OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA ROBO MUHULA WA PILI KIDATO CHA NNE
015 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU
(Kwa watahiniwa walioko na wasiokuwa shuleni)
Muda: Saa 3 — SEPTEMBA 2026
Maelekezo
SEHEMU A (Alama 16)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Chagua jibu sahihi katika kipengele cha (i) – (x) kisha andika herufi yake katika kijitabu chako cha kujibia.
(i) Mtu aliyeelimika anatofautiana vipi na yule ambaye hajaelimika?
(ii) Ni kwa namna gani wanadamu wanahisi uwepo wa Allah (S.W) katika maisha yao?
(iii) Kwa mujibu wa Uislamu, kwanini haiwezekani mtu kuishi bila ya kuwa na dini?
(iv) Njia ipi inakamilisha kupatikana kwa Ijtihadi kama msingi wa sharia za Uislamu?
(v) Ni lipi lengo kuu la kuamrishwa kusimamisha nguzo tano za Uislamu?
(vi) Muandaaji wa sanda ya mtoto anapaswa kuzingatia jambo gani kati ya haya?
(vii) Nuun Sakna au Tan wiin inapokutana na Yaaun inapatikana hukumu gani?
(viii) Bwana Mikebe anamiliki dhahabu gramu 150 iliyokidhi vigezo vyote vya kutolewa Zakat. Gramu ngapi za dhahabu anapaswa kutoa kama Zakat?
(ix) Ni yapi makusudio ya kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani?
(x) Bani israil ni kizazi cha nabii yupi?
2. Oanisha sifa za swala za Sunnah zilizo katika Orodha A na swala za Sunnah husika zilizo katika Orodha B. kisha jaza herufi yake katika kijitabu cha kujibia.
| ORODHA A | ORODHA B |
|---|---|
| A. Swalatu dhuhaa B. Swalatul Kusuf C. Swalatul Haajah D. Walaatul Witr E. Swalatul-Istisqaa F. Swalatul Tawbah G. Swalatul Idd H. Swalatul Istikharah |
SEHEMU B (Alama 54)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
3. Uislamu ulileta mageuzi makubwa kuhusu utumwa ukizingatia hali ilivyokuwa mbaya kabla ya Mtume Muhammad (SAW). Ukiwa kama mwanahistoria ya dini ya Kiislamu, thibitisha Kwa hoja sita namna hali ilivyokuwa kipindi hicho kabla ya mjumbe wa Allah (S.W) kuletwa kufanya ukombozi.
4. Baada ya kusikia watu wakisema kuwa Uislamu haumthamini mwanamke, Zainabu alimuuliza mwalimu wake ili kutaka kufahamu kama kweli mwanamke hathaminiwi katika Uislamu. Kama mwanafunzi wa dini ya Kiislamu, eleza hoja sita alizopewa Zainab na mwalimu wake.
5. Baada ya Mtume Muhammad (S.A.W) kufariki, makundi mbalimbali ya harakati yaliibuka kuhuisha Uislamu. Kwa kutumia makundi yaliyoanzishwa mnamo Karne ya 20 A.D, chambua mafunzo matatu ambayo Waislamu wa zama za sasa wanapaswa kuishi nayo.
6. Baadhi ya watu katika jamii wanadai kwamba mkataba wa Hudaybiya haukuwanufaisha Waislamu. Kosoa madai ya watu hao kwa kutumia hoja sita.
7. Wanafunzi wa kidato cha nne wanajadili uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2025 nchini Tanzania. Mwalimu wao anawaelekeza kutazama uchaguzi huo kwa jicho la Kiislamu, kwa kuzingatia sifa za viongozi wanaofaa kuchaguliwa ili kuongoza kwa haki na uadilifu. Eleza sifa sita za kuzingatia katika kuwachagua watu hao.
8. Wanafunzi wa kidato cha nne wanajadili sababu zinazomfanya Muislamu ajiepushe na shirki. Mwalimu anasisitiza umuhimu wa kuelewa dhana ya shirk na aina zake ili kuimarisha Tauhidi. Fafanua aina tatu za dhana hiyo.
SEHEMU C (Alama 30)
Jibu maswali mawili (2) tu katika sehemu hii.
9. Baada ya kusoma Suratul Asr, Zuberi alijiuliza: “Je, sura hii fupi ina ujumbe gani mkubwa kwa Waislamu? Tumia nukta nne kumueleza mafunzo yanayopatikana katika Suratul hiyo.
10. Katika kikao cha vijana wa Kiislamu, mmoja wao alidai kwamba kwa kuwa kuna kitabu cha Qur’ani hakuna ulazima wa kufuata mwenendo wa Mtume Muhammad (S.A.W) katika maisha ya kila siku. Kwa kutumia hoja nne, kosoa dai hilo kwa kuonesha umuhimu wa kufuata mwenendo huo katika maisha ya Muislamu.
