Sura ya 02 : Maendeleo ya fasihi simulizi
Utangulizi
Katika sura hii utajifunza kuhusu dhana, tanzu, utungaji, usimulizi, uwasilishaji, uenezaji na uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi. Aidha, utapata ujuzi wa kutunga, kusimulia na kuhifadhi kazi za fasihi simulizi.
Dhana ya fasihi simulizi
Fasihi simulizi ni fasihi inayotungwa kichwani kabla ya uwasilishaji, au papo kwa papo, na kuwasilishwa kwa njia ya mdomo, vitendo na/au ishara. Fasihi simulizi ina tanzu nne. Kila utanzu una vipera anuwai. Katika madarasa ya chini, ulijifunza kuhusu tanzu hizo za fasihi simulizi. Sura hii inafafanua kwa ufi1Pi sifa, utunzi, dhima na maendeleo ya tanzu hizo.
Sifa za fasihi simulizi
Fasihi simulizi ina sifa mahususi zifuatazo:
(i) Huwasilishwa kwa mdomo, vitendo na ishara;
(ii) Ufanisi wake kisanaa hutegemea uwezo wa fanani au wahusika;
(iii) Masimulizi yake huweza kuathiriwa na mazingira, hisia na hali;
(iv) Kwa kiasi kikubwa, huwa ni mali yajamii;
Huweza kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi au katika mazingira mbalimbali kutegemea ufundi na kumbukumbu ya fanani.
Tanzu za fasihi simulizi
Fasihi simulizi imegawanyika katika tanzu mbalimbali kufuatana na wataalamu walivyoainisha. Baadhi ya hizo ni hadithi, ushairi, semi na sanaa za maonesho. Kila utanzu umegawanyika katika vipera mbalimbali kama inavyoonekana katika kielelezo kifuatacho:
Kielelezo Namba 2.1 Tanzu na vipera vya fasihi simulizi |
Kwa ujumla, fasihi simulizi kugawanyika katika tanzu kadhaa kulingana na uchanganuzi wa wataalamu mbalimbali, na tanzu hizo zimegawanyika katika vipera. Pia kuna mwingiliano mkubwa wa tanzu na vipera hivyo. Ni nadra kukuta kazi moja ya fasihi inayobebwa na utanzu au kipera kimoja. Tanzu zinaainishwa kwa kupewa jina fulani kutokana na siafa zake za kifani na maudhui. Sasa tuangalie maendeleo ya tanzu na vipera hivyo.
1. Hadithi
Ni utungo unaotumia lugha ya mjazo (nathari). Hadithi hueleza kisa fulani kwa mpangilio wa matukio unaotumia wahusika ambao ndio watendaji wa matukio hayo. Hadithi huwa na kisa kinachofululiza tangu mwanzo hadi mwisho ili kukamilisha muundo wake.
Hadithi huwasilishwa na msimuliaji mbele ya hadhira katika mandhari maalumu kama vile chini ya mti mkubwa, sebuleni, darasani au uwanjani. Aghalabu, masimulizi hufanyika katika mudd maalumu, hususani baada ya kazi. Kama inavyoonekana hapo juu katika kielelezo namba 2. I, utanzu wa hadithi una vipera sita ambavyo ni ngano, tarihis visasili, vigano, soga na visasuli.
(a) Ngano
Ngano ni hadithi za kimapokeo zitumiazo wahusika kama wanyama, miti na watu. Ni kipera cha mwanzo kabisa katika utanzu wa hadithi. Kwa kawaida, mtunzi wa ngano hajulikani; ngano hupokezanwa na kuendelezwa kutoka kizazi hadi kizazi. . Maudhui yake hujikita katika maadili, mahusiano na m wenendo ndani yajamii. Aghal abu, ngano ni hadithi za maadili na burudani ambazo husimuliwa katika mazingira ya starehe na mapumziko. Ngano ina Vipera vidogo kadha; baadhi yake ni hurafa, hekaya na istiara.
Hurafa ni ngano zenye wahusika wanyama tu. Wanyama hao huwakilisha tabia na matendo ya binadamu kwa kurejelea masuala yanayopatikana katika jamii.
Mafunzo katika hurafa huweza kuhusu tabia nzuri au mbaya za binadamu, kama Vile woga, ulafi na tamaa. Katika hurafa, wanyama wanaotumiwa ni kama Vile sungura, fisi na kobe. Sungura huwakilisha ujanja, kutokata tamaa na kutochoka. Fisi huwakilisha tamaa, ulafi, woga, uzembe na ujinga. Kobe huwakilisha ukimya, busara na utulivu; ni mhusika ambaye hufanya Vitu kimya kimya lakini huibuka mshindi.
Hekaya ni ngano zenye Visa visivyo vya kawaida vinavyoambatana na masaibu na pengine hata ujanja wa mhusika mkuu ambaye huweza kuwa mtu au mnyama. Hekaya hujengwa na Visa vingi tofautitofauti. Mhusika mkuu katika hekaya hupi tia misukosuko mingi hadi kukaribia kushindwa. Hata hivyo, katika hatua za mwisho kabisa, mhusika huyu huweza kuibukamshindi kwa namna isiyotarajiwa. Lengo la hekaya ni kumtia mtu moyo asikate tamaa anapopitia changamoto za aina mbalimbali. Kimsingi, kinachohimizwa ni kutumia akili kutatua matatizo ya maisha. Kwa kumtumia mhusika sungura, kwa mfano, tunahimizwa kuwa wajanja na kutokujidharau hata kama ni wadogo. Umbile dogo linaweza kuwakilisha pia uwezo wa kiuchumi kama Vile kuwa na mtaji mdogo. Mtu anaweza kutumia mtaj i mdogo akafanya biashara mpaka kufikia kiwango cha kuwa mfanyabiashara mkubwa. Ufuatao ni mfano wa hekaya:
Hapo zamani, kulitokea mfanyabiashara mmoja aliyekuwa na mali nyingi sana. Basi alioa mke na baadaye akaongeza Bi. Mdogo (mke mdogo). Wakaishi hivyo. Alitokea kumpenda zaidi Bi. Mdogo na kumnyanyasa Bi. Mkubwa (mke mkubwa).
Siku moja alikuwa na safari ya kwenda kununua bidhaa za duka lake. Basi akamwambia Bi. Mdogo ataje mahitaji yote ambayo angependa aletewe kama zawadi. Bi. Mdogo akataja Vitu vingi. Naam, kwa Vile mfanyabiashara yule alikuwa akimpenda sana, hakusita kumhakikishia kwamba atamletea. Kwa shingo upande, alimwendea vilevile Bi. Mkubwa na kumwambia ataje zawadi ya kumletea. Yule Bi. Mkubwa akamwambia mumewe asisumbuke ila amletee pete na kipande cha akili. Basi, kwa dharau yule bwana akakubali.
Basi tajiri akafunga safari akafika huko, akanunua vifaa vyake vyote alivyovihitaji kwa ajili ya duka Iake. Vilevile, akanunua vitu vyote kama vile nguo ambazo Bi. Mdogo alimtuma, pamoja na pete ya Bi. Mkubwa. Sasa akakwama wapi apate kipande cha akili. Akazunguka maduka yote, asipate. Mwishowe, akaona ni upuuzi kuendelea kutafuta kipande hicho.
Basi, katika ghadhabu yake, akawa anamtukana huyo Bi. Mkubwa, jinsi alivyo mpumbavu. Ikatokea kwamba Bi. Kizee mmoja akamsikia alivyolalamika na kuapiza. Yule Bi. Kizee akamuuliza kwa nini analalamika. Yule bwana akamsimulia kisa chote. Bi. Kizee akamwambia yule bwana kuwa asipate taabu kwani kipande hicho anacho nyumbani. Wakafuatana kuelekea nyumbani kwa huyo Bi. Kizee. Kufika karibu na kule nyumbani, Bi. Kizee akamweleza kwamba kipande hicho kiko nyumbani kwa yule bwana, ila tu akitaka kukipata sharti ni kwamba atakapokaribia nyumbani kwake ajipake mavi, halafu aone jinsi wake zake watakavyorupokea.
Basi tajiri akafanya kama alivyoagizwa. Alipokaribia nyumbani kwake, akajipaka mavi mwili mzima, akawa hovyo kabisa kisha akapiga hodi kwanza nyumbani kwa Bi. Mdogo. Bi. Mdogo kufungua mlango katika harakati za kumlaki, akaona mumewe kajaa mavi mwili wote. Bi. Mdogo akafoka sana na kumwambia asithubutu kuingia mie ndani hadi ameoga vizuri.
Basi yule bwana katika hali hiyohiyo, akaenda kwa Bi. Mkubwa. Bi. Mkubwa akamwona mumewe katika hali ile, akasikitika sana. Akamvua nguo zenye mavi, akamwosha, akamvika nguo nyingine.
Ndipo yule bwana akamwambia mke wake, 'Tete na kipande cha akili vyote nimepata. Isipokuwa kipande cha akili nimekipata hapahapa." Akachuka zawadi zote hata zile za Bi. Mdogo, akampa yule Bi. Mkubwa, na kumfukuza Bi. Mdogo.
Wakaishi raha mustarehe.
Hadithi inapatikana katika kitabu cha Riwaya ya Kiswahili (Joshua Madumulla, 2009 kurasa 94-95)
Istiara ni hadithi ambayo maana yake ya wazi inawakilisha maana iliyofichika. Kwa hiyo, maana huwasilishwa kwa njia ya mafumbo. Kwa mfano, hadithi mashuhuri ya zimwi linalovamia kijiji na kuwameza wanakij iji wote isipokuwa m wanamke mmoja mjamzito ni istiara. Katika hadithi hiyo, mamahuyo mjamzito baadaye anajifungua mtoto na kumlea akiwa mafichoni. Mtoto anapokua anamuuliza mama yake kwa nini wako peke yao kijijini, wakazi wengine walikwenda wapi. Mama yake anamweleza kuwa watu wote walimezwa na zimwi ambalo linaishi katika msitu ulio karibu na kijiji hicho. Mtoto anaamua kwenda kupambana na zimwi hilo hadi analiua, analipasua tumbo na kuwatoa watu wote liliowameza wakiwa bado hai. Watu wanafurahi na kumfanya mtoto huyo kuwa kiongozi wao. Kiistiara, hadithi hii huweza kuwakilisha ukoloni na mapambano ya kujikomboa. Zimwi linamwakilisha Mkoloni, na mtoto ni mkombozi. Ufuatao ni mfano mmojawapo wa Istiara.
Kisa cha Shemakumbi
Hapo zamani za kale katika kijiji kimoja, palitokea nyoka aina ya nondo. Nondo huyu aliitwa Nungu. Yeye mwenyewe alijiita Shemakumbi. Nyoka huyu alikuwa ana vichwa saba. Watu wengi walimuogopa; kila mtu alijitahidi kuwa mbali naye kwa sababu ya umbile na tabia yake ya kuwashambulia watu.
Siku moja, kulizuka uvumi kuwa nondo amekuwa hatari na tishio kubwa kwa wananchi. Alimshambulia kila aliyemkuta. Watu wa kijiji hiki waliogopa sana hata wakashindwa kuamua kuwa wafanye nini. Kila mtu alijitetea mwenyewe; kwanza, kwa kujaribu kumuua nondo, pia kukimbia. Ingawa watu wote walijitahidi kumkimbia nondo, walikamatwa na kuuawa isipokuwa mwanamke mmoja aliyekuwa mjamzito.
Mara baada ya kusikia maafa yaliyosababishwa na nondo, mama huyu alikimbia haraka haraka mpaka akafika nyumbani kwao. Hapo alipanda hadi ghalani na huko alijificha ndani ya mtungi mkubwa. Alijiingiza humo ili ajinusuru yeye pamoja na mwanawe mtarajiwa. Mama aliishi ndani ya mtungi ule kwa muda wa siku nyingi akiwa amezongwa na upweke, kwani watu wote walishamezwa na nondo. Naye nondo baada ya kujiridhisha kuwa hakukuwapo na mtu yeyote aliyebakia, alienda kuishi katika jangwa na nyika iliyokuwa pembezoni mwa kijiji hicho.
