ELIMU YA DINI YA KIISLAMU FORM TWO REGIONAL EXAMS (MOCK, PRE-NATIONAL, etc.)

OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

OFISI YA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO

MTIHANI WA UTIMILIFU KIDATO CHA PILI

Msimbo: 021 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU

Muda: Saa 2:30 Ijumaa 22 Mei, 2026 Mchana

MAELEKEZO

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10).
  2. Jibu maswali yote.
  3. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
  4. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa.
  5. Vifaa vyote vya mawasiliano visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  6. Andika Namba yako ya Upimaji katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia.

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. Katika kipengele (i)–(x) chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake katika kisanduku cha swali husika. (Alama 10)

(i) Na Allah akamfundisha Adam majina ya kila kitu (2:31). Kwa mujibu wa aya hii kinathibitishwa kitu gani?

  1. Jambo la kwanza alilopewa mwanadamu na Mola wake ni roho
  2. Jambo la kwanza alilopewa mwanadamu na Mola wake ni uhai
  3. Jambo la kwanza alilopewa mwanadamu na Mola wake ni elimu
  4. Jambo la kwanza alilopewa mwanadamu na Mola wake ni akili

(ii) Mwanasayansi Mbovu anadai kuwa kutokana na elimu uliyonayo hawezi kufuata dini yoyote. Bainisha hoja inayopinga dai lake hili.

  1. Mwanasayansi hana mahusiano mazuri na Mola wake
  2. Dai lake halina ushahidi wa kisayansi
  3. Mwanasayansi huyo hana elimu ya dini ya kutosha
  4. Umbile la mwanasayansi huyu ni la kidini

(iii) Mja anapotaka kuingia katika Uislamu anatakiwa kuchukua ahadi ya utiifu. Bainisha ahadi hiyo kati ya hizi zifuatazo:

  1. Kuishi kwa kufuata barabara Sunnah
  2. Kuishi kwa mujibu wa kitabu na Sunnah
  3. Kuishi kwa kutekeleza swala tano na funga
  4. Kuishi kwa kufuata barabara Qur’an

(iv) Bwana Mwende amefanya tendo la ndoa mchana wa Ramadhani akiwa amefunga. Uislamu unamtaka afanye nini ili ibada yake ya funga iwe sahihi?

  1. Alishe masikini sitini na kufunga siku sitini nje ya Ramadhani
  2. Afunge kwa kulipa siku hiyo bila ya kutoa kafara
  3. Atekeleze kafara kwa kufunga siku sitini mfululizo, ikiwa hawezi alishe masikini sitini
  4. Atekeleze utaratibu wa kafara bila ya kulipa funga hiyo

(v) Wanafunzi wa shule ya sekondari Mungu Mmoja wanasoma Qur’an kila baada ya swala ya alfajiri. Ni jambo gani wanapaswa kuzingatia katika usomaji wao?

  1. Kuanza kwa kutaja jina la Allah Muumba
  2. Kuanza kwa kujilinda kutokana na shetani
  3. Kuanza kwa kumlaani na kumuweka mbali shetani
  4. Kuanza kusoma Alhamdu kisha sura nyingine

(vi) Hadithi isemayo kuwa tabia za Mtume Muhammad (Sallallahu Alayhi Wasallam) ni Qur’an inamaanisha nini?

  1. Mtume Muhammad (Sallallahu Alayhi Wasallam) aliishi kwa mafundisho ya Qur’an
  2. Mtume Muhammad (Sallallahu Alayhi Wasallam) aliishi kwa kusoma sana Qur’an
  3. Mtume Muhammad (Sallallahu Alayhi Wasallam) aliishi kwa kuifundisha Qur’an
  4. Mtume Muhammad (Sallallahu Alayhi Wasallam) aliishi kwa kulingania Qur’an

(vii) Ikiwa nuni yenye sakna “نْ” imekutana na herufi “Laam (ل)” hukumu gani ya usomaji wa Qur’an inatokea?

  1. Kuchanganya
  2. Kudhihirisha
  3. Kuficha
  4. Kugeuza

(viii) Katika utaratibu wa Mwalimu wako wa Dini wa kutoa nasaha kwa wanafunzi, alikunasihi kutoa sadaka kwa siri. Kwanini alihimiza jambo hilo?