11. Katika hotuba ya Swala ya Ijumaa, khatibu aliwasisitiza Waislamu kuwa funga si tu ni ibada ya kujizuia kula na kunywa, bali pia ni njia ya kukuza ucha- Mungu na maadili ya jamii. Kwa kutumia hoja nne, fafanua namna ibada hiyo inavyosaidia kukuza ucha-Mungu na maadili ya jamii.
FORM FOUR EDK EXAM SERIES 265
FORM FOUR EDK EXAM SERIES 265
OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA NUSU MUHULA - KIDATO CHA NNE
015 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU
(Kwa watahiniwa walioko na wasiokuwa shuleni)
Maelekezo
SEHEMU A (Alama 16)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Katika kipengele (i) – (x), chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake katika kijitabu chako cha kujibia.
i) Kwanini Waislamu wa leo wanapaswa kuipa elimu kipaumbele?
ii) Umeombwa kuwaelezea wanafunzi wenzio kuhusu historia ya madhehebu ya Ki-Fiqh. Utachagua yapi kati ya haya kutekeleza jambo hilo?
iii) Kosa gani walilofanya watu wa Madyan tu ambalo hadi sasa linafanywa?
iv) Mwalimu amekusimamisha useme ulichojifunza kutokana na maandalizi ya kimafunzo ya Mtume wa mwisho. Utasema lipi kati ya haya yafuatayo?
v) Bwana Mbundu ni mwanasayansi anayetaka kuanzisha mfumo wa maisha utakaowasaidia watu wote kuishi kwa raha kwa kutumia ujuzi wake, lakini akaambiwa hawezi kufanya hivyo. Kwanini bwana huyu asiweze?
vi) Kwa ujumla kanuni zinazotumika kuweka sheria za Kiislamu hujulikana kwa jina gani?
vii) Bwana Ngugu ametokewa na jambo fulani mchana wa Ramadhani lakini
akaambiwa funga yake haijaharibika. Bwana huyu ametokewa na nini?
viii) Muandaaji wa sanda ya mtoto wa kike anapaswa kuzingatia jambo gani kati ya haya?
(ix)
Nuun Sakna ) ((Ù† au (Tan wiin) inapokutana na Qaaf yenye fat-ha inapatikana hukumu gani?
x) Bwana Ng’ombo anamiliki mbuzi na mbuzi 40. Baada ya kupinduka mwaka nini anapaswa kutoa kama Zakat katika hiki alichonacho?
2. Oanisha maelezo ya shahada yaliyo katika Oradha A na aina za shahada zilizo katika Orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihih katika kijitabu chako cha kujibia.
| ORODHA A | ORODHA B |
|
|
SEHEMU B (ALAMA 54)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
Jibu maswali yote katika sehemu hii. Andika majibu yako kwa ufupi na ufasaha.
3. Wewe kama Muislamu unapaswa kuvifanyia nini viungo vyako vifuatavyo?
4. Tumia hoja tatu kuwafafanulia wanajamii wa mtaani kwako ni kwa namna gani mahari inaweza kushusha hadhi ya mwanamke?
5. Umekutana na vijana watatu wanaotetea sheria zilizotungwa kwenye mabunge mbalimbali kuwa hazina kasoro.
6. Wayahudi walifanya jitihada kubwa ya kuuzima Uislamu Madinah kwa kufanya vitimbi mbalimbali dhidi ya Dola na Waislamu. Wewe kama khatibu wa Ijumaa wafahamishe Waumini wa msikitini hapo mambo sita hayo ili waweze kuchukua tahadhari na wanaofanana na hao.
7. Umekaribishwa katika mjadala wa wasioamini siku ya mwisho kwa kutoa hoja zao mbalimbali. Wathibitishie ulazima wa kuwepo siku hiyo kwa kuwabainishia hoja tatu ili waondokane na fikra yao hiyo potofu.
8. Katika jamii ya Waislamu wapo watu wasiokubali ukhalifa wa Khalifa wa kwanza kwa kutokana na mitazamo tofauti juu ya uchaguzi wake. Tumia hoja mbili madhubuti kuwafafanulia waislamu hao mitazamo hiyo ili wasije kuingia kwenye makosa.
SEHEMU C (Alama 30)
Jibu maswali mawili (2) kutoka sehemu hii
9. Miongoni mwa hoja wanazozitumia wasio waislamu katika kuichafua Qur’an ni kudai kuwa ni kitabu cha mashairi ya Mtume Muhammad (Sallallahu Alayhi Wasallam). Toa hoja nne kuwadhihirishia watu hawa kuwa wanachokidai si sahihi.
10. Umealikwa kutoa semina kwa mahujaji watarajiwa juu ya utekelezaji wa ibada ya Hijjah. Waambie namna watakavyoweza kufikia kumpenda Allah kikwelikweli kwa kupitia utekelezaji wa ibada hiyo? (Hoja tano)
11. Mwalimu ameingia darasani kufundisha usahihi wa hadith za Mtume Muhammad (Sallallahu Alayhi Wasallam) kwa kuangalia matini yake. Atatumia hoja gani kuelezea mada hii? (Hoja tano)
FORM FOUR EDK EXAM SERIES 244
FORM FOUR EDK EXAM SERIES 244