Akiwa katika lindi la upweke na woga, mama alijifungua mtoto wa kiume. Taratibu, hofu yake ilianza kupungua. Kadri mtoto alivyokuwa mkubwa, upweke na woga viliendelea kuihama kaya ya mama yule. Hata mtoto alipokuwa mtu mzima, mama alikuwa na matumaini kuwa angalau kwa wakati huu, yeye pamoja na mwanawe wanaweza kushirikiana kupambana na hatari yoyote itakayojitokeza. Siku moja wakiwa wamepumzika mtoto alimuuliza mama, 'Mama, mbona katika maeneo yanayotuzunguka kuna magofu mengi, inaelekea kulikuwapo na watu wakiishi kwenye maeneo haya. Tafadhali, nieleze nini kilitokea hata hali ikawa hivi?" Mama yake akamjibu bila hamaki:
"Ni kweli mwanangu, hapo zamani za kale katika kijiji hiki, palitokea kuishi watu wengi, Tena wengi sana, wake kwa waume, watoto kwa vikongwe, lakini yaliyotokea siku hizo sitakueleza leo hii. Subiri utakapokuwa mtu mzima nitakusimulia habari yote. Kwa sasa wewe bado u mtoto. Si vizuri kukuambia suala hili. Tafadhali subiri, kwani subira yavuta kheri."
Ingawa mwana ålimbembeleza mama yake amuelezee kisa hiki, mama alikataa katakata kusimulia habari ya maangamizi ya kijiji hicho kwa kuhofia kuwa bado mwanawe si mtu mzima, na kumuahidi _kuwa atakapokuwa mtu mzima atamueleza. Kila siku na kila mara mwana alijitahidi kuwa karibu na mama yake akijaribu kumshawishi amsimulie lakini mama hakufanya hivyo mpaka ulipofika waka ti muafaka wa kufanya hivyo. Siku ilipowadia mama alianza kisa chake:
'Mwanangu sasa umekuwa mtu mzima na yanipasa nikueleze habari za kijiji chako. Basi katika ukao wao hapo zamani, wakazi hao pamoja na mimi nikiwamo walifikwa na dhoruba ya nondo mla watu. Nondo huyu alikuwa ana vichwa saba, na aliazimia kummeza kilå mwanadamu katika kijiji hiki. Dhoruba hii ilipotokea, kila mtu alihaha.Wengine walijaribu kumuua lakini walishindwa. Wengine walilia lakini vilio vyao viliishia kwenye kimya kirefu; na wengine walikimbia lakini mbio zao ziliishia sakafuni. Wote waliishia kwenye midomo saba ya nondo mla watu isipokuwa mimi mama yako, kipindi hicho nilikuwa mjamzito wa uzao wako."
Mama alipofika hapa, mtoto alihema kama chatu na kutokwa na kijasho chembamba kama mtu aliyekuwa akikwea mlima mrefu. Licha ya hivyo, mtoto alibaki kinywa wazi kwa mshangao na hamaki kwa yale aliyohadithiwa. Baada ya kitambo, mtoto alipata nguvu za kuuliza. Alisema:
"Ehe, wewe ulitumia mbinu gani? Na huyo nondo alienda wapi?” Mama akaendelea kuhadithia, "Basi, kwa msaada wa Mungu, mimi nikatumai kuwa ningeweza kujiokoa pamoja na kuiokoa nafsi ya kile kilichokuwa tumboni mwangu kwa kuingia _kwenye mtungi. Nilikimbia mpaka nyumbani kwetu, nikapanda ghalani, nikajificha kwenye mtungi, Kwa muda wote huo nilikula akiba za vyakula vya wanakijiji wenzangu, Kila mara nilitoka mara moja na kisha mara baada ya kumaliza shida zangu nilirudi kwenye mtungi. Humo nilijificha mpaka Siku ulipozaliwa wewe, ukakua na hata sasa wewe u mtu mzima. Nondo alipodhani kuwa amemaliza kazi yake, alienda kuishi katika nyika na msitu ulee unaouona pembezoni mwa kijiji hiki. Sijawahi kumuona tena nondo katika kijiji hiki, lakini hata wewe nakusihi endelea _na shughuli zako kwa uangalifu na wala usijisumbue kumtafuta.”
Alipomaliza kuhadithia, kijana alitabasamu kidogo ingawa kwa namna fulani alijawa na huzuni na woga. Alimwambia mama yake:
"Kuna sababu gani ya kuendelea kuishi ikiwa watu wote katika kijiji hiki walishamezwa na nondo? Mimi nitaenda kumtafuta nondo, ama nitamuua au ataniua.”
Mama yake alimsihi mwanawe asifanye hivyo, lakini mtoto wake alikataa. Hata mwisho mama akasema, ”Haya mwanangu, kama umedhamiria kufanya mapambano na nondo, nadhani mimi nitaendelea kuishi peke yangu, Jakini angalia hali yangu kwa sasa, mimi sina nguvu. Nishakuwa mzee. Je, nitawezaje kujitafutia mahitaji yangu bila wewe? Mimi nakuhitaji sana wewe mwanangu. Kwa nini usikubali kuachana na nondo?”
Mwana akajibu, "Ikiwa nondo ataniua mimi, bila shaka atakuua hata wewe. Pia, kama mimi nitamuua nondo, wewe, wanakijiji waliomezwa siku nyingi na mimi tutakuwa salama. Hakuna haja ya wewe kumhofia nondo aliyeweza kuwameza wanakijiji wote. Mimi naondoka sasa hivi."
Basi, mtoto akaehukua silaha za namna mbalimbali kama vile shoka, panga, kisu, upinde na mishale, Alipofika pembezoni mwa ile nyika, alizikumbatia vizuri silaha zake kisha akaanza kumuita nondo kwa kuimba wimbo:
| Kisambaa | Tafsiri ya Kiswahili |
|
|
Aliendelea kuukariri wimbo huu mara kadhaa, hata yule nondo aliposikia sauti ya mwanadamu aliamka akanyanyua Shingo yake. Nondo alijiuliza, "Ni nani huyo ambaye bado yungali hai katika kijiji hiki?" Lakini hakupata jibu. Mwisho kabla hajaja kuona nani anayemuita naye alianza kuimba:
| Kisambaa | Tafsiri ya Kiswahili |
|
|
Mara baada ya kusikia sauti hii yule kijana alikariri tena ule wimbo wake kwa sauti nzuri. Kila alivyoimba naye nondo aliimba na kuzidi kusogea karibu na mahali alipo yule kijana Alipofika karibu yake, kijana aliamua kuwa hatamkata Nondo kwa kutumia panga, kisu walakumchoma mshale. Ila atanyamaza na kukumbatia silaha zake, ili atakapomezwa amezwe pamoja na silaha hizo.
Kama alivyokuwa amepanga, kijana alijikunyata kama mtu mnyonge sana. Naye nyoka alimmeza kijana akiwa na silaha zake. Mara baada ya kumezwa, yule kijana alianza kumchanachana nondo. Aliehana kila sehemu ya mwili wa nondo, nondo akatokwa na damu nyingi isiyo kifani na mwishowe akafa.
Lo! Damu iliyokuwa inatiririka kutoka mwilini mwa nondo ilipokatika palionekana miili ya watu wengi ajabu. Wengine walikuwa wamekufa na wengine walikuwa wazima. Walikuwamo wanaume na wanawake, vichwa vyao vilijawa na nywele zenye mvi. Mvi mvi mvikila mahali. Wale waliokuwa hai, walifurahi sana kutokea tena katika ulimwengu wa dunia. Waliuliza kwa sauti moja:
"Ni nani aliyetuamsha toka katika usingizi wetu mwanana?" Kwa urefu na kwa kina mama wa yule mtoto akasimulia yote yaliyotokea. Alipofika mwisho, wanakijiji wote wakaazimia kumuita mtoto yule jina la kishujaa la "Nondo MlawatuShemakumbi." Si hivyo tu, pia walimtawaza yeye awe kiongozi na mfalme wao na wakaishi raha mustarehe. (Hadithi ilikuçanywa na Ramadhan Thomas, 2011).
Kwa kawaida, ngano huwa fupi kwa sababu ya mu undo wake wa kuwa na kisa kimoja.Wahusika wa ngano ni bapa kwa maana kwamba mhusika akiwa mwema ni nawema mwanzo hadi mwisho wa hadithi, vivyo hivyo kwa mhusika mwovu. Lengo kuu la ngano, mbali na kuburudisha, nikuadibu, kuadili na kuelimisha jamii. Hujaribu kujenga utu bora kwa kueleza wema na ubaya.
(b) Tarihi
Tarihi ni hadithi zinazohusu matukio muhimu ya kihistoria, Msingi wa hadithi hizi ni matukio ya kihistoria. Matukio haya yanaweza kuwa ya kweli au ya kubuni au mchanganyiko wa ukweli na ubunifu. Aghalabu, wahusika wa hadithi hizi ni binadamu. Mifano maarufu ya tarihi ni Tarihi ya Kilwa na Tarihi ya Pate (Whiteley,1969:34) Tazama mfano ufuatao:
Habari za mji wa KisakiAwali kabisa, aliyejenga Kisaki ni Jamitambo aliyekuwa Sultani mkubwa. Kazi ya sultani huyu ilikuwa ni kulima mtama na mpunga pamoja na kuwinda ndovu, huku akiuza pembe za ndovu hao. Wakati wa utawala wake, Jamitambo alipigana na Wakamba ambao hatimaye waliondoka. Baada ya muda, Jamitambo naye alifariki na utawala ukatwaliwa na mtu aliyejulikana kama Mwinyi Mgeni. Kazi ya Mwinyi Mgeni ilikuwa kulima mpunga, mtama, mahindi na ufuta. Katika utawala wake, Mwinyi Mgeni alipigana pia na Sultani aliyejulikana kama Makobe. Baada ya kufa kwa Mwinyi Mgeni, mwanawe aliyejulikana kama Abdalah alichukua uongozi wa makao makuu ya ufalme huo; yeye vilevile, kazi yake ilikuwa kulima mahindi, mtama na ufuta, na alikuwa pia na mazoea ya kwenda porini kuwinda ndovu kwa ajili ya pembe zake (Kyallo Wamitila, 2008).
(c) Visasili
Visasili ni hadithi zinazoelezea chimbuko au asili ya jamii, ukoos au kundi fulani. Huelezea pia tamaduni mbalimbali na namna jamii fulani ilivyofika katika eneo fulani, Kadhalika, visasili huelezea na kufafanua masuala ya kimaumbile na kiimani yanayomhusu na kumsumbua binadamu kama vile maradhi na kifo. Visasili hueleza pia maana ya maisha na hatima ya mwanadamu kulingana na imani_za jamii inayohusika. Kwa kawaida, visasili huheshimiwa na kuaminiwa na wanadamu, nahuhusishwa na kuwa vielelezo vya miviga na ibada zao. Mfano wa kisasili nihadithi za mataifa mbalimbali kuhusu kuumbwa kwa ulimwengu na vilivyomo. Mfano mzuri ni hadithi ya Wakikuyu ya "Gikuyu na Mumbi" (ambayo inapatikana katika kitabu cha Naushangilia Mlima Kenya, (Kenyatta na Kibui, 1966) na simulizi ya "Adamu na Hawa"ambayo i_napatikana katika Biblia na Kurani.
(d) Vigano
Vigano ni hadithi fupifupi. Mafunzo yake hutolewa kwa kutumia lugha ya picha kama ilivyo kwa methali. Hadithi hizi Zina hadhi ya methali ingawa hutumia taswira pana kuliko methali. Kimsingi, hadithi za namna hii hutolewa kama vielelezo hasa wakati wa mazungumzo au maongezi. Lengo kuu huwa ni kumkanya na kumfunza anayesikiliza.
Kigano, kwa mfano, kinaweza kueleza kuhusu mzazi aliyempenda mno mtoto wake wa pekee. Kwa hiyo, hakuthubutu kumkemea au kumrudi yule mtoto. Hatimaye, mtoto alijenga tabia mbaya. Basi, msimulizi husema kwa methali: Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe.
