja tano).
SEHEMU C (Alama 45)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
9. Eleza jinsi ukoloni ulivyoharibu maadili ya umiliki wa pamoja na kuleta umiliki wa kibinafsi (hoja tano).
10. Jadili kwa nini ni muhimu kurudisha na kuimarisha maadili ya jadi ya Kitanzania katika enzi ya kisasa (hoja tano).
11. Toa hoja tano za jinsi historia ya Tanzania na maadili inavyoweza kusaidia katika kuzuia migogoro ya kikabila na kidini leo.
FORM II HISTORIA EXAM SERIES 226
FORM II HISTORIA EXAM SERIES 226