FORM ONE ELIMU YA DINI YA KIISLAMU EXAMS SERIES

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA NUSU MUHULA

KIDATO CHA KWANZA

021 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU

Muda Saa: 2:30 Septemba, 2026

Maelekezo

  1. Upimaji huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali Kumi (10)
  2. Jibu maswali yote kwenye nafasi ulizopewa.
  3. Andika kwa kutumia kalamu yenye wino wa bluu au mweusi
  4. Vifaa vyote vya mawasiliano na vitu visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani
  5. Andika jina lako kamili katika kila ukurasa sehemu ya juu ya karatasi

SEHEMU A (ALAMA 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. Chagua jawabu sahihi kisha Andika herufi ya jawabu katika kitabu chako cha kujibia

(i) Kwa mujibu wa uislamu, mtu aliye elimika anajitofautisha na wasioelimika kwa sifa hii

  1. Mtu mwenye alama za ufaulu katika vyeti
  2. Mtu mwenye uwezo wa kuchambua na kuelezea
  3. Mtu mwenye ujuzi unaoambatana na utendaji
  4. Mtu anaesoma sana vitabu

(ii) Hutokea iwapo Nun-sakinah na Tanwiin zitakuja kabla ya herufi sita za idh-haar

  1. Idh-haar
  2. Idghaam
  3. Iqlaab
  4. Ikhfaau

(iii) Katika uislamu kufuata sunnah ni utekelezaji wa shahada ya pili . Ni ipi kati ya zifuatazo ni dhana sahihi kuhusu sunnah?

  1. Kuswali qablaya na baadiyyah
  2. Mwenendo au tabia ya Mtume (S.A.W)
  3. Upweke wa ALLAH (SW)
  4. Kumuamini Mtume (S.A.W)

(iv) Jambo gani ni lazima kutekeleza katika mchakato wa kumuosha maiti

  1. Kuanz ana kumuweka maiti udhu
  2. Kutumia maji ya kisima au mto
  3. Kutumia kitanda kilichotobolewa
  4. Kumfunika maiti kwa shuka gubigubi mwili nzima

(v) Wahyi wa kwanza kumshukia Mtume (S.A.W) ulisisitiza juu ya jambo gani

  1. Kujielimisha kwa ajili ya Allah (S.W)
  2. Kumuamni ALLAH (S.W) pekee
  3. Kumcha ALLA (S.W) katika maisha
  4. Kulingania Uislamu katika jamii

(vi) Bwana Bakari anajizuia na vyakula vizuri, anavaa nguo chakavu na kuishi katika nyumba isiyo na sakafu, akiamini kuwa kufanya hivyo ni kujikurubisha zaidi kwa Mungu . Bwana Bakari atakuwa ameathiriwa na mfumo gaani wa maisha?

  1. Uislamu
  2. Uyahudi
  3. Utawa
  4. Ukristo

(vii) Mwanaadamu analazimika kuisoma Qur’an kwa kuzingatia lengo kuu. Ni lipi lengo la kitabu hicho ?

  1. Kusomwa mara kwa mara
  2. Kutumika katika swala
  3. Kuongoza maisha ya watu
  4. Kufundisha Tawhiid

(viii) Ni nguzo ya tano miongoni mwa nguzo za Uislamu ambayo hufanywa katika miezi maalum kwa mwenye uwezo

  1. Kufunga Ramadhani
  2. Kuhiji Makkah
  3. Kutoa zakat
  4. Kupigana jihad

(ix) Sentensi ipi inabainisha njia zilizotumika kuhifadhi Qur’an wakati wa Mtume (S.A.W)

  1. Kufundisha na kuhifadhi kichwani
  2. Katika vifua na katika maandishi
  3. usomwa ndani ya msikiti
  4. Kuandikwa na kubandikwa Al-kaaba

(x) Hadithi ndio njia kuu inayotumika kuhifadhi sunnah ya Mtume (S.A.W) Katika zama hizi. Ni ipi kati ya dhana zifuatazo ni sahihi kuhusu hadithi

  1. Tamthilia za watu wa kale
  2. Historia zilizoandikwa vitabuni
  3. Simulizi au taarifa juu ya sunnah ya Mtume (S.A.W)
  4. Mwenendo au tabia ya Mtume

MAJIBU

i ii iii iv v vi vii viii ix x









.