Vigano, aghalabu, hutokea katika mazungumzo na, wakati mwingine, hutungwa papo hapo. Kwa mantiki hiyo, vigano vingi huwa havienei kwa sababu hufungamanishwa na muktadha wa maongezi na hutungwa kwa aj ili ya mada husika tu. Kwa hiyo, hupotea baada ya mada kuwasilishwa,
(e) SogaSoga ni hadithi fupifupi za utani na ucheshi. Hadithi hizi husimuliwa kwa mfuatano wa matukio yanayochekesha. Soga hujengwa juu ya tukio moja tu. Tukio hilo, aghalabu, hulenga kuchekesha kwa kubeza na kukejeli. Pia, hueleza mambo ya ukweli unaoumiza kwa njia ya ucheshi ili kupunguza ukali wa ukweli huo. Soga hupatikana au hufanywa na watu wajamii zenye historia ya kufanyiana utani kama Vile jamii za Wanyaturu na Wakurya, Wahaya na Waha, Wachaga na Wapare. Kwa ujumla, soga hujikita katika kuburudisha na kuelimisha jamii. Tazama mfano wa soga inayowahusu Wamakonde hapa chini:
Kisa cha Mmakonde na Ngedere
Mmakonde mmoja alikwenda shambani kwake, akakuta ngedere anakula mahindi yake. Ngedere alipomwona Mmakonde akakimbilia juu ya mti. Mmakonde akamwona kule alikojificha, akamwambia: "Wee ngedere nimechakuona; uch(ftfanye n'janja, telenka hapa Chini nikupige nchale ili upate adhåbu mpja tu. Vinginevyo,n 'kupige nchale ukiwa hukohuko juu ya nti, upate adhabu mbili: Adhabu ya _kupigwa nchale, na adhabu ya kuanguka kutoka j uu ya nti baada ya _kupigwa nchale. Je, wewe ungekuwa ngedere ungefanyaje?
(f) Visasuli
Kisasuli ni hadithi yenye kueleza usuli na sababu za jambo, tukio au hali. Visasuli havina uzito rNubwa kama visasili, na si lazima viaminiwe na wanajamii. Mathalani, zipo hadithi zinazoeleza kwa nini mnyama fulani anapenda kushirikiana na wanadamu, au ameumbika kwa namna fulani. Mfano wa kisasuli ni hadithi ya "Kwa nini nyokahana miguu?"
Kwa nini nyoka hana miguu?
Siku moja nyoka pamoja na wanyama wengine walialikwa kwenye sherehe nyumbani kwa mfalme. Kule walikula na kunywa! Baadaye mfalme aliwaita wapewe zawadi. Nyoka, kwa sababu ya uroho, hakusikia wito. Alipozinduka, alikuta miguu yote, hata ile hafifu ya tandu na buibui, imeshatolewa; akabakia anajiburuza kwa tumbo lake. Mpaka leo hii nyoka hana miguu (May Balisidya, 1987)
2. Semi
Semi ni tungo fupifupi za fasihi simulizi, na aghalabu, hutumia picha, tamathali na ishara. Semi hutumika kutoa mafunzo, nazo zimegawanyika katika vipera mbalimbali kama vile methali, misemo, nahau, mafumbo, lakabu, mizungu, misimu na vitendawili.
(a) Methali
Methali ni semi za kimapokeo zenye hekima na busara zinazoelezea falsafa na uzoefu wa jamii fulani kwa muhtasari. Semi hizi hubeba maana pana kuliko maneno yenyewe yanayotumiwa. Methali hutumika kusisitiza, kuelimisha, kuonya au kupongeza kwa njia za busara. Aghalabu, methali hujengwa kwa sitiari. Sitiari hizo hujitokeza katika pande mbili za methali ambazo hubainishwa kwa mkato,
Angalia mifano ifuatayo:
(i) Mtaka yote kwa pupa / hukosa yote.
(ii) Usipoziba ufa / utajenga ukuta.
(iii) Aisifuye m vua / imemnyea.
(iv) Chanda chema / huvikwa pete.
(v) Mtaka cha uvunguni sharti ainame.
Mifano ya hapo juu inaonesha kuwa methali hubeba dhima mahususi. Kwa mfano, methali (i) inawaasa wanajamii kutofanya mambo mengi kwa wakati mmoja. Ni vema kumakinikia jambo moja ili kulifanya kwa ufanisi, ndipo uanze jambo jinglne. Katika mfano (ii), jamii inaaswa kurekebisha tatizo katika hatua za mwanzo, yaani kabla madhara makubwa hayajatokea.
(b) Misemo
Misemo ni tungo zitumiazo picha, ishara na tamathali kueleza kitu au wazo kwa ufupi ili kuelimisha au kuadilisha. Misemo hufananisha maisha na matukio au vitu. Wakati mwingine, misemo hutumika kutambulisha mazingira maalumu au kuijulisha hadhira wakati au mahali fasihi hiyo ilipotungwa.
Angalia mifano ifuatayo:
(i) Bendera hufuata upepo.
(ii) Elimu ni bahari.
(iii) Ukubwa jalala.
Mfano (i) unaonesha hali ya maisha, ambapo wapo watu ambao hufuata mkumbo bila kufikiria au kuhoji kwa nini wanafanya jambo fulani na, hatimaye, kujikuta kwenye matatizo. Katika mfano (ii) elimu inafananishwa na bahari. Bahari ni kubwa, na haina mwisho, vivyo hivyo na elimu. Elimu hutupatia maarifa na ujuzi wa aina mbalimbali. Pia, elimu haina ukomo. Binadamu hujifunza kila siku. Mfano (iii) unalinganisha hali ya mtu kuwa mkubwa wa umri au Cheo, na kutupiwa lawama hata kama hajatenda kosa, kama lilivyo jalala ambapo watu hutupa taka.
(c) Nahau
Nahau ni fungu la maneno lenye maana maalumu isiyotokana na maana za kawaida za maneno hayo. Kwa kawaida, nahau huanza na kitenzi wakati misemo huanza na nomino.
Mifano yanahau ni:
(i) Kuj ikaza kisabuni (kuvumilia)
(ii) Piga kikumbo (sukuma)
(iii) Kula bakora (kupewa adhabu ya viboko)
(iv) Tia chumvi (shadidia kupita kiasi )
Ukichunguza mifano hiyo hapo juu, utaona kwamba nahau huhitaji ujuzi wa maarifa ya kiutamaduni na kimazingira ya lugha husika ili kuzielewa. Nahau hutumika kupunguza ukali wa maneno, kupamba lugha na kuhifadhi amali za jamii.
Ni kauli zenye mafumbo zinazoonesha ukinzani wa fikra au tukio. Mbali na vitendawili vya kawaida, kuna vitendawili vingine vijulikanavyo kama mizungu. Hii hutumia zaidi mafumbo. Kwa mfano inaelezwa kwamba mtu hawezi kumwoa ndugu wa damu. Ukinzani huu umetumika kuonya ndugu wasiwe na uhusiano wa kimapenzi. Mizungu hutumia mafumbo ya hali ya juu, hivyo, hutumiwa na watu wazima katika miviga ili kueleza dhana na mawazo mbalimbali kwa maongezi au nyimbo. Mizungu hutumia lugha ya picha inayoonesha ukinzani wa fikra. Ukinzani husaidia kumfikirisha msikilizaji na kumpa changamoto ya kutafuta jibu. Mifano mizuri ya mizungu ni:
(i) Uazuri sana limeota kwenye miiba; hivyo, huwezi kulichuma.
(ii) Papai limeiva nyumbani, ila siwezi kulila.
(e) Mafumbo
Mafumbo ni kauli au maelezo yanayoficha maana ambayo humtaka msikilizaji kuyafumbua. Kwa mfano, watu wanamteta mtu, mietwaji akawa anakuja mahali walipo, mmoja wao anaweza kusema wifi kaja au shangazi kaja. Hii huwasaidia kubadilisha maongezi baada ya kufumbua wifi au shangazi kuwa ndiye mtu anayetetwa ingawa mtu huyo si wifi wala shangazi wa mtu yeyote katika kundi hilo.
Aidha, kwenye mazingira ambapo watu wanaongea Iakini hawataki mmoja wao ajue maongezi yao, labda kwa sababu ni domokaya, mmoja wao anaweza kuwatahadharisha kwa kusema hivi, Ooho! Mkorosho umeanguka! Inabidi waelewe kwamba "mkorosho ulioanguka" ni mmoja wao. HiVY0i wataongea kwa tahadhari kubwa. Aghalabu, mafumbo mengi huwa ni kejeli dhidi ya watu wenye tabia mbaya.
Mafumbo yana malengo ya kuelimisha, kuburudisha, kukosoa na kuonya kuhusu mambo yanayotendeka miongoni mwa wanajamii
(f) Lakabu
Lakabu ni majina ya kupanga (ambayo sio halisi) ambayo baadhi ya watu hupewa au hujipa kutokana na sifa zao za kimaumbile, kinasaba, kitabia, kiujuzi au kimatendo. Majina haya huwa na maneno yenye maana iliyofumbwa, yaani maana ya kisitiarim Majina haya huwa na dhima ya kusifia, kukosoa au hata kudhalilisha.
Angalia mifano ifuatayo:
(i) Baba wa Tara - J. K. Nyerere (Rais wa Kwanza wa Tanzania)
(ii) Simba waVita - Mzee Rashid Kawawa
(iii) Komandoo - Dkt. Salmin Amour
(iv) Kulakulala - Mvivu
(v) Jembe - MChapakazi
Wasanii wengi hujipa majina ya kilakabu. Mathalani, Mrisho Mpoto (Mjomba), Naseeb Abdul (Diamond/Simba), Judith Wambura (Binti Machozi/Lady Jay Dee) na Joseph Mbilinyi (Mm: 11/ Sugu). Pia, waganga wa tiba mbadala hutumia majina ya namna hii, mfano Steven Ngonyani (Pref. Maji Marefu).
(g) Misimu
Misimu ni semi ambazo huzuka mahali au kipindi fulani kisha hutoweka. Misimu huambatana na matukio au shughuli zinazotokea katika jamii Aghalabu, misimu hutumiwa na makundi mahususi ya kijamii, hususani yanayoendana kikazi, kirika au kimasomo. Misimu mingi haina maisha marefu. Ikidumu, husanifiwa na kuingizwa katika matumizi ya lugha husika.
Tazama mifano ifuatayo:
(i) Fataki -mtu mzima anayefuata watoto/vijana kwa nia ya kufanya nao mapenzi.
(ii) Marioo - vijana wanaoishi kwa kuwategemea wanawake wanaowazidi kipato.
(iii) Kutema ngeli - kuongea Kiingereza vizuri.
(iv) Bodaboda - pikipiki inayotumiwa kusafirisha watu/mizigo kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa malipo.
Ijapokuwa misimu katika mifano (ii) na (iii) inatumika katika jamii, haijaingizwa katika matumizi rasmi. Mifano (i) na (iv) inaonesha misimu ambayo imesanifiwa na kuingizwa katika matumizi rasrm.
(h) Vitendawili
Vitendawili ni semi fupi fupi za mafumbo zenye kutumia lugha ya picha, tamathali na ishara kueleza jambo lililofichika. Jambo hilo ndilo jibu la fumbo. Kwa kawaida, kitendawili hupewa jibu kwa neno moja au zaidi au maelezo. Kama ilivyo katika kazi nyingine za fasihi, vitendawili hutumika Kuburudisha, kuelimisha, kupamba lugha, kukosoa au hata kukej eli. Tazama mifano ifuatayo:
(i) Pango langu limejaa mawe—kinywa.
(ii) Nyumba yangu ina nguzo moja - uyoga/mwavuli.
(iii) Blanketi la babu lina chawa - mbingu na nyota. (iv) Bibi amejitwisha machicha ya nazi -mvi.
Uundaji wa vitendawili hutegemea mazingira ambako kitendawili hicho hutumika. Tazama rmfano ifuatayo:
(i) Watoto wa sultani wamevaa kofia.
(ii) Nimenunua sungura nimemvika kofia. (iii) Nikune kichwa nikupe moto.
Jibu la vitendawili hivi vyote ni njiti ya kiberiti.
Tofauti ya vitendawili (i), (ii) na (iii) inatokana na mazingira. Kitendawili (i) kimeundwa katika mazingira ambayo sultani aliwahi kuishi. Kitendawili (ii) kimeundwa katika sehemu yenye wafugaji au pori lenye sungura. Kitendawili (iii) kimeundwa katika mazingira yanayoakisi udugu, ambapo ni rahisi _mtu kuomba kukunwa kichwa.
3. Ushairi
Ushairi ni utanzu wa fasihi simulizi ambao Lhuwasilishwa kwa hadhira kwa njia ya uimbaji au ughani badala ya usemaji wa kawaida. Ushairi hujipambanua na tanzu nyingine za fasihi simulizi kutokana na matumizi ya mizani, lugha ya mkato, lugha ya mafumbo na uimbaji au ughani. Ushairi una vipera vitano; vipera hivyo ni nyimbo, mashairi, ngonjera, maghani, na tenzi.