  1. Ili ujiepushe na hasadi
  2. Ili ujiepushe na husda
  3. Ili ujiepushe na kijicho
  4. Ili ujiepushe na ria

(ix) “Abdullah bin Umar amesema kuwa Mtume wa Allah amesema, ‘Yule ashikaye silaha dhidi yetu si pamoja na sisi.’ (Muslim).” Ni ipi sehemu ya Isnad katika Hadithi hii?

  1. “Ashikaye silaha dhidi yetu si pamoja na sisi”
  2. “Mtume wa Allah amesema”
  3. “Abdullah bin Umar ameeleza kuwa”
  4. “Muslim”

(x) Mwakanyoka anapata mkanganyiko na hatimaye anashindwa kutofautisha baina ya kuswali na kusimamisha swala. Ni ipi maana sahihi ya kusimamisha swala?

  1. Kuswali kwa kufuata nguzo za swala
  2. Kuswali kwa kusujudu, kurukuu na kuitidali
  3. Kuswali kwa kuzingatia nguzo za swala
  4. Kuswali kwa kuzingatia masharti na nguzo za swala kikamilifu

2. Oanisha mali zinazoingizwa kutokana na zakat zilizokidhi vigezo vyote zilizo katika Orodha A na viwango stahiki kutolewa vilivyo katika Orodha B. (Alama 5)

Orodha A Orodha B
  1. Dhahabu iliyookotwa 3g
  2. Zabibu kilo 900
  3. Fedha taslimu Tsh 100,000
  4. Mali ya biashara yenye thamani ya Tsh 200,000
  5. Mbuzi na kondoo 50
  1. Tsh. 2500
  2. 0.075g
  3. Tsh 5000
  4. Mbuzi 1
  5. 0.6g
  6. Mbuzi 1 na kondoo 1
  7. 90kg
  8. Kilo 22.5

SEHEMU B (Alama 70)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. Ili Hadithi ya Mtume Muhammad (Sallallahu Alayhi Wasallam) izingatiwe kuwa ni sahihi ni lazima Isnad yake ikidhi vigezo. Bainisha vigezo hivyo vilikuthibitisha ukweli huu.

4. Jirani yako Muislamu amefariki na ukapewa jukumu la kumuosha. Eleza kwa ufupi masharti matano utakayoyazingatia ili ibada hiyo ikamilike kwa usahihi.

5. Katika Uislamu jambo lolote linalowezesha Uislamu kwenda mbele hapana budi kuliwekea mikakati madhubuti ili lifanikiwe. Thibitisha kauli hii kwa kutaja na kufafanua mipango ya safari ya Mtume Muhammad (Sallallahu Alayhi Wasallam) na Abubakar walipokuwa wakihamia Madinah. (Hoja nne)

6. Tofautisha mtazamo wa Uislamu juu ya historia na ule wa makafiri kwa kuzingatia yafuatayo:

  1. Asili ya mwanadamu
  2. Lengo la kuumbwa mwanadamu
  3. Hadhi ya mwanadamu hapa ulimwenguni
  4. Hatima ya mwanadamu

7. Katika rakaa ya pili ya swala ya Magharibi Imam alisoma Suratul-Ikhlas. Waelimishe waumini wa Msikiti huo ujumbe unaopatikana katika sura hiyo kwa kuwapa mafunzo manne.

8. Sheria za Uislamu zinapatikana juu ya misingi madhubuti mitatu. Fafanua misingi hiyo na namna inavyoshughulikia sheria hizo.

9. Kwa kipindi kirefu makafiri wamekuwa wakikanusha uwepo wa Mwenyezi Mungu (S.W) kwa hoja ambazo hata hivyo hazina mashiko yoyote. Wathibitishie kuwa Mwenyezi Mungu muumba yupo pasina shaka yoyote kwa kutaja ishara tano (5) zinazodhihirisha uwepo wa Allah (S.W).