2. Oanisha nyakati mahsusi za swala kulingana na mwenendo wa jua katika orodha A na majina ya swala zinazotekelezwa katika nyakati hizo katika orodha B kisha Andika herufi ya jawabu sahihi kwa kila kipengele.

ORODHA  ORODHA B
  1. Kuanzia jua linapozama hadi pale mawingu mekundu yanapobadilika
  2. Baada ya jua kugeuka upande wa magharibi hadi pale urefu wa kivuli unapokuwa sawasawa na kitu halisi
  3. Kuanzia pale ambapo alama ya mstari mweupe unapojitokeza upande wa mashariki hadi mwangaza unapodhihiri
  4. Kuanzia mawingu yanapobadilika na kuwa ya njano hadi usiku wa manane
  5. Kuanzia urefu wa kivuli unapokuwa sawa na kitu halisi hadi kivuli kinapokuwa maradufu ya urefu wa kitu halisi
  1. Al-ishaa
  2. Al-fajr
  3. Al-asr
  4. Adhuhuri
  5. Maghrib
  6. Qabliya
  7. Baadiya

MAJIBU

ORODHA A i ii iii iv v
ORODHA B




SEHEMU B (Alama 70)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. Aya zifuatazo za suratul-Ikhlasw (112:1-4) zimechanganywa . Pangilia kwa usahihi kama ilivyoshuka katika Qur’an.

  1. Hakuzaa wala hakuzaliwa
  2. Sema, yeye ni Allah mmoja tu
  3. Wala hana anayefanana naye hata mmoja
  4. Allah tu ndiye anastahiki kukusudiwa

4.a) Allah anasema “Na anayetaka dini nyengine isiyokuwa Uislamu basi haitokubaliwa kwake. Naye akhera atakuwa katika wenye khasara” Qur’an (al-Imran :85). Aya hii inaonyesha dini zilizobuniwa na watu. Bainisha dini hizo

b) Elezea hatua za kushuka Qur’an

5. a) Eleza kwa kutoa hoja mbili(02) kwa nini ni muhimu kufauta sunnah ya Mtume (S.A.W) katika maisha ya kila siku

b) wewe kama mtaalamu wa sunnah na hadithi elezea tofauti tatu(03) zilizopo baina ya sunnah na hadithi

6.a) Suratul-faatihah imepewa majina mbalimbali kutokana na maudhui yanayopatikana ndani yake. Bainisha Majina Matano ya suratul-faatiha

b) Wanafunzi wengi wanaosoma elimu ya dini ya kiislamu hawaelewi uhusiano uliopo baina ya elimu ya dini ya kiislamu na masomo mengine. Wewe kama mtaalamu wa kidato cha kwanza wawafafanulie uhusiano uliopo kwa hoja tatu

c) Elezea sababu mbili zinazoruhusiwa na uislamu kwa mtu kutayammamu

7.a) Mtume (S.A.W) ametufahamisha kuwa uislamu umejengwa juu ya nguzo tano . Fafanua nguzo hizo kwa mpangilio.

b) Wakati ukiwa shule mzazi wako alipaiga simu kwa Mwalimu wako na kumtaarifu kuwa Jirani yenu amafarki na hakuna mwenye elimu ya kuosha maiti isipokuwa wewe mtaani kwenu, mama akaomba ruhusa ya wewe Kwenda kuosha maiti. Elezea hatua kwa hatua namna utakavyomuosha maiti huyo.

8.a) Bainisha makundi ya najisi na mifano yake

b) Bainisha namna ya kujitwaharisha kwa kila kindi

c) Elezea maana ya hedhi, nifasi na janaba

  1. Hedhi
  2. Nifasi
  3. Janaba

9. a) Shirki imegawanyika katika makundi mawaili. Bainisha makundi hayo

b) Mtu anae mshirikisha Allah (S.W) atajidhihirisha maeneo matatu. Fafanua maeneo hayo

SEHEMU C (ALAMA 15)

Jibu swali la kumi (10)

10. Juma hatekelezi ibada ya swala kwa sababu anasumbuliwa na maradhi mbalimbali. Kama mwanafunzi wa kidato cha kwanza, toa elimu kwa Juma namna gani mgonjwa anaweza kutekeleza swala za faradhi.

FORM ONE EDK EXAM SERIES 284  

FORM ONE EDK EXAM SERIES 284  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256