(a) Nyimbo
Nyimbo ni tungo za kishairi zinazowasilishwa kimuziki kwa kutumia sauti iliyo katika _mpangilio fulani wa mahadhi na melodia, na inayozingatia mapigo ya kiurari. Mahadhi au tuni ni sauti mahususi ya uimbaji wa wimbo fulani, na melodia ni mpangilio na mwendo wa uimbaji wenye kuzingatia urari wa mapigo au ridhimu. Nyimbo huweza kuimbwa na kuchezwa pamoja na ala za muziki. Nyimbo huimbwa na mtu mmoja au kundi la watu. Wakati mwingine, kikundi cha waimbaji huwa na kiongozi na wafuasi wake. Kiongozi huanzisha wimbo, halafu wafuasi huitikia mkarara. Kiongozi wa
nyimbo huitwa manju. Nyimbo zinaainishwakwa kuzingatia dhima, hadhira ınayoimbiwa na muktadha unaofungamana nazo. Kutokana na vigezo hivyo, tunapata baadhi ya aina kama ifuatavyo: tumbuizo, bembea, kongozü nyimbo za dini na wawe. Yafuatayo ni maelezo mafupi kuhusu aina hizi:
(i) Tumbuizo ni nyimbo za furaha ziimbwazo katika matukio mbalimbali kama vile hamsini na ngomani.
(ü) Bembea ni nyimbo za kubembeleza watoto.
(iii) Kongozi ninyimbo za kuaga na kukaribisha mwaka.
(iv) Nyimbo za dini ni nyimbo zinazoimbwa kwa lengo la kumsifu Mungu au miungu,
(v) Waweni nyimbo za kilimo; zinapatikana karibu katika makabila yote ya Tanzania.
(b) Mashairi
Mashairi ni tango zenye kuelezea au kuonesha kwa ufupİ wazo au jambo au hisi fulani kuhusu binadamu na mazingira yake. Mambo hayo huelezwa katika mpangilio maalumu wa maneno fasaha yenye muwala, aghalabu kwa lugha ya kitamathali yenye kugusa moyo. Tunaposema mpangilio wa maneno tunamaanisha kuwa mpangilio wa maneno katika shairi hufuata kanuni tofauti na ule wa nathari. Si lazima shairi kufuata kanuni za miundo ya sentensi İnayotumika katika lugha husika. Mathalani, badala ya kuandika usikate tamua maishani tungo hiİ İnaweza kuandİkwa maisha usikate tamaa, mpangilİo ambao unakubalika katika shairi. Mbali na kuzingatia mambo hayo yanayohusu ushairi kwa jumla, ushairi simulizi una şifa ya kutungwa papo kwa papo na kufungamana na muktadha au tukio _mahususi. Wakati mwingine, ushairi simulizi huambatana na ala za muziki. K wa _mfano, baadhi ya tungo za iaarabu ni ushairi simulizi. Ufuatao ni mfano wa beti za wimbo wa taarabu:
Macho yanacheka, moyo unalia
Macho yanacheka, moyo unalia x4
Nikimkumbuka, wangu maridhia x4
Chozi hunitoka, kwa zake tabia x4 La la la la la oooh!
Nenda nateseka, nalia na njia x3
Siku zikifika, kukugeukia x4
Waja hangaika, ulie na njiax4
La la la la la oooh!
(Shakila said, miaka ya 1960)
(c) Ngonjera
Ngomera ni neno la Kigogo lenye maana ya "twende pamoja" au "tuambatane." Baadhi ya wataalamu wanasema kipera hiki kilikuwapo toka zamani na kina historia ndefu. Ila kilihuishwa mwishoni mwa miaka ya 1960 na Mathias Mnyampala katika harakati zake za kuelezea siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.
Ngonjera ni mazungumzo au majibizano ya kishairi kuhusu mada fulani. Kwa maana hii, ngonjera haziimbwi, husemwa bila kutazama karatasi au kitabu chochote. Aghalabu, majibizano hayo huwa na washiriki wa pande mbili, upande wa wanaopinga na upande wa wanaotetea hoja. Wahusika hawa hutumia lugha ya ishara pamoja na miondoko ya mwili kama vile mikono, macho na midomo. Kutokana na wahusika kutumia miondoko, ngonjera huitwa ushairi wa maigizo. Katika ngonjera, suluhisho hupatikana mwisho wa majibizano, ambapo pande mbili .zinazopingana hukubaliana. Ingawa ngonjera za Mathias Mnyampala ni fasihi andishi, lakini ngonjera hupatikana pia katika fasihi simulizi ya Kiswahili. Mfano mzuri ni majibizano ya Amiri Andanenga (Sauti ya Kiza) na Abdallah Matawa (Mbwenzi) ambayo yalifanywa kishairi, ubeti kwa ubeti, papo kwa papo (Tazama Elimu ya Bahari ya Ushairi (Amiri Andanenga, 2002:117-119)
(d) Maghani
Maghani ni tungo za ushairi zinazotongolewa kwa kutumia sauti iliyo kati ya uimbaji na uzungumzaji. Maghani hutongolewa kwa kutumia mapigo ya m wendo na kasi inayokubalika. Kiimbo cha sauti hupangiliwa i Ii kuleta ladha na maana katika maghani. Wakati mwingine, kiimbo cha kati (ambacho si chajuu wala cha chini) hutumiwa. Kina ehajuu na cha chini cha sauti katika kiimbo hurudiwa ili kuburudisha na kuweka uzito katika mama. Mfano mzuri wa maghani ni utambaji wa majigambo na tendi simulizi, kama zile za nanga (Ukanda wa Ziwa) na zeze.
(e) Tenzi
Tenzi ni tungo ndefu zinazoeleza tukio fulani linalotokea au lililowahi kutokea katikajamii; au zinazofafanuajambo au fikra fulani. Tenzi huwa na kisa kimoja kinachoelezwa kwa kina. Kisa hicho kinaweza kuwa ni maelezo kuhusu wasifu wamtu fulani,jambo fulani Iakihistoria aujambo Iolote. Sifa ya kusimulia au kuelezea jambo kwa urefu ndio husababisha tenzi kuwa na beti nyingi kuliko mashairi au aina nyingine za ushairi. Tenzi za wasifu au matukio ya kishujaa huitwa tendi.
Utendi ni utenzi wa matendo wenye masimulizi kuhusu mashujaa. Kimuundo, tenzi simulizi huwa na muundo wenye kufungamana na mahadhi ya ala ya muziki Inayotumika au melodia ya uimbaji. Kwa kawaida, hazina urari wa vina na mizani. Tenzi zenye urari wa vina na mizani ni zile zenye kufuata kanum za ushairi andishi wa Kiswahili japo chimbuko au utungaji wake ni wa kisimulizi. Mifano ni Uten:iwa Nyakiiru Kibi (Mugyabuso Mulokozi, 1997) na Utendi wa Fumo Liyongo (MuhammadKijumwa, 1913) katika Ten:i Tatu za Kale (Mh. Mugyabuso Mulokozi, 1999). Katika tenzi hizo, mishororo haikugawanywa katika vipande viwili. Kila ubeti huwa una mistari minne; mistari mitatu ya kwanza ikiwa na vina vyenye urari sawa na ule wa mwisho ukiwa na kina tofauti. Pamoja na vina hivyo kuwa na urari sawa, hubadilika toka ubeti mmoja hadi ubeti mwingine. Kina kinachorudiwa katika mstari wa mwisho, huitwa kina bahari. Ufuatao ni mfano wa beti za Utendi wa Fumo Liyongo ambao unatokana na utendi simulizi:
Niweleze kwa utungo,
Hadithi yake Liyongo,
Niweleze na mazingo,
Mambo yalomzingiya.
Liyongo kitamakali,
Akabarighi rijali,
Akawa mtu wa kweli,
Na haiba kaongeya.
Kimo kawa mtukufu,
Mpana sana mrefu,
Majimboni yu marufu,
Watu huya kwangaliya.
Ni mwanamume swahihi,
Kama simba unazihi,
Usiku na asubuhi,
Kutembea ni mamoya.
Kisa katiti kutuwa,
Mkobani akatowa,
Zi tu alizotukuwa,
Nyumba ndima nisikiya
Katowa kinu na mti,
Na jiwe na kupaza kuti,
Na zunguze si katiti,
Na mawe ya kupikiya.
Mohammed Kijumwa katika Tenzi Tatu za Kale Mugyabuso Mulokozi [Mh] (2012)
Beti hizi ni sehemu ya masimulizi ya kiutendi yanayomhusu Fumo Liyongo. Masimulizi haya yanaakisi maudhui ya kipindi cha miaka ya 900-1500 BK. Hivyo, lugha iliyotumika ni ile inayoakisi kipindi hicho. Masimulizi hayo yanahusu masuala kama vile nguvu za kimwili, kiakili, kisihiri, kivita na kiume (urijali).
4, Sanaa za Maonesho
Sanaa .za maonesho zinajumuisha sanaa ambazo huwasilisha wazo ana kwa ana kwa kutumia usanii wa utendaji. Utanzu huu hujumuisha kipera chochote chenye mambo yafuatayo:
(i) Dhana ya kutendeka (tendo)
(ii) Mtendaji (fanani)
(iii) Uwanja wa kutendéa (jukwaa)
(iv) Watazamaji (hadhira)
(v) Kusudio la kisanaa (maudhui).
Hivyo, sanaa za maonesho huwa kwenye umbo linalotendeka. Sanaa za maonesho huweza kugawanyika katika makundi mawili ambayo ni sanaa za maonesho za jadi na sanaa za maonesho mamboleo. Sanaa za maonesho za jadi
ni zile zilizochipuka katika jamii za Kiafrika (Tanzania). Sanaa hizi hujumuisha ngoma, matambiko, majigambo na miviga. Ingawa miviga kama vile ibada, sherehe, jando na unyago ni matukio ya kijamii au kimila yenye kuvuka mipaka ya kisanaa, lakini inajumuishwa hapa kwa kuwa sanaa hutawala utendaji na uwasilishaji wa maudhui yake. Wakati wa uwasilishaji wa shughuli hizi, watu hufanya vitendo vya kisanaa kama vile uigizaji wa visasili, uchezaji ngoma, uimbaji na utongoaji mashairi, vikiambatana na matendo ya mwili. Kwa njia hii, watu huweza kuwasiliana wao kwa wao au kuwasiliana na miungu. Ijapokuwa dhima ya sanaa hizi hufanana kwa namna ya jumla, huwa kuna tofauti mahususi katika vipengele vya utendaji kati yajamii au kabila moja na jingine.
Wakati wa ukoloni, sanaa za jadi, hasa zile zilizohusiana na Imani za dini, zilipigwa Vita. Hali hii ilisababisha sanaa kama vile matambiko kupotea katika baadhi ya jamii. Sanaa nyingine zimedumu mpaka Ieo kutokana na wito wa kitaifa wa kudumisha utamaduni wa Kitanzania.
Sanaa za maonesho mamboleo ni zile zilizotokana na athari za ujio wa wageni. Sanaa za namna hii ni vichekesho na maigizo. Vipera vya sanaa za maonesho za jadi ni majigambo, miviga, vichekesho, ngomezi, tambiko, utani, maigizo na michezo ya watoto.
(a) Majigambo
Majigambo ni masimulizi ya kujisifia au kujikweza kwa mtu kuhusu mambo aliyowahi kufanya. Mambo hayo huwa ni ya kishujaa kama vile kupigana vita na kuua wanyama wakali. Kwa kawaida, majigambo husimuliwa katika lugha ya kishairi. Mjigambi hufanya matendo mbalimbali. Aghalabu, mjigambi hubeba silaha kama vile mkuki na ngao au upinde na mishale. Kama mjigambi ametoka kuua simba, kwa mfano, ataonesha matendo ya jinsi alivyopambana na simba hadi kumshinda.
Makabila yenye sanaa za majigambo ni yale ya Ukanda wa Ziwa (kama vile Wakurya, Wasukuma na Wahaya), yale ya Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania, hususani Wahehe, na ya Kaskazini mwa Tanzania, hasa Wamasai. Majigambo hufanyika wakati wa sherehe za harusi na za kuwapokea au kuwapongeza mashujaa. Pia, hufanyika kwenye mikutano inayoitishwa na watawala, Majigambo huambatana na ngoma na nyimbo za kusifu. Mjigambi hutokea katika kikundi kinaehocheza na kujigamba; amalizapo mjigambi mwingine hufuata, Mara nyingi, mjigambi wa mwisho huwa ni yule aliyetendajambo Ia kishujaa kuliko wote au yule anayeij ua vizuri sanaa ya majigambo.
Lengo kuu Ia majigambo ni kujenga ari ya ushujaa, ukakamavu na ujasiri. Mtu anayefanya kitendo cha kishujaa, hushangiliwa na kupewa heshima kubwa katikajamii yake. Kwa msingi huu, vijana huhamasika kuwajasiri na wakakamavu ili kulinda hadhi na heshima ya jamii zao. Ikumbukwe kuwa, kwa kawaida, wanaojigamba ni wanaume tu; katika jamii nyingi mwanamke haruhusiwi kujigamba hata akifanya kitu cha kishujaa. Hii inatokana na ukweli kwamba, katika jamii nyingi washiriki wa ngoma za kujigamba huwa wanaume. Aidha, katika mazingira mengine yaliyotumika kujigamba, wanawake hawakuruhusiwa kuwqpo, mathalani, kwenye vikao vya pombe. Kwa ujumla, maj igambo ni sanaa ya wanaume ambayo inalenga kudumisha utu na heshima yao katika jamii. Ufuatao ni mfano wa majigambo kutoka katika wimbo wa "Ndiyo Mzee":
Ok ok naitwa Joseph Haule mwana Msolopagazi
Nadhani nimeletwa kuokoa hiki kizazi
Mimi ni mwanasiasa niliyebarikiwa na Mungu
Nimeletwa kwenu waungwana niwapunguzie machungu
Mimi ni mteule Kusini mwa jangwa Ia Sahara
Ndio maana nimetunukiwa cheti cha juu cha utawala
Nina hekima kuliko mfalme S ulemani msiwe na wasi
Na hii nitadhihirisha pindi mtakaponipa nafasi
Actually, nimedhamiria kuwasaidia
Taifa Ienye nguvu duniani Iiwe Tanzania
Haule 'Profesa Jay', Macho:i, Jasho na Damu, (2001)
Katika dondoo hili, msanii anajigamba kuwa anatoka katika nchi ya Kusini mwa Jangwa Ia Sahara. Zaidi, anajigamba kwamba anatoka katika ukoo wa Msolopagazi (Umslopogaas). Kwa mujibu wa Samwel (2012), Msolopagazi ni mhusika wa Kizulu katika riwaya ya Allan Quatermain iliyoandikwa na (Ridder Haggard). Katika riwaya hiyo, Msolopagazi anaambatana na Wazungu (Sir Henry Curtis na John Good). Anamsaidia rafiki yake, Allan Quatermain, katika safari zake barani Afrika. Katika wimbo huu, Joseph Haule, ambaye ni Mngoni,. anajinasibishana ehimbuko lake Ia Afrika Kusini kama historia inavyotufundisha, Kwa hiyo, katika mujigambo haya, msanii anahifadhi historia hiyo ya jamii yake,
(b) Matambiko
Matambiko ni ibada zinazoambatana na utoaji wa sadaka kwa Mungu, miungu na mizimu, Tangu zamani, jamii mbalimbali zilifanya matambiko ili kutoa shukrani, kusifu, kuomba msamaha na kutatua matatizo. Tambiko ni tukio halisi ambalo hutendwa kisanaa, ndiyo maana linaingizwa katika kundi la sanaa za maonesho. Usanii wa tambiko hutokana na uzingatizi wa vipengele vifuatavyo: maleba, umri- mandhari, malengo, hatua na namna (ya kunena na kutenda). Kwa kawaida, matambiko hufanywa na watu maalumu katika jamii zao. Matambiko hufanyika katika mandhari maalumu. Kwa mfano, watambikaji katika baadhi ya jamii za Kanda ya Ziwa huelekeza maombi yao kwa Namhanga (Mungu Mkuu), Mugasa (mungu wa wavuvi) au Ka/ungu (mungu wa wawindaj i). Utendaji wa tambiko hili huenda sanjari na matumizi ya maleba, vyungu na pembe maalumu. Sadaka zinazotolewa hujumuisha kuku, mbuzi, kondoo, ng'ombe, vyakula Vya nafaka na pombe iitwayo na Wakerewe empahe.
(c) Miviga
Miviga ni sherehe au shughuli zinazofanywa najamii katika kipindi maalumu cha mwaka au katika muktadha maalumu. Sherehe hizo zinaweza kuwa za jando na unyago, kutawazwa kwa Mtemi au harusi. Miviga huwa ni sherehe zihusuzo mtu kutoka katika kundi au wadhifa fulani na kuingia katika wadhifa mwingine Mathalani, anaweza kutoka katika rika la utoto kwenda ujana Gando na unyago) na ujana kwenda utu uzima (kuoa au kuolewa), Kadhalika, miviga ni matendo ya kimila ambayo wakati mwingine huhusisha sehemu kubwa ya jamii.
Miviga huambatana na maigizo na nyimbo zinazoendana na tukio husika. Katika harusi, nyimbo zinazoimbwa ni za ndoa na katika mazishi nyimbo zinazoimbwa ni za maombolezo. Katika miviga, ngoma mbalimbali huchezwa. Aghalabu, wazee hutoa mafunzo na mawaidha, hususani kwa watoto na vijana.
(d) Vichekesho
Vichekesho ni aina ya sanaa ya fasihi simulizi ambayo watu hutoa vihadithi vifupi ambavyo huwafanya wasikilizaji na watazamaji wacheke. Vichekesho vinahitaji ubunifu mkubwa ili kupata jambo litakaloibua hisia na kuvunja mbavu. Lugha inayotumika katika vichekesho ni nyepesi na iliyojaa picha ambazo watazamaji wana uwezo wa kuzitambua. Hii ni kwa sababu hutumia mifano ya vitu vinavyojulikana wazi kwa hadhira au vinavyopatikana katika mazingira yao. Aidha, vichekesho hutumia mbinu ya kejeli na chuki.
Kama ilivyodokezwa katika maelezo ya sanaa za maonesho kwa ujumla, vichekesho ni mojawapo ya sanaa mamboleo; vichekesho vimetokana na kuletwa kwa tamthiliya za kizungu. Tamthiliya hizi zilibeba na kuongelea utamaduni wa kizungu. Baadhi ziliongelea matatizo ya kijamii ya wakati wa ukoloni, mathalani suala la mgongano kati ya miji na shamba, na uzuzu au ushamba wa Mwafrika anayetoka kijijini na kuingia mjini kwa mara ya kwanza. Maigizo hayo hayakuwa na maana kubwa kwa Waafrika zaidi ya kuwachekesha kupitia katika vitendo vilivyofanywa kwenye jukwaa. Kwa hiyo, Waafrika wakadhani kuwa jambo muhimu katika vichekesho ni kuchekesha.
Kimsingi, dhima ya vichekesho si kuchekesha tu, bali vichekesho huelimisha pia. Mifano ya vichekesho ni kama ile inayopatikana katika vipindi vinavyorushwa na vituo vya redio na televisheni. Mifano ya viprndi vya kwenye televisheni ni Mizengwe (ITV), Ze Comedy (EATV) na Vitimbi Show (Channel Ten).
(e) Ngomezi
Hii ni sanaa ya kuwasiliana kupitia midundo ya ngoma. Baadhi ya makabila huweza kupeana taarifa za matukio mbalimbali kupitia ngoma. Aghalabu, taarifa hizo huwa katika hali ya mafumbo, kiasi kwamba, wenyeji wa jamii husika tu huweza kubaini maana ya midundo husika. Hii yatokana na ukweli kuwa midundo katika sanaa hii hufuata kanuni maalumu zinazojulikana na wanajamii hao tu. Kanuni hizo hubebwa kupitia vipengele vya aina ya ngoma zinazotumika, muda wa kupigwa kwa ngoma pamoja na kasi au mwachano wa upigaji. Kanuni hizi huwasaidia wanajamii kupata ujumbe unaowasilishwa. Kwa mfano, katika jamii ya Wayao kuna ngoma ya Ngulantwe inayopigwa kwa ajili ya kutoa ujumbe kuhusu matukio mbalimbali ya kitanzia. Ujumbe huo huweza kuwa: "Simba amevamia na kuua mifugo", "Simba amejeruhi mtu ila hajamuua", "Simba ameua mtu", au "Kesho wanaume wote wanatakiwa kwenda kwenye msako wa simba mvamizi."
(f) Utani
Ni hali ya kufanyiana mizaha au masihara baina ya watu ambapo hali hii ni tofauti na desturi za kutokuheshimiana. Wanajamii wenye uhusiano wa kutaniana, hutaniana mahali popote wakutanapo kama vile msibani,
harusini, hata kwenye sehemu za kazi. Utani huweza kuwa kati ya mtu na mtu, ukoo na ukoo au kabila na kabila. Utani kati ya mtu na mtu huwa ni kati ya babu/bibi na wajukuu, mtu na shemeji au wifi na wifi. Kadhalika, utani kati ya kabila na kabila, aghalabu, huwa kati ya makabila yenye asili ya kuishi katika eneo moja au yaliyokuwa na maingiliano ya muda mrefu. Makabila yote ya mkoa wa Mara, kwa mfano, ni watani wa Wanyaturu na Wanyiramba (Singida) na Wahaya (Kagera).
Utani hujenga uhusiano na ushirikiano mzuri baina ya wanajamii. Vilevile, utani hutunza historia ya jamii zinazotaniana. Aidha, utani huwafunza watoto upendo na majukumu, mathalani, utani wa mjukuu wa kike na babu anapomwita mke wake na kuomba amfanyie jukumu fulani, mtoto huyo hujifunza jukumu lake atakalolitekeleza akiwa mkubwa.Vilevile, utani hukumbusha wanajamii majukumu yao. Mathalani, katika misiba, watani hutumia tukio kukumbusha watu kujuliana hali wanapokuwa wazima na kusaidia kazi zihusuzo msiba. Kama zilivyo dhima nyingine za fasihis utani huburudisha kwenye matukio ya furaha na huzuni. Ikumbukwe kwamba, utani unaweza kusababisha ugomvi endapo mhusika hajui kuwa anayemfanyia mzaha ni mtani Wake.
(g) Maigizo
Maigizo ni sanaa inayotumia watendaji kuiga tabia na matendo ya watu au viumbe wengine ili kuburudisha au kutoa ujumbe fulani. Maigizo haya yanapoletwa jukwaani na kuoneshwa kwa hadhira huitwa drama. Mara nyingi, maigizo ya Kiafrika huambatana na utambaji wa hadithi, vichekesho, nyimbo, matendo ya kijadi kama Vile harusis jando na unyago. Wahusika hutakiwa kutumia lugha ya kifasihi inayoendana na hadhira. Zipo aina mbalimbali za maigizo zikiwamo: maigizo ya misibani na mivigani, maigizo ya watoto na ya burudani.
(h) Michezo ya watoto
Watoto hucheza michezo mingi yenye kuambatana na usanii. Miehezo Iliyo hutofautiana majina kulingana na mahali. Katika michezo hiyo, kuna kuimba, kucheza, kurukaruka, kukimbia„ kughani, kujigamba na kuigiza. Baadhi ya michezo hiyo ni: kiota, ukuti, pembea (bembea), kitikiti, kibuzi na kombolela. Michezo hiyo inawekwa hapa kwa sababu aghalabu huambatana na nyimbo, majibizano, vitendo na maigizo. Kwa mfano, katika mehezo wa kiota, watoto hunyanyuka pale walipoketi na kuanza kutangatanga huku na huku ilihali wakiimba mpaka kila mmoja anapopata mahali pake na kukaa. Watoto huimba hivi:
Kiota
Sisi ndege twaruka
Twatafuta kiota
Kiota
Kiota
Kiota
Tala la la la la
Kiota
Wimbo wa mchezo huu umetumia mbinu za takriri, urari na uimbaji mbali na kuambatana na vitendo vya kutembea na kuzunguka. Michezo mingi ya watoto huunganisha sanaa ya uimbaji na vitendo.