10. Licha ya Msorwa kuwa na umri mkubwa amekataa kuoa kwa madai ya kwamba hana imani na wanawake, kuoa ni kuongeza bajeti zisizo na lazima, na sababu nyingine kama hizo. Kwa kuwa wewe ni mtaalamu wa Elimu ya Dini ya Kiislamu, wasaidie wazazi, ndugu na jamaa wa kijana Msorwa katika aoe. Tumia hoja tano (05).

FORM TWO EDK EXAM SERIES 183  

FORM TWO EDK EXAM SERIES 183  

Namba ya upimaji ya Mwanafunzi. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Bismillaahir rahmaanir rahiim 

OFISI YA RAIS OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUFIJI

image

 MTIHANI WA UMAHIRI KIDATO CHA PILI

015 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU

 MUDA: SAA 2:30 MWAKA: 2025

 Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10).
  2. Jibu maswali yote kwenye nafasi ullizopewa
  3. Sehemu A na C zina alama kumi na tano (15) kila moja na sehemu B ina alam,a sabini (70)
  4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali
  5. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi
  6. Vifaa vyote vya mawasiliano visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha upimaji
  7. Andinka Namba yako ya upimaji katika kila ukurasa sehemu ya juu upande wa kulia.

KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU

NAMBA YA MASWALI


ALAMA

SAHIHI YA MSAHIHISHAJI
1.

2.

3.

4.

5.

6.

7.

8.

9.

10.

TOTAL

SAHIHI YA MHAKIKI

SEHEMU ‘A’ (Alama 15 %)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. Katika kipengele (i) – (x) Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake katika sehemu iliyowazi.

(i) Je utawezaje kumtambua muislamu aliyeelimika?

  1. Kwa kuwa na fani nyingi za kielimu
  2. Kwa kuwa elimu nyingi za fiq-hi
  3. Kwa kuwa na ufanisi katika utendaji
  4. Kwa kuwa na ujuzi mwingi wa kihistoria.

(ii) Wana wa chuoni wanatuambia Tawhid maana yake ni kumpwekesha Allh (sw). ni Tawhid ipi inaohusika na kumpwekesha Allah katika uungu wake?

  1. Tawhidul-asmaa was sifaat.
  2. Tawhidur-rubuiah 
  3. Tawhidul-uluhiyah
  4. Tawhidul-ibada.

(iii) Muandaaji wa Sanda anapaswa kuzingatia mambo gani katika uandaaji wa Sanda ya Mwanamke?

  1. Mapande matatu
  2. Uzito na aina ya kitambaa
  3. Kuwa na mapande matano
  4. Cheo cha aliyefariki

(iv) Pamoja na kutoonekana Allah wala kudirikika katika milango mikuu ya fahamu ila huwasiliana na waja wake kupitia njia zifuatazo:

  1. Ilham, maandishi, ndoto za kweli, na qur-an 
  2. Ilham, maandishi, ndoto za kweli na hadithi.
  3. Ilham, maandishi, ndoto za kweli na sunnah
  4. Ilham, maandishi, ndoto za kweli na malaika.

(v) Fafanua sunnah katika elimu ya hadithi lina maana gani? 

  1. Thawabu za ziada.
  2. Mwenendo au millah ya Mtume (saw)
  3. Swala isiyo ya faradhi.
  4. Jambo la khiyari kulifanya.

(vi) Jozi ipi klati yua zifuatazo inawakilisha nguzo za funga?

  1. Kusaidia wagonjwa na yatima
  2. Kutia nia na kujizuia na vifunguzi
  3. Kutokula na kunywa
  4. Kutotenda maovu na machafu

(vii) Kwa mujibu wa uislamu kuna aina kuu mbili za Dini “dini ya Allah na Dini za watu, fafanua aina tatu za Dini za watu.

  1. Utawa, ushirikina na ukristo.
  2. Ukristo, utawa na uyahuni.
  3. Uislamu, uyahudi na ukafiri.
  4. Utawa, ushirikina na ukafiri.

(viii) Changanua mkanganyiko ufuatao;

  1. Qur-an ina juzuu 30, sura 114 na ina aya 6326.
  2. Qur-an ina juzuu 30, sura 114 na ina aya 6236.
  3. Qur-an ina juzuu 30, sura 114 na ina aya 6336.
  4. Qur-an ina juzuu 30, sura 114 na ina aya 6366.