Mchezo mwmgine ni wa kubembea kwenye kamba. Mchezo huu huambatana na wimbo wa "Pembea". Ufuatao ni wimbo huo uliorekodiwa zaidi ya miaka mia moja iliyopita:
Pembea
Pembea iyo pembea
Pembea iyo pembea Wewe Maasisi
Kalaga hasi pembea
Mtama ukigwa pembea
Tule tuta pembea
Tuta kaya pembea
Ya mgambo pembea
Amiri Andanenga, Bahari ya Elimuya Ushairi ( 2002: 168)
Pia, kuna mchezo wa "Kibe." Mchezo huu huchezwa na watoto wa kike na wa kiume ambao hujipanga katika mistari miwili inayotazamana. Uehezaji wake huambatana na wimbo. Wachezaji huongozwa na kiongozi kuimba na kucheza. Kiini cha uchezaji wake hubebwa na vitendo vya kila mmoja kuchagua mwenza kutoka mstari wa wachezaji wa jinsi tofauti. Ufuatao ni wimbo wenyewe:
Wimbo wa "Kibe"
Kiongozi: Kibee mama kibeeex2
Wote: Hayaaa Kiongozi: Nilikwenda matembezi
Wote: Hayaaa
Kiongozi: Nikamkuta msichana mrembo Wote: Hayaaa
Kiongozi: Akaniuliza wenda wapi?
Wote: Hayaaa
Kiongozi: Nikamwambia naenda kurithi matanga Wote: Hayaaa
Kiitikio:
Haya msichana wa sawa.
Chagua mumeo sawa.
Mumeo akikuita nenda.
Usije ukatonesha donda.
Maigizo yawatoto ni aina nyingine ya michezo ya watoto. Watoto huigiza miehezo inayoakisi mazingira yanayowazunguka kama vile nyumbani, shuleni, shambani, hospitalini, barabarani, kanisani, msikitini na porini. Pia, watoto huigiza mambo wanayoyaona kwenye runinga, hasa watoto waishio mijini, mfano michezo ya kivita, sherehe mbalimbali, vikundi vya nyimbo, miziki na michezo ya kuigiza.
Maigizo ya watoto, kama ilivyo kwa kazi nyingine za fasihi, yana vipengele vya fani na maudhui. Maudhui ya michezo ya watoto, kwanza, huhusu maisha ya nyumbani kwa sababu ndiyo maisha wanayoyaona mara kwa mara.Watoto huigiza _maisha ya nyumbani kwa kuakisi maisha halisi ya familia, hususani yale wanayoyaona kwenye familia zao. .Mathalani, kama baba ni mkali, mtoto atakayeigiza kama baba, ni lazima atakuwa mkali, pengine kuzidi ukali anaouona kwa baba; vivyo hivyo, kama baba ni mpole na mkarimu basi muigizaji ataigiza upole na ukarimu. Kwa upande mwingine, watoto waigizao nafasi ya mama, huakisi tabia ya mama. [kiwa mama ni mchapakazi, basi muigizaji atakuwa na tabia hiyo; kama ni nadhifu, mwigizaji naye atajitahidi kuwa nadhifu.
Watoto waigizapo sherehe za harusi, hujumuisha matendo kama vile ufungaji wa ndoa. Baada ya kufunga ndoa, huigiza kwenda ukumbini au eneo lolote ambapo sherehe za harusi hufanyika. Tukio hili huambatana na nyimbo mbalimbali.
Nyimbo hizo ni kama:
(i) Kiongozi: Anameremeta
Wote: Anameremeta
Kiongozi: Bwana Harusi anameremeta
Wote: Anameremeta
Kiongozi: Bibi Harusi anameremeta
Wote: Anameremeta
(ii) Aiya iya kuolewa, utarudi nyumbani kutembea,
Kwa heri ndugu zangu, kuonana majaliwa
Kwa heri majirani, kuonana majaliwa.
Nyimbo hizi husaidia kuburudisha, kupamba na kuupa mchezo wao hadhi ya kuwa fasihi simulizi. Aghalabu, watoto hupenda kuigiza maisha ya vitimbi na ubabe kuliko kuigiza maisha ya kawaida.
Maigizo ya watoto hubuniwa pale wanapokutana, hakuna matini inayokuwa imeandaliwa kabla ya mchezo. Watoto wanapokutana hukubaliana aina ya mchezo na kugawana uhusika na majukumu ya kila mhusika; wakati mwingine, watoto wenyewe huchagua nafasi watakazoigiza. Uigizaji wa michezo ya watoto huambatana na ubunifu ambapo kila mtoto (mhusika) hubuni uigizaji wa sehemu yake anayoigiza. Maigizo ya watoto huwa na muundo wa moja kwa moja.
Wahusika katika maigizo hayo ni watoto wenyewe ambao hupanga nafasi zao za uhusika kulingana na mchezo wanaoigiza. Katika maigizo yanayohusisha wanyama, kwa mfano, kama igizo lina mhusika Simba, mtoto anayeigiza kama simba, ni lazima awe na sifa za ubabe, sauti nzito na nguvu. Hali kadhalika, atakayeigiza kama jogoo, awe na sauti kali, ili atakapowika isikike.
Aidha, watoto huchagua nafasi kulingana na jinsi zao na jinsi jamii ilivyogawa majukumu ya jinsi hizo. Mathalani, watoto wa kike huchagua nafasi za kuigiza kutokana na kazi ambazo hufanywa na wanawake katika jamii kama vile uuguzi, uyaya,upishi,ufanyaji usafi na ukatibu muhtasi.Vivyo hivyo, watoto wa kiume
huchagua nafasi za kuigiza kutokana na kazi ambazo hufanywa na wanaume kama vile udereva, urubani, kuchinja na kuuza nyama, uaskari na kazi nyingme ngumu. Kupitia michezo hii, ndimo ndoto za watoto huehomoza na watoto wengine huanza kuishi na ndoto zao. Maigizo ya watoto hayahitaji maleba mahususi.
Dhima za michezo ya watoto
Michezo ya watoto ina dhima nyingi kwa watoto wenyewe.
Zifuatazo ni baadhi ya dhima hizo:
(i) Kuchochea ubunifu miongoni mwa watoto
.Miehezo ya watoto huwa na sifa za kisanaa kama vile ubunifu, urari wa matukio, uigizaji na matumizi maalumu ya lugha na sauti. Mambo haya huhitaji kiasi fulani cha ubunifu na usanii. Kwa njia hii, watoto hujifunza kuwa wabunifu.
(ii) Kujijengea uwezo wa usimulizi na usemaji wenye t!fundi
Michezo ya watoto huwa na wahusika wanaohusiana ili kuumba mtiririko wake. Uhusiano huu hujengwa kwa njia ya mazungumzo yenye uhalisi. Mathalani, "mama" anapaswa aongee kama mama kweli; hali kadhalika, "baba" aongee kama baba, na wanapoongea waoneshe uhusiano wa "mke" na "mume." Kadhalika, usimuliaji wa matukio na maelezo uwe na ushawishi.
(iii) Kuchochea umahiri wa lugha
Baadhi ya michezo hutumia lugha. Maongezi, majibizano na maelezo ya wahusika hujenga uwezo wao wa kutumia lugha kwa njia mbalimbali kulingana na muktadha. Uzoefu huo hatimaye huwajengea umahiri wa kutumia lugha katika maisha halisi.
(iv) Kuchochea udadisi
UUmbaji wa mchezo huwafanya wahusika wahoji na kudadisi mambo mbalimbali na kuyatafutia ufumbuzi, Udadisi huo hatimaye huweza kutumika katika maisha halisi.
(v) Kuburudisha watoto na kuwafanya wawe wachangamfu
Watoto hufurahina kucheka wanapokuwa wakitunga na kuigiza au kucheza mchezo wao, kwa mfano Kach iri au Ukuti. Hizi ni sh ughuli zinazopumzisha akili na miili yao baada ya shughuli zao za kawaida ambazo, wakati mwingine, ni ngumu na zinachosha.
(vi) Kuhimiza umuhimu wa kazi
Ndani ya miehezo ya watoto huwa kuna vitendo vinavyoiga kazi na amali mbalimbali zifanywazo na watu wazima, Kwa njia hii, watoto hujifunza umuhimu wa kazi.
(vii) Kuibua vipaji mbalimbali vya watoto
Uigizaji huibua vipaji vilivyolala kwa watoto wenye uwezo wa kuongoza, wengine wana vipaji vya kuongea, kuimba, kukimbia, kuruka kamba na vingmevyo. Vipaji hivyo huweza kujidhihirisha wakati wa michezo hiyo.
(viii) Kujenga kumbukumbu
Michezo ya watoto hubuniwa kichwani bila maandishi; kila mhusika hupaswa kutunga maneno au hotuba zake mwenyewe, kukumbuka maelezo ya wenzake, na kuwajibu bila kusahau au kukosea. Kwa njia hii, watoto hujifunza kuwa na kumbukumbu.
(ix) Kuchochea na kujenga ujasiri
Baadhi ya michezo huhitaji kiwango cha ujasiri na uthubutu. Kwa mfano, hujenga ujasiri wa namna ya kumkabili mtu mwenye nguvu anayemzidi, anayetaka kumuonea, pamoja na kutoogopa kushindwa.
(x) Kufundisha watoto majukumu ya baadaye katika maisha
Kama ilivyoelezwa hapo juu, watoto huchukua uhusika wa watu wazima katika michezo yao. Wengine huwa waume, wake, walezi wa watoto, wakulima, wawindaji, viongozi wa mtaa au kijiji na mengineyo. Kwa njia hii, watoto hujiandaa kuyabeba majukumu hayo pindi watakapokuwa watu wazima.
(xi) Kujenga uhusiano mwema miongoni mwa wanafamilia
Michezo ya watoto, mbali na kujenga uhusiano mwema miongoni mwa wanafamilia wenyewe, huweza kuwgpanua upeo kuhusu uhusiano unaopaswa kuwapo katika familia au ukoo kwa jumla. Mathalani, kati ya watoto na wazazi, na wazazi na wanandugu.
(xii) Kujenga moyo wa ushirikiano
Watoto wanapoigiza au kucheza pamoja hujenga urafiki na hujifunza kushirikiana katika kufanya mambo mbalimbali yenye umuhimu kwao na kwa jamii.
(xiii) Kujenga afya njema kwa watoto
Michezo ya watoto ni vitendo vinavyotumia mwili na akili. Watoto wanapoigiza huchakarika na kushughulika: husimama, huketi, hulala, huamka, hukimbia na kutembea. Shughuli zote hizi huwajengea afya kimwili na kiakili.
Changamoto za michezo ya watoto
Pamoja na dhima zilizoelezwa hapo juu, michezo ya watoto ina changamoto zifuatazo:
(i) Kupoteza muda wa kufanya shughuli nyingine, hasa kwa watoto wenye umri wa miaka saba na kuendelea. Watoto wa umri huu, wana majukumu mengine kama vile kazi za Shule na kazi ndogo ndogo za nyumbani.
(ii) Kusababisha mmomonyoko wa maadili, hasa kwa watoto wenye umri mkubwa kidogo, kuiga tabia na matendo yasiyoendana na umri wao.
(iii) Michezo minginehusababishakupotea kwa watoto, hasa kwawatoto waishio mijini, endapo watacheza michezo inayowapeleka mbali na nyumbani kwao.
(iv) Kusababisha migogoro kati ya watoto na watoto, wazazi na wazazi; pamoja na migogoro ya namna hii kutodumu, huweza kusababisha hasara fulani kama kuwekeana vinyongo.
(v) Kuibua tabia za ukatili, hasa watoto wakishiriki michezo yenye ubabe.
(vi) Kuhatarisha maisha ya watoto na kusababisha ajali hata kifo.
(vii)Maudhui yake huweza kuendeleza unyanyasaji na ubaguzi wa kijinsia.
Kazi ya kufanya
Soma mfano ufuatao wa ngonjera iitwayo "BAKITA" kutoka katika ki tabu cha Dakar( ya Elimu ya Ushairi (Amiri A.S. Andanenga, 2002: uk 117-119), kisha tunga ngonjera simulizi yenye bed zisizopungua sita.
BAKITA
Baraza la Kiswahili, lililokuja Dodoma,
Eti kuja kujadili, mambo ya leo na nyuma,
Mnalaumiwa kweli, mliyotenda si mema, Msizikwepe lawama. (Mbwezi)
Matawa ukome gubu, kwa tungo zenye viroja,
Ni Muhamedi Khatibu, ufunguzini kutaja, Bakita ni mahabubu,
kwa Lugha ni yenye tija,
Mbwenzi wacha kubwabwaja.
(Andanenga)
Nyote mlokokotwa, kimbelembeic kizima,
Nikipi mlichokutwa, kimyakimya kijitoma,
Dhamiri zenu zasutwa, imepungua heshima,
Hata kama washairi
(Mbwezi)
Kamwe hatulcuburutwa. donge Iinakusogoja,
Kwa barua tuliitwa, za kupandishwa daraja.
Wewe Mbwenzi umepetwa, tungo zako ni harija.
Walia kwa kukuchuja!
(Andanenga)
Kumuenzi Mathias, Mzee wetu wa zama.
Pasi kutujuza sisi, washairi wenye dhima,
Ni ukuu wa utusi. ni dalili ya dhuluma,
Mliyotenda si haki.
(Mbwezi)
Una dhima gani wewe, mambo ungaliyafuja,
Mathias ni wanawe, kizuka chake pamoja.
Walikuwa ndo wenyewe. tungefikwa na mauja,
Ungenusa tafrija.
(Andanenga)
Mngefanya huko huko, katu tusingeloloma.
Yanini malalamiko. mngekutana Kigoma,
Hamuepi maepuko, za haki hizi shutuma,
Mnashutumiwa hasa.
(Mbwezi)
Matawa siyo mzima. Kichwa chako kinavuja,
Mathias wa Dodoma, Mgogo si Muunguja,
Isingekuwa hekima. kumuenzia Miteja.
Kwa udaku wewe Meja.
(Andanenga)
Mnadhiki ya akili, dira zetu zikipima,
Vipimo vya maadili. utu na tabia njema
Dodoma si mafidhuli, hatuogopi kusema,
Hatuogopi kusema.
(Mbwenzi)
Asodhiki ya akili. pekee Mola mmoja,
Siwo nyinyi ngunubili. mlao na wenda haja.
Mbogo zcnu zimedhuti. kwcnyc uzembe watcja.
Wewe Mbwenzi ni Meneja.
(Andanenga)
Kitu gani kongamano, upuuzi na unyama,
Wa kupcana mikono. na mgcni wa hcshima.
Beti sita ya mabano, na hii ni kaditama,
Tutawaponda daima.
(Mbwenzi)
Waziri kwa zake hima. kwa kufungua akaja.
Na lsdori Shirima, kwa kufunga alikuja,
Wawavunjia heshima. tutosheleze kwa hoja.
Mbwcnzi kesi yakungoja. (Andonertga)
Utunzi wa kazi za fasihi simulizi
Katika mada ndogo ya şifa za fasihi simulizi, ulijifunza kwamba, kwa kawaida, kazi nyingi za fasihi simulizi ni mali ya jamii. Kazi za fasihi ni kazi za kisanaa; hivyo, utunzi wake unahitaji kuzingatia kanuni za sanaa inayohusika. Kwa hiyo, katika mada hii ndogo, utajifunza kanuni -mbalimbali za utunzi wa baadhi ya kazi za fasihi simulizİ.
Utunzi ni kazi inayohitaji umakini sana. Nİ muhimu kwa mtunzi kujua jamii anayoitungia kazi husika. Mtunzi ni mhakiki wa jamii yake katika masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Faida mojawapo ya utungaji wa kazi za fasihi simulizi ni kusawiri na kuhakiki uhalisi wa maisha ya jamii.
Jambo la kusisitiza hapa ni kwamba utunzi wa fasihi simulizi hutofautiana na utunzi wa fasihi andishi. Fasihi andishi hutungwa na mwandishi mahususi kwa kutumia kalamu na karatasi (au vifaa bora zaidi kama kompyuta). Mwandishi huyo hujiwekea malengo na kuamua maudhui anayotaka kuyatoa. Akishaandika mswada Wake, huweza kuusoma tena kwa makini na kuudurusu au kuusahihisha ili ufikie kiwango anachokitaka. Huweza pia kumpa mtu mwingine amsomee na kumpa maoni au kupendekeza marekebisho. Kwa upande mwingine, mtunzi wa fasihi simulizi ana fursa finyu ya kufanya hivyo. Hivyo, kazi yake hufungamana na muktadha wa utendaji au uwasilishaji. Baadhi ya kazi za fasihi simulizi zinazopata umaarufu huendelea kutumika katika jamii huku zikirekebishwa na kubadilishwa kulingana na wakati.
Utunzi wa fasihi simulizi hutofautiana kwa kutegemea kipera kinachotungwa. Mathalani, utunzi wa nyimbo mara nyingi hutokea wakati wa ngoma au tukio mahususi. Manju huibua wimbo kulingana na muktadha na mahitaji ya wakati huo. Utunzi wa fani nyingine za kishairi, kama tendi na majigambo, huweza kuwa na michakato mirefu zaidi inayoongozwa na kanuni za utunzi simulizi. Utendi au majigambo huweza kuandaliwa kwa kipindi fulani na kufanyiwa mazoezi kabla, na hatimaye kuwasilishwa hadharani.
Kwa upande wa ngano, ni vigumukujua wakatizinapotungwa. Nyingi hupokewa kutoka vizazi vilivyotangulia, na hubadilika kidogo wakati wa kusimuliwa kulingana na mahitaji ya _muktadha huo. Vilevile, semi hupokewa kutoka kwa wahenga na kurekebishwa kidogo kidogo kutegemea muktadha. Semi mpya, zikiwamo methali na vitendawili, huibuka wakati wowote; lakini ni vigumu kujua mtunzi kwa kuwa hazitungwi kwa kukusudia, yaani hakuna tukio mahususi la utungaji wa methali au vitendawili, japo linaweza kuwapo tukio la utambaji wa vitendawili. Methali ni fani tegemezi ambayo huegemezwa kwenye fani nyinglne kama hotuba, simulizi na nyinginezo.
Kanuni za utunzi wa kazi za fasihi simulizi
Katika utunzi wakazi za fasihi simulizi, mtunzi nilazima awe najambo linalomgusa kwa kumfurahisha au kumkera. Baada ya kuwa na jambo linalomgusa, mtunzi huliweka jambo hilo hadharani kwa kutunga kazi ya fasihi simulizi. Mtunzi huamua kuhusu fani inayofaa kutumika. Aidha, uamuzi wa fani ya kutumia hutegemea ujuzi na kipaji cha mtunzi katika fani inayohusika.
Utunzi wa hadithi
Hadithi ni masimulizi yaliyopangiliwa katika mfuatano fulani wa matukio yanayoambatana na matendo ya wahusika. Hadithi hutoa ujumbe fulani katika jamii. Kwa kawaida, hadithi huwa katika lugha ya mjazo. Mtunzi wa hadithi ni lazima azingatie kanuni mbalimbali katika utunzi wake. Takribani hadithi zote, ziwe simulizi au andishi, huwa na mambo yafuatayo:
(a) Mfuatano wa matukio yaliyopangiliwa kiwakati au bila kufuata wakati na yenye ukamilifu wa kimasimulizi na kiujumi.
(b) Muundo wenye mwanzo, kati na mwisho. Mpangilio wa matukio yanayosimuliwa kwa namna inayodhihirisha usababishano na hivyo kujenga mgogoro na taharuki.
(c) Wahusika wenye kuwakilisha pande mbiliau zaidi zamgogoro wa hadithi na ambao mahusiano na matendo yao ndiyo husukuma mbele hadithi kuelekea kileleni.
(d) Matumizi ya lugha ya masimulizi na maelezo ili kusawiri matukio na migogoro ya hadithi.
(e) Maudhui (mawazo, dhamira,mafunzona falsafa) yanayoibuliwanamuundos msuko na lugha inayotumika.
Haya ni mambo ya jumla yanayotarajiwa kuwamo katika hadithi, iwe simulizi au andishi. Kwa kuwa hapa tunazungumzia utunzi wa fasihi simulizi, ni muhimu pia kuzingatia mambo mahususi yanayohusu utunzi simulizi tu.
Mambo hayo ni:
(i) Kutokuandikwa;
(ii) Utungaji kichwani kabla ya tukio au papo kwa papo;
(iii) Ufungamano na muktadha; na
(iv) Upokezi na urithishwaji.
Ni vigumu kutunga ngano au Lhekaya papo kwa papo. Kinachoweza kufanyika ni kuandaa mazingira ya uwasilishaji au utambaji wa hadithi hadharani kutokana na kumbukumbu za watambaji. Kufuatia kutamba ngano hizo, watambaji watakuwa wanatunga kwa maana ya kuziumba upya kwa maneno yao wenyewe, huku wakizihusisha na muktadha husika. Utambaji huo unapaswa kuzingatia taratibu zake zinazofahamika katika jamii husika. Taratibu hizo ni pamoja na: namna ya kuanza (mianzo).
Mwanzo huweza kuwa:
| | Mtambaji: | Paukwa |
| Hadhira: | Pakawa | |
| Mtambaji: | Hapo zamani za kale. . . | |
| (ii) | Mtambaji: | Hadithi hadi thi |
| Hadhira: | Hadithi njoo, uongo njoo, utamu kolea. | |
| Mtambaji: | Hapo zamani za kale | |
| Hadhira: | Eeeh! | |
| (iii) | Mtambaji: | Alitokeani... |
| Hadhira: | Naam twaib! | |
| Mtambaji: | Alitokeani.. | |
| Hadhira: | Naam twaib | |
| (iv) | Kaondokea chanjagaa Kajenga nyumba kakaa Mwanangu Mwanasiti Kijino kama kijiti Cha kujengea kikuta Na vilango vya kupita. | |
| (v) | (v) Hapo kale alikuwako/walikuwako... Na, mwisho unaweza kuwa: (i) Wakaishi raha mustarehe... (ii) Ndiyo maana mpaka leo. (Paka na panya hawapendani au mbwa na mwanadamu ni marafiki, n.k.) (iii) Nahadithi yangu imeishia hapo... | |
Utunzi wa ushairi
Ushairi simulizi una vipera vya nyimbo, mashairi, ngonjera na maghani. Vipera vyote hivi vinapotungwa kisimulizi, hutungwa kichwani bila kuandikwa na kuwasilishwa hadharani kwa kusemwa, kuimbwa, kutambwa au kughanwau Watunzi wa vipera hivi walioathiriwa na ushairi andishi huweza kutunga kwa kufuata kanuni za urari wa vina na mizani, na bado tungo zao zikawa simulizi endapo hazitaandikwa.
Kwa kuwa ushairi simulizi hautungwi kwa kuandikwa, inabidi ufanywe darasani au shuleni kwa vitendo. Mathalani, wakati wa sherehe za Shule au darasa, wanafunzi wanaweza kuhamasishwa kutunga na kutamba ngonjera, shairi au maghani mbele ya wenzao. Kama kuna uwezekano, ala za muziki au muziki wa ala uliorekodiwa kabla, unaweza kutumika. Katika utunzi simulizi, matumizi ya lugha, hasa tamathali, ishara na mafumbo hupewa uzito. Vilevile, msanii hujizoeza kuongea au kuimba mbele ya watu, na namna ya kushirikisha hadhira katika utambaji wake.
Mtunzi wa maghani kama majigambo na tendi huongozwa na kaida za sanaa hiyo katika jamii inayohusika. Kwa mfano, muundo wa majigambo katika jamii ya Wahaya hutakiwa uzingatie yafuatayo: jina halisi au la sifa (lakabu) la mjigambi; nasaba na mbari yake upande wa baba; jina la mama yake nanasaba yake; matendo ya ushujaa aliyoyafanya na namna alivyoyatekeleza; hitimisho na kujikabidhi kwa mtemi au kiongozi.
Mtunzi wa tendi sharti afanye utafiti kidogo kuhusu tukio au historia anayotaka kuisimulia. Baada ya kupata taarifa za kutosha, hujaribu kuzisimulia (bila maandishi) kwa kutumia mbinu mbalimbali za kisanaa kulingana na jamii inayohusika.
Utunzi wa maigizo (sanaa za maonesho)
Maigizo ni kipera muhimu cha sanaa za maonesho. Kuna maigizo ya watoto na maigizo ya watu wazima. Maigizo yote hayo ni faraguzi; hutungwa kichwani na hayaandikwi. Kwa kawaida waigizaji hujitungia maneno yao wenyewe wawapo jukwaani. Jambo la muhimu ni kuwa na hadithi au tukio la kuigiza lenye wahusika, mwanzo, kati na kilele. Waigizaji huchagua uhusika wao na kufanya mazoezi hadi wanapojiridhisha kuwa igizo liko tayari kuoneshwa hadharani. Igizo linaweza kuhusu jambo lolote linalowagusa, kuwakera au kuwafurahisha watu. Kwa mfano igizo kuhusu tatizo la utoro shuleni, uhalifu na kadhalika.