(ix) Allah (sw) alishawahi kuangamiza baadhi ya familia za mitume wake, ni mtume gani aliyeangamiziwa mke na mtoto wake.

  1. Nabii Mussa (as)
  2. Nabii Luti (as)
  3. Nabii Nuhu (as)
  4. Nabii Shuaibu (as)

(x) Mambo ya lazima kufanyiwa maiti wa kiislam bainisha ni katika faradhi gani?

  1. Faradhi a`ini.
  2. Faradhi mustahabu.
  3. Faradhi mutlaq.
  4. Faradhi kifaya.

2. Oanisha maneno kutoka orodha “B” na sentensi kutoka orodha “A” kisha jaza herufi yake kwenye jedwali hapo chini.

A

B

(i) Huswaliwa qabla na baada ya swala za faradhi.

(ii) Huswaliwa kwaajili ya kuomba mvua.

(iii) Huswaliwa muda wowote mara tu uingiapo msikitini.

(iv) Huswaliwa pindi lipatwapo jua au mwezi.

(v) Huswaliwa rakaa mbilimbili hadi nane usiku wa manane.

  1. At-tahajud
  2. Swalatul-khusufu au Al- kusufu
  3. At-tawba
  4. Tahiyatul-masjidi
  5. Al-istisqaai
  6. Istikhara
  7. Qabliyyah au Baadiyyah.

i

I

iii

iv

V





.

SEHEMU “B” (ALAMA 70)

Jibu maswali yote kwa ufupi katika sehemu hii

3. Fafanua njia kuu tano zinazomuwezesha mwanadamu kumtambua Mola wake

4. Makafiri hawaamini kama kuna maisha baada ya kufa. Fafanua hatua tano(5) anazopitia mwanaadamu kuyaendea maisha hayo.

5. a) Waislamu wengi na hata wasiokuwa waislamu(makafiri) hawaelewi maana halisi ya neno dini, wewe ukiwa kama mjuzi katika masuala haya, toa maana yake halisi kwa mitazamo yote miwili.

5 b) Ainisha sababu tatu za kwanini mwanadamu hawezi kusibi bila ya Dini.

6. (a) Waislamu wangi wanadhani kuwa Ibada ni kuswali, kufunga, kutoa zaka na kuhiji, wakati si sahihi. Wewe ukiwa mwana wa zuoni ifafanulie jamii maana yake halisi kilugha na kisheria;

(i) Kilugha

(ii) Kisheria

(b) Kuna mlevi mmoja maeneo ya Tandale alikuwa akiropoka kuwa hakuna lengo lolote la kuumbwa mwanaadamu ulimwenguni na vilivyomo. Wewe kama muislamu unayejitambua hebu fafanua lengo la kuumbwa kila kimoja

7. (a) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayo katiba ya kuendeshea nchi, na uislamu una sheria zake. Ni ipi misingi inayotumika kuendeshea sheria mbalimbali za kiislamu

(b) Kuna mkanganyiko mkubwa kati ya Sharia na Fiq-hi, toa maelezo yatakayoondoa mkanganyiko huo.

  1. Sharia
  2. Fiq-hi

8. Mtume (saw) na maswahaba wake walitumia njia madhubuti na makini katika kuilinda na kuihifadhi Qur-an, na ndio maana makafiri wanajaribu kuikejeli na kuichafua lakini wanashindwa, toa njia tano (5) zilizotumika kuilinda na kuihifadhi Qur-an.

9. Kuna waislamu wanadai kuwa sunnah hazina umuhimu na nafasi yoyote katika uislamu, kwa kutumia nukta tano (5), fafanua umuhimu na nafasi yake katika uislamu.

SEHEMU “C” (ALAMA 15)

Jibu swali lifuatalo katika mfumo wa insha.

10. Wanafunzi wa kidato cha kwanza hawana elimu juu ya mambo ambayo wakiyafanya swaumu zao zitakuwa zimeharibika. Wewe kama mjuzi wa somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu waelimishe wanafunzi hao juu ya mambo yanayobatilisha funga (Hoja tano)

FORM TWO EDK EXAM SERIES 128  

FORM TWO EDK EXAM SERIES 128  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256