Mbali na utaratibu wa kifaraguzis igizo simulizi lina sifa kadhaa za igizo andishi la kitamthiliya, kama vile wahusika wanaokinzana, mgogoro, mazungumzo na vitendo. Mambo haya sharti yazingatiwe.
Utunzi wa semi
Kama ulivyokwishajifunza, semi ni tungo fupifupi zenye kutumiapicha, tamathali na ishara ili kutoa ujumbe. Ni mafumbo yanayosawiri mandhari kulingana na kipera husika. Semi hueleza mambo kwa muhtasari.
Semizinazozungumziwa hapa niza ainambili: methali na vitendawili. Tunazitumia kuwakilisha serm zote kwa jumla. Kanuni ya msingi katika utungaji wa semi ni kwamba hakuna utaratibu rasmi wa kutunga, bali huibuka katika miktadha mahususi au hupokewa kutoka kwa wahenga. Mathalani, methali huwa katika kumbukumbu za wanajamii kwa muda mrefu na hujitokeza katika matumizi pale tu zinapohitajika. Ifuatayo ni mifano ya methali zinazoweza kukumbukwa na kutumiwa katika miktadha mbalimbali:
(i) Uzuri wa mkakasi, ndani kipande cha mti.
(ii) Mwenda tezina omo, marejeo ni ngamani.
(iii) Ng'ombe akivunjika mguu malishoni, hujikokota zizini.
(iv) Simba mwenda kimya, ndiye mla nyama.
Vilevile, vitendawili huibuka au kukumbukwa wakati wa utendaji wake, maana vyenyewe vina fursa za kutendwa. Mara nyingis utendaji wa vitendawili hufanywa na watoto, na huwa ni aina ya chemshabongo. Ifuatayo ni mifano ya vitendawili.
(i) Hawapandi wala hawatafuti chakula lakini wanashiba - mdomo na tumbo
(ii) Adui mpenzi -moto.
(iii) Mgonjwa wa ndui ananing'inia mtini—fenesi.
(iv) Tunda langu la ajabu; juu nyama, katikati ngozi, ndani mehanga firigisi.
Njia za uwasilishaji na uenezaji wa fasihi simulizi
Fasihi simulizi huwasilishwa na kuenezwa kwa njia ya mdomo na utendaji. Hii ndiyo njia ya mwanzo kabisa kutumika. Katika njia hii, masimulizi huhifadhiwa kichwani, kisha huwasilishwa kwa hadhira kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Kwa mfano masimulizi ya hadithi, hufanyika kwajamii au familia. Watu wazima hasa babu au bibi, hukaa pamoja jioni sehemu yenye molo kutegemea na mazingira na kuwasimulia watoto hadithi mbalimbali. Utendaji mbele ya hadhira ndiyo njia kuu ya kuwasilisha na kueneza fani za fasihi simulizi.
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamesaidia sana katika uwasilishaji na uenezaji wa fasihi simulizi. Maendeleo haya yamewezesha kuwapo kwa vyombo mbalimbali vya uwasilishaji kama redio, runinga na simu. Redio na runinga zimekuwana mchango mkubwakatika uwasilishaji na uenezaji wakazi za fasihi simulizi. Redio Tanzania (kwa sasa TBC Taifa) imekuwa na vipindi ambavyo vimesaidia sana fasihi simulizi kuwafikia watu wengi. Kipindi kama vile Mama na Mwana kilipendwa na watu wengi, hasa watoto, kwa sababu ya masimulizi ya hadithi mbalimbali. Kipindi kingine ni Cheichei Shangazi ambacho kimekuwa na masimulizi ya hadithi, vitendawili na nyimbo. Aidha, kuanzishwa kwa vituo vingine vya redio kumeongeza mawanda ya uwasilishaji na uenezaji wa kazi za fasihi simulizi. Kwamfano Redio One Stereo, hurusha kipindi cha Watoto Wetuambacho hupambwa na wimbo maarufu wa Watoto Wasqfi Moyoni. Kipindi hiki hurushwa kila Jumamosi, ambapo watoto walioko studio na nyumbani huweza kushiriki katika uwasilishaji wa hadithi, methali, vitendawili, mafumbo na nyimbo.
Pamoja na watoto kutoonana ana kwa ana wanaweza kushiriki kwa njia ya kusikiliza. Hivyo, hadithi ambazo awali zilisimuliwa kwa watu wachache, zinaweza kujulikana kwa wote wanaosikiliza. Mbali na vipindi vya watoto, redio zimekuwa zikirusha vipindi vingrne vya fasihi simulizi. Baadhi ya vipindi hivyo ni Mkoa kwa Mkoa, Malenga Wetu, Ngoma Zetu, Zilipendwa, Salamu kwa Wagonjwa, Mchana Mwema (TBC Taifa), Hi-i Nazo (Redio One Stereo), Kwa Raha Zetu (Redio Clouds FM) na Mitikisiko ya Pwani (Times FM).
Kwa upande wa runinga, uwasilishaji umekuwa tofauti kidogo. Katika runinga washiriki wana fursa ya kuona matendo yanayotendwa. Kama ilivyo kwenye redio. Pia katika runinga kuna viprndi vya watoto ambamo kazi za fasihi simulizi huwasilishwa. Mfano wa vipindi hivyo ni Bongo Kids (TBC I ) ambacho kinahusu somo la hisabati lakini huwa na matumizi ya nymbo na wahusika ambao ni wa fasihi simulizi. Aidha, kituo cha ITV hurusha kipindi cha Watoto Show ambacho hujuimusha nyimbo, ngoma, methali, vitendawili na hadithi. Hali kadhalika, runinga zimekuwa zikirusha vipindi kama vile, Mizengwe, Sanaa na Msanii, Mashamushamu ya Pwani na Hawavumi lakini Wamo (ITV); Futuhi, Bongo
Beats na Msanii Wetu (Star TV) Fataki, Ngoma Zetu, Mchikicho wa Pvvani Club Raha Leo Show (TBCI) na Mirindimo ya Pwani (Channel Ten). VIPindi vyote hivyo vimekuwa vikisaidia uwasilishaji na uenezaji wa fasihi simulizi.
Matumizi ya simu nayo yana mchango mkubwa katika jamii. Watu wengi hutumia simu kwa mawasiliano ya mazungumzo. Kuwapo kwa mawasiliano ya mitandao ya kijamii kwa kutumia simu kumewezesha uwasilishaji na uenezaji wa fasihi simulizi. Baadhi ya simu zina uwezo wa kurekodi na kutuma nyimbo, masimulizi na picha. Pia, zina uwezo wa kunasa vituo mbalimbali vya redio na runinga na, hivyo, kuwawezesha watumiaji wake kusikiliza kazi za kifasihi.
Matamasha mbalimbali yamesaidia kukuza na kueneza fasihi simulizi. Kwa mfano, Tamasha la Sauti za Busara ambalo hufanyika kila mwaka visiwani Zanzibar, hujumuisha washiriki wa fani mbalimbali za fasihi simulizi kutoka ndani na nje ya Tanzania. Kupitia tamasha hili, kazi mbalimbali za fasihi simulizi huwasilishwa na kuenezwa.
Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, fasihi simulizi pia imekuwa ikiwasilishwa kwa njia ya maandishi. Hii inatokana na fasihi kuhifadhiwa katika vitabu na machapisho mbalimbali, hivyo kuifikia hadhira kwa njia ya maandishi. Njia hii ya uwasilishaji huwatenganisha fanani na hadhira. Mifano ya vitabu vya fasihi simulizi ni: Kuku, Njiwa, Kicheche na Hadithi Nyinginezo (Abasi, 1996), Mkia wa Chura (Baitu Richard, 2002) na mfululizo wa Fasihi Simuliziya Mtanzania -Hadithi, Methali na Jätendawili (TUKI, 1976).
Pia, baadhi ya magazeti, yamekuwa na makala maalumu za watoto ambazo, mara nyingi, huwa na kipengele cha fasihi simulizi, hususani hadithi. Kwa njia hiyo, fasihi simulizi huwasilishwa na kuenezwa.
Athari za sayansi na teknolojia katika fasihi simulizi
Kama ilivyoelezwa katika kipengele kilichotangulia, kuna njia mbalimbali za uwasilishaji na uenezaji wa fasihi simulizi. Nj ia ambazo zimetokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia zina athari kwa fasihi simulizi. Uwasilishaji na uenezaji wa fasihi simulizi kwa njia ya redio hauwawezeshi wasikilizaji kuona matendo yanayotendeka kwa sababu fanani na hadhira hawaonani ana kwa ana.
Katika njia ya runinga na simu, watazamaji hushindwa kushiriki anakwa ana. Watazamaji hushindwa kuuliza maswali, hasa kwa wale ambao hawana simu. Kuna changamoto ya gharama kwani si kila mtu ana uwezo wa kununua runinga na simu. Vilevile, matumizi yaruninga huhitaji kifaa kijulikanacho kama kisimbuzi. Kifaa hiki huhitaji fedha kulipia huduma za vituo mbalimbali. Hata hivyo, pamoja na changamoto hizi, fasihi simulizi imepata sura mpya katika uwasilishaji na ueneaji wake tofauti na awali ilipokuwa inawasilishwa kwa njia ya mdomo tu.
Uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi
Uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi una manufaa makubwa kwa jamii. Kazi za fasihi zilizohifadhiwa kwa njia mbalimbali kama sidii na machapisho huwasaidia wanajamii kujifunza kuhusu fasihi simulizi. Pia, kazi hizo hutunza kumbukumbu za jamii; hivyo, huwawezesha wanajamii kujifunza historia ya jamii yao. Kutokana na uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi, watafiti hupata data ambazo husaidia kufikia mahitimisho na kupata matokeo ambayo hutumika katika shughuli za maendeleo. Hivyo, ni vema kuhifadhi na kutunza kazi mbalimbali za fasihi simulizi.
Mbinu za kuhithdhi kazi za fasihi simulizi
Kuna mbinu mbalimbali za kuhifadhi kazi za fasihi simulizi. Zifuatazo ni miongoni mwa mbinu hizo:
(a) Kuhiftdhi kiamali
Njia kuu na bora zaidi ya kuhifadhi fasihi simulizi ni kuitenda na kuitumia katika maisha ya kawaida ya kila siku. Huko ndiko kunaitwa kuhifadhi kiamali, yaani kuifanya iwe sehemu ya maisha. Hii ni kwa kuwa uhai wa fasihi simulizi hutegemea muktadha na matumizi. Fasihi simulizi hukua na kudumu inapohitajika na kutumika katika jamii, vinginevyo hufifia na hatimaye hufa.
(b) Kuhifadhi kichwani
Njia hii ni kongwe kuliko njia zote kwani ilianza tangu fasihi simulizi ilipoanza. Katika njia hii, fanani huhifadhi yale anayoyajua kichwani mwake. Baadaye, huyasimulia kwa wengine. Kwa kutumia njia hii, fasihi simulizi imekuwa ikisimuliwa kizazi hadi kizazi. Njia hii humpa fanani ujuzi wa kuhifadhi mambo anayoyajua. Kwa upande mwingine, usimuliaji huweza kubadilika kama fanani atapoteza uwezo wa kutunza kumbukumbu na kusimulia.
(C) Kuhifadhi katika maandishi
Fasihi simulizi huweza kuhifadhiwa katika maandishi baada ya fanani kusimulia. Njia hii inasadia kuhifadhi kazi kwa muda mrefu. Njia hii ni ya gharama kwa sababu huhitaji vitendea kazi wakati wa kuandika, mahali pa kuhifadhi na msomaji ni lazima anunue kazi hizo. Aidha, njia hii huifanya kazi ya fasihi simulizi kuwa mali ya mtu binafsi.
(d) Kuhifadhi katika vinasa sauti
Hizi ni mbinu ya kutumia vifaa vya kurekodi sauti. Njia hii huruhusu kurekodi sauti za alazinazotumika katika kazi husika. Kwa mfano nyimbo, huambatana na mlio wa ngoma, Ubora wa mbinu hii ni kuwawezesha watu kusikia sauti hata kama hawaoni vitendo. Njia hİi ina gharama ya kununua vinasa sauti pamoja na vifaa vya kusikilizia kama vile